SOMO LA 10: MAKISIO YA FEDHA KWENYE MPANGO WA BIASHARA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SOMO LA 10: MAKISIO YA FEDHA KWENYE MPANGO WA BIASHARA

7.0 MAKISIO YA FEDHA
Mchanganuo wa biashara ni mchanganyiko wa maelezo na namba zinazowakilisha hesabu na taarifa mbalimbali. Tangu sehemu zilizopita huko nyuma tulikwishaanza kuona baadhi ya hesabu kwa mfano katika maelezo ya kampuni tuliona jedwali la vyanzo vya mahitaji kwa biashara mpya pamoja na jedwali la hesabu za kipindi cha nyuma kwa biashara ya zamani. Tuliona pia hesabu ya makisio ya mauzo, gharama za mauzo, gharama za uendeshaji na jedwali la mishahara kwenye kipengele cha uongozi na wafanyakazi.

Katika kipengele hiki cha makisio ya fedha ndipo unapotakiwa kuunganisha hesabu hizo nyingine ndogondogo zote na kutengeneza makisio ya taarifa tatu muhimu ambazo ni, Faida na Hasara, Fedha taslimu na Mizania ya biashara.

Kimsingi hesabu za mpango wa biashara ni tofauti na hesabu halisi za kawaida za biashara kwani ni makisio, zinafanana tu kimuundo. Kwa hiyo mtu hauhitaji kuwa mhasibu au mtaalamu wa biashara aliyebobea ndipo uweze kukisia taarifa hizo ingawa pia mtu atahitajika kuwa na uelewa wa msingi wa hesabu za biashara. Ikiwa unaandikampango wa biashara na sehemu hii inakutatiza unaweza ukamtafuta mtaalamu akakusaidia eneo hili.

Tofauti nyingine ni kwamba, hakuna mtu atakayeweza kukuwajibisha kisheria kwa kukisia mahesabu ya mpango wa biashara yanayotofautiana na hesabu halisi lakini katika uhasibu unaweza hata kufungwa jela kwa kuandika ripoti za hesabu zisizokuwa sahihi.

Makisio ya mpango wa biashara mara nyingi huwa tofauti na hesabu halisi wakati wa kutekeleza mpango na unatakiwa uwe unafanya mapitio kujua mpango wako wa biashara na hali halisi vimepishana kwa kiasi gani na hivyo ufanye kitu gani zaidi kurekebisha.

Vipengele vidogo katika sehemu hii ni hivi vifuatavyo,

7.1 Makisio muhimu
7.2 Mauzo yatakayorudisha gharama zote
7.3 Makisio ya Faida na Hasara
7.4 Makisio ya Fedha taslimu
7.5 Makisio ya Mali na madeni(Mizania ya biashara)
7.6 Uwiano waSehemu muhimu za biashara

………………………………………………………………
Ndugu msomaji, somo la kumi katika mfululizo wa masomo 11 linapatikana likiwa zima katika blogu ya Masomo ya Semina ya Michanganuo ya biashara ambayo kiingilio chake ni shilingi elfu 10 tu na unapewa kitabu cha michanganuo ya biashara na ujasiriamali bure. Lipia kupitia namba za simu 0712202244  au  0765 553030 kisha tuma kwa meseji anuani yako ya e-mail(GMAIL) kwa ajili ya kukuunganisha na blogu hiyo.

Unajifunza masomo 11 ya jinsi ya kuandika Mchanganuo kamili wa biashara na ili kujua kama umeelewa vizuri unaandika mpango mmoja wa biashara ambapo utakuwa ukipewa usaidizi wowote ule utakaouhitaji kutoka kwa mkufunzi wa semina. Hakuna ukomo wa semina ukishalipia, ni mpaka pale utakapoelewa.


·         Zifahamu HUDUMA ZETU nyingine tunazozitoa.

·         Soma RATIBA YA M,ASOMO yote yaliyopo kwenye semina hii.

·       Ikiwa unafanya biashara ya rejareja usikose kusoma kitabu hiki cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA.



 somo la 11 vielelezo muhimu




0 Response to "SOMO LA 10: MAKISIO YA FEDHA KWENYE MPANGO WA BIASHARA"

Post a Comment