NUFUVI(SWOT ANALYSIS), TATHMINI MUHIMU KABLA HUJAANZA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NUFUVI(SWOT ANALYSIS), TATHMINI MUHIMU KABLA HUJAANZA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO

Tathmini  hii haifanywi tu na wale wanaofanya biashara hapana, bali hata na mtu mwingine yeyote yule anayetaka kufanya maamuzi yanayoweza kumletea matokeo chanya au hasi baadae.

NUFUVI au kwa kiingereza SWOT analysis ni ufupisho wa maneno NGUVU, UDHAIFU, FURSA na VIKWAZO(Strength, Weaknesses, Oportunity and Threats).

Umuhimu wa kufanya NUFUVI ni nini?

1.  Husaidia katika kazi ya kutengeneza mikakati yako utakayoitumia ili kufikia malengo unayokusudia.

2.  Husaidia kujua ni vipaumbele gani utakavyoweka katika biashara/mradi wako.

3.  Humsukuma mtu kuwa na mtazamo na mwelekeo mpya juu ya biashara anayoifanya kwa kutumia vizuri nguvu na fursa zilizopo huku akikwepa udhaifu na vikwazo.

4.  Husaidia katika kazi ya kuandika mpango wako wa biashara kwani unafahamu kabla mema na mabaya yote yanayoizunguka biashara husika.

Kufanya tathmini hii maana yake ni kwamba unatafakari mazingira yote hasi na chanya yanayoizunguka biashara yako kwa nje na kwa ndani. Hivyo katika NUFUVI kuna mazingira ya aina mbili, yale ya ndani ambayo ni Nguvu na Udhaifu halafu yale ya nje ambayo ni Fursa na Vikwazo. Unaweza pia kuyaweka katika makundi mawili kama hivi, Mazingira wezeshi(Nguvu na Fursa) halafu Mazingira Pingamizi(Udhaifu na Vikwazo)

MAZINGIRA YA NDANI(Nguvu & Udhaifu)

NGUVU:
Nguvu ni vile vitu vyote kwenye biashara au kampuni yako vilivyokuwa na mchango chanya(mzuri) na ambavyo vipo ndani ya uwezo wako. Vitu hivyo mfano ni;

·       Rasilimali unazozimiliki
·       Ujuzi/elimu uliyokuwa nayo
·       Jina zuri, heshima au sifa njema ya biashara yako
·       Timu nzuri ya wafanyakazi
·       Wateja ulio nao
·       Eneo zuri la biashara
·       Teknolojia ya kisasa
·       Mtaji wa kutosha
·       Hakimiliki ya kitu
·       Na nguvu shindani nyingine yeyote ile unayoweza kuwa nayo dhidi ya washindani/wapinzani wako.

UDHAIFU:
Udhaifu ni igezo au vitu vyote vile vinavyokinzana na nguvu ulizokuwa nazo katika biashara yako na ambavyo pia vipo ndani ya uwezo wako. Nikisema ndani ya uwezo wako namaanisha unaweza kuvirekebisha ikiwa utaamua. Vitu hivyo vinaweza vikawa ni vile vyote nilivyovitaja katika NGUVU hapo juu lakini katika mtazamo HASI, nikimaanisha kwamba ikiwa vitu hivyo utakuwa hauna basi itakuwa ni UDHAIFU kwako badala ya NGUVU. Navyo ni kama hivi hapa chini;

·       Kutokuwa na rasilimali za kutosha kama mtaji
·       Mapungufu kwenye timu yako ya wafanyakazi au uongozi
·       Vifaa na teknolojia duni
·       Kutokuwa na jina sokoni
·       Bei isiyowaridhisha wateja
·       Kifungashio kibaya nk.

MAZINGIRA YA NJE:(Fursa & Vikwazo)

FURSA:
Ni vitu au mazingira kutoka nje ya biashara vyenye athari chanya au vinavyochangia mafanikio ya biashara yako. Mifano ni hivi vifuatavyo;
·       Kukua kwa soko lako
·       Mwelekeo fulani wa soko unaohamasisha watu kununua kile unachouza, kwa mfano ikiwa unatengeneza mifuko mbadala halafu kunakuwa na katazo la mifuko ya plastiki nk. hiyo ni fursa
·       Tukio lolote lile linalotazamiwa ambalo biashara yako inaweza ikalitumia katika kujitanua zaidi.
·       Mabadiliko yeyote yale ya kisheria au ya kiserikali yanayoweza yakaleta matokeo chanya katika biashara yako.
·       Mtazamo chanya wa wateja juu ya biashara yako.

VIKWAZO:
Hivi ni vile vitu au vigezo hasi kutoka nje ya biashara ambavyo huna uwezo wa kuvizuia visitokee lakini unaweza tu kuweka mipango ya dharura kwa ajili ya kupunguza makali yake yasiweze kuiua biashara yako endapo vitatokea. Navyo ni kama hivi vifuatavyo;

·       Washindani watarajiwa wanaoweza kuibuka muda wowote ule
·       Uwezekano wa wale wanaokusambazia bidhaa au kukuuzia jumla kupandisha bei
·       Mabadiliko ya teknolojia unayotumia
·       Janga lolote lile la asili au moto
·       Wateja kubadili mwenendo wao wa ununuaji  kama vile kupunguza kunuua kutokana na sababu mbalimbali
·       Na mwelekeo mwingine wowote ule wa soko unaoweza kuhatarisha biashara yako.

MFANO WA JEDWALI LA NUFUVI(SWOT)
Tathmini hii siyo ngumu hata kidogo na hufanyika kwa kuchora tu jedwali linaloonyesha sehemu kuu nne 4(vyumba 4) na katika kila chumba basi unaorodhesha vigezo husika. Katika mfano nitakaoutoa hapa ni wa biashara ya tofali za saruji tunayokwenda kuandika mchanganuo wake hatua kwa hatua kwenye semina yetu siku ya Alhamisi  August 15.


Tathmini ya NUFUVI(SWOT Analysis)

Ukishamaliza tathmini yako hii, sasa unaweza ukaibadilisha kuwa mikakati ya kufanikisha biashara yako kama tutakavyokwenda kuona kwenye mchanganuo wetu hatua kwa hatua siku ya Alhamisi. Kwanza kabisa unatakiwa kutumia mazingira wezeshi ya ndani na nje(Nguvu na Fursa) kukabiliana na Mazingira yote pingamizi ya ndani na nje(Udhaifu na Vikwazo).


....................................................

Mpenzi msomaji wangu ikiwa unapenda kujifunza zaidi jinsi ya kuandaa mpango wa biashara yako, basi karibu sana siku ya Alhamisi Tarehe 15 August katika kundi la watsap la MICHANGANUO-ONLINE GROUP. Mbali na semina hiyo pia nitakupatia offa kubwa ya vitabu, michanganuo na masomo mbalimbali yanayohusiana na Michanganuo ya biashara.

Offa hii si ya kukosa hata kidogo kwani ukisema uje uvinunue baadae gharama yake ni karibu mara 9 zaidi.

Kujiunga na semina hiyo lipia kiingilio chako sh. Elfu 10 na nitakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia kila kitu nilichoahidi halafu utasubiri semina siku ya Alhamisi na nyinginezo zitakazofuata bila kuchajiwa pesa ya ziada. Siku ya mwisho kulipia ni tarehe 14 usiku.



0 Response to "NUFUVI(SWOT ANALYSIS), TATHMINI MUHIMU KABLA HUJAANZA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO"

Post a Comment