Makala hii imetokana na mazungumzo yangu na ndugu Aois
Francis juu ya suala la uaminifu kwenye biashara, Alois alinieleza jinsi ambavyo watu huweza
kufanya biashara na wakaingiza pesa pasipokuwa na senti tano au wakati mwingine
wakiwa na mtaji mdogo sana.
Akitolea mfano kwa Wahindi alisema, wanautumia vizuri
sana mtaji huu na huwa unawapa mafanikio makubwa wao wenyewe na hata wale wadau
wengine wanaofanya nao biashara kama
vile wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali wanapofika katika jiji la Dar es
salaam, wengi hwa na mitaji midogo sana. Baada ya kununua bidhaa kutoka dukani
kwa Mhindi mara nyingi na Mhindi akagundua mtaji wake haukidhi mahitaji, basi
atadiriki kumpa mzigo “malikauli” ilimradi tu mauzo yake yanaongezeka. Lakini
hafanyi hivyo kiholela, ni baada ya ‘kumsoma’ kwa kipindi kirefu na
kujiridhisha kweli kuwa ni mfanyabiashara mwenye malengo ya ukweli.
Alois anasema siyo Wahindi tu wanaoweza kunufaika na mbinu
hii, bali hata na mtu mwingine yeyote anaweza kuitumia .Unapokuwa mwaminifu
katika biashara na mdau yeyote yuke iwe ni wateja , wanaokusambazia bidhaa au taasisi
za kifedha, unajijengea hazina ya kuja
kupata usaidizi wa namna yeyote ile katika biashara yako iwe ni kukopeshwa,
kupata wateja zaidi baada ya wale uliowaonyesha uaminifu kwenda kuwatonya na
wenzao au wa namna nyingine yeyote ule. Kwa mtindo huo unakuwa umejijengea
mtandao mzuri wa biashara yako.
Anasema, yeye binafsi uaminifu katika kazi na biashara
umemsaidia kwa kiasi kikubwa sana katika maisha yake ya kila siku, ukizingatia
kwamba yeye ana kazi yake ya msingi lakini wakati huo huo hutumia “Mifereji" mingine
tofauti tofauti katika kujiongezea kipato cha maisha yake ili aweze kufikia
malengo yake makuu aliyojiwekea katika maisha.
Bwana Alois Francis ukiacha ajira yake, yeye ni
Mwezeshaji na Mhamasishaji katika vikundi vya ujasiriamali na jamii kwa ujumla,
anayo taaluma ya masoko na uuzaji “Great Salesman” na anao uzoefu wa siku
nyingi. Yeye pia ni Msambazaji mkuu wa vitabu, DVDs na bidhaa zote za kampuni
ya “SELF HELP BOOKS PUBLISHERS LTD” mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani, isipokuwa
Dar es salaam peke yake.
Ana ‘dili’ pia na nchi za kanda ya Afrika Mashariki na ya
Kati. Ukihitaji vitabu kwa bei ya jumla
au reja reja huko mikoani, mpigie simu: 0713
462590 au 0753 262590 Ama waweza kuwasiliana na makao makuu Dar es
salaam tukakuunganisha naye. Anapatikana zaidi Mkoa wa Iringa, Makambako lakini
pia hutembea mikoa mbalimbali Tanzania katika mtandao wake wa kimasoko.
0 Response to "UAMINIFU NI MTAJI MKUBWA KATIKA BIASHARA KUSHINDA FEDHA."
Post a Comment