Kwanza hebu tufahamu maana
ya neno lenyewe Saikolojia ni kitu gani, Saikolojia ni elimu ya akili au nafsi.
Kwahiyo saikolojia ya fedha ni elimu ya jinsi tunavyoichukulia fedha ndani ya
akili zetu.
Saikolojia ya pesa ni kitu
muhimu sana tunapozungumzia suala zima la mali na utajiri kwa sababu fedha
maana yake ni NGUVU na vilevile ni
muhimu sana nguvu hii mtu ukajifunza kuitendea matendo yaliyokuwa chanya ikiwa
utataka iongezeke na kuwa nyingi.
SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na
utajiri wa haraka.
Ili kutambua hasa ni jinsi
gani mtu unavyoweza ukatengeneza pesa nyingi ni lazima kwanza ufahamu ni
kwanini watu hawapati pesa, kuna sababu kadhaa ni kwanini watu hukosa pesa na
kumi kati yake ni hizi zifuatazo;
1.
Fedha ni lazima ipendwe.
Mara nyingi watu huwa hawana
mapenzi na fedha, je unafahamu maana ya kuipenda fedha na saikolojia chanya ya
fedha? Hebu jaribu kufikiria kidogo kisha utoe jibu, wengine watajibu kwamba, “mimi
ninachokipenda ni kutumia pesa” na bila shaka hayo ndiyo mawazo ya
waliokuwa wengi. Kwamba mapenzi yao kwenye pesa yameegemea zaidi katika MATUMIZI. Watu hawapendi pesa bali
wanachokipenda wao ni kile kitu pesa inachoweza kununua na hili ni kosa kubwa
sana!
SOMA: Hatua
6 na kanuni ya kuingiza kiasi chochote cha pesa unachotaka maishani.
Hebu jiulize tena swali jingine
hili, “Kwanini wikiendi unawatoa out watoto wako na kuwanunulia midoli na
magari ya kuchezea?” Jibu rahisi unaweza ukajibu ni kwa sababu unawapenda.
Kuwapeleka matembezini na kuwanunulia watoto wako zawadi hakumaanishi kuwa
unawapenda sana bali upendo wa kweli kwao unadhihirishwa na jinsi UNAVYOWAJALI. Hivi ndio kusema kwamba
yoote yale unayowafanyia wanao lengo lake kubwa ni kuwajali na kuwatunza na
hali ni hivyohivyo ilivyo kwa pesa, pesa inahitaji matunzo na kupendwa.
Nitatoa mfano wa watu wawili
wanaokwenda sokoni kununua pochi (wallet) ya kutunzia fedha. Wazo la mtu wa
kwanza ni kwamba yeye anahitaji tu pochi mpya kama urembo ingawa pia ataitumia
kuwekea fedha zake. Mtu wa pili yeye lengo lake mahsusi anahitaji pochi kwa ajili ya kuzifanya fedha
zake zikae salama kwa raha mustarehe. Sasa hebu tuseme kama wewe ndio
ungelikuwa PESA, niambie
ungelichagua kuingia katika pochi ipi kati ya hizo pochi mbili?
SOMA: Je wajua kitu
binadamu anachopenda kuliko vyote duniani?
Bila shaka yeyote ile wengi
mngelichagua pochi ya mtu wa pili kwa kuwa hakuna asiyependa kupendwa, usalama,
starehe, amani na kujaliwa!!! Na hii ndio saikolojia yenyewe ya pesa, ukitaka
pesa iwe rafiki kwako na kuongezeka ni lazima uipende, kuijali na
kuithamini
2.
Kauli hasi(-) kuhusiana na pesa.
Kuwa makini sana kuhusiana
na maneno uayotamka kama vile, Sina pesa, Vyuma vimekaza, hali yangu kifedha ni
tete sana nk. Maneno kama haya yanaweza yakasababisha kweli ukakosa kabisa
pesa. Badala ya maneno hasi kama hayo unaweza ukatamka hivi, Pesa
ipo njiani kuja kwangu, ipo siku tu, one day yes!, pesa tayari inagonga
mlangoni pangu, pesa naziona zinanichungulia dirishani nk.
SOMA: Wanaosema
nikishinda bahati na sibu milioni 100 nitafanya hiki na kile wakishinda hufanya
kinyume.
Kuwa kama Dokta Shika (Mungu amrehemu) yule jamaa aliyekwenda kununua maghorofa posta
akiwa senti tano mfukoni hana, unajua saikolojia aliyotumia yule jamaa
ilivyomsaidia? Hata madai ya fedha zake Urusi pengine hayakuwa na mashiko
kivile lakini saikolojia ile ya kuamini pesa ilikuwa ikimchungulia dirishani,
iliweza kumfanya apate ‘shavu’ la nguvu kutoka kwa makampuni kibao nchini
yakiwemo ya bahati na sibu hatimaye akapata ‘mpunga’ (pesa) iliyomsaidia kuvuka
mahali pagumu alipokuwa.
Katika Saikolojia ya pesa,
pesa pia unaweza ukaifananisha na mtoto mchanga, mtoto mdogo anapoanza
kujifunza vitu mbalimbali kama vile kutambaa au kutembea wazazi wake na walezi
humsifia na kumpa moyo kwa kusema, “Umekua mwanangu ee” “Kazana nitakununulia
pipi” nk. hapo mtoto kweli hukazana mpaka ameweza kabisa kile anachojifunza
tena kwa muda mfupi ajabu!
SOMA: Kinamama
huwabeba watoto wao kipindi kifupi lakini mioyo yao huwabeba milele.
Pia ASILI hututendea sisi
binadamu kwa namna kama hiyohiyo ya mtoto mdogo anavyotendewa na wazazi wake,
pindi tu tunapoanza kuchukua hatua chanya za awali katika jambo lolote lile
maishani ikiwemo kutafuta pesa, asili hutupa mara moja matokeo ya upendeleo
kusudi tuweze kuwa na uhakika na nguvu ya kuendelea mbele tukifahamu kwamba
tupo katika uelekeo sahihi na tunahitaji kufika mbali zaidi ya pale tulipokuwa.
Jitahidi kubadilisha kabisa mtazamo wako wa fedha kuwa chanya kwa maneno kama
haya;
·
Napenda pesa na nazipata kwa urahisi
·
Natengeneza pesa na kuzitumia kwa
urahisi
·
Mara zote naweza kuingiza pesa kiasi
ninachotaka nk.
3.
Wekeza ndani yako mwenyewe
Usiache kununua kile
ulichopanga kununua kwa ajili yako mwenyewe, vinginevyo ASILI itaichukua fedha
hiyo kwa namna nyingine tofauti kabisa. Kwa mfano anaweza kuja rafiki au ndugu
akajifanya kukukopa na asijekukulipa tena kamwe au anaweza kutokea kibaka/mwizi
kusikojulikana na kuikwapua fedha hiyo hivihivi ikapotea nk.
SOMA: Njia
7 za kubana matumizi bila kuhisi unajitesa kuboresha bajeti yako.
4.
Kuwa Mkarimu na mtoaji kwa watu wengine
Ukarimu hapa haumaanishi
utapanye ovyo pesa zako kuwaridhisha watu hapana, inamaanisha usiwe bahili
kupita kiasi, kwa mfano pale unapotakiwa kufanya malipo au kumlipa mtu chake
fanya hivyo bila manunguniko wala kisirani rohoni, unaponunua vitu vipya nk.
unahitaji kuwa na saikolojia nzuri ya fedha.
5.
Woga wa kufikwa na majanga au kufilisika
Fedha ni aina ya NGUVU na
inatakiwa kutunzwa(unapoiweka kama akiba) ukitumia maneno chanya+ mfano;
· Akiba
hii ni kwa ajili ya safari na wala siyo “kwa ajili ya kipindi cha uzeeni”
· Kwa
ajili ya dharura na wala siyo kwa ajili ya majanga
· Kwa
ajili ya kuboresha afya na wala siyo kwa ajili ya kutibu magonjwa
6.
Kuwa makini unapo mkopesha mtu
Kisaikolojia unapokopesha
pesa zako inamaanisha kwamba pesa hiyo huna kazi nayo, vinginevyo basi
unatakiwa ukopeshe kwa DHAMANA.
Dhamana haimaanishi kwamba unayemkopesha hafai au hatalipa hapana, bali ni kwa
sababu hamna mtu anayeweza kuwa na uhakika na mambo yajayo, mtu anaweza baada
ya kukopa akaja kupata majanga kama ya kufungwa jela, kuuguliwa nk. na pesa
yako ikapotea hivihivi, lakini kama aliweka dhamana fulani itakusaidia
kurudisha fedha zako.
SOMA: Je kukopa ili ukalipe deni la zamani kunawezaje kuboresha
mzunguko wa fedha kwenye biashara yako?
Ndio maana Waswahili
wakasema, “Ukitaka kumpoteza rafiki basi
wewe mkopeshe tu pesa” Ikiwa mtu atakataa kukulipa deni unalomdai basi ujue
amekufundisha somo kubwa ili usije tena hapo baadae kurudia kumkopesha mtu
mwingine kizembe. Saikolojia ya pesa huwa haina tabia ya kusamehe wala kumuonea
mtu huruma.
7.
Hesabu fedha zako
Neno “Umasikini” (Poverty) asili yake ni neno, “Usihesabu”. Njia pekee ya kudhibiti fedha zako ni kuzihesabu. Acha
mara moja kuwaachia wasaidizi wako biashara kizembezembe bila ya mahesabu ya
uhakika, wakishakuliza saikolojia ya pesa haina cha kukusaidia zaidi ya
kukuadhibu vikali na kukucheka..............................................................................................................................................................................................................................................................................................
.................Somo hili halijafika
mwisho litaendelea leo saa 3 usiku katika Group la masomo ya kila siku la
MICHANGANUO-ONLINE. Bado kanuni 3
Kujiunga na kupata masomo kamili kila
siku pamoja na masomo yote mengine zaidi ya 100 unalipia ada ya mwaka shilingi
elfu 10 tu.
Unapata pia na Offa ya vitabu na michanganuo
ya Biashara jumla vitu 14. Offa ni ya muda mfupi itaondolewa ama kupunguzwa
vitu.
Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244
jina ni Peter Augustino Tarimo. Ukishalipia tuma ujumbe usemao. "NATAKA OFFA YA VITU 14 NA GROUP LA MASOMO
YA FEDHA"
CHINI NI ORODHA YA VITU 14
VYA HIYO OFFA;
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa Kiswahili
2.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu - kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani, hutumika
vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
5.
KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO
CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa
kiswahili
6.
COMPILLATION: Masomo 30 ya fedha
usiyoweza kuyapata popote, mengine 70 utayapata kwenye group kila siku - kwa Kiswahili
7.
MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji
Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
8.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa
kiingereza
9.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa Kiswahili
10. MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili
11. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiswahili
13. MCHANGANUO: Kiwanda cha mvinyo na juisi ya Rosella –Choya Investment – kwa kiswahili
14. MCHANGANUO: Kilimo cha Tikiti maji:- Kibada Watermelon Fruits – kwa kiswahili
0 Response to "SAIKOLOJIA YA PESA NA KANUNI 10 ZA KUFUATA ILI UWE MTU ULIYEFANIKIWA KIMAISHA"
Post a Comment