JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA LAKINI USIIGE KILA KITU KAMA KILIVYO UTAFELI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA LAKINI USIIGE KILA KITU KAMA KILIVYO UTAFELI

Moo na Elon musk

Katika nyingi ya nukuu za waliofanikiwa kuna moja inayosema hivi; njia rahisi na bora zaidi ya kufanikiwa katika jambo lolote lile ni kuiga na kujifunza kutoka kwa wale waliofanikiwa kwenye jambo hilo.

Kwa mjasiriamali yeyote anayetaka kufanikiwa ama kutajirika, mtu wake mkubwa wa mfano ni yile mtu ambaye tayari ni tajiri aliyefanikiwa. Ingawa kauli hii inaweza kuwa kweli lakini inaweza ikawa na matatizo makubwa.

SOMA: Jinsi ya kupata mafaniko maishani; usipande mlima bila kiongozi

Unapotazama tabia za mtu mwenye mafanikio tayari, usije ukafikiria kwamba anafanya mambo yaleyale aliyokuwa akiyafanya wakati kabla hajafanikiwa. Tabia za matajiri ni kwamba wanafanya vitu tofauti kabisa ukilinganisha na kipindi kile walipokuwa hawajapata pesa/hawana kitu. Ukiwa mdadisi wa historia za mafanikio ya watu wengi matajiri, utakubaliana nami juu ya hilo.

Mfano mmoja mkubwa unaweza kuuona kwa matajiri na tabia yao ya kuwa au kumiliki mifereji mingi ya kipato, utasikia watu wengi wa kipato cha chini nao wakijaribu kuiga tabia hii lakini huishia kukata tamaa na kuona ni jambo gumu lisilowezekana kirahisi. Kumbe wanafanya kosa kubwa bila kujua! Unajua ni kwanini hii haiwasaidii? Nitaelezea baadae kidogo....

SOMA: Ukaribu na wajasiriamali mashuhuri waliofanikiwa kunavyoweza kukuinua kimtaji ( Networking) 

Binafsi mimi mwenyewe kuna nyakati niliwahi kujihusisha na biashara nyingi nikidhania kwamba kufanya biashara moja ni hatari inaweza ikafa muda wowote.... Chakushangaza biashara zote hamna hata moja iliyoweza kufanikiwa kama nilivyotamani ziwe. Mpaka nakuja kugundua siri ilikuwa ni nini, nilijuta sana kwani nilishapoteza muda wangu mwingi wa thamani.

SABABU KUBWA 2 KWANINI WATU WANAOIGA KWA WALIOFANIKIWA HUFELI KIRAHISI

1. Wanataka utajiri wa haraka:

Hakuna kitu kama utajiri wa haraka chini ya jua, huu ni ukweli mchungu kila mtu anatakiwa kuujua. Zinahitajika juhudi na umakini (Focus) kwanza ili mtu aweze kufanikiwa katika jambo lolote lile. Utajiri wa haraka unaweza kutokea mara chache sana, mmoja katika watu maelfu, ni kwa waliokuwa na bahati ya mtende kama vile washindi wachache wa bingo na michezo ya kubahatisha. Sifa za utajiri hautaki haraka.

Kinachoonekana mara zote kuwa ni utajiri au mafanikio ya haraka mara nyingi ni watu waliofanya kazi usiku na mchana kwa miaka mingi kabla hawajafanikiwa. Watu waliofanikiwa kupitia kilimo kwa mfano unaweza kudhania ndio waliofanya kazi ngumu zaidi lakini hata shughuli zingingine kama muziki msanii ataonekana kama kafanikiwa haraka lakini watu hawawezi kufikiria kipindi msanii alipokuwa akikariri mashairi ya nyimbo za wasanii wakubwa wenye majina alivyosota.

SOMA: Wanaofanikiwa maishani wengi husema no (hapana) kwa vitu hivi 3 

Sisemi haiwezekani kabisa mtu kutajirika haraka hapana, bali ninachosisitiza hapa ni kuwa ili ufanikiwe ni lazima uonyeshe hali fulani ya uvumilivu, bidii, nidhamu ya fedha na msimamo, na haya ndiyo miongoni mwa mambo yaliyosisitizwa sana ndani ya kitabu cha Think & Grow Rich ambacho sasa hivi kinapatikana pia kwa lugha adhimu ya Kiswahili katika kiungo hiki,  FIKIRI & UTAJIRIKE  

2. KIU YA KUTAKA KUWA NA MIFEREJI MINGI YA KIPATO MAPEMA MNO

Tunarudi katika mada yetu tuliyoanza nayo pale mwanzo. Nimewahi hata kutunga kitabu kiitwacho, MIFEREJI 7 YA PESA NASIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA kusisitiza dhana hiyo  lakini ndani ya kitabu kuna mahali nilisema Mifereji 7 ya kipato siyo kwa masikini bali kwa watu ambao tayari wameshafanikiwa kwa kiasi fulani.

Ukweli ni kwamba ukiwa masikini na ukatawanya nguvu na rasilimali zako kwenye miradi zaidi ya mmoja kabla haijafanikiwa kusimama yenyewe kwa miguu yake ni lazima tu utaanguka/utafeli. Ikiwa hautatumia asilimia 100% ya nguvu zako kuanzisha biashara fulani mpaka isimame kwanza ndipo uanzishe nyingine, utakuwa ukicheza patapotea. Hauwezi kutajiruka kwa kuanza na utitiri wa biashara bali ni kwa kuwa kwanza na msimamo na biashara moja mpaka pale itakaposimama imara ndipo uanzishe nyingine hivyo hivyo na ukitaka hata kuwa na biashara 10.

SOMA: Mifereji ya kipato ni kwa waliofanikiwa, kwa wajasiriamali wadogo ni kupoteza muda, nguvu na malengo bure

Natumaini hautafanya makosa niliyowahi kuyafanya kwa kuingia mtego wa kuanzisha biashara nyingi wakati hazijasimama imara. Natamani haya nikwambiayo ningeambiwa mika 10 au 15 iliyopita, ndiyo maana nikaamua kuanzisha darasa langu kwenye Group la Telegtam na Wasap liitwalo MICHANGANUO-ONLINE kwa ajili ya kufundisha watu mbinu mbalimbali za biashara na ujasiriamali.

Kujiunga na Group letu ambalo kwa sasa tuna somo la SIRI ZA BIASHARA YA SUPU TAMU NA CHAPATI LAINI linaloendelea, lipia tu kiingilio cha mwaka mzima shilingi elfu 10 kwa namba 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha nitumie kwa meseji namba yako ya TELEGRAMU na anuani ya Email kisha ujumbe usemao; NIUNGE NA MASTERMING GROUP NA OFFA YA VITU 21 YA KUFUNGA MWAKA. Utatumiwa muda huohuo kila kitu na kuunganishwa na group.

Kama utahitaji na kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE nijulishe ili nikupe link na kuponi ya kukinunua kutoka mtandao wa GETVALUE kwa sh. Elfu 5 tu badala ya elfu 10

ZAWADI hii itadumu kwa muda mfupi sana kabla hatujaiondoa.

 

ZAWADI YENYEWE YA KUFUNGA MWAKA (VITU 22) NI HII HAPA CHINI;

 

              1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

              2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

              3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

              4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

              5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

              6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

              7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

              8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

              9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

            10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

            11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

            12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

            13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

            14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

            15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

            16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

            17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

            18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

            19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

            20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

            21.    KITABU CHA SEMINA: Masomo 11 ya  michanganuo ya Biashara

 

            22.    Kujiunga GROUP LA WHATSAP & TELEGRAM LA MICHANGANUO-ONLINE

 

0 Response to "JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA LAKINI USIIGE KILA KITU KAMA KILIVYO UTAFELI"

Post a Comment