GHARAMA ZA UJENZI WA BANDA LA KUKU 100 CHOTARA AU KIENYEJI NI SHILINGI NGAPI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

GHARAMA ZA UJENZI WA BANDA LA KUKU 100 CHOTARA AU KIENYEJI NI SHILINGI NGAPI?

Banda la kuku

Hellow mdau na mfuatailiaji wa blogu yako hii ya jifunzeujasiriamali, katika makala hii naenda kukushirikisha majibu niliyompatia mdau wetu mmoja aishiye nchini Irani aliyeuliza kama ifuatavyo;

Mimi ni ndugu yako mtanzania

 

Niko nchini Iran

 

Nimesoma articles mbalimbali ulizoandika na kuziweka mtandaoni kuhusu ujasiriamali wa ufugaji wa kuku wa mayai

 

Na kuku wa nyama

Naomba nikuulize swali la Kitaalamu ndugu yangu

Ninachotaka kujua ni bei tu ya banda la kuku kwa kukisia..

 

Yaani:

 

Mfano:

Kuku 1000 chotara au kienyeji

Banda lao zuri na la kisasa linaweza kutengenezwa kwa *Shilingi ngapi (kwa bei ya kukisia kwa haraka haraka)?*

Asante kaka.......

Habari kaka


Namimi nilimjibu kamaifuatavyo;-

Kwa kuku 1000, tuchukulie ni kuku wa kienyeji wakubwa au wa kisasa ambapo kuku 6 mpaka 10 wanapaswa kukaa ndani ya eneo la mita 1 ya mraba yaani upana mita 1 na urefu wa mita 1. Kumbuka ujenzi wa banda la kuku wa kienyeji ni tofauti na ule wa banda la kuku wa `kisasa katika ukubwa tu, kuku wa kisasa banda lao hukaa kwenye eneo dogo zaidi.

Tutatumia idadi ya kuku 6 kwenye eneo la mita moja ya mraba ambapo kwa kuku 1000 watahitaji; (1000/6) eneo la miata za mraba 166 sawa na makisio ya mita 160 au Urefu wa mita 16 na upana wa mita 10

SOMA: Muongozo kamili wa jinsi ya kufuga kuku wa nyama (Broilers) kitaalamu

Tukichukulia ukubwa wa chumba  kimoja cha kawaida cha mita 3 kwa upana wa mita 3 sawa na mita za mraba 9 eneo hilo linatakiwa kuwa na wastani wa vyumba vipatavyo(160/9) = 18

Ikiwa chumba kimoja kinaweza kugharimu shilingi mpaka milioni 2 kwakuwa ni banda tu la kuku hakuna finishing wala nini, basi mabanda yote jumla yatagharimu wastani wa shilingi milioni 36. Picha za banda la kuku la mfano unaweza ukaziona katika makala yangu nyingine niliyoiandika hapa isemayo, Banda la kuku 100 wa kienyeji, vipimo, ramani, picha na jinsi ya kulijenga kwa ubora

Nimetumia milioni 2 kwa makadirio tu, unaweza mwenyewe ukauliza mafundi gharama, mahitaji ya 'let say' bati zinazotosheleza chumba kimoja ni ngapi, tofali, wavu wa kuku, gharama za fundi, mchanga, misumari, sementi nk. kisha ukajumlisha zote na kupata gharama za chumba kimoja cha mita za mraba 9 kisha gharama hiyo ukazidisha kwa vyumba vyote 18 kupata gharama kuu. Hivyo bei ya mabanda ya kuku hutofautiana kulingana na materials zilizotumika kujengea

SOMA: Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai? naomba mchanganuo

Ikiwa ni mabanda ya mbao tupu utafuata njia hiyohiyo niliyotumia. Hivyo unaweza kuona siwezi kuwa na jibu kamili moja kwa swali lako kwakuwa sijui utaamua kutumia material gani kujengea mabanda yako, hata hivyo mafundi wana utaalamu mzuri zaidi wa kukadiria gharama za ujenzi wa nyumba yeyote ile hata ikiwa ni ya kuku utakapokuwa tayari na kuita fundi ataweza kukusaidia zaidi. Mabanda ya kuku yapo ya aina nyingi sana mfano kuna mpaka banda la kuku la ghorofa nk. Hivyo gharama zake zitakuwa tofauti

Majibu ukubwa wa banda la kuku 100

Ni mimi,

PETER AUGUSTINO 

Mtaalamu wa kuandika michanganuo ya Biashara za aina mbalimbali zikiwemo za ufugaji wa kuku aina zote, blogger na mjasiriamali

 

Karibu kwenye Group langu la MICHANGANUO-ONLINE kwa masomo zaidi na mijadala ya kila siku. 0712202244  au  0765553030

0 Response to "GHARAMA ZA UJENZI WA BANDA LA KUKU 100 CHOTARA AU KIENYEJI NI SHILINGI NGAPI?"

Post a Comment