IJUE FALSAFA YA KITABU ILIYOTENGENEZA MATAJIRI & MABILIONEA WENGI ZAIDI DUNIANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

IJUE FALSAFA YA KITABU ILIYOTENGENEZA MATAJIRI & MABILIONEA WENGI ZAIDI DUNIANI

Mabilionea, mamilionea, matajiri na watu mashuhuri Duniani

Habari mpenzi msomaji wa blogu yako hii ya jifunze ujasiriamali, sina shaka umewahi kusikia juu ya kitabu hiki cha Think & Grow Rich, lakini pengine hujawahi kuchunguza kwa undani ni kwanini watu wengi hivyo Duniani huwa wanakihusudu, pengine ni shauri ya lugha ya kizungu iliyotumika, lakini uzuri sasa hivi ni kwamba hata nakala ya kitabu hicho kwa Kiswahili ipo. 

Katika makala hii ya leo na nyingine nitakazoendelea kukuletea utapata kujua kwa undani kile kinachofanya kitabu hiki kipendwe mno na watu kote Duniani. Mwishoni kabisa mwa makala hii pia kuna habari njema kwa wale wote wanaopenda kujifunza zaidi.

KARIBU....

 

Falsafa za kitabu mashuhuri cha fedha na mafanikio cha THINK & GROW RICH (Fikiri & Utajirike) zimetumiwa na matajiri na watu wengi waliofanikiwa kimaisha pasipo hata wao wenyewe kujua kama wamezitumia.

Mwishoni mwa makala hii pia nitaelezea jinsi baadhi ya watu mashuhuri na matajiri Duniani walivyoweza kuitumia falsafa mojawapo kwenye hiki kitabu na kufanikiwa kupata utajiri mkubwa, nitaanza na hapa hapa nyumbani Tanzania kwa kumzungumzia Diamond Platnumz, Harmonize kisha wengine wa nje kama kina Elon Musk tajiri namba moja duniani, Michael Jackson, Muhamad Ali, Pele, Maradona, Neymar, Messi na Ronaldo,

Jambo la kustaajabisha ni pale tu utakapojaribu kuwafuatilia mabilionea na mamilionea au yeyote aliyepata mafanikio makubwa katika maisha yake na kubaini kumbe walitumia falsafa na kanuni zilezile walizotumia wengine wote waliofanikiwa kama yeye, awe ni mtoto tajiri zaidi Duniani kama Kylie Jenner mwenye biashara ya urembo na vipodozi kule nchini Marekani au mtu mwingine yeyote tajiri kama alivyokuwa Vladmir Putin wa Urusi na Rais tajiri zaidi Duniani kwa utajiri wa dola bilioni 69. Wala haijalishi ni kutoka nchi tajiri zaidi duniani ama ni kutoka nchi masikini.

Katika kitabu hiki chenye siri za matajiri mwandishi ameziweka falsafa (13) za mafanikio na Utajiri lakini mimi hapa leo nitajikita zaidi kwenye ile falsafa ama kanuni ya 13 na ya mwisho katika Sura ya 14 kwenye kitabu iitwayo; MLANGO FAHAMU WA SITA ( Mlango wa hekalu la hekima) kwa anayesoma nakala ya kitabu ya kiingereza sura hii inaitwa; THE SIXTH SENSE (The door to the Temple of Wisdom) Kwenye nakala ya kitabu ya Kiswahili iliyotafsiriwa na Peter Augustino Tarimo mwaka 2021, sura hii inapatikana ukurasa wa 335

Falsafa zote 13 za kitabu hiki zinatengeneza orodha ya matajiri wengi sana duniani wasiokuwa na idadi ila mimi kama nilivyotangulia kusema nitakwenda kukupatia tu baadhi yao kama mifano

Falsafa ya Mlango fahamu wa sita ni watu wachache sana wanaoifahamu vizuri na sababu ya kutokueleweka vizuri ni sharti la mwandishi kwamba ili uweze kuishika vyema ni sharti kwanza uzijue na kuzifanyia kazi falsafa nyingine zote 12 zinazotangulia. Hata hivyo kwa wale walioweza kuitumia na bado wakafanikiwa pasipokujua kama walichotumia ni falsafa/kanuni hii inawezekana kabisa pia walizitumia na hizo kanuni nyingine 12 pasipo hata wao wenyewe kubaini kama wamezitumia.

Kwani Mlango Fahamu wa Sita ni kitu gani hasa?

Binadamu tunao ufahamu wa aina mbili, kwanza ni ule ufahamu wa kawaida tunaoutumia kupitia milango nitano (5) ya kawaida ya fahamu yaani pua, masikio, ulimi, macho na ngozi, lakini tunao mlango wa fahamu mwingine wa 6 uliojificha ndani kabisa katika ubongo wetu, na ambao ni tofauti sana na hiyo mitano. Watu wengi tumezoea kuuita “MAONO”, ‘MACHALE’ au ‘UFUNUO’.

Je, Umewahi siku moja kutaka kupanda basi stendi lakini ukasita kidogo kisha ukaamua kurudi nyumbani halafu baadae ukaja kupata taarifa kwamba lile basi lilienda kupata ajali mbaya ya kutisha? Basi ikiwa ulikuwa hujui kitu kilichokushitua mpaka ukaahirisha safari kilikuwa ni huo mlango fahamu wa sita tunaouzungumzia leo na hufanya kazi yake kimaajabu sana kiasi kwamba wengi huuhusisha na miujiza na siyo kila mtu mlango huu unafanya kazi, isipokuwa tu habari njema ni kwamba unaweza kujizoesha mwenyewe kwa kutumia kanuni zilizo ndani ya hii sura ili mlango huo uweze kukufanyia mambo makubwa ikiwemo kupata utajiri au hata kukulinda na majanga kama ajali nk.

Katika Sura hii ya 14 ya kitabu cha Think & Grow Rich kuna maelezo ya kutosha ya jinsi mlango fahamu wa 6 unavyofanya kazi na namna unavyoweza kuutumia kwa manufaa yako mwenyewe.

Sipendi nikuchoshe na maelezo meengi, hebu twende moja kwa moja kwenye orodha ya matajiri na watu walio na mafanikio kimaisha nilioahidi pale mwanzoni kukudadavulia jinsi walivyoweza kuutumia mlango fahamu wa sita kujipatia mafanikio ya kustaajabisha kimaisha. Tutaanzia hapahapa nyumbani Tanzania;

DIAMOND PLATNUMZ

Kuna mbinu za kufanya kusudi uweze kujenga uwezo mkubwa wa kiubunifu (kimaono) kwa kutumia kanuni hii. Mbinu hizo mwandishi mwenyewe alizitumia  kwenye jaribio lake na zikafanya kazi vizuri katika kile alichodai ni Mikutano na Washauri wake wasioonekana uk. Wa 338 Sura ya 14

“Zamani kabla hata sijawahi kuandika mstari wa chapisho, au kujaribu kutoa hotuba kwenye hadhara nilifuatilia tabia ya kurekebisha tabia yangu mwenyewe kwa kujaribu kuwaiga watu tisa ambao maisha yao na kazi vilinivutia sana. Watu hao tisa walikuwa ni, Emerson, Paine, Edison, Darwin, Lincoln, Burbank, Napoleon, Ford na Carnegie. Kila siku kwa kipindi kirefu cha miaka niliitisha mkutano wa kufikirika na kundi hili niliowaita, ‘Washauri wangu wasioonekana’”

Na unapomwangalia msanii Diamond Platnum anafanya vitu vilevile vinavyofanana na vile alivyoshauri mwandishi vifanyike kumuwezesha mtu anayetamani kuukuza uwezo wake wa mlango fahamu wa 6. Nisichokijua ni  ikiwa Diamond anafahamu kama anachokitumia ni falsafa hii.

Mbinu ya Kujishauri Binafsi, kwa kimombo “Autosuggestion

Katika mbinu hii mhusika anayetaka mafanikio, iwe ni utajiri wa pesa, mafanikio kwenye sanaa au michezo mfano kwenye mchezo wa mpira wa miguu (soka), Kuimba (uanamuziki), mchezo wa ngumi (ndondi) nk. huwa wana iga ama kujifananisha na magwiji waliowatangulia, unaweza ukasema wanawatazama Role models wao na kukariri ama kujizoesha vitendo na nyendo zao zote nzuri mpaka kufikia hatua ya akili zao za ndani kabisa au tunaweza kusema Milango fahamu yao ya sita kuwasaidia moja kwa moja kutimiza ndoto zao tofauti na wale wanaotamani tu kutimiza ndoto zao kwa kutumia milango fahamu mitano (5) ya kawaida bila ya mafanikio.

 Kupitia msaada wa Mlango-fahamu wa sita utatahadharishwa juu ya hatari zinazokunyemelea katika muda muafaka ili kuzikwepa, na kuarifiwa juu ya fursa kwa wakati ili kuzitumia.

Unapoukuza mlango-fahamu wa sita unakupa msaada, na kufanya kile utakacho, huja malaika mlinzi ambaye muda wote atakufungulia mlango kuelekea hekalu la hekima”  Uk. 336 Sura: 14

Hali kadhalika unapomtazama Mwanamuziki Diamond au Naseeb Abdul, ijapokuwa watu wengi wanaweza wakawa hawajastukia lakini huu ndio ukweli wenyewe, kuna mahali Diamond anapokuwa jukwaani hahasa kwenye uchezaji wake utabaini fika kuna mahali anaigilizia miondoko ya Mfalme wa Pop Duniani Michael Jackson, Diamond hakuna mahali amewahi kutamka rasmi anavutiwa na Michael Jackson, hii ni observation yangu binafsi tu kama mimi. Hata katika video ya wimbo wake mmoja uitwao Baba lao na baadhi ya show zake nyingine kuna vitu vingi unaweza ukafananaisha na filamu ya Thriller ya Michael Jackson.

Diamond kama michael jackson

Inawezekana kabisa Diamondo hukaa mahali na kutizama magwiji kwenye tasnia yake Ulimwenguni wanaomvutia, jinsi walivyokuwa wakifanya, wanamsisimua kiasi mpaka mlango fahamu wake wa 6 unaiga hata pasipo mwenyewe kujua ameiga kitu kwao. Diamond aliwahi kunukuliwa na media akitamka kwamba, ‘Hakuna jipya chini ya jua, miziki inayoimbwa leo ilishaimbwa kitambo na kikubwa wanamuziki ni kuongezea tu ubunifu.’

HARMONIZE

Ukiwacheki vizuri wanafunzi wa Diamond na hasahasa Harmonize, utabaini hakuwa vile kabla hajajiunga na bosi wake huyo, Sasa hivi Harmonize anafanya mambo yake mengi utadhani ni Diamond, ‘swaga’ zake na hata miondoko unaweza ukaifananisha na ile ya bosi wake mpaka vaa yao. Harmonize ameiga mpaka ile hulka ya Diamond ya kutokutulia na kina dada.

Harmonize
Hii haikutokea tu kwa bahati mbaya hapana, ni matokeo ya kazi ya kujishauribinafsi chini ya mlango fahamu wa 6 harmonize alipokuwa kwa kila hali akijitahidi kuwa kama mentor wake Diamond na ndiyo sabau na yeye ameweza kupata mafanikio kwa kiasi tunachokiona. Ni kama bile alikuwa akijifunza jinsi ya kuwa tajiri kwa kumuiga Diamond njia alizopita. Ukitaka kufahamu siri za matajiri basi ni uwe nao karibu na kujaribu kufanya vile wafanyavyo hadi mlango wako wa 6 wa fahamu utakapoanza kutenda kulingana nao.

MICHAEL JACKSON MWENYEWE

Usije ukadhani labda Michael Jackson staili na ‘swaga’ zake zoote zile alizipata tu hewani hivihivi kutokea kusikojulikana hapana, tunaporejea ule msemo, Hakuna jipya chini ya jua, Michael Jackson kuna magwiji hata zaidi yake nao waliokuwa wamemtangulia na ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliomfanya awe kama alivyokuwa.

Kushoto ni Michael Jackson na Kulia ni Elvis Presley

Mwimbaji mwingine mashuhuri wa Pop na Rock duniani miaka ya 50 na 60 Elvis Presley maarufu kama Sukari ya Warembo kwa jinsi alivyopendwa mno na kina dada, uchezaji wake hata leo ukiamua kutizama video zake utakubaliana nami kwamba ulimwathiri kwa kiasi kikubwa sana Michael Jackson ingawa yeye mwenyewe Michael Jackson alikuwa akikanusha kwamba Presley hakuwa kabisa akimhamasisha. Wimbo wa Michael Jackson wa “This Place Hotel” ambao kwa kiasi kikubwa ulifanana sana na ule wa Ellvis uitwao “Heart break Hotel.” ni ushahidi tosha kwamba Elvis alimhamasisha sana Michael Jackson sema tu ni vile hulka ya watu wengi wanapopata umaarufu huwa hawapendi sana kuweka wazi watu halisi waliowahamasisha, pengine kutokana na kuhofia ushindani au watu kushusha thamani yake. Hivyo hapana shaka Michael Jackson alikuwa akivutiwa sana na Elvis Presley.

AKINA NEYMAR, LEONEL MESSI NA RONALDO

Inasemekana hakuna kipya hata kimoja wanachokifanya wanasoka mashuhuri wakati wa leo, mengi wanayarudia yaleyale aliyokuwa akiyafanya Mfalme wa soka duniani Pele miaka ile ya 60, 70 na 80 pamoja na wengineo kama vile Maradona miaka ya 80 na 90. Neymar hata pale alipofariki Pele hivi karibuni alisikika akisema kwamba alikuwa ndiyo mtu wake wa mfano, role model, na si yeye tu bali ni takriban karibu wanasoka wote wakubwa duniani walijaribu  kuwa kama Pele. 

Pele na Neymar, magwiji wa Soka Duniani

MUHAMMAD ALI

Mfalme huyu wa Masumbwi  Duniani wa wakati wote wala yeye hakuhangaika kuwatumia watu wa mifano katika kuukuza mlango fahamu wake  wa 6 bali alitumia mbinu ya kujishauri binafsi yeye mwenyewe kwa kuuzoesha maono ya ushindi mlango fahamu wake wa 6 mwenyewe kiasi kwamba kufanikiwa kwake hakukuepukika kabisa. Alisifika kwa kauli zake mashuhuri za kimaono kama vile, “you’ve got to float like a butterfly and sting like a bee.”  (Unapaswa kuelea kama kipepeo na kuuma kama nyuki).  Nyingine ni; "I am the greatest, I said that even before I knew I was." (Mimi ni mkali, na nilisema hivyo hata kabla sijajua nilikuwa hivyo)

Muhammad Ali

Miaka ya nyuma kidogo hapa nchini kulikuwa na wimbi la vijana wasanii kupenda kuwaigiza wasanii wakubwa wa muziki kutoka nje kama vile kina Michael Jackson, Kanda Bongoman na wengineo, ungesikia watu wakisema Kanda Bongoman wa Tanzania. Michael Jackson wa Bongo nk. na kweli walifanana nao kwa karibu kila kitu kuanzia uchezaji, uimbaji na hata mavazi yao. lakini nafikiri walichokuwa wakikikosa hapa ni ile kutumia milango fahamu yao ya 6 sawa na wale niliowataja pale juu na ndio sababu pengine hatukuweza kuwashuhudia wakifika mbali sana na hata kuwazidi waimbaji orijino, waliishia tu kusikojulikana na maslahi kidogo waliyojipatia.

Kanda bongo man


ELON MUSK

Tajiri wa kwanza Duniani 2022 Elon Musk, wakati alipokuwa akianza miradi yake ya anga za juu Space X na ule wa magari ya umeme Tesla hakuwa na mtaji wa kutosha akajaribu kuwafuata wawekezaji wakubwa lakini kila aliyemfuata alikataa kwa madai kwamba miradi hii ilikuwa ni ndoto za alinacha (pipe fantacy/dream) na kweli walikuwa sahihi kwani ni watu wengi walikuwa wamekwishajaribu miradi kama hiyo ikawashinda, hata NASA wenyewe ingawa walifanikiwa miaka ya 60 na 70 lakini ilikuja kuwashinda shauri ya gharama kuwa mno kubwa.

Elon musk

Lakini ni kwa msaada tu wa Mlango Fahamu wa Sita wa bwana Elon Musk uliomwambia hata kila mtu akiona haiwezekani, lakini itawezekana. Elon akatumia mpaka senti yake ya mwisho kabisa kugharamia miradi hii kwa ugumu ajabu! na mwishowe mwanaume akatoboa na mpaka hivi niandikapo hapa ndio Tajiri mkubwa zaidi Duniani  akimiliki Dola Bilioni 239.2

Amewezesha tena mashindano ya kwenda sayari za mbali kuanza upya kwa kuvumbua roketi ya gharama nafuu yenye uwezo wa kwenda sayari za mbali na kurudi Duniani ikaja kutumika tena badala ya zile za NASA na za Warusi za miaka ya 60 zilizokuwa zikishaenda huko anga za mbali huishia hukohuko na hivyo kufanya zoezi zima kuwa la gharama za kutisha.

 

HITIMISHO

Kitabu hiki cha Think & Grow Rich kina kanuni nyingi na hatua za mafanikio za kuchukua kusudi mtu uweze kufanikiwa katika jambo lolote lile maishani ikiwemo kifedha na leo nimegusa tu falsafa moja ama mbinu moja kati ya zile 13. Vyanzo vya utajiri wa matajiri wengi utakuta asili yake ni matumizi ya falsafa hizi wawe wanajua au hawajui kama walizitumia. Huna haja ya kwenda kwa mganga kusaka dawa ya mafanikio wakati unaweza kujifunza elimu ya pesa na jinsi ya kuwa tajiri haraka kupitia vitabu kama hiki cha Think and Grow Rich, tena kwa lugha yako ya mama.

Ikiwa utapenda kusoma nakala yako ya Kiswahili basi unaweza kuamua moja kati ya haya mawili;

1. Kusoma nakala laini (softcopy) kupitia simu yako ya mkononi-smartphone.

Bonyeza link ifuatayo,  >>GETVALUE,  kisha kwenye mtandao huo wa GETVALUE, fanya manunuzi kwa kujaza taarifa zote utakazoelekezwa pamoja na kulipia kitabu sh. Elfu 10 kwa mitandao ya simu. Kisha nenda play store download application(APP) ya GETVALUE, Jaza tena taarifa ulizotumia wakati wa manuuzi, ambazo ni email na password na hapo APP itafunguka utasoma kitabu chako.


2. Kusoma Nakala ngumu (Hardcopy)

Wasiliana nasi kwa namba 0712202244  na tutakuletea mpaka pale ulipo Dar es salaam kwa sh. 25,000/= Mikoani tunatuma kwa mabasi kwa sh. 35,000/=

 

HABARI NJEMA ZAIDI KWA WALIOKOSA OFFA ZETU 2022

Kutokana na maombi ya wadau wetu wengi tumeamua kusogeza mbele kidogo muda wa zawadi yetu au OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA tuliyofunga nayo mwaka. Sababu kubwa ni kwamba wadau wengi wanasema muda ulikuwa mfupi mno na hawakuwa wamejiandaa vizuri.

Hata hivyo kutokana na nafasi za kujiunga na group letu la masomo ya pesa ya kila siku kuwa chache, OFFA hii itadumu hewani mpaka tu watakapotimia idadi ya members waliobakia group lijae na muda huo hautazidi mwezi huu wa January 2023.

Hivyo naomba sana wadau mliotuma maoni yenu msichelewe tena safari hii kwani mimi sitaangalia ni nani aliyelalamika bali ni nani aliyechukua hatua ya kuhitaji zawadi hii. Kumbuka vitabu na michanganuo ninayoitoa kama zawadi kwa sh. Elfu 10 thamani yake halisi inazidi sh. Laki moja!

 

VITU VYA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA NI HIVI VIFUATAVYO;-

KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali

KITABU: Siri ya Mafanikio ya Biashara Duka la Rejareja

KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa

KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE

KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30

MCHANGANUO: Kuku wa mayai

MCHANGANUO: Kuku wa nyama - kwa kiswahili

MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

MCHANGANUO: Kuku wa kienyeji

MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji

MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa Kiswahili

MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa kiingereza

MCHANGANUO: Kiwanda cha Dona (Usado milling)

SEMINA: Jinsi ya kuandika mchanganuo wa kiwanda cha unga

SEMINA: Kuandika mchanganuo wa kuku wa nyama

MCHANGANUO: Kuandika mchanganuo wa Cafe

 

Lipia offa yako kupitia namba zangu, 0712202244  au 0765553030 kisha ujumbe watsap au sms usemao;

“NATAKA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA

Na utapata offa zako ndani ya dk. 3 tu

 

Thamani halisi ya offa hii ni sh. 180,000/= lakini lipa sh elfu 10 tu uokoe sh 170,000/= !

 

Ukitaka kuthibitisha uaminifu wetu bonyeza hapa kuona baadhi ya wadau wengine waliowahi kuchangamkia offa na vitabu vyetu. SOMA PIA NA MAKALA HIZI HAPA ZIFUATAZO;

1. Mwanasoka Eusebio Da Silva Ferreira ni kama EdsonPele, Muhammad ali na Michael jackson

2.Diamond kama Michael Jackson na wimbo wake My Number One

3. Ili ufanikiwe kuwa Tajiri mkubwa jiepushe kabisa na kauli hizi 4

4. Kanuni kuu ya mafanikio duniani iliyo kubwa kushinda zote

5. Kanuni za mafanikio (The success principles) by Jack Canfield

6. Jifunze kwa waliofanikiwa lakini usiige kila kitu kamakilivyo utafeli0 Response to "IJUE FALSAFA YA KITABU ILIYOTENGENEZA MATAJIRI & MABILIONEA WENGI ZAIDI DUNIANI"

Post a Comment