KUANZISHA BIASHARA BILA MTAJI, HIVI INAWEZEKANA AU NI KUTIANA MOYO TU? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUANZISHA BIASHARA BILA MTAJI, HIVI INAWEZEKANA AU NI KUTIANA MOYO TU?

Biashara zisizokuwa na mtaji

Inawezekana, hauhitaji mtaji wowote ule wa pesa ili kuanzisha biashara. Aidha biashara zinatofautiana kwani zipo biashara rahisi zaidi kuanza bila mtaji kabisa mfano hizi hapa 7, na nyingine zitahitaji mtaji angalao kidogo katika hatua fulani. 

Kama mwandishi na mshauri wa biashara na ujasiriamali, nimewahi kuulizwa swali hili mara nyingi sana na waulizaji wengi waliuliza kama ifutavyo;

·      Ni kwa Jinsi gani naweza kuanza biashara bila mtaji wa pesa?

·      Kuanza biashara bila mtaji au kwa mtaji mdogo sana inawezekana?

·      Biashara za bila mtaji ni zipi?

·      Naweza kuanzisha biashara yangu pasipokuwa na pesa kabisa?

Katika maswali yote hayo na mengine yanayofanana nayo huwa nawajibu; Inawezekana, huhitaji mtaji wowote ule wa pesa ili kuanza biashara ijapokuwa unaweza kuhitaji aina nyinginezo za mitaji mfano muda, nguvu na maarifa.

Kitu kimoja cha kustaajabisha kwenye kuanzisha biashara ni kwamba kufeli ama kuanguka kwa biashara fulani hakuna uhusiano wowote ule na kiasi cha mtaji wa kuanzia.

SOMA: Biashara 5 za mtaji kidogo kuanzia elfu 2, kumi mpaka laki moja unazoweza kuanza zikakutoa.

Takwimu zimethibitisha mahali pengi kuwa asilimia 90% ya biashara zote zinazoanza (Startups) ziwe zilianzishwa kwa mtaji wa kutosha ama bila ya mtaji wa pesa kabisa, zote huishia kufeli muda mfupi tu baada ya kuanzishwa kwake jambo linalosababisha maisha ya biashara kuonekana ya kuchanganya na watu wengi kuamua kukomaa na ajira zao maisha yao yote.

Lakini faida za biashara ni nyingi ikiwa mtu ataamua kujifunza biashara vizuri hasa mbinu mbalimbali za kuanzisha biashara isiishie njiani.

Njia za kuanzisha Biashara bila ya kuwa na Pesa kabisa (Biashara bila Mtaji)   

Kutokana na maswali ya badhi ya wasomaji wangu pale juu nimeona ni vyema nikaweka muongozo kidogo wa namna mtu anavyoweza akaanzisha biashara yake angali hana hata senti tano mfukoni.

SOMA: Kupata mtaji wa biashara cha msingi ni wazo na muda wako, pesa baadae.

Hatua karibia zote nitakazozielezea hapa hazihitaji mtaji wa pesa isipokuwa labda aina nyinginezo za mitaji kama vile muda, nguvukazi na maarifa.  

1. Kitu cha kwanza kabisa ni lazima uwe na wazo la Biashara.

Kutafuta wazo la bishara inayokufaa hauhitaji mpaka uwe na fedha, ni suala tu la kutumia ubongo wako. Kuna njia mbalimbali za kuweza kupata wazo la biashara itakayokulipa zikiwemo;

·      Kuchunguza ni mahitaji gani katika jamii uliyopo watu wanayakosa

·      Ujuzi, uzoefu au fani uliyonayo na jinsi unavyoweza kuvitumia katika kujiingizia pesa.

·      Mapungufu katika biashara za watu wengine unayoweza kuyarekebisha.

·      Kubuni bidhaa/huduma mpya kabisa sokoni

·      Kupeleka au kuleta bidhaa/huduma katika soko/eneo ambalo hapo kabla zilikuwa hazijafika nk.

2. Kufanya utafiti wa soko

Kama nilivyoeleza kwenye kitabu changu cha MICHANGANUO YA BIASHARA & UJASIRIAMALI, utafiti wa biashara ama feasibility Study unaweza ukaufanya mwenyewe binafsi hata pasipo kuyahusisha makampuni ya ushauri ama wataalamu wa biashara. Kwenye kitabu niliweka hadi majedwali ya dodoso na sampuli mtu wa kawaida kabisa anaweza akayakopi na kuanza utafiti wa biashara yake mara moja bila gharama zozote.

SOMA: Utafiti wa soko la biashara yako/Upembuzi yakinifu -1

Kifupi tu ni kwamba kwenye utafiti wa biashara na sekta uliyochagua kufanya unatakiwa uhakikishe unalifahamu barabara soko lako, washindani wako na njia unazoweza kutumia ili kuwapiku.

Fahamu wateja wako wanajishughulisha na nini, kiwango chao cha elimu, umri, tabia zao na mahali wanapopatikana, Ongea nao uso kwa uso ili kujua kile wanachokikosa kutoka kwa washindani waliopo sasa.

Mpaka hapo inawezekana kufanya yote niliyoorodhesha pasipo kutumia hata shilingi moja.

3. Kulijaribu wazo lako la biashara sokoni.

Katika hatua hii pia huhitaji bado kuweka pesa yeyote labda kiasi kidogo sana kwa ajili tu ya bando la kwenye simu yako au kompyuta. Unafanya majaribio bidhaa au huduma zako pasipo kutumia gharama kubwa kuona ikiwa kama wateja wanazihitaji kweli ama la.

SOMA: Jinsi ya kuuza wazo la biashara au ubunifu kwa wawekezaji na watu wengine

Utatumia mbinu gani isiyokuwa na gharama? Siku hizi njia bora kabisa isiyohitaji mtaji pesa mkubwa ni kupitia mitandao ya kijamii kwa kupost wazo lako, picha au hata makala zinazohusiana nalo kisha kuona mirejesho ya wateja wako ikoje. Hapa unaweza kuanza kupata oda, pongezi, likes na maoni mbalimbali yanayoashiria kwamba watu wanavutiwa au wana uhitaji na kile unachotaka kuwauzia.

Kumbuka lakini mpaka hapo hujaingiza pesa yeyoye ya maana kwenye biashara yako zaidi ya bando tu la simu.

4. Tengeneza mpango wa biashara na kisha uanze na kile ulichokuwa nacho kwanza.

Hapa sishauri utengeneze mpango rasmi wa biashara kama ile ya kuombea mikopo benki hapana bali mpango kichwani mwako au ukitaka unaandika mpango wa biashara uitwao “Ukurasa mmoja wa mchanganuo”, aina hii fupi ya mchanganuo wa biashara mifano yake halisi inapatikana katika kitabu changu kingine kiitwacho JINSI YA KUANDIKA MPANGO MFUPI WA  BIASHARA (UKURASA MMOJA) na haichukui zaidi ya dakika 15 mpaka 30 kuuandika.

SOMA: Pata kitabu cha bure (Free E-book) jinsi ya kuandika mchanganuo mchanganuo mfupi wa biashara yako

Ni moja kati ya njia zenye nguvu mno za kuandika mpango wa biashara kwa mtu anayeanza sifuri pasipokuwa na mtaji wa fedha kwani unaweza kuuboresha kuwa mpango sanifu wenye kila kitu baadaye.

5. Tengeneza bidhaa/huduma yako ya kwanza kabisa.

Hapa sasa nisikudanganye maanake Motivational Writers na Motivational Speakers ndipo tunapoonekana manabii wa uwongo au matapeli kwa kuwaaminisha watu kuwa biashara inaweza ikafanyika pasipo kuwa na mtaji kabisa mwanzo mwisho.

Kiukweli kama ulivyosoma kipengele cha 1 – 4 yapo mambo unayoweza kuyafanya bila kutumia hata shilingi lakini kuna mahali fulani utafika hamna ujanja lazima uweke tu angalau kiasi kidogo cha fedha biashara iweze kusonga mbele vinginevyo itabakia kuwa wazo tu.

Naomba nieleweke vizuri hapa, nilisema kuanzisha biashara bila mtaji wowote wa pesa inawezekana lakini ili biashara hiyo iendelee na kukua katika mazingira ya karne ya sasa ni lazima uweke pesa na si vinginevyo. Hata biashara ya udalali inayosifiwa zaidi kutohitaji mtaji wa pesa lakini kuna wakati utapiga simu, kuhitaji kula muda unapozunguka, nauli nk. Hii yote maana yake ni pesa huwezi kukataa.

SOMA: Mtaji wangu ni mdogo sana lakini nahitaji kufanya biashara na sina ajira naomba ushauri wako

Tukirudi kwenye mada yetu kwa kuwa sasa tayari umeshapata uhalali wa wazo lako, soko umejua lipo la uhakika, umeshawafahamu washindani wako vizuri, unaweza hata kuazima fedha kidogo kwa  mtu wako wa karibu utakazogharamia bidhaa au huduma yako ya mwanzo kabisa. Si unajua utauza?

6. Tengeneza utaratibu rahisi wa malipo

Amua wateja wako wakulipe kupitia njia ipi, kwa fedha taslimu mkononi au kupitia mitandao ya simu? Kumbuka wateja mara zote wanapendelea njia nyepesi na rafiki ya kufanya malipo pindi wafanyapo manunuzi. Itategemea aina ya biashara yako.

7. Tumia njia za bure kujitangaza

Kwa kuwa huna pesa jitahidi sana kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako. Sahau kwa muda matangazo ya kulipia (sponser ads) hadi pale mapato yako yatakapokuwa makubwa. Tumia tovuti au blogu kupatikana ‘gugo’ na search engine nyinginezo kwa urahisi.

SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara unayoipenda

8. Tafuta njia nyinginezo za kupata mtaji

Ukishafika hatua hii ukitaka kukua zaidi na zaidi ni lazima utafute mtaji wa kutosha na njia maarufu zaidi ni mikopo ya benki au taasisi nyinginezo za kifedha. Unaweza kuomba mikopo ya ndugu au jamaa lakini hakikisha mmepeana kimaandishi/kimkataba kusudi undugu wenu usijekufa kisa pesa

..............................................................

 

OFFA MPYA YA VITU 12 KUELEKEA NUSU YA PILI YA MWAKA 2023

 

Ni offa ya kukata na shoka !

 

Ukilipia Tsh. 10,000/= Unapata vitu hivi vyote 12 papo hapo;

·      Course kamili ya uandishi wa michanganuo ya biashara

·      Vitabu, E-books vitano (5), michanganuo kamili sita (6) ya biashara, Tempates/vielezo vya michanganuo viwili (2), kwa kiingereza na Kiswahili.  Vitu vyote ni kwa kupitia njia ya email au watsap

·      Kujiunga na group letu la masomo ya kila siku ya fedha mwaka mzima ukipenda.

·      Ni kwa shilingi elfu 10 tu !

OFFA hii ni ya muda mfupi sana na itaondolewa au kupunguzwa vitu! Aidha magroup yakijaa itasitishwa pia.

 

VITU HIVYO 12 VYA OFFA NI HIVI VIFUATAVYO;-

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)

 

Lipia offa yako kupitia namba zangu, 0712202244  au 0765553030 jina, Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe watsap au sms usemao;

“NATAKA OFFA MPYA YA VITU 12

Ukihitaji kuunganishwa na group, kwenye ujumbe ongeza maneno; “NATAKA OFFA MPYA YA VITU 12 & GROUP

 

Na utapata OFFA zako ndani ya dk. 3 tu

Thamani halisi ya offa hii ni Tsh. 90,000/= lakini lipa Tsh. elfu 10 tu uokoe sh. 80,000/= !

Ukitaka kuthibitisha uaminifu wetu bonyeza hapo chini kuona baadhi ya wadau wengine waliowahi kuchangamkia offa na vitabu vyetu siku za nyuma bofya hapa>>>TESTIMONIAL

..................................................


Kwa zaidi ya miaka 4 sasa tumewasaidia wajasiriamali na makampuni mbalimbali kuandika michanganuo ya biashara zao kwa madhumuni mbalimbali hasa ya kuombea mikopo toka mabenki & taasisi za kifedha, ruzuku na hata mipango mikakati kwa ajili ya kuendeshea biashara zao kwa ufanisi.

Badhi ya biashara na makampuni hayo tumeweka sehemu ndogo ya mihutasari ya michanganuo yao hapa bila ya kufichua utambulisho wao, bofyahapa>>>BAADHI YA KAZI ZETU

Ikiwa na wewe ungependa tukuandikie Mpango kamili wa biashara yako unaolingana na maono, dhima na malengo ya biashara au kampuni yako, tunakukaribisha kwa mikono miwili. Tunaandika Michangauo ya Biashara yeyote, iwe kubwa au ndogo, na katika lugha za Kiingereza au Kiswahili kulingana na matakwa ya mteja.

Michanganuo yetu tofauti na kwingineko huwa tunatumia taarifa(Data) unazotupatia wewe mwenyewe mteja lakini pia na sisi huwa tunafanya tafiti katika yale maeneo tunayoona hukuyatafiti vya kutosha. Kamwe hatukopi na kupesti taarifa kwa lengo la kutengeneza michanganuo inayoakisi maono halisi ya mteja.

Mawasiliano yetu ni;

Simu/Whatsap: 0765553030 au 0712202244

Peter Augustino Tarimo


(Get a comprehensive, customized Business Plan that fits your unique vision, goals and challenges)



 

0 Response to "KUANZISHA BIASHARA BILA MTAJI, HIVI INAWEZEKANA AU NI KUTIANA MOYO TU?"

Post a Comment