Kubana matumizi siyo kitu kibaya hata kidogo ilimradi tu
kile unachotumia kina kidhi mahitaji yako na kukufanya uendelee kuishi kama ni
chakula unashiba sawasawa tu na yule aliyekula biriani na kama ni kiu pia
inakatika sawasawa tu na yule aliyekunywa juisi au soda. Shida haipo kwenye
kukidhi haja bali ipo kwenye hisia za mtu, ile hali ya kuhisi akilini kwamba
unajitesa. Isingelikuwa hivyo wala
kusingelikuwa na shida yeyote ile kwenye kubana matumizi.
Kwa bahati mbaya sana linapokuja suala la matumizi ya
pesa, suala la kubana matumizi siyo rahisirahisi kama mtu unavyoweza kufikiria,
hakuna mtu hata mmoja anayefurahia kujinyima kitu wakati anakiona na anaona
wenzake wanatumia wala hakuna mtu anayefurahia kula ugali wa mchicha na dagaa
wakati jirani yake kila siku anakaanga samaki na maini. Kusema ule ukweli hali
hiyo mbaya ya kihisia hatimaye huwafanya watu wengi badala ya kuendelea kubana
matumizi ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea kimaisha wanaamua kujiingiza
kwenye matumizi mabaya zaidi kushinda hata ilivyokuwa mwanzoni.
SOMA: Kufikia ndoto na malengo yako, hizi hapa ni hatua 3 za kutengeneza bajeti ya jambo lolote maishani.
Mtu anaamua kuvaa miwani ya mbao, kuvaa miwani ya mbao
maana yake ni kujifanya kama vile tatizo halioni, ni sawa na mtu anayeamua
kulewa pombe na kufanya mapenzi na mtu ambaye katika hali ya kawaida
asingeliweza kabisa kufanya hivyo. Kwahiyo mtu anaamua kuingia kwenye matumizi
makubwa na kuharibu kabisa bajeti yake bila kujali kitu kutokana na hisia zile
za kujitesa anazozipata pindi anapokuwa akibana matumizi, hali ya kuhisi kutokuwa
nacho, wengi huamua kujisemea, “niache
niponde mali bwana kwani kufa kwaja”
Kwa hiyo leo hii katika group la masomo ya kila siku,
somo letu la fedha ambalo ni somo la 3 miongoni mwa masomo 30 ya mwezi huu wote
wa 12 tutakwenda kujifunza njia 7 mtu unazoweza kuzitumia na kuishi maisha
kulingana na kipato chako unachopata bila ya kuhisi kabisa kama unajitesa wala
kubana matumizi kupita kiasi.
Ndugu
msomaji, masomo haya si ya kukosa ikiwa wewe unapenda kujifunza masuala ya
fedha na ujasiriamali. Tulianza tangu mwezi January na sasa tuna masomo
yanayojaza vitabu 3 vikubwa ambavyo pamoja na vitu vingine kama semina,
michanganuo ya biashara mbalimbali zinazolipa na vitabu vya jinsi ya kuandika mpango
wa biashara kwa Kiswahili na kiingereza vyote hivi tumevikusanya na tunakutumia
katika mfumo wa softcopy( PDF.)
Ili kujiunga unalipia ada ambayo ni shilingi elfu 10 na
muda huohuo tunakutumia masomo pamoja na kukuunganisha na group. Ada hiyo ni ya
kudumu kwa mwaka mzima wa 2019 hutalipia tena chochote.
Namba za malipo ni 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo.
WHATSAP ni 0765553030
Ukishalipia tuma ujumbe wa kawaida au wa wasap usemao, “NIUNGANISHE
NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”
Ikiwa hutumii Whatsapp hamna shida, masomo yote
tunakutumia kupitia E-mail yako.
Mwisho wa offa ya masomo haya ni tarehe 30 Desemba 2018.
Baada ya hapo tunaanza programu nyingine na masomo yote ya 2018 hayatakuwepo
tena. Wahi kwani nafasi katika group pia zimebakia chache.
Pamoja na vitu vingine 10, Hapa chini ni vitabu 3 vyenye masomo na semina za toka Januari mpaka Novemba;
0 Response to "NJIA 7 ZA KUBANA MATUMIZI BILA KUHISI UNAJITESA KUBORESHA BAJETI YAKO"
Post a Comment