Ni
stadi gani muhimu kuliko nyingine zote maishani inayochangia mtu kung’ara kwa
urahisi kwenye biashara / kazi anayoifanya? (Get a chance to shine easily in
business or a job) Nikimaanisha kwamba stadi inayomwezesha mtu aweze kufanikiwa
kwa urahisi zaidi kwenye biashara au kazi yake.
Asilimia
kubwa ya watu wanaohitimu vyuoni na mashuleni huja kushituka wawapo kazini au
kwenye biashara pale wanapobaini vitu vingi walivyokuwa wakijifunza darasani
kumbe havifanyi kazi kwenye ulimwengu halisi kama walivyokuwa wakifikiri.
Tafiti mbalimbali zimedhihirisha pasi na shaka kwamba, ni stadi za mahusianao na za kijamii zinazoongoza katika kusababisha mafanikio yatokee kwenye biashara au kazi na miongoni mwa stadi hizo niliwahi kuziandika kwenye makala yangu nyingine moja iitwayo, JINSI YAKUTENGENEZA MVUTO WA AJABU WA KUPENDWA HARAKA NA KILA MTU, WAPENZI, WATEJA,NDUGU NA HATA JAMAA. Katika makala hiyo nilizitaja stadi tano (5)
Lakini
leo tena nimevutiwa na stadi nyingine ya maisha ya mtu kuwa ni mtu wa Kuaminika
ama Kutegemewa na watu wengine. Kuwa mtu wa kutumainiwa na watu ni moja kati ya
sifa/stadi muhimu mno na ambayo watu wengi huichukulia poa au kutokuipa umuhimu
unaostahili .
Ni
stadi ya kuaminika inayokosekana mpaka mwanamke au mwanaume anafunga safari
kwenda kwa mganga wa kienyeji kusaka dawa ya kupendwa na mpenzi wake. Ni kutokuaminika
kunakosababisha mfanyabiashara kwenda kutafuta dawa ya kupendwa na wateja. Ni
ukosefu wa sifa ya kutegemewa kunakosababisha mwajiriwa kwenda kwa ‘wataalamu’
kutengeneza dawa ya kupendwa kazini.
Hakuna
dawa ya mvuto wa mapenzi duniani (kupendwa) zaidi ya wewe mwenyewe kujenga upendo na kuaminika kwa wengine. Kwenya
uchumba kisa cha watu kukaa hata miaka 5 wakichunguzana ni ili kila mmoja ajue
tabia za mwenzake na hasa kama ni mwaminifu, ana upendo wa dhati au la.
Hali
ni hivyohivyo ilivyo kwenye biashara, wateja hawawezi kamwe kununua bidhaa ama
huduma zako ikiwa kama bado hawajakuamini, hawakupendi na wala hawajakuzoea.
SASA NI JINSI GANI UTANG’ARA KWA
URAHISI KWENYE BIASHARA AU KAZI
YAKO ILI UPATE MAFANIKIO HARAKA?
Ili
ung’are kwenye biashara au kazini kwako inakubidi utengeneze stadi hii ya kuwa
mtu wa kuaminika na kutegemewa. Unaweza ukasema, mbona kila mtu analiweza hili?
Ni kweli siyo jambo gumu kwa kulitazama harakaharaka lakini linahitaji mtu kuwa
na nidhamu ya hali ya juu sana katika kutekeleza kila unachoahidi kukifanya kwa
watu wengine.
SOMA: The sky is very wide, every star can shine (Mbingu ni kubwa mno, kila nyota inaweza kung'ara)
Kwa
mfano tuchukulie wewe ni fundi cherehani umemuahidi mteja siku ya ijumaa aje kuchukua
nguo yake. Ijumaa ikifika kweli akija aikute nguo yake ikiwa tayari na siyo
kuanza longolongo.
Unapojenga
tabia ya kuwa mtu wa kuaminika na kutegemewa ndipo utakapoanza kupata wateja
zaidi na zaidi, utapata fursa ya kung’ara (kushine) kuwazidi wengine wote
wanaokuzunguka iwe ni kazini, kwenye biashara, shuleni au katika jamii nyingine
yeyote unayoishi. Kwa njia hii unaweza kupata miradi ya kila aina
itakayokuingizia maelfu ya pesa kama siyo mamilioni ya shilingi kwani kila mtu
anakuamini na anatamani kufanya na wewe biashara au kazi.
SOMA: Uaminifu ni mtaji mkubwa katika biashara kushinda fedha
Hakikisha
unatimiza kile unachoahidi kila mara bila ya kutoa sababu zozote zile na stadi
nyinginezo zitafuata taratibu. Sidhani kama kipo chuo ama shule inayofundisha
somo la kuwa mtu wa kuaminika na kutegemewa lakini jambo la msingi ni mtu
kutambua ni kwa jinsi gani KUAMINIKA na watu ilivyokuwa muhimu na hivyo kulenga
katika kujenga nidhamu ya kuikuza stadi hii itakayokuwezesha kung’ara na
kufanikiwa popote pale ulipo iwe ni kazini, kwenye biashara, shuleni, chuoni
ama mahali pengine popote kwenye jamii.
………………………………….
Mpenzi
msomaji wa makala hii, unaweza pia kujipatia huduma zetu nyingine za malipo
zifuatazo;
1. Course kamili ya jinsi ya
kuandaa mchanganuo wa biashara yeyote pamoja na
OFFA ya vitabu, michanganuo, Templates & kuungwa group la masomo ya fedha
na michanganuo kwa mwaka mzima. Course hii ni Tsh. 10,000/= badala ya bei
halisi ya sh. Elfu 90
2. Vitabu vyetu mbalimbali
na Michanganuo kamili ya Biashara iliyokwisha andikwa
tayari. Unaweza kuvicheki kwenye duka letu hapa, SMARTBOOKSTZ
3. Huduma ya kuandikiwa
mchanganuo wa Biashara yako. Gharama hutegemea ukubwa wa
mtaji wa biashara husika. Tumekwisha waandalia Makampuni na biashara za watu
mmoja mmoja, unaweza kuona baadhi yao hapa>BAADHI YA KAZI ZETU
0 Response to "JINSI YA KUNG’ARA KWA URAHISI KWENYE BIASHARA / KAZI (GET A CHANCE TO SHINE EASILY)"
Post a Comment