2023 MWAKA WA UBUNIFU ZAIDI KWENYE BIASHARA KUKABILIANA NA MAJANGA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

2023 MWAKA WA UBUNIFU ZAIDI KWENYE BIASHARA KUKABILIANA NA MAJANGA

Tumsaidie Rais Mama Samia kuwatua kinamama kuni vichwani

Tukiwa tunakaribia kuingia mwaka mpya wa 2023 sisi blogu ya jifunzeujasiriamali kama ilivyokuwa ada kwetu ni wakati wa kutoa tathmini ya mwaka mmoja uliopita, pia kutoa Dira na mwelekeo wa mwaka unaofuata, tumekuwa tukifanya hivi kwa miaka mingine yote ya nyuma.

Mwaka unaomalizika wa 2022 kaulimbiu yetu kuu ilikuwa ni; “BADILISHA TABIA KUJENGA TIJA NA UFANISIZAIDI” na tumeweza kuona jinsi ambavyo tabia ya kufanya mambo kidogokidogo bila ya kuahirishaahirisha inavyoweza kufanikisha mtu kutimiza lengo kubwa alilojiwekea. Falsafa hii si kama niliielezea tu kinadharia hapana, ni uzoefu wangu binafsi nilioupata wakati nafanya kazi ya kukitafsiri kitabu cha THINK & GROW RICH katika lugha ya Kiswahili kazi niliyoikamilisha mwishoni mwa mwaka 2021 wakati naandika kaulimbiu hiyo.

Ni matumaini yangu kwamba wote wale tuliokuwa pamoja katika safari nzima ya mwaka 2022 hasahasa Wanamastermind Group wenzangu wa MICHANGANUO-ONLINE wameshuhudia jinsi falsafa hii ilivyo na uwezo wa ajabu wa kufanya kazi licha ya vikwazo kadhaa. Vikwazo hivi yalikuwa ni majanga ya asili kama vile ukame, vita na magonjwa ya mlipuko kama corona na ebola, vitu ambavyo kibinadamu ni vigumu sana kuvizuia.

Biashara hazikwenda vizuri kama ilivyotarajiwa jambo lililopelekea malengo mengi kushindwa kufikiwa. Gojwa la Covid 19, Vita ya Urusi na Ukraine, Ukame mkali na mfumuko mkubwa wa bei hasa za vyakula, nishati na zana za ujenzi ni matatizo ambayo mpaka sasa hivi yanaisumbua siyo Tanzania tu peke yake bali Dunia nzima kwa ujumla.

SOMA: Amua hatma yako tengeneza mwaka uliokuw bora zaidi kushinda mingine yote iliyopita

Katika kitabu cha Think & Grow Rich hali kama hii naweza kuifananisha na kipindi cha mdororo mkubwa zaidi wa kiuchumi Duniani (The Great Depression) 1929 1939, kipindi ambacho ndipo kitabu hiki kiliandikwa muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa vita kuu ya pili ya Dunia.

Licha ya maelfu ya watu wakati huo kutokuwa na kazi huku mfumo mzima wa kibenki ukiwa umefeli na kila mtu akihaha kutafuta mlo wa siku, lakini Napoleon Hill katika kitabu chake hiki mashuhuri aliweza kuwathihirishia Wamarekani kwamba bado maisha yangeweza kuwa bora kwa mara nyingine tena na ukweli ikaja kuwa hivyo. Wamarekani na hatimaye Dunia nzima ikaimarika tena kiuchumi licha ya kuwepo kwa vita kuu ya ii ya dunia.

SOMA: Heri ya Krismasi na mwaka mpya wenye mafanikio. 2019 ishi kama Mbayuwayu

Magumu tunayopitia sasa hivi kama Tanzania na Dunia kwa ujumla ni kama tone tu la maji kwenye bahari kubwa ukilinganisha na hayo niliyoyataja ya Great Depression na Vita kuu ya Dunia mika ya 30. Matumaini Napoleon Hill aliyowapa Wamarekani miaka hiyo ya 30 yanafanya kazi hata na leo hii kupitia kitabu chake cha FIKIRI & UTAJIRIKE (think & grow rich)

Hivyo basi namimi kwa mwaka huu tunaouanza leo wa 2023 kama mfuasi wa Napoleon Hill nimeamua kujitolea kwa dhati ya moyo wangu kutumia fikra na ubunifu kusaidia kubadilisha hali iliyokuwepo sasa hivi na kurudisha tena matumaini yanayokaribia kupotea.

Katika madarasa yangu Group za watsap na Telegram au makala nitakazoandika hapa katika blogu hii ya jifunzeujasiriamali, nimelenga zaidi katika mambo makuu 3 yafuatayo;

1.  Ububifu na teknolojia katika biashara kubwa na ndogo kwa lengo la kutengeneza faida kubwa haraka zaidi

 

2.  Uhamasishaji matuimizi ya nishati mbadala na rafiki kwa mazingira kupunguza ujoto duniani

 

3.  Elimu ya kujitambua binafsi na matumizi ya akili katika kujiletea maendeleo binafsi.

Tayari kwa kuanza leo hii kwenye MASETRMIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE tunaanza masomo yetu chini ya mwavuli wa maudhui niliyoyataja hapo juu, Tunaanza na biashara rahisi tu ya chakula, ‘SUPU NA CHAPATI’. Kwa juu juu unaweza kuona ni biashara ndogo rahisi zisizokuwa na maana yeyote lakini tunachokitaka hapa ni kuwajengea uwezo na matumaini wajasiriamali wadogowadogo wa kawaida kabisa “wanaostraggle na maisha yao ya kila siku.

SOMA: Biashara ya chakula, mchanganuo na mtaji mdogo wa kuanzia

Ingawa sehemu ya masomo haya pia tutayaweka katika blogu yako hii pendwa lakini kwa kiasi kikubwa yatakuwa yakifanyika ndani ya MASTERMIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE. Huu ni mwanzo tu, tutakuwa na masomo mengi ya thamani huku wanachama wakiwa na uwezo wa kuyapata pia baadhi ya masomo mengine mazuri ya zamani. Tunafanya hivi kwani si kila mtu anapenda kujifunza kwa kina, mwingine angependa kusoma kwa kifupi tu kwenye blogu hii basi.

Ikiwa wewe ni mtu unayependa kujifunza mambo kwa kina pamoja na kushea na wenzako kile unachokijua, nakukaribisha sana kwenye MASTERMING GROUP LETU LA MICHANGANUO-ONLINE, kiingilio cha mwaka mzima ni shilingi elfu 10 tu  na hii tumeweka kwa ajili tu ya kulipa group thamani, magroup ya bure mara nyingi watu huwa hawayathamini wala kuzingatia kile wanachojifunza humo.

ZAWADI YA KUFUNGA MWAKA (Haijawahi kutokea)

Kwa watu wachache wa mwanzo watakaolipia viingilio vyao vya mwaka sh. 10,000/= nitawapatia zawadi ya vitabu vyangu muhimu pamoja na michanganuo ifuatayo,( Jumla ni vitu 22); Offa hii ni ya muda mfupi na itamalizika muda wowote kuanzia sasa hivi idadi inayohitajika ikitimia.

Thamani halisi ya vitu vyote 22 ni zaidi ya Tsh. laki moja na nusu lakini unalipa sh. Elfu 10 tu! Na ninakutumia papo hapo kila kitu kama nakalatete mara unapomaliza kulipia kisha kukuunganisha na magroup yetu Whatsap & Telegram.

Ikiwa hupendi kuungwa kwenye group niambie nikutumie zawadi zako peke yake, na pia kama hutumii Whatsap wala Telegram, email inatosha kukutumia kila kitu.

Lipia mapema kiingilio chako sh. Elfu 10 kupitia namba zangu, 0712202244 au 0765553030 Jina ni Peter Augustino Tarimo kisha ujumbe wa SMS au Watsap usemao;

 “NATAKA OFFA YA MWISHO WA MWAKA YA VITU 22”

 

ZAWADI YENYEWE YA KUFUNGA MWAKA 2022, VITABU NA MICHANGANUO JUMLA VITU 22 NI HII HAPA CHINI;

 

              1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

              2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

              3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

              4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

              5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

              6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

              7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

              8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

              9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

            10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

            11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

            12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

            13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

            14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

            15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

            16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

            17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

            18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

            19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

            20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

            21.    KITABU CHA SEMINA: Masomo 11 ya  michanganuo ya Biashara

 

            22.    Kujiunga GROUP LA WHATSAP & TELEGRAM LA MICHANGANUO-ONLINE

 

Ukishajipatia offa hii na pia kama ungependa kupata na kitabu cha THINK & GROW RICH nakala ya Kiswahili, na una Smartphone unaweza kujipatia kwa shilingi elfu 5 tu badala ya sh. elfu 10 bei ya kawaida. Maelezo zaidi ya namna ya kukipata tuwasiliane nikupatie. Kama hujajipatia offa hiyo hapo juu bei ya kitabu FIKIRI & UTAJIRIKE inasalia kuwa sh. Elfu 10 kama kawaida.

Zawadi kama hizi huwa tunazitoa mara chache sana hivyo nakuomba ikiwa upo makini na masomo ninayoyatoa basi ni fursa ya kipekee kujipatia mafunzo hayo kwa kina kwa gharama hii sawa na bure. Njoo kwa pamoja tumsaidie Rais wetu mama Samia Hassan Suluhu kuwatua kinamama kuni vichwani mwao pamoja na maswala mengine kibao tutakayojadiliana kwenye group letu na channel ya telegram.

Tukutane tena jioni kwa masomo ya kila siku ndani ya MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE

Ni mimi, mwandishi na mhamasishaji wako;

PETER TARIMO 


0 Response to "2023 MWAKA WA UBUNIFU ZAIDI KWENYE BIASHARA KUKABILIANA NA MAJANGA"

Post a Comment