IKIWA IMEBAKIA MIEZI 3 KAMILI MWAKA UISHE, POKEA ZAWADI HII YA VITABU 3 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

IKIWA IMEBAKIA MIEZI 3 KAMILI MWAKA UISHE, POKEA ZAWADI HII YA VITABU 3


NI MWISHO WA MWAKA SASA
Ni miezi miwili tu na siku 9 zimebakia tokea leo hii ili mwaka wa kawaida uishe, lakini ni miezi 3 kamili imebakia ili kampeni yetu ya mwaka huu imalizike rasmi. Kampeni au kauli mbiu yetu ya mwaka 2018 ilikuwa inasema hivi, MZUNGUKO MZURI WA FEDHA NDIYO NJIA BORA ZAIDI YAKUFIKIA MALENGO YAKO MWAKA 2018 na ilikuwa ikitekelezwa kupitia blogu ya jifunzeujasiriamali, Group la whatsapp la Michanganuo-online na katika mitandao mingine ya kijamii mbalimbali. Tulianza rasmi tarehe 19/1/2018.




Muda huu mfupi uliobakia tutamalizia baadhi ya malengo tuliyojiwekea huku tukifanya tathmini ya yale tuliyokwishatimiza kama ilivyokuwa kwa kampeni nyingine zote zilizopita huko nyuma. Kumbuka tuliwahi kuwa na kampeni nyingine mbili miaka iliyopita, ile ya "Kuelekea utajiri" na nyingine ilikuwa ikiitwa, "Kujirudishia ukuu wako tena"au “Make yourself Great Again”.


Malengo yetu makuu kwa mwaka huu yalikuwa ni haya yafutayo;

1.  Kutoa masomo kila siku yanayohusu mzunguko chanya wa fedha katika biashara na mtu binafsi.

2.  Kuandika Hatua kwa hatua mipango ya biashara 12. Hii ni michanganuo bunifu ya biashara zile zenye uwezo mkubwa wa kuzalisha faida haraka.

Utekelezaji wake.
Mpaka sasa lengo la 1 tumelitimiza kwa zaidi ya asilimia 95, wale waliojiunga na group la wasap la Michanganuo-online ni mashahidi. Tumetoa masomo mbalimbali ambayo mkusanyiko wake tumetengeneza vitabu 2 vyenye kurasa zipatazo 100 kila kimoja. Masomo hayo ni ya hali ya juu yanayolenga kumfanya mtu aweze kuboresha mzunguko wake wa fedha katika biashara yake na pia mfukoni mwake. Ni furaha yangu kubwa kuwa wewe rafiki na mdau wangu muhimu kabisa hautakosa kuvisoma vitabu hivi 3 vilivyokusanya madini mengi ya mwaka mzima.


Katika lengo letu la pili tumeweza kulitimiza kwa asilimia 35 mpaka sasa hivi na tumechanganua hatua kwa hatua michanganuo ya biashara nne 4, mitatu ya ufugaji wa kuku wa aina zote na mmoja kilimo cha matikiti maji. Michanganuo hiyo yote tuliandika hatua kwa hatua huku kila mshiriki akijifunza jinsi michanganuo ya biashara hizo inavyoandikwa kuanzia mwanzo hadi mwisho na kisha kila mtu kupata kopi yake ya mchanganuo uliokamilika kila kitu.

Muda uliobakia wa miezi 3
Tutafanyia kazi lengo letu hili la pili ambalo halijakamilika bado tumalizie asilimia 65% zilizobakia . Tutaanza tarehe 3/11/2018 tukiandika hatua kwa hatua mpango wa biashara ya Mgahawa wa chakula. Chakula ni moja kati ya biashara zinazolipa sana ukiifanya kwa ubunifu, hivyo tutaanza nayo na kila baada ya wiki moja tena tutaendelea kuchanganua biashara nyingine zilizobakia mpaka zitimie zote 12 ifikapo Januari 19 2019 tutakapohitimisha rasmi kampeni yetu hii na kuanza tena nyingine mpya.


Wito wangu kwako na zawadi ya vitabu 3
Ikiwa bado hukuwa umejiunga na kampeni yetu hii, nafasi bado ipo na utaweza kupata kila kitu walichopata wale waliotangulia. Masomo yote ya mtiririko wa fedha tumeyakusanya(compile) katika vitabu vikubwa 2 na yale yahusuyo kuandika Michanganuo hatua kwa hatua tumeyakusanya pia katika kitabu kimoja kikubwa chenye kurasa 100. Isitoshe kuna vitu vingine unapata kama kile kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali, vitabu vingine na masomo mbalimbali ambayo hayapo katika vitabu hivyo. Orodha kamili ya vitu vyote unavyopata baada ya kujiunga ni hivi hapa chini;
  
1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

9.  Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

10.      Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

11.      Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

12.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

Mwisho wa offa na vitabu hivi ni Januari 19, 2019 lakini pia itategemea muda group hili la Michanganuo litakapojaa watu 250, iwapo litajaa kabla ya tarehe hiyo jambo ambalo nategemea litatokea kwani sasa group lina zaidi ya watu 100, basi na nafasi nazo zitakuwa zimejaa. 

Baada ya hapo tena vitu vyote hivyo vitakuwa kila kimoja kikiuzwa peke yake kwa bei tofauti. Hivyo ni bora mtu ukawahi mapema kusudi uweze kupata kila kitu kwa shilingi elfu 10 tu. Ni punguzo kubwa ambalo halitakaa litokee tena na halijawahi kutokea popote. Ukisema uje ununue kila kimoja peke yake, vyote utalazimika kulipa zaidi ya shilingi laki moja.


Ikiwa unapenda kujiunga na group la Michanganuo-online uweze kushiriki semina zinazoanza tarehe 3, Novemba pamoja na kupata vitabu hivyo vipya 3 na offa nyingine zilizotajwa hapo juu zote, lipa kiingilio chako ambacho ni shilingi elfu 10 kupitia namba zetu za simu, 0712202244 au 0765553030, jina ni Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe wa whatsapp au wa kawaida usemao, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO” Namba ya whatsapp ni 0765553030. Baada ya hapo utaunganishwa muda huohuo na kutumiwa kila kitu.

Kama hutumii whatsapp, masomo haya na kila kitu tunatuma kupitia email na blogu ya private hivyo utatutumia tu anuani yako ya gmail unayotumia.

Ufuatao ni muonekano wa vitabu vyako vipya vitatu;


Kitabu cha 1



Kitabu cha 2



Kitabu cha 3






0 Response to "IKIWA IMEBAKIA MIEZI 3 KAMILI MWAKA UISHE, POKEA ZAWADI HII YA VITABU 3"

Post a Comment