Mwajabu ni mama mwenye duka la vyakula la rejareja katika
mtaa wa Kumekucha Sinza jijini Dr es salaam. Jirani na duka lake amezungukwa na
washindani watatu wanaomiliki maduka kama lakwake na yaliyo na bidhaa
mchanganyiko zinazofanana na zakwake pia jambo linalosababisha pawe na
ushindani mkali na wateja kuchagua ni wapi pakununua mahitaji yao ya nyumbani kila
siku kulingana na unafuu ama huduma wanazopewa na maduka haya manne.
Ingawa Mwajabu hujitahidi kwa kila hali kutimiza mahitaji
yote ya wateja wake ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora zinazozidi matarajio
yao lakini bado alishangaa kuona kuna mteja mmoja tena mwanamke mwenzake
humpita kila siku na na kwenda kununua bidhaa katika moja ya duka la washindani
wake. Baada ya kujaribu kuchunguza sana ni nini mteja huyu anachovutiwa nacho
kwa mshindani wake ambacho yeye hana hakuweza kupata jibu dhahiri.............................
SOMA: Chuma ulete anavyowatesa wenye maduka na wafanyakazi wao dar
Nitamalizia baadae kidogo stori hii ya Mwajabu lakini
hebu kidogo tujadili sababu zinazowafanya wateja kuchagua duka au mahali pa
kujipatia mahitaji yao/kununua bidhaa ama huduma zao. Kitu cha kwanza kabisa
mteja anataka kutatua shida inayomkabili katika mazingira rafiki na rahisi kwa
kadiri inavyowezekana. Kwahiyo inawezekana kabisa pamoja na kuwa na suluhisho
la shida ya mteja lakini kuna mazingira fulani hujaweza kuyatimiza ndiyo maana
mteja anaamua kukupita na kwenda kununua kwa mshindani wako.
Kuna sababu nyingi wateja huangalia kwa mfano bei, huduma
bora, ucheshi wa muuzaji, ubora wa bidhaa/huduma, bidhaa na huduma
tofautitofauti (mteja Napata kila kitu chini ya mwavuli mmoja), ukaribu na
anapoishi mteja, mpangilio mzuri wa bidhaa, uhusiano wa karibu na mteja, punguzo
la bei(discount), nyongeza nk. Mteja inawezekana hukupita tu kwa sababu muuzaji
duka la jirani ana mahusiano naye kimapenzi lakini wewe huwezi kulijua hilo
kirahisi.
SOMA: Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja
Vigezo vyote hivi na vingine ambavyo sikuvitaja hapa vinaweza
kuwa ndiyo sababu kubwa ya mteja fulani kukupita kila siku na kwenda kununua
kwa mshindani wako.
Nikimalizia ile stori niliyoanza nayo ni hivi; Mwajabu
baada ya kujiuliza kwa muda mrefu ni kwanini mteja yule huwa anampita kila siku
ili hali na yeye ana kila kitu maduka mengine walichokuwa nacho aliamua tu
kutulia tuli na wala hakuweka kinyongo kwa yule mteja akimshukuru Mwenyezi
Mungu kwani hamnyimi wateja kabisa na anauza tu kila siku mauzo ya kuridhisha.
Akipita, tena Mwajabu humsalimia bila hiyana huku akiendelea na hamsini zake.
SOMA: Mbinu hizi 2 za uendeshaji duka la rejareja kwa mafanikio hazipo mahali pengine popote
Subira huvuta kheri, hatimaye siku moja yule mteja
alifika dukani kwa Mwajabu na kumtaka amuuzie bidhaa mbalimbali, jumla ni kama
vitu vya shilingi elfu ishirini (20,000/=) hivi! Mwajabu hakuamini macho yake,
akamfungia mzigo wake wakaagana akaondoka. Tangu siku ile yule mteja
aliendelea kuwa mteja mwaminifu wa Mwajabu ingawa pia siku moja moja aliendelea
kumpita kama kawaida yake.
Hitimisho
Stori hii ya duka la rejareja la Mwajabu inatufunza somo
muhimu la uvumilivu na kutokukata tamaa. Mwajabu hakukimbilia kunena, “Ona
sisi wanawake tusivyopendana kabisa, ningekuwa mwanaume angeshakuja kununua
kwangu siku nyingi tu, muone ananipita kila siku na kwenda kutafuta duka
analouza mwanaume” bali alivuta subira kwani hakuijua bayana ni sababu
ipi iliyokuwa ikimfanya asinunue kwake siku zote hizo
Hebu jaribu kufikiria wewe mwenyewe ni maduka mangapi
umewahi kuyaacha na kwenda mbali maduka mengine kutafuta kitu ulichokuwa
ukikihitaji kutokana na sababu mbalimbali? Lakini si kuna siku pia unaamua
kuwaungisha maduka hayo uliyoyapita kwa kuwa wanakidhi haja ya kile
unachoihitaji wakati huo? Basi na wateja wako ni hivyohivyo walivyo wala
hawakupiti kwa bahati mbaya, wewe wavumilie tu wala usiwanenee mabaya au
kuwatukana kwani ipo siku isiyokuwa na jina utashangaa kuwaona wakija kwenye
biashara yako kununua.
SOMA: Biashara ya soda maji juisi na sigara: tumia siri hii kuongeza mauzo × 2
Na zaidi ya hapo kila siku tafiti na kuboresha huduma
zako, weka bidhaa mpya, inawezekana kabisa ukarekebisha udhaifu ulio nao unaowafanya
baadhi ya wateja wakupite na mwishowe wakarudi kwako.
Kwa elimu ya kina zaidi na mifumo itakayokuwezesha
kusimamia biashara yako ya duka la rejareja au biashara yeyote nyingine ile ya
rejareja hata kama ni Genge la matunda na mboga usiache kupata nakala ya kitabu
chako cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA
LA REJAREJA
Kinapatikana kwa bei ya sh. elfu 6 tu kupitia namba zetu
hizi; 0765553030 au 0712202244 lipia nikutumie muda huohuo katika simu au
kompyuta yako au unaweza ukakidownload
mwenyewe kutoka katika duka hili la mtandaoni.
........................................................
Ndugu Msomaji wa makala hii, HERI YA MWAKA MPYA 2025-01-01
Tulishasema kwamba mwaka huu ni wa kujirudishia ukuu wako
tena (MAKE YOURSELF GREAT AGAIN) kwa
kutumia ubunifu, akili mnemba na kasi ya kutenda mambo tofauti na ilivyokuwa
mwaka uliopita
Programu zetu pia kwa mwaka huu nilishaweka wazi tangu
Octoba 2024 kwamba tutaendelea kutoa huduma kupitia blogu ya
jifunzeujasiriamali bure kabisa lakini pia kwa anayehitaji kujifunza kwa kina
ikiwa ni pamoja na kushiriki moja kwa moja madarasa yetu(Mastermind Groups)
basi atachangia ada kidogo ya shilingi elfu 10
Endelea kufuatilia kila siku makala katika blogu yako hii
kujua ni kipi kinachojiri.
Peter Tarimo
Simu: 0712202244 /
0765553030
Watsap: 0765553030
0 Response to "DAWA YA MTEJA ANAYEKUPITA KILA SIKU NA KWENDA KUNUNUA KWA WASHINDANI WAKO HII HAPA"
Post a Comment