JE, UPO KWENYE KAZI AU FANI ULIYOTAMANI KUWA TANGU ULIPOKUWA MTOTO MDOGO? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE, UPO KWENYE KAZI AU FANI ULIYOTAMANI KUWA TANGU ULIPOKUWA MTOTO MDOGO?

dada mjasiriamali akifanya kazi anayoipenda

Unapomuuliza mtoto au mwanafunzi katika shule yeyote ile kuwa angependa kuja kuwa nani hapo baadae atakapomaliza masomo yake, atakujibu haraka sana na moja kati ya majibu anayoweza kukupa ni haya yafuatayo;

·       Nataka kuja kuwa mwanasheria.
·       Nitakuja kuwa dokta.
·       Nataka nije kuwa Rais kama Dokta John Pombe Magufuli
·       Mwandishi wa habari, mtangazaji.
·       Nataka kuwa mwalimu
·       Nataka niwe Rubani wa ndege
·       Nataka niwe mwanamuziki kama Diamond
·       Nitakuwa mtaalamu wa kompyuta
·       Nataka nije niwe injinia
·       Nitakuwa Polisi, Mwanajeshi nk.

Sababu kubwa za kuchagua kuwa katika fani au kazi tofauti ni Mapenzi(Passion) waliyokuwa nayo watoto katika kazi ama fani husika. Shauku waliyokuwa nayo katika kutimiza kitu fulani kwenye fani hizo, wanataka waje kufanya kitu tofauti sana lakini pia kuna lengo jingine la mwisho ambalo ni kujipatia kipato kitakachowawezesha kuishi. Ingawa kujiingizia kipato ni moja ya malengo yao katika kuchagua fani, lakini siyo sababu  kuu hasa inayopewa kipaumbele cha kwanza katika kuchagua fani wakati huo. Hatima ya kila kitu ni kuja kupata kipato cha kuendeleza maisha lakini kuna malengo mengine muhimu pia.

SOMA: Njia za kuingiza kipato cha ziada nje ya kazi yako.

Mtoto au mwanafuzni husukumwa zaidi na ubora wa kukamilisha ndoto yake hiyo na jinsi atakavyoweza kuwa kinara kwenye hiyo fani miongoni mwa wenzake au watu wengine, kipato siyo kipaumbele peke yake. Lakini pamoja na nia hiyo njema, katika maisha ya kawaida tunachokuja kukishuhudia baadae ni kinyume kabisa na jinsi tulivyotamani tuje kuwa.

Mtoto yuleyule anapokuja kuingia katika maisha ya kazi husahau kabisa matamanio (mapenzi) yake ya utotoni na kujikuta akichukua muelekeo tofauti kabisa ambao wala hakuutegemea. Anasahau malengo mengine yote na kuanza kusaka kipato cha muda mfupi badala ya ya ubora kwenye fani aliyotamani kuwa tokea utotoni. Hamasa ya kile anachokifanya inakuwa haipo tena anabakia kufanya kazi ni kazi tu ilimradi imuingizie kipato. Kipato sasa kinageuka kuwa ndiyo lengo lake la msingi kuliko kitu kingine chochote kile.

SOMA: Kwanini ni rahisi zidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?

Ni kitu gani hufanyika mpaka hali hii kutokea ukubwani? Ikiwa utaamua kuwauliza wengi wa watu hawa wataishia kukupa majibu mbalimbali na mengi yakiwa katika mtindo wa lawama kwa vitu na watu mbalimbali. Wengine watatoa lawama kwa Waajiri wao wakidai kuwa waajiri hao huwapunja mishahara, wanawabana mno kiasi kwamba wanashindwa kutumia ubunifu waliokuwa nao nk. Wengine utawasikia wakiwalaumu wateja wao na kusema, hawataki kununua bidhaa zao au wananunua kwa bei ya chini. Wengine watatoa lawama zao kwa mfumo wa elimu na serikali kwa ujumla wakisema elimu waliyoipata haiwezi kuwafanya watimize ndoto zao, ni duni na haikuwaandaa vizuri kukabiliana na soko la ajira lililopo au kazi walizochagua kuzifanya.

Lakini ukweli halisi ni kwamba, watu tumekuwa tukipenda kupitia njia za mkato mno katika maisha. Watu tunapenda kuwa na mambo mazuri pasipo kutoa jasho na ili kujiridhisha nafsi zetu tunaamua kufanya kazi yeyote ile itakayotuwezesha kulifikia lengo la mwisho ambalo ni kujipatia kipato(riziki) wakati kipato kinatakiwa kuwa ni matokeo ya kazi ile uliyoichagua kufanya kwa mapenzi.

SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi.

Ukimuuliza mtu ni kwanini anafanya kazi fulani atakujibu anaifanya ili kupata kipato cha kuendeshea maisha yake, hautamsikia tena akisema ni mapenzi aliyonayo kwenye kazi hiyo ndiyo yanayomchochea kuifanya kama alivyokuwa akifikiria wakati akiwa bado mtoto. Mtu wakati anapokuwa mtoto angali bado shuleni husukumwa zaidi na mapenzi ya dhati kwenye fani, anapokuja kuingia katika hali halisi baada ya masomo husukumwa na mahitaji ya muda mfupi ambayo ni pesa au kujikimu kimaisha.

Na anapokuwa akipata mahitaji hayo ya muda mfupi hubadilisha kabisa muelekeo wake aliokuwa nao mwanzoni, hafanyi tena kazi kwa mapenzi kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo tokea utotoni za kuwa mahiri katika fani aliyochagua.

Kwahiyo ili mtu uweze kuwa kama vile ulivyotaka uwe wakati ulipokuwa mtoto ni lazima uhakikishe kwanza unaishikilia ndoto yako kikamilifu na kudumu nayo, kumbuka hakuna kitu chochote kinachoweza kupatikana kirahisi na ni lazima ukutane na vikwazo vingi njiani, kikubwa tu ni kwamba “usifuate njia ya mkato”

SOMA: Unawezaje kuyakabili magunu, maanguko na mikasa ya kutisha maishani kama hii?

Wakati ukifanya kazi kwa bidii na maarifa kutimiza ndoto yako ya kuwa kili ulichotaka kuwa tangia utotoni, moja kwa moja pia na malengo yako kifedha yatakuwa yakitimia pasipo hata wewe mwenyewe kujua na wakati mwingine unaweza kuingiza pesa nyingi kuliko kama vile ungeliamua kutumia njia za mkato.

.................................................

Ndugu msomaji wa makala hii, nakukaribisha kwenye group letu la Watsap la masomo kila siku pamoja na semina kila mara. Masomo yanahusiana na mzunguko wa fedha katika biashara zetu na mifukoni mwetu wenyewe kwa ujumla. Semina zinahusiana na jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara na kwa kila semina huwa tunaandika mchanganuo 1 wa biashara yenye fursa kubwa hatua  kwa hatua. 

Kujiunga kuna kiingilio cha sh. elfu 10 na unapata masomo yote yaliyopita, semina, vitabu na michanganuo mbalimbali ikiwemo ya kuku aina zote na kilimo cha matikiti maji. Unapewa bure kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali ambacho kina masomo ya kila aina ya ujasiriamali na namna ya kuandaa michanganuo ya biashara. Vitu unavyotumiwa punde tu baada ya malipo ni hivi vifuatavyo na kisha kila siku unaendelea kupokea masomo kupitia wasap au email yako;

SIMU:       0712202244
Whatsap: 0765553030


Unaweza pia ukajipatia vitabu mbalimbali vya ujasiriamali kutoka kwetu katika lugha ya kiswahili kwa kutembelea ukurasa wetu wa vitabu wa; Smart Books Tanzania 

Kwenye group leo tarehe 19 August siku ya Jumapili  tutakuwa na somo la fedha lisemalo; 

"CHANGAMOTO KUBWA 3 NA MBINU ZA KUBAJETI FEDHA KIDOGO KWENYE BIASHARA MPYA INAYOANZA"


   

0 Response to "JE, UPO KWENYE KAZI AU FANI ULIYOTAMANI KUWA TANGU ULIPOKUWA MTOTO MDOGO?"

Post a Comment