Habari za muda huu mpendwa msomaji wa blogu hii na karibu sana kwenye
kampeni ya kufanya mabadiliko makubwa kimaisha 2025. Mwaka hauna rangi na
kinachobadilika ni tarehe tu kwahiyo ikiwa kama wewe ni mtu unayependa mwaka
huu uwe tofauti na miaka mingine yote naomba usome makala hii yote hadi mwisho.
Lakini ikiwa hupendi mabadiliko yeyote yale basi achana nayo usipoteze muda
wako wa thamani bure.
Karibu Sana!
Bila shaka katika maisha yako tangu
ulipokuwa mtoto mdogo uliwahi kuwa na ndoto kuwa utakapofikisha umri wa utu
uzima utafanya hiki na kile au utamiliki kitu fulani. Ulijiwekea malengo
makubwa na pengine mpaka hivi leo haujaweza kuyatimiza yote kama ulivyojiwekea.
Wapo walioota kuja kumiliki majumba
makubwa, kuwa na kazi nzuri, kuendesha ndege, kuwa kiongozi wa ngazi ya juu
serikalini au siasa, kuwa na mke mzuri, familia nk.
Siyo hivyo tu, katika maisha hayo ya
utotoni au hata ujanani inawezekana ulikuwa na vipaji mbalimbali, uwezo katika
masomo, uwezo katika nyanja fulani na hata inawezekana sasa hivi wewe ni mzee
au mtu wa makamo na katika nyakati fulani za maisha yako uliwahi “kutesa” kwa
maana nyingine uliwahi kuwa na maisha mazuri iwe ni katika kipato, masomo
darasani, afya au hata mafanikio mengineyo yeyote yale kimaisha ambapo kwa sasa
hivi, furaha, amani na mafanikio yote hayo vimetoweka mithili ya donge la
barafu.
Wakati ulipokuwa katika nyakati hizo
nzuri (Ukiwa katika kilele cha UBORA WAKO), kwa lugha nyingine “ulipokuwa
katika good times” watu wengine walikuwa wakikuheshimu na hata
wewe mwenyewe jambo ulilokuwa ukilisema mbele ya jamii iliyokuwa ikikuzunguka
lilikuwa likiheshimika na kufanyiwa kazi mara moja hata ikiwa watu waliokuwepo
kwa muda huo walikuwa wamekuzidi umri. Kwa kweli kilikuwa ni kipindi cha furaha
kubwa isiyokuwa na kifani kwako.
Kumbuka wakati
huo ninaouzungumzia mimi siyo lazima iwe ni wakati ulikuwa umeshakuwa mtu mzima
la hasha, kilele cha ubora wako kinaweza hata kikawa ni kipindi ulipokuwa
ukisoma shule ya msingi, ukiwa mtoto, ukiwa chuoni, ukiwa kazini nk.Kwa mfano
mimi binafsi kipindi cha ubora wangu nakumbuka kilikuwa ni wakati nilipokuwa
nasoma shule ya msingi.
Kuna mambo mengi mazuri nayakumbuka
niliyokuwa nayafanya wakati huo na moja lilikuwa ni Ucha Mungu uliokuwa
umekamilika, nilikuwa na uwezo wa kuombea jambo na kweli nikaona matokeo yake,
pia ni kipindi ambacho karibu kila jambo nililolifanya lilifanikiwa kuanzia
darasani mpaka shughuli zangu za ufugaji wa kuku na kilimo cha bustani ya
mbogamboga na matunda nyumbani.
Sasa hivi ukiwa unajiuliza ni nini hapo
katikati kilichokuja kutokea mpaka mambo yakaenda mrama ukapoteza ule ukuu wako
uliokuwa nao, nadhani utakuwa na sababu nyingi sana, nyingine ukijilaumu kwa
kuzisababisha wewe mwenyewe na nyingi ukitoa lawama kwa watu mbalimbali na hata
serikali kwamba bila ya wao leo hii usingelikuwa umepoteza ukuu uliokuwa nao.
Lakini lawama kwako au hata kwa watu
wengine na serikali haziwezi zikabadilisha kitu chochote kile kwani hatima ya
maisha yako ipo mikononi mwako mwenyewe na ni wewe unayeweza kuamua
kuibadilisha au kufanya iendelee kuwa vilevile kama ilivyo leo.
Mwaka huu mpya wa 2025, nimeandaa
kampeni kubwa maalumu kwa ajili yako wewe ambaye unapenda KURUDISHA TENA UKUU
WAKO ULIOKUWA NAO lakini kwa sababu mbalimbali ukaja kukuponyoka, KUJIHUISHA
TENA au KURUDISHA UWEZO ULIOKUWA NAO KWA MARA NYINGINE TENA. Nimeamua kuitumia
kaulimbiu ya ushindi aliyoitumia Rais mteule wa Taifa la Marekani Bwana Donald
Trump kuingia ikulu ya White House kwa mara nyingine tena kinyume kabisa na
matarajio ya wengi baada ya ule ushindi wa mara ya kwanza kumponyoka.
Vivyo hivyo kinyume kabisa na matarajio
ya wale wanaokufahamu na wanaodhania ya kwamba huu ndiyo mwisho wako na
hautakaa uje uinuke tena watashangazwa na jinsi utakavyoweza kurudisha ukuu
wako kwa mara nyingine tena. Kuwa tena mtu mwenye thamani mbele ya jamii, kuwa
tena mtu unayejitegemea, usiyeombaomba kama ‘Matonya’, kuwa tena mtu wa ibada unayetii maagizo ya Mwenyezi Mungu
na kurudi tena kuwa mtu mwenye malengo na msimamo usioyumbishwa ovyo na watu
wenye pesa au mamlaka.
Kama unafuatilia vizuri makala zetu
hapa utakumbuka nilianza kuizungumzia kampeni hii ya MAKE YOURSEL GREAT AGAIN mwezi
November kabla hata Trump hajaonyesha dalili za kushinda uchaguzi wa 2025, na
nikasema kwamba ashinde asishinde mimi siasa siyo kipaumbele changu bali sera
zake juu ya uchumi na biashara, hivyo hata ikiwa asingeshinda bado kaulimbiu
hii ingeendelea kama kawaida.
Pia kwa wanafunzi wangu hasa katika
MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE nimekuwa kimya kidogo tangu mwezi Desemba
na nilifanya hivi kwa madhumuni ya likizo lakini pia kuhakikisha kampeni yetu
inaanza rasmi sambamba na kuapishwa rasmi kwa Rais Mteule Donald Trump tarehe
20 January 2025 ambayo pia ni siku ya kumbukumbu ya Mwanaharakati mwingine wa Marekani Martin
Luther King Jr.
Kwahiyo kama wewe unayesoma hapa ni
mwanafunzi wa Michanganuo-online nichukue nafasi hii kukuomba radhi kwa ucheleweshaji
wa baadhi ya programu zetu hasa ile ya semina ya siku 7 ya Usagishaji unga wa
Sembe & Dona lakini kukujulisha kwamba sasa tunakwenda kuuwasha tena moto
upyaa! Na haijawahi kutokea toka group hili limeanzishwa.
Ikiwa uliwahi kuupoteza ukuu wako
utaurudisha upya na pia ikiwa wewe ni kijana unayetamani kuujenga ukuu wako kwa
mara ya kwanza utafanikiwa kuujenga kwani haimaanishi tunadili na waliopoteza
ukuu wao tu bali hata na wale wanaotamani kuujenga kwa mara ya kwanza kabisa.
Trump ameapa kuijenga upya tena
marekani (Make America Great Again),
akimaanisha Marekani kuzidisha uzalendo mara dufu. Uzalendo maana yake ni
kujali zaidi mambo yako na kuachana au kupunguza kuhangaikia ya watu wengine
kwa madhumuni ya kujijengea uwezo mkubwa zaidi. Kwa mfano badala ya kufadhili
vita kwenye nchi nyingine Marekani sasa itaelekeza nguvu na rasilimali zake
nyingi kwenye kuujenga zaidi uchumi wake ili izidi kuwa na nguvu kwenye kila
nyanja.
Na sisi kwa kutumia falsafa hii hii,
tunaweza pia kutumia muda na rasilimali zetu kizalendo zaidi kusudi tuweze
kujijengea uwezo mkubwa na wa haraka zaidi kiuchumi. Kwa mfano badala ya
kuendelea kupoteza muda wetu wa thamani kujaribu kumridhisha kila mtu, jamaa na
marafiki kwa masuala mengine ambayo hata hayana faida kwetu wala kwao ili tu
eti wasituone wabaya, muda huo tunaweza kuutumia kikamilifu kukamilisha
majukumu yetu mengine ya maana zaidi maishani ikiwemo kutafuta pesa.
Kampeni hii kama kampeni nyingine
tulizoendesha huko nyuma kwa mafanikio makubwa mfano ile tuliyoibatiza jina,
“KUELEKEAUTAJIRI” itaendeshwa kupitia Watsap, Telegram blog, vitabu na mitandao
ya kijamii yote ya Self Help Books Publishers kwa njia mbalimbali zikiwemo
makala, picha, video, na sauti.
Msomaji kwa kufuatilia kampeni hii
utapata manufaa makubwa katika maisha yako siyo tu katika suala zima la
biashara na ujasiriamali, bali hata na mtazamo wako kifikra katika maisha ya
kila siku. Utajirudishia maisha yako yaliyokuwa yamejaa heri, fanaka na
matumaini makubwa, maisha yaliyojaa mafanikio katika kila jambo unalolifanya.
Ili kwenda sambamba na kampeni hii
nitakuomba ufanye mambo kadhaa, nasema nitakuomba kwa sababu ni hiari yako siyo
lazima, unaweza tu kufuatilia kampeni bila kutimiza vitu hivyo na ikakusaidia
lakini itakusaidia zaidi na utaona matokeo bora na chanya zaidi endapo utaweza
kutimiza ombi ninalotaka kukuomba. Ombi lenyewe ni hili hapa chini,
1. Jitahidi sana upate hivi vitabu
mashuhuri vinne kutoka Self Help Books Publishers vya elimu ya pesa, biashara,
ujasiriamali na maendeleo binafsi) huwa napenda kuviita “The books
of all Times” /vitabu vya wakati wote visivyopitwa na wakati kwani
biashara itaendelea kuwepo muda wote binadamu atakaoishi duniani. Si lazima
usome vyote ingawa ukipata vyote itakuwa bora zaidi, vitabu hivyo ni hivi
vifuatavyo;-
(i) MICHANGANUO
YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
Kitabu cha kurasa 438 kwa lugha ya
kiswahili kilichobeba masomo yote ya ujasiriamali na biashara pamoja na
michanganuo halisi ya biashara na mawazo ya biashara zinazolipa zaidi ya 50.
(ii) THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION
(Fikiri & Utajirike)
Fikiri na Utajirike cha Napoleon Hill
ni Kitabu cha elimu ya fedha na mafanikio maarufu zaidi duniani na kimewahi
kusomwa na watu zadi ya milioni 200. Kimetengeneza na kinaendelea kutengeneza mabilionea
na mamilionea wengi zaidi duniani kuliko kitabu kingine chochote kile chini ya
jua. Sasa hivi unaweza kujipatia nakala yako kwa Kiswahili sanifu ukasoma
(iii) SIRIYA
MAFANIKIO YA BIASHARA YA REJAREJA
Kitabu kinachokupa muongozo kamili wa
namna ya kufanya biashara yeyote ile ya rejareja kwa ufanisi wa hali ya juu.
“Baadhi ya watu hudai eti, Duka halina faida, lakini usidanganyike, kwanini
watu wasiyafunge na kila siku unayaona mapya yakifunguliwa? Gundua siri
iliyojificha nyuma ya pazia kwa muda mrefu huku ukidanganywa biashara za
rejareja hazina faida wakati wengine wakinunua magari, kusomesha watoto shule
nzuri na hata kujenga majumba kwa biashara hizohizo.
(iv) MIFEREJI
7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA
Huwa nakiita kitabu cha maajabu kwani
kitabu hiki kimebadilisha mno maisha ya watu wengi. Ukitaka kufahamu kama kitu
ni kizuri basi utaona watu wakikazana kukiiga. Kitabu hiki nilichokitoa tangu
mwaka 2012 kimeigwa na watu mbalimbali wengine wakiita vya kwao, Mifereji 9 ya
pesa, Mifereji 10 ya kipatao nk. Lakini Kitabu Original ni ‘Mifereji 7 ya Pesa’
kilichoandikwa na Peter Augustino.
Kwa kifupi unaposoma kitabu hiki kama
ulikuwa umeajiriwa unaweza siku hiyo hiyo ukaenda kumwambia bosi wako “Naacha
kazi bosi nikaanzishe biashara yangu mwenyewe” Lakini nakusihi
utakapokisoma usije ukadhubutu kufanya hivyo kwani unahitaji muda wa
matayarisho kufanya jambo kama hilo na hata katika kitabu chenyewe mwishoni
nimekuwekea tahathari hiyo.
(v) KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO
(Toleo jipya 2024)
Umuhimu wa kitabu hiki utaujua baada ya
kukisoma.
2. Kitu kingine ninachokushauri kukifanya kusudi
uweze kwenda na sisi sambamba katika Kampeni hii kubwa ya kihistoria ya Make
yourself Great Again ni kujiunga na MASTERMIND GROUP LA
MICHANGANUO-ONLINE-2025.
Tiketi ya kujiunga na familia hii ya
kipekee kwa mwaka mzima ni kulipia kifurushi cha OFFA ya vitabu, michanganuo ya
biashara na vitu vingine mbalimbali kwa shilingi elfu 10 tu! Orodha ya vitu
hivyo imeongezwa mpaka kufikia vitu 20 kwa siku hizi 2 mpaka tarehe 20
itakapomalizika rasmi na ipo pale chini mwisho kabisa mwa makala hii.
Habari njema tu ni kwamba ikiwa
utalipia kifurushi hiki, moja kwa moja pia utakuwa umejipatia vitabu nilivyovitaja
pale juu kasoro vitabu viwili tu, cha Fikiri & Utajirike na kile cha
Mafanikio ya biashara ya Rejareja.
Punde tu ulipiapo OFFA yako hii unatumiwa papo hapo vitu vyote 20 kisha kuunganishwa
na MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE. Ukijiunga masomo na semina vinaanza
siku hiyohiyo. Ndani ya group kuna programu mbalimbali utakazoshiriki ambazo
ndizo kwa pamoja zitakazorudisha tena au kuujenga ukuu wako (Make
yourself great), kubwa zikiwa
ni hizi programu 5 zifuatazo;
1)
Semina ya siku 7 (Seven Days Business plan Master class) – Semina hii mwanachama huanza hima siku anajiunga ambapo tunajifunza
jinsi ya kuandika mchanganuo kamili na sanifu wa biashara yeyote ile kwa
kutumia mfano halisi wa biashara mojawapo. Kwa sasa hivi tuko na biashara ya
usagishaji wa unga wa Sembe na Dona.
2)
Masomo ya mtiririko wa fedha (Cash flow classes) – Haya ni masomo ya kila siku yanayohusiana na nzunguko wa fedha
binafsi na kwenye biashara zetu kwani biashara nyingi hufa si kwa sababu ya
kukosa wateja bali kukosa mzunguko wa kutosha wa fedha.
3)
Michanganuo bunifu mifupi mifupi ya biashara zenye fursa kubwa ya
kutengeneza faida haraka- Hapa tutakwenda kujifunza mbinu,
mikakati na ubunifu (Bootstrapping strategies) kwa ajili
ya kukuza biashara ndogondogo haraka kwa mitaji kidogo. Ni maalumu kwa wale
wafanyabiashara ndogondogo wasiokopesheka kirahisi na taasisi kubwa za kifedha,
wanaotamani kutoka pale walipo na kusogea hatua kubwa zaidi ndani ya muda mfupi
kadiri iwezekanavyo.
4)
Biashara Shamba Darasa: Hii ni programu maalumu itakayohusu
mafunzo kwa vitendo katika biashara ambazo tayari tumekwishafanya mazungumzo na
wamiliki wake. Washiriki watapata fursa ya kuzifuatilia biashara hizo kwa picha
na video huku na wao kama wakipenda wakiendesha biashara zakwao zinazofanana
nayo sambamba na hiyo kwa ajili ya kupata matokeo sawa au bora zaidi. Wamiliki
wa biashara hizo ni watu walionufaika na ushauri wetu kwa muda mrefu na
kuridhika na matokeo wanayoyapata.
5)
Uchambuzi wa Kitabu Think & Grow Rich kwa Kiswahili- Mfasiri wa kitabu hiki kwa Kiswahili ni sisi wenyewe Self Help Books
Tanzania, hivyo hapana shaka washiriki wa group hili watapata ladha halisi ya
uchambuzi wa kina kutoka nakala Orijino isiyogushiwa aliyochapisha Napoleon
Hill mwenyewe mnamo mwaka 1937
6)
Washiriki watakuwa na fursa ya kujitangaza wao na biashara zao au
shughuli wazifanyazo bila vikwazo visivyo na msingi- Mastermind group ni ushirika wa kusaidiana kila mmoja hivyo mtu akikosea
tunarekebishana kistaarabu. Kundi litaongozwa kwa mtindo uliotumiwa na
mwandishi NAPOLEON HILL kwenye madarasa na Semina zake
katika Mastermind Group na Mikutano yake na washauri wasioonekaka kwenye kitabu
cha Think & Grow Rich.
Wakufunzi huwa tunawahi darasani masaa
2 mpaka 3 kabla ya muda halisi kusudi kusuluhisha changamoto mbalimbali za
wanafunzi wakiwemo wale waliochelewa kujiunga na semina au ambao hawakuelewa
barabara somo lililopita.Tunakuwa tayari masaa yote hata nje ya darasa
kusikiliza na kujibu maswali ya wanafunzi wetu
Ikiwa utafuatilia na kuzingatia vyema
kampeni hii ya “KUJIRUDISHIA TENA UKUU WAKO” au “MAKE YOURSELF GREAT AGAIN” ya
mwaka 2025, Sina shaka yeyote kwamba mwaka huu utakwenda kuwa wa Mafanikio
makubwa na Baraka nyingi kwako. Anza mwaka kwa furaha na amani kama
atakavyofanya Raisi Mteule wa Taifa la Marekani Donald Trump na familia yake,
mkewe Melanie na wanawe, Donald Trump Jr. Ivanka, Eric na Barron.
..........................................
JINSI YA KUFANYA MALIPO (TZS 10,000/=)
Namba ya malipo ni; 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe sms au
watsap usemao “NATAKA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA YA SIKU 2 TU” Mara
moja nitakutumia zawadi zako zote 20 pamoja na kukuunganisha na
MASTERMIND-GROUP letu la mwaka 2025
AU
Unaweza kuingia mwenyewe kwenye duka letu hili la mtandaoni la, Selar.co/augustinopeter na kulipia moja kwa moja sh. elfu 10
pasipo kuwasiliana hata na sisi ukitumia mtandao wowote ule wa simu unaotumia
halafu utapewa kifurushi cha ZIP utakachodownload
zawadi. Unzip kifurushi hicho na kutoa zawadi zako zote 20.
Kisha nitakuunga mara moja kwenye MASTERMIND GROUP
NB: Unaweza kunikumbusha kwa meseji
nikuunganishe endapo nitachelewa kucheki mfumo wa selar.
*Kumbuka pia hii OFFA ya vitu 20 itadumu kwa siku 2 tu, tarehe 18 na 19
Januari 2025 kabla ya siku rasmi ya kuapishwa Donald Trump, na wanahitajika
watu 20 tu kukamilisha idadi ya group la 2025 kabla hatujauwasha moto rasmi wa
kampeni ya kujirudishia ukuu wetu tena, hivyo nakusihi chukua hatua mapema
ikiwa utahitaji kuwa mwanafamilia ‘onboard’
HUDUMA ZETU NYINGINE
Mbali na vitabu, michanganuo na kampeni yetu hiyo kubwa pia tunayo
huduma nyingine muhimu ya kuwaandikia wafanyabiashara na makampuni Michanganuo
ya Biashara zao. Mpaka sasa hivi tumekwisha waandikia mamia ya watu na
makampuni ‘Bplans’ zao. Baadhi yao
tumeweka kwa kifupi mihutasari ya michanganuo hiyo (Executive summaries) bila kutaja utambulisho wao hapa: >>OUR PORTFOLIO>>. Bado tunaendelea
kuorodhesha michanganuo zaidi ambayo hatukuwa tumeiweka hapo
Ikiwa unahitaji kuandikiwa mchanganuo
wa biashara yako yeyote ile kubwa au ndogo, kuombea mkopo au kuendeshea tu
biashara kwa ufanisi, basi tafadhali tunaomba hiyo kazi, tutakuandikia
mpango-biashara unaoendana na maono yako halisi kwa gharama rafiki sana
usiyoweza kuipata mahali pengine popote.
...........................................
Makala hii imeandaliwa na;
Peter Augustino Tarimo
Mtaalamu wa Michanganuo ya Biashara
Simu/sms: 0712202244
Watsap: 0765553030
ORODHA YA KIFURUSHI CHA OFFA ISIYOWAHI
KUTOKEA YA SIKU 2 TU! (Tarehe 18 & 19 Januari 2025)
*Ukifanikiwa kuiona Offa hii tafadhali usimwambie mtu mwingine yeyote
kwani akija kuikosa itakuwa lawama kwako bure.
Nikuibie tu siri kidogo..... Kuna
vitabu na michanganuo hapa huwezi kuvipata mahali kwingine kokote na ukivikosa
hapa kuvipata tena labda mwakani kipindi kama hiki.
VITU HIVYO 20 VYA OFFA NI
HIVI HAPA;-
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
2.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa –kwa kiswahili
3.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.- kwa kiswahili
4.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu! - kwa kiswahili
5.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani hutumika
vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
6.
KITABU: THE BOOK ON BUSINESS PLANNING- A step by step guide; cha mwandishi
nguli wa michanganuo Tim Berry.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama-Tumaini
Broilers .-kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Poultry Production 5000
Broilers (Delicious Poultry Production) .-kwa kiingereza
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. MCHANGANUO: Kiwanda kidogo cha mvinyo na juisi ya Rosella -kwa Kiswahili
14. MCHANGANUO: Kiwanda kidogo cha kukoboa mpunga (Kikundi cha kina mama) - kwa Kiswahili
15. MCHANGANUO: Kiwanda cha kufyatua tofali za saruji (Kiluvya bricks) - kwa kiswahili
16. MCHANGANUO: Event planning and Management (Margareta Events in Dar) –kwa kiingereza
17. MCHANGANUO: Biashara ya kuuza chipsi (Amani chipsi centre Buguruni) –kwa Kiswahili
18. MCHANGANUO MFUPI: Biashara ya Steshenari (Neema Stationery) –kwa Kiswahili
19. B/PLAN TEMPLATE (KIELEZO): –kwa kiingereza
20. B/PLAN TEMPLATE(KIELEZO): –kwa kiswahili
21. Kuunganishwa Mastermind
Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima(Mentorship group)
Namba ya malipo ni 0712202244 (Peter Auustino Tarimo). Lipia sh. elfu 10 kupata Offa
hii sasa hivi na kuunganishwa Mastermind Group la Michanganuo kwa mwaka mzima
wa 2025
0 Response to "JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA (MAKE YOURSELF GREAT AGAIN) "
Post a Comment