MISINGI MIKUU (4) YA UANZILISHI WA BIASHARA YENYE FAIDA TANZANIA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MISINGI MIKUU (4) YA UANZILISHI WA BIASHARA YENYE FAIDA TANZANIA

SPORTS BETTING

Wakati wa kuanzisha biashara yenye faida ni wakati ambao akili inakuwa na mambo mengi yenye matamanio juu ya biashara ipi itakuwa bora kuliko nyingine. Suala hili limekua likiumiza vichwa waanzilishi wengi wa biashara kutokana na hatari wanayoenda kuipitia wakati wa kuanzisha biashara mpya haswa katika upande wa kufa kwa mitaji yao.

Yafuatayo ni mambo ama misingi mikuu minne (4) ambayo inaweza kufanya biashara yako ikawa rahisi kama utayazingatia kabla na baada ya kuanzisha biashara inayolipa Tanzania na hata ikiwa ni sehemu nyingine yeyote ile duniani.

1. Wazo la biashara

Huu ndio msingi wa kwanza wakati wa kuanzisha biashara na hii ni kwasababu mwanzilishi wa biashara hujiweka katika nafasi ya kuchagua ni biashara gani itakuwa rahisi kwake kutokana na uzoefu alio nao pamoja na chaguo ambalo analipendelea yeye kama wazo la biashara yenye uwezekano wa kuleta faida.

Kwa mfano mtu ambaye ni mpenzi wa mpira wa miguu au soka na akachagua kuanzisha kampuni ya Sports betting huwa rahisi kwake kufanya biashara hiyo ya michezo ya kubahatisha kutokana na ujuzi na mapenzi yake katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.

2. Mtaji wa biashara

Mara nyingi katika upande wa mtaji jambo la muhimu hutajwa kuwa ni pesa, lakini pia mtaji unaweza kuwa kitu chochote ambacho kinaweza kuanzisha biashara hiyo. Zipo biashara za mitaji midogo na zile za mitaji mikubwa kwa hiyo kwa yule anayeanzisha biashara ya mtaji mdogo tuseme labda biashara ya mtaji wa laki tano (500,000/=) hana kazi kubwa ya kufanya kama yule anayeanzisha biashara ya mtaji mkubwa tuseme labda biashara ya mtaji wa milioni hamsini (50,000,000/=) na kuendelea.

Kwa upande wa upatikanaji wa mtaji unaweza kuwa wa muda mrefu au muda mfupi kwa mfano uwekaji wa akiba kwa ajili ya kuanzisha biashara hutajwa kama ni mpango wa muda mrefu au uamuzi wa kukopa katika vikundi vya SACCOSS au benki pia hizi ni njia za upatikanaji wa mtaji wa biashara inayokusudiwa kutengeneza faida.

3. Ufahamu wa soko

Kila mfanyabiashara huwa na aina ya soko ambalo mara nyingi ndilo humpa umaarufu kutokana na upekee wa soko hilo. Kwa mfano katika biashara ya chakula mfanyabiashara akiamua ya kuwa soko lake liwe la watumiaji wa vyakula vya asili ya kitanzania, hivyo watumiaji wote wataelekea sehemu hiyo kutokana na utambulisho wa upekee wa vyakula vyenye asili ya kitanzania jambo litakaloifanya ionekane ni biashara yenye faida haraka.

4 (a) Mipango pamoja na mikakati katika biashara

Wakati wa uanzilishi wa biashara ni bora zaidi mfanyabiashara akawa na mikakati kabla ya kuanzisha biashara. Mipango hiyo inaanzia tangu pale alipopata wazo na kujiwekea malengo katika biashara hiyo. Mara nyingi suala hili hugusa jinsi ya kukuza soko ili kukuza zaidi matumizi ya biashara.

   (b) Kuwa mdadisi, mbunifu na kukubali kujifunza

Kila biashara huwa na changamoto zake hivyo ingekuwa vizuri zaidi kufahamu changamoto mapema na kufahamu utatuzi wa changamoto hizo. Kujifunza pia hujumuisha kufahamu aina ya washindani ulio nao katika biashara na jinsi ya kuwa mbunifu zaidi katika kuweka biashara yako eneo lenye upekee kwa ajili ya soko lako ulilolilenga.Ubunifu na udadisi ni vitu vitakavyoifanya biashara yako kuwa moja ya biashara zenye faida zaidi Tanzania na nje ya nchi pia.

..........................................


Makala hii ni kwa hisani ya SPORTS BETTING


Unaweza pia kusoma na hizi hapa chini;

1. Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

2. Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala

3. Ijue falsafa ya kitabu iliyotengeneza matajiri na mabilionea wengi zaidi Duniani

0 Response to "MISINGI MIKUU (4) YA UANZILISHI WA BIASHARA YENYE FAIDA TANZANIA"

Post a Comment