SEMINA YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KIWANDA CHA TOFALI ZA SEMENTI - BADO SIKU 4 TU

Mpenzi msomaji wa blogu hii ya Jifunzeujasiriamali, napenda kukujulisha kwamba zile semina zetu 4 za kuchanganua biashara bunifu za viwanda sasa zinakaribia kuanza rasmi na siku ya Alhamisi tarehe 15 ndio tutaanza na kiwanda kidogo cha kufyatua tofali za block kilichopo Kiluvya mkoa wa Pwani.Semina hii itaanza saa 5 asubuhi kwa maelezo kuhusu utafiti wa biashara hiyo, kisha baadae ndipo tutaandika hatua kwa hatua mchanganuo huo mzima tukianza na Maelezo ya mradi mpaka Sura ya mwisho ya vielelezo. Kisha mwishoni kabisa tutaandika Muhtasari wa mchanganuo wetu.

Siku ya pili tutachambua kwa undani hesabu za mchanganuo huo ili kila mshiriki aweze kuelewa vyema jinsi ya kukokotoa makisio ya taarifa zote muhimu za fedha hasa makisio ya faida na hasara, mtiririko wa fedha, Mizania ya biashara, Mauzo ya kurudisha gharama(Break even Analysis na Muda mradi utakaporudisha mtaji uliotumika(Pay back Period)

Ikiwa unapenda kushiriki Semina hii unakaribishwa na utaratibu uliopo ni kwamba, Unalipa kiingilio shilingi Elfu 10 kupitia namba zifuatazo, 0712202244  au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo. Muda wa mwisho ni siku ya Jumatano tarehe 14 usiku. Ada hii utaweza kushiriki Michanganuo mingine yote 3 iliyobakia hadi mwezi Novemba.

Tuna offa kubwa kwa wale watakaoshiriki ya kupewa vitabu na masomo yetu mbalimbali ya siku zilizopita. Offa ya vitu vilivyoorodheshwa hapo chini ni ya muda mfupi sana hivyo watakaowahi tu ndio watanufaika nayo.

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

14.              SEMINA ya Mahesabu ya mpango wa biashara(ADVANCED BUSINESS PLAN FINANCIALS)0 Response to "SEMINA YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KIWANDA CHA TOFALI ZA SEMENTI - BADO SIKU 4 TU"

Post a Comment