UKARIBU NA WAJASIRIAMALI MASHUHURI WALIOFANIKIWA KUNAVYOWEZA KUKUINUA KIMTAJI(NETWORKING)


WAJASIRIAMALI WALIOFANIKIWA
Ukweli kwamba mtu unaweza ukafanikiwa haraka katika biashara yako bila ya kuwa na mtaji mkubwa ni jambo gumu lakini pia ni jambo linalowezekana kabisa. Kuna watu wengi waliowahi kutumia mazingira ama fursa hii ya kujenga mtandao(networking) na wajasiriamali waliofanikiwa na wakapata mafanikio ya kushangaza.


Hata hivyo mafanikio katika biashara au uwekezaji yanategemea vigezo vingi ikiwa ni pamoja na hiki cha kujenga ukaribu ama mtandao na wajasiriamali mashuhuri waliofanikiwa katika biashara au sekta unayotamani kubobea. Miongoni mwa vigezo hivyo ni hivi nitakavyovitaja hapa chini;

1.  Uwezo wako wa kujenga mtandao na watu hasa wale waliokuwa na uzoefu wa kutosha na biashara ile unayotaka kuifanya.

2.  Uwezo wako wa kujenga biashara yenye faida na inayoweza kujitanua kwa urahisi.

3.  Uwezo wako wa kuendelea kubakia kuwa mvumilivu huku ukikataa kushindwa.

4.  Kiasi cha muda na rasilimali unazotumia katika kujifunza ili kuwa mahiri katika sekta yako(eneo ulipo)

5.  Uwezo wako wa kukopa kwa riba kidogo na kuutumia mkopo huo kwa faida.

6.  Uwezo wako wa kuwa na mali(asseti) zinazokuingizia fedha badala ya zile zinazokuondolea fedha(Liabilities)

7.  Utayari wako wa kujifunza kutoka kwa wale walio na uzoefu.

8.  Jinsi unavyoweza kukabiliana na wasiwasi, kukatishwa tamaa, kushindwa na kukataliwa.

9.  Bahati.


Leo hii usiku Group letu la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo, MICHAGANUO ONLINE, tutakwenda kukizungumzia kwa undani kabisa moja kati ya vigezo vya mafanikio makubwa kibiashara vilivyotajwa hapo juu, kipengele cha kwanza cha kujenga ukaribu au mtandao(networking) na wajasiriamali au watu mashuhuri katika sekta unayofanyia biashara yako.

Kwa mfano unaweza ukawaza na kudhani kwamba ni jambo lisilowezekana kabisa wewe kama mjasiriamali mdogo kuwafuata na kuzungumza na wafanyabiashara wakubwa kabisa nchini wenye uwezo ukabadilishana nao mawazo, kweli siyo jambo rahisi hata kidogo na ugumu huo hautokani na wajasiriamali hao kujiona wako juu hawahitaji kuzungumza na watu wadogo hapana, wanapenda sana kujenga mitandao na watu wa kawaida lakini tatizo ni kwamba, wale wanaohitaji kujenga nao mitandao ni wengi mno.

Ratiba zao ziko ‘tight’ kiasi kwamba haiwezekani kabisa kusema wamsikilize kila mtu anayetaka kujenga nao ukaribu. Ndio maana ukifika maofisini mwao wakati mwingine utaishia tu kuzungumza na masekretary wao, huwezi ukaonana nao ana kwa ana sembuse kujenga nao mitandao.


Sasa swali ni je, utawezaje wewe kama mjasiriamali mdogo kujenga ukaribu(mtandao) na wajasiriamali wakubwa waliofanikiwa katika kukuwezesha haraka kibiashara?

Kumbuka wajasiriamali hao wanao uwezo mkubwa siyo kifedha tu bali zaidi ni katika uzoefu waliokuwa nao. Kuwa tu karibu nao hata kama hawatakupa pesa inatosha kabisa kukufanya wewe uzione fursa ambazo kabla usingeliweza kuziona.

Watu wengi tunakosea kufikiri kwamba, mtu ni lazima kwanza uwe na pesa ndipo uweze kupata pesa, lakini ukweli siyo kila wakati inakuwa hivyo. Kuna fursa nyingine kama hii ya kujenga mtandao na wajasiriamali wakubwa wenye uzofu inayoweza kumuinua mtu haraka kimtaji.


Karibu sana kwenye GROUP letu tujifunze pamoja kila siku. Hili siyo somo la kukosa hata kidogo. 

Ni kwa jinsi gani unavyoweza kujenga mtandao na wajasiriamali wakubwa kabisa waliofanikiwa wakati huna kitu mfukoni na wakati huohuo ukawafanya wakupe siri za wewe kuweza kutoka pale ulipo kimtaji na kibiashara ndiyo mada kuu ya siku ya leo.

Wanaojiunga na programu hii baada ya kulipia kiingilio shilingi elfu 10, huwa tunawatumia na offa ya vitu vyote vifuatavyo bila gharama nyingine zozote zile za ziada;


WHATSAPP:  0765553030
SIMU:             0712202244
JINA:              Peter Augustino Tarimo


0 Response to "UKARIBU NA WAJASIRIAMALI MASHUHURI WALIOFANIKIWA KUNAVYOWEZA KUKUINUA KIMTAJI(NETWORKING)"

Post a Comment