BADO UNASUBIRI KIBALI KUTIMIZA NDOTO ZAKO? TUMIA NJIA HIZI 7 UFANIKISHE MWENYEWE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BADO UNASUBIRI KIBALI KUTIMIZA NDOTO ZAKO? TUMIA NJIA HIZI 7 UFANIKISHE MWENYEWE

KUTIMIZA NDOTO ZAKO
Nakukaribisha kusoma makala hii inayohusiana na utimizaji wa malengo, mengi utayakuta ndani yake karibu sana! Usisahau pia kuwahi nafasi yako kwenye ile semina yetu iliyoahirishwa mwezi uliopita ya JINSI YA KUANDAA HESABU KATIKA MPANGO WA BIASHARA. Sasa itafanyika 20/3/2019  

1.Usisubiri ruksa wala kibali
Acha kuwa kama wanariadha au wacheza soka kusubiri kipenga(filimbi)  ilie ndipo uanze kucheza mechi. Watu wengi linapokuja suala la kutimiza ndoto zao hawana tofauti na mwanamichezo anayesubiri filimbi au kengele ilie ndipo aanze jambo.

Ulimwengu wa namna hiyo wanaishi watoto. Hebu kumbuka ulipokuwa mtoto unasoma tangu chekechea mpaka chuo kikuu au ngazi nyingine yeyote ile. Katika kipindi hicho ulizoea kuishi kwa kufuata ratiba matukio karibu yote, mfano ulizoea shule kufunguliwa January na kufungwa June, somo la hesabu kuanza saa 4 na kumalizika saa 5 kisha unaenda mapumziko au kupata kikombe cha uji nk.

SOMA: Mbinu 2 za ushindi za kufanikiwa jambo lolote, hazifundishwi shuleni, vyuoni wala katika masarasa ya ujasiriamali.

Mtindo huo jinsi akili ya binadamu ilivyoumbwa, hushika vitu kulingana na ratiba na hujizoesha yenyewe kutegemea ratiba. Kwahiyo mtu anapokuja kuwa mtu mzima na kuingia mtaani katika maisha ya kawaida hushtuka baada ya kukuta dunia tofauti kabisa na ile aliyoizoea shuleni, hukuta hamna ratiba tena, kipenga wala kengele kila anapotaka kuanza jambo.

Katika maisha hupaswi kusubiri wingu lipungue, mvua wala wimbi litulie ndipo eti uanze safari, wewe anza hivyohivyo, ikiwa utasema usubiri basi utasubiri hapo milele.

SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena(make yourself great again)

2.Usisubiri zamu yako.
Kuna dhana moja watu husema hivi; “Ili ufanikiwe inakubidi uwe na roho mbaya” Unajua ni kwanini wenye roho mbaya hufanikiwa haraka?  Ukweli ni kwamba hawafanikiwi kwa sababu wana roho mbaya hapana, bali kinachowafanya watu wabaya wafanikiwe ni kule kutokufuata utaratibu wa kawaida kama wa kukaa foleni na kusubiri jambo, wapo radhi hata kuhonga au kutumia nguvu na kumpita mtu aliye hoi mstarini akisubiri ilimradi tu yeye awahi kupata huduma, hamwogopi mtu na hivyo kufanikiwa haraka. Tabia hii pia wanayo watu wazuri wanaofanikiwa lakini wao hawatumii njia haramu kutimiza ndoto zao.


3. Jitoe ndani ya ukanda wako wa faraja  
Sawa sawa na kama tulivyoona kwenye mbinu ile ya kwanza, baadhi  ya wasomi, sio wote lakini, hata wanaotoka vyuo vikuu hujikuta wanashindwa kuendana na mazingira ya nje ya mfumo wa vyuo na kutafsiri maarifa waliyoyapata kwa vitendo kwasababu wamezoea maisha ya kufanya kila kitu kwa maelekezo kutoka kwa maprofesa, wakufunzi, serikali na mfumo mzima wa chuo kwani kila upande unataka mwanafuzi huyo afanikiwe.

Lakini katika maisha halisi kwenye uwanja wa mapambano goli halitulii sehemu moja tena ili iwe rahisi kwako kufunga bao, linazunguka kusini, kaskazini, mashariki na magharibi. Uwanja muda wote umejaa ukungu na tope, siyo shwari tena kama ilivyokuwa chuoni, tena hamna refarii wala mshika kibendera, na hata ukivunjika mguu hamna yeyote anayejali na mpira utaendelea kama kawa.

SOMA; Je upo kwenye fani au kazi uliyotamani kuwa tangu ulipokuwa mtoto mdogo?

4. Kuwa makini na wale wanaokuzunguka.
Pingu nyingine inayoweza kukuzuia usisonge mbele kabisa kutimiza ndoto zako ni aina ya watu wanaokuzunguka wewe mwenyewe.

Nakushauri kafanye jaribio lifuatalo;
Buni kitu chako na kitu hicho chaweza kuwa ni biashara, kazi ya sanaa kama vile wimbo, igizo, hadithi, shairi au chochote kile na kisha wafuate marafiki zako unaopenda kupiga nao stori waonyeshe hiyo kazi kisha waombe wakupe maoni yao kukukosoa.

Ikiwa marafiki hao mrejesho wao wa awali kabisa utaonyesha ukosoaji unaolenga kukusahihisha ili kazi yako iweze kuwa bora zaidi, basi ujue unao marafiki wazuri. Lakini ukiwaona wanabeza na kukukatisha tamaa kwa kusema wao wangeweza kubuni kitu kizuri kushinda hicho cha kwako, basi ujue kabisa marafiki zako hao hawakufai na tambua hilo siyo tatizo lako bali lakwao hivyo fikiria mara mbilimbili kupoteza muda wako mwingi ukiwa nao. Unahitaji marafiki watakaokuokoa na wala siyo kukuzamisha zaidi majini uangamie. Chagua kuwa nao au kukaa nao mbali lakini ndoto zako zitimie.

5. Muda mzuri wa kuanza ni sasa.
Pengine unatamani sana kufanya kazi fulani lakini kazi hiyo inahitaji kwanza mtu upate shahada(digirii). Ina maana kwamba utahitaji miaka 3-4 ili uweze kuwa na sifa za kupata kazi hiyo. Ikiwa una umri wa miaka 20 sasa ina maana utamaliza shahada yako ukiwa na miaka 25 au 26. Sasa unaweza kuona kama ni muda mrefu lakini hebu fikiria kama utaamua kuja kuanza ukiwa na miaka 30 au 40 utamaliza ukiwa na umri gani na kazi  hiyo utaifanya lini? Itakuchukua muda mwingi sana ukijutia kutokuanza mapema. Kadiri utakavyoanza mapema ndivyo pia utakavyo timiza ndoto zako mapema.

SOMA: Njia 10 za kuhamasika na kuendelea kubakia na hamasa hiyo kwa muda mrefu ujao.

6.Ondoa woga
Woga mkubwa watu wanaokuwa nao wanapotaka kutimiza ndoto zao ni woga wa kushindwa. Hebu  jaribu kuwafikiria wanamichezo tena. Wachezaji hufanya makosa mengi sana wakati wa mazoezi wanapokuwa wakijiandaa na michuano. Lakini pia hata siku yenyewe ya mashindano(fainali) bado hufanya makosa na hata kushindwa au kufungwa magoli. Lakini hiyo haiwezi kuwafanya wasicheze tena michezo kwani kushindwa ni sehemu ya kujifunza ili wafanye vizuri zaidi hapo baadae.

7. Kuwa na Mshauri/mtu wako wa mfano
Umewahi kuwaona wapanda milima? Kwanini wanakuwa na waongozaji(Guids)? Mshauri si lazima awe ni yule uliyemtafuta mwenyewe hapana, wengine hujitokeza wenyewe tu kulingana na jinsi mwenyewe unavyoonyesha juhudi zako kwa watu na jamii. Mshauri anaweza kuibuka miongoni mwa watazamaji, wale wanaoshuhudia kile ufanyacho sawa na ilivyo kwa wachezaji chipukizi wazuri wa mpira wanaochaguliwa na kocha katika mechi za majaribio mchangani. Wachezaji wakati mwingine wala hawajui kama miongoni mwa watazamaji wapo makocha wanaofuatilia, hivyo usifichefiche tena kile unachokifanya.

Hitimisho
Sasa umepta mwangaza kuwa hakuna chohchote kile kinachoweza kukuzuia usitimize ndoto zako, amua ni nini unachohitaji kukamilisha ndoto zako kisha unaweza kuweka katika vitendo mbinu nilizokueleza hapo juu. Anza hata kama ni kidogo usiogope kama utashindwa wala usisubiri ruksa na kibali kutoka kwa mtu yeyote.

…………………………………………………..

TAARIFA HII NI KWA YULE TU AMBAYE BADO HAJAJIUNGA NA SEMINA ZETU.

·       Napenda kukujulisha kwamba ile semina yetu kubwa na iliyokuwa muhimu zaidi kuliko semina zote tulizowahi kufanya ya JINSI YA KUANDAA MAHESABU KATIKA MCHANGANUO WA BIASHARA itafanyika kuanzia siku ya tarehe 20/3/2019 kupitia group la wasap na kwenye email.

·       Mshiriki wa semina hii ni mtu yeyote aliyekwishajiunga na group letu la masomo ya pesa ya kila siku la whatsapp liitwalo Michanganuo-online au yeyote yule anayelipa kiingilio ambacho ni sh. Elfu 10.

·       Lengo kubwa la semina hii ni kuwaandaa washiriki kwa ajili ya uandaaji wa michanganuo ya uanzishaji wa viwanda ambalo ndio lengo letu la mwaka huu. Tumepanga kuandaa michanganuo 4 ya viwanda vidogo na vya kati vinavyolipa na ambavyo vitampa mtu uzoefu mkubwa wa kuandaa mpango wa kiwanda cha aina yeyote ile kikubwa au kidogo.

·       Kwakuwa mwaka jana tulibaini changamoto kubwa ya watu katika michanganuo ipo katika hesabu na namba ndio maana tukaona eneo hilo tulifanyie semina maalumu.

·       Ili kukamilisha idadi ya watu darasa linatakiwa kuwa na watu 250 tu ambao bado kidogo sana idadi hiyo itimie. Kwahiyo ikiwa unahitaji hizi semina nakusihi usichelewe wahi nafasi yako. Sina hakika kama tarehe 20 itafika kabla idadi hiyo haijatimia.

·       Inawezekana hupendi kujiunga na magroup ya wasap, hilo lisikusumbue kwani natuma semina nzima kwa email pia.

·       Ada ya sh. Elfu 10 ni ya mwaka mzima, utapata semina zote zijazo na masomo katika group. Usisahau pia kwamba nitakutumia masomo na semina zilizopita, vitabu  na michanganuo mbalimbali na baadhi  yake ni hivi hapa chini;


1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

Ukihitaji kujiunga na Semina hii, tuma kiingilio chako sh. Elfu 10 kupitia namba 0765553030  au  0712202244 jina hutokea Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe wa, “NIUNGANISHE NA SEMINA”

Ikiwa hutapenda kuingia kwenye group la whatsapp, nijulishe lakini pia nitumie na anuani yako ya email kwa ajili ya kukutumia masomo ya semina na vitu vilivyotajwa pale juu.

ASANTE SANA
Peter Augustino Tarimo
0765553030
0712202244


0 Response to "BADO UNASUBIRI KIBALI KUTIMIZA NDOTO ZAKO? TUMIA NJIA HIZI 7 UFANIKISHE MWENYEWE"

Post a Comment