2017 NI MWAKA WA KUJIRUDISHIA UKUU WAKO TENA(MAKE YOURSELF GREAT AGAIN) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

2017 NI MWAKA WA KUJIRUDISHIA UKUU WAKO TENA(MAKE YOURSELF GREAT AGAIN)
Mpenzi msomaji wa blogu hii ya Jifunzeujasiriamali, bila shaka katika maisha yako tangu ulipokuwa mtoto mdogo uliwahi kuwa na ndoto kuwa utakapofikisha umri wa utu uzima utafanya kitu fulani au utakuwa na kitu fulani. Ulijiwekea malengo makubwa na pengine mpaka hivi leo haujaweza kuyatimiza yote kama ulivyojiwekea. Wapo walioota kuja kumiliki majumba makubwa, kuwa na kazi nzuri, kuendesha ndege, kuwa kiongozi wa ngazi ya juu serikalini au siasa, kuwa na mke mzuri, familia nk.

Siyo hivyo tu, katika maisha hayo ya utoto au hata ujanani inawezekana ulikuwa na vipaji mbalimbali, uwezo katika masomo, uwezo katika nyanja mbalimbali na hata inawezekana sasa hivi wewe ni mzee au mtu wa makamo na katika nyakati fulani za maisha yako uliwahi “kutesa” kwa maana nyingine uliwahi kuwa na maisha mazuri iwe ni katika kipato, masomo darasani, afya au hata mafanikio mengineyo yeyote yale kimaisha ambapo kwa sasa hivi, furaha, amani na mafanikio yote hayo vimetoweka mithili ya donge la barafu.

Wakati ulipokuwa katika nyakati hizo nzuri(Ukiwa katika kilele cha UBORA WAKO), kwa lugha ya mitaani wanasema “ulipokuwa katika good times watu wengine walikuwa wanakuheshimu na hata wewe mwenyewe jambo ulilokuwa ukilisema mbele ya jamii iliyokuwa ikikuzunguka lilikuwa likiheshimika na kufanyiwa kazi mara moja hata ikiwa watu waliokuwepo kwa muda huo walikuwa wamekuzidi umri. Kwa kweli kilikuwa ni kipindi cha furaha kubwa isiyokuwa na kifani.

Kumbuka wakati huo ninaouzungumzia siyo lazima uwe ni wakati umeshakuwa mtu mzima la hasha, kilele cha ubora wako kinaweza hata kikawa ni kipindi ulipokuwa ukisoma shule ya msingi, ukiwa mtoto, ukiwa chuoni, ukiwa kazini nk.Kwa mfano mimi binafsi kipindi cha ubora wangu nakumbuka kilikuwa ni wakati nilipokuwa nasoma shule ya msingi.

Kuna mambo mengi mazuri nayakumbuka niliyokuwa nayafanya na moja lilikuwa ni Ucha Mungu uliokuwa umekamilika, nilikuwa na uwezo wa kuombea jambo na kweli nikaona matokeo yake, pia ni kipindi ambacho karibu kila jambo nililolifanya lilifanikiwa kuanzia darasani mpaka shughuli zangu za ufugaji wa kuku na kilimo cha bustani nyumbani.

Sasa hivi ukiwa unajiuliza ni nini hapo katikati kilichokuja kwenda mrama mpaka ukapoteza ule ukuu wako uliokuwa nao, nadhani utakuwa na sababu nyingi sana, nyingine ukijilaumu kwa kuzisababisha mwenyewe na nyingi ukitoa lawama kwa watu mbalimbali na hata serikali kwamba bila ya wao leo hii usingelikuwa umepoteza ukuu uliokuwa nao. Lakini lawama kwako au hata kwa watu wengine na serikali haziwezi zikabadilisha kitu chochote kile kwani hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako mwenyewe na ni wewe unayeweza kuamua kuibadilisha au kufanya iendelee kuwa kama ilivyo leo.

Mwaka huu mpya ujao wa 2017, nimeandaa kampeni kubwa maalumu kwa ajili yako wewe ambaye unapenda KURUDISHA TENA UKUU ULIOKUWA NAO lakini kwa sababu mbalimbali ukaja kukuponyoka, KUJIHUISHA TENA au KURUDISHA UWEZO ULIOKUWA NAO KWA MARA NYINGINE TENA. Nimeamua kuitumia kaulimbiu ya ushindi aliyoitumia Rais mteule wa Taifa la Marekani Bwana Donald Trump kuingia ikulu ya White House kinyume kabisa na matarajio ya wengi.

Vivyo hivyo kinyume kabisa na matarajio ya wale wanaokufahamu na wanaodhania ya kwamba huu ndiyo mwisho wako na hautakaa uje uinuke tena watashangazwa na jinsi utakavyoweza kurudisha ukuu wako kwa mara nyingine tena. Kuwa tena mtu mwenye thamani mbele ya jamii, kuwa tena mtu unayejitegemea, usiyeombaomba kama Matonya, kuwa tena mtu wa ibada unayetii maagizo ya Mwenyezi Mungu na Kurudi tena kuwa mtu mwenye malengo na msimamo usioyumbishwa ovyo na watu wenye pesa au mamlaka.

Kampeni hii kama kampeni nyingine tulizoendesha huko nyuma kwa mafanikio makubwa mfano ile tuliyoibatiza jina, “KUELEKEAUTAJIRI” itaendeshwa kupitia blogs, vitabu na mitandao ya kijamii yote ya Self Help Books Publishers kwa njia mbalimbali zikiwemo makala, picha, video, na sauti.

Msomaji kwa kufuatilia kampeni hii utapata manufaa makubwa katika maisha yako siyo tu katika suala zima la biashara na ujasiriamali, bali hata na mtazamo wako kifikra katika maisha ya kila siku. Utajirudishia maisha yako yaliyokuwa yamejaa heri, fanaka na matumaini makubwa. Maisha yaliyojaa mafanikio katika kila jambo unalolifanya hapa duniani.

Ili kwenda sambamba na kampeni hii nitakuomba ufanye mambo kadhaa, nasema nitakuomba kwa sababu ni hiari yako siyo lazima, unaweza tu kufuatilia kampeni bila kutimiza vitu hivyo na ikakusaidia lakini itakusaidia zaidi na utaona matokeo bora na chanya zaidi endapo utaweza kutimiza ombi ninalotaka kukuomba. Ombi lenyewe ni hili hapa chini,

Jitahidi sana upate package(kifurushi cha self help books), vile vitabu 3 mashuhuri vya elimu ya biashara , ujasiriamali na maendeleo binafsi) “The books of all Times” /vitabu vya wakati wote visivyopitwa na wakati, biashara itaendelea kuwepo muda wote binadamu atakaoishi duniani. Vitabu hivyo ni hivi vifuatavyo;-

Kitabu cha kurasa zaidi ya 400 kilichobeba masomo yote ya ujasiriamali na biashara pamoja na michanganuo halisi ya biashara na mawazo ya biashara zinazolipa zaidi ya 50.

Kitabu kinachokupa muongozo kamili wa namna ya kufanya biashara yeyote ile ya rejareja kwa ufanisi wa hali ya juu. “Baadhi ya watu hudai eti, Duka halina faida, lakini usidanganyike, kwanini wasiyafunge na kila siku unayaona mapya yakifunguliwa? Gundua siri iliyojificha nyuma ya pazia kwa muda mrefu huku ukidanganywa biashara za rejareja hazina faida wakati wengine wakinunua magari na kujenga majumba kwa biashara hizohizo.

Huwa nakiita kitabu cha maajabu kwani kitabu hiki kimebadilisha mno maisha ya watu wengi. Ukitaka kufahamu kama kitu ni kizuri basi utaona watu wakikazana kukiiga. Kitabu hiki nilichokitoa tangu mwaka 2012 kimeigwa na watu mbalimbali wengine wakiita vya kwao, Mifereji 9 ya pesa, Mifereji 10 ya kipatao nk.Lakini Kitabu Original ni ‘Mifereji 7 ya Pesa’ kilichoandikwa na Peter Augustino.

Kwa kifupi unaposoma kitabu hiki kama ulikuwa umeajiriwa unaweza siku hiyo hiyo ukaenda kumwambia bosi wako “Naacha kazi bosi nikaanzishe biashara yangu mwenyewe” Lakini nakusihi utakapokisoma usije ukadhubutu kufanya hivyo kwani unahitaji muda wa matayarisho kufanya jambo kama hilo na hata katika kitabu chenyewe mwishoni nimekuwekea tahathari hiyo.

Wala siyo lazima upate vitabu vyote 3 unaweza hata ukachukua kimoja tu ingawa pia kuvipata vyote ni vizuri zaidi.

Kitu kingine ninachokuomba ujitahidi kukipata ili uweze kwenda na mimi sambamba katika Kampeni hii kubwa ya kihistoria ni Kitabu ninachokigawa bure kwa njia ya E-mail kiitwacho, “KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO” Umuhimu wa kitabu hiki utaujua baada ya kukisoma. Kukipata unajiunga na blogu hii hapa.

Zana hizo 4 ukiwa nazo pamoja na kuifuatilia kikamilifu kampeni tunayokwenda kuianza ya “KUJIRUDISHIA UKUU TENA” au “MAKE YOURSELF GREAT AGAIN” , Sina shaka yeyote kwamba mwaka tunaoenda kuuanza wa 2017 utakwenda kuwa wa Mafanikio na Baraka nyingi kwako. Anza mwaka huo kwa furaha na amani kama atakavyofanya Raisi  Mteule Donald Trump na familia yake, mkewe wa 3, Melania, wanawe, Donald Trump Jr. Ivanka, Eric na Barron.

Familia ya Rais Mteule wa Taifa la Marekani Donald Trump


0 Response to " 2017 NI MWAKA WA KUJIRUDISHIA UKUU WAKO TENA(MAKE YOURSELF GREAT AGAIN)"

Post a Comment