DUKA UNALOTEMBEA NALO: BIASHARA NZURI UKIANZISHA INAKUPA UHURU KAMILI KIFEDHA


DUKA LINALOTEMBEA BARABARANI
SEHEMU YA I

Kumiliki biashara ndiyo njia pekee ya haraka inayoweza kumfanya mtu kuufikia uhuru kamili wa kifedha. Lakini siyo biashara zote au kila aina ya biashara iliyokuwa na uwezo wa namna hiyo. Biashara nyingine zinamwezesha mtu kuufikia uhuru kifedha taratibu mno wakati kuna nyingine zinamwezesha mtu kutoka haraka zaidi.

Zipo biashara nyingi mtu anaweza kuanzisha kama vile, biashara ya duka, biashara ya nguo, biashara ya mazao kama vile mchele, mahindi, mpunga, mtama, karanga, ngano nk. Katika somo hili la leo nitakwenda kuzungumzia biashara moja ya mtaji mdogo sana ambayo wengi walioamua kuifanya wameweza kuona matokeo yake haraka sana na wametajirika au kuwa huru kifedha. Biashara hiyo haina tofauti na Duka mtu unalotembea nalo kwani hauhitaji fremu kubwa Kariakoo wala sijui wapi ndipo uweze kufanya biashara yako.

SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala

Biashara nitakayoizungumzia inafanyika katika mtandao wa Intaneti lakini ni tofauti  na zile biashara nyingi za kwenye mtandao watu wengi tulizozizoea. Wachache wanaoijua hata hapa Tanzania wanatengeneza wengine hadi millioni 7 na zaidi kwa mwezi huku wenyewe wakiwa wametumia kiasi kidogo sana cha mtaji.

Kabla hatujaendelea mbele zaidi hebu tuone kwanza Uhuru wa kifedha maana yake ni  kitu gani. Mtu anakuwa huru kifedha pale kipato chake cha ziada (Passive income) kinapozidi matumizi yake.  Mfano kama kipato cha mtu cha ziada ni sh. millioni moja kwa mwezi na matumizi yake ni shilingi laki 6 kwa mwezi basi mtu huyo yupo huru kifedha. Hapo sijahusisha kipato chake cha kila siku cha kawaida kama mshahara au biashara, nimezungumzia tu kipato cha ziada.

SOMA: Je, unajua unaweza kumiliki kiwanja au nyumba bila kutoa senti 5 mfukoni? Soma kitabu cha dola miioni tano ujue yote

Sasa utaona hapo kwamba mtu huyu anao uwezo wa kuacha kazi yake ya kila siku au biashara na akaamua kuishi kwa kutumia kipato chake cha ziada tu, na akamudu bila matatizo yeyote wala haja ya kufanya kazi kama vile mwanzoni kabala ya kupata huo uhuru wa kifedha.

Kuwa huru kifedha unahitaji kumiliki rasilimali(Assets) zitakazokuingizia pesa kila mwezi hata kama hufanyi kazi, na njia pekee ya kuzipata hizo asseti ni kwa kupitia kuwekeza kidogokidogo katika miradi mfano katika ardhi na majengo, kwenye hisa za makampuni au pia unaweza kuwa na biashara ya kawaida tu lakini iliyo na mfumo unaoiwezesha kujiendesha yenyewe, mfano mmojawapo ni zile biashara za kwenye mtandao wa intaneti nk.

Katika miradi niliyotaja hapo juu yote, biashara inayojiendesha kimfumo ndiyo rahisi zaidi kuliko nyingine kwa mtu wa kawaida. Uwekezaji kwa mfano kwenye ardhi na majumba unahitaji pesa nyingi sana mtu wa kawaida kuweza kumudu. Sasa basi ni biashara ipi nzuri zaidi unayoweza kuijengea mfumo hatimaye ikakupa uhuru kamili wa kifedha?

SOMA: Kipato cha ziada ambacho watu wengi hawakijui

Wazo la biashara ya namna hiyo linatakiwa liwe ni lile wazo mtu unaweza ukatumia nyenzo mbalimbali (Leverage) kulitekeleza. Kutumia nyenzo(leveraging) maana yake ni kutumia rasilimali za watu wengine  kupata faida haraka. Kwa mfano unaweza ukatumia muda, pesa, maarifa, bidhaa, au mfumo nk. vya watu wengine katika kujiingizia faida. Nikupe mfano mmoja, mtaalamu wa kutengeneza  tovuti anaweza akasaidia watu kutengeneza website zao na wakamlipa pesa.

Mtaalamu huyo akiamua mwenyewe kumtengenezea mtu mmojammoja tovuti maana yake ni kwamba biashara yake haina mfumo endelevu kwani siku tu akiugua au kupata dharura yeyote ile na kipato nacho hakuna. Lakini endapo ataamua kutengeneza mafunzo(courses) ya jinsi mtu anavyoweza kujitengenezea tovuti mwenyewe, akaelezea hatua kwa hatua kwa kutumia video nk. ataweza kuziuza kozi hizo hata kama ikiwa atakuwa na safari ya mbali au amelala. Lakini huduma ni ileile ya utengenezaji wa tovuti ila mfumo tu ndio uliobadilika.

SOMA: Biashara ndogondogo Tanzania zenye faida ya haraka ni hizi hapa zipo 4

Ili kufanya biashaa mtandaoni na kupata pesa utahitaji vitu muhimu vifuatabvyo;

1.  Uwezekano wa kufikia mtandao wa Inaneti kupitia kompyuta au simu yako ya mkononi(smartphone)

2.  Jukwaa au platform, na hii inaweza ikawa ni tovuti, au jukwaa lingine lolote lile mfano kurasa katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, Instagram na mingineyo. Jukwaa hilo ndilo litakalokuwezesha wewe kuwasiliana na wateja wako mtandaoni.

3.  Kuaminika na kujenga mtandao imara. Bila kitu hiki biashara mtandaoni haiwezi ikaleta matokeo mazuri kwani wateja ni watu wa kawaida kama wale wale unaofanya nao biashara zingine nje ya mtandao.

SOMA: Njia mpya za kufanya mambo: Dunia, biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu

Karibu kila biashara siku hizi hata na zile zinazofanyikia kwenye eneo maalumu kama ofisini au katika fremu zinahitaji kuwa na uwepo wake katika mtandao wa Intaneti, ni trend haiwezi kukwepeka tena kirahisi sasa hivi na faida kubwa za biashara yako kuwa mtandaoni ni hizi zifuatazo;

1.  Kuwafikia wateja wengi na wa mbali zaidi(Kitaifa na Kimataifa)

2.  Hupunguza gharama za uendeshaji wa biashara

3.  Kuingiza kipato(pesa) muda wowote ule hata ukiwa umelala.

Lakini vipi kama ikiwa huna uzoefu na mtandao wa intaneti? Si ishu tena siku hizi kwani mambo yamefanywa kuwa rahisi mno tofauti na ilivyokuwa miaka miwili mitatu iliyopita huko nyuma. Siku hizi tovuti/blog mtu yeyote yule anaweza akaanzisha ilimradi tu awe ana uelewa wa kuifungua na kuweka vitu ndani yake(contents). Na mitandao ya kijamii ndio usiseme kabisaa kwani hata mtoto wa miaka 7 anaweza akafungua ukurasa wake.

SEHEMU YA II
Katika sehemu yetu ya pili tutakwenda kuiona biashara ambayo watu wengi bado hawajaishitukia. Ungana na mimi leo saa 3 usiku katika group jingine la Michanganuo-online-Premium ujue kila kitu kuhusiana na biashara hiyo.

SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado

Kujiunga na group la Premium, lipia vitabu na masomo yaliyoorodheshwa hapo chini, nitakutumia muda huohuo kisha kukuunganisha na group hilo mara moja. Ni sh. Elfu 10 tu itakayokupa pia uanachama wa kudumu.

Pia utaweza kushiriki katika semina yetu ya tarehe 15 August 2019 ambapo tutakwenda kuandika hatua kwa hatua mchanganuo wa kiwanda cha ufyatuaji wa tofali za block. Mwisho Mchanganuo huo utakuwa na kila kitu, vipengele yote, mahesabu na katika lugha ya kiswahili na kiingereza. 

Watu wa mwanzo 10, Nitawapa pia vitabu vya DUKA LA REJAREJA na kile cha MIFEREJI 7 ya fedha pamoja na SEMINA ILIYOPITA YA HESABU ZA MICHANGANUO(Advanced Business Plan Financials) tunayoiuza sh. elfu 20 utaipata free of charge!

ASANTE SANA

Peter A. Tarimo
    

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

0 Response to "DUKA UNALOTEMBEA NALO: BIASHARA NZURI UKIANZISHA INAKUPA UHURU KAMILI KIFEDHA"

Post a Comment