UZOEFU WANGU BINAFSI KWENYE BIASHARA YA SUPU NA CHAPATI LAINI ZA KUSUKUMA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UZOEFU WANGU BINAFSI KWENYE BIASHARA YA SUPU NA CHAPATI LAINI ZA KUSUKUMA

Chapati za kusukuma

Usije ukadhani labda hapa naandika nadharia tupu nilizosoma mahali hapana, ni biashara niliyowahi kuifanya mimi na mke wangu tulipoamua kuanzisha mgahawa mdogo. Hapo kabla hatukuwa tunafahamu kabisa kama chapati zingeliweza kutupa changamoto tulizozipata. Kila mke wangu alipojaribu kutengeneza chapati za wateja zilionekana laini tu pale zinapotoka jikoni lakini baada ya muda kidogo kupita zikianza kupoa zinageuka kuwa ngumu ajabu utafikiri ni ngozi ya mnyama.

Tulifanya majaribio ya kununua chapati kutoka kwa mtu ambaye chapatti zake zilikuwa zikipendwa sana na wateja tukabaini zilikuwa na uwezo wa kukaa hata siku nzima(saa 24) pasipo kugeuka kuwa ngumu. Tukajaribu kuingia mitandaoni, Utube nk. Lakini maelezo yote tuliyopata huko hayakutusadia sana.

SOMA: Uzuri wa mafunzo ya mapishi ya vitafunwa, chakula, lambalamba whatsap mtandaoni

Mke wangu aliamua aende kwa rafiki yake mmoja hivi kusudi aweze kumfundisha, akamsimulia tu kwa mdomo jinsi ya kuchanganya unga na kila kitu hadi kukaanga. Maelezo yalifanana kidogo na yale ya kwenye mitandao na aliporudi tukajaribu kwa shauku lakini cha kushangaza hatukuweza kupata matokeo ya kutia moyo.

Wateja waliendelea kulalamika kuwa chapati zetu ni ngumu, wengine hata wakadiriki kuhama. Kuna waliotushauri tubadilishe vitafunwa ikibidi tuchemshe ndizi badala ya chapati, lakini ukweli ni kwamba wateja wengi hupendelea chapati kwa supu au chai kuliko ndizi za kuchemsha.

SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1

Binafsi nilichukua uamuzi wa kufanya utafiti sehemu mbalimbali ndipo nikakutana na dada mmoja Kariakoo ambaye chapatti zake nilionja na kuona zilikuwa za kiwango kinachostahili. Bila kusita nilimuomba anipatie darasa la vitendo nimlipe kiasi cha fedha atakacho akanikubalia lakini kwa kuwa ilikuwa ni kipindi cha mfumgo wa Ramadhani alikuwa na ratiba ngumu akanipangia niende baada ya siku kadhaa.

Sikuweza kuvumilia zile siku zifike nikamfuata dada mwingine aliyekuwa akiuzia chapatti maeneo ya Mbezi Mwisho, huyu alikubali kunifundisha siku ileile na akaniagiza nikanunue vifaa nije saa 12 jioni baada ya kumaliza kazi zake za mama lishe. Aliniagiza Unga nusu kilo, mafuta ya kula Robolita na mkaa kiasi kama wa mia tano hivi, mimi nilinunua wa buku kabisa ukibaki nimwachie.

SOMA:Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka Tanzania hizi hapa, zipo nne(4)

Tulianza darasa letu saa 12, huku nikimfuatalilia kwa umakini mkubwa kila hatua aliyopitia. Dada alinieleza kwamba chapati zake ni simple sana na kwanza hajisumbui hata kutumia maji ya moto au ya uvuguvugu na bado chapatti zake zinatoka nzuri, alidai kuchemsha maji ya kusukumia chapati za biashara ni kupoteza muda.

Kwenye ukandaji alikadiria tu maji, mafuta na chumvi na wala hakuonyesha kipimo exactly ni kiasi gani mtu unapaswa kuweka, (hapa kama huna uzoefu imekula kwako) Baada ya kukanda ukalainika alilifunika donge la unga kama dakika kumi kisha akaanza kukata matonge madogomadogo saizi ya limao na kuyapanga mle kwenye beseni alilokandia.

SOMA: Jinsi kiwanda kidogo kinavyoweza kukutoa kimaisha na kuwa tajiri wa kutupa

Alipomaliza madonge yote, yalikuwa kama 7 au 8 hivi kama sikosei, aliweka kikaangio(frying pan) jikoni ili kianze kupata moto kisha akaanza kusukuma lile donge la mwanzo kabisa tayari kwa kuanza kukaanga chapati zetu. Alinisisitizia sana juu ya kuhakikisha moto unakuwa wa kutosha lakini usizidi sana kwani chapatti zinaweza zikababuka bila ya kuwiva sawasawa, pia moto ukiwa kidogo sana zinakuwa ngumu.

Baada ya zoezi la kukaanga kumalizika alinikabidhi chapatti zangu tukaonja hapo moja mbili huku nyingine nikiwabebea watoto nyumbani, nyumbani nilihakikisha nabakiza chapati mbili ili nione ingechukua muda gani zikiwa laini. Asubuhi kweli nilizikuta bado laini ingawa kuna kitu kimoja hakikunipendeza, chapati za huyu dada hazikuwa zimewiva sawasawa jambo ambalo nadhani wateja pia huwa hawalipendi na mara nyingi utakuta wakikata vipande maeneo yanayoonyesha weupe au ubichi, nilifikiria huyu dada alifanya vile kusudi chapati zionekane laini.

SOMA: Unajua biashara  yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

Pamoja na hayo yote tulijipa moyo na kujiambia labda mambo yatakuwa tu mazuri tutakapozidi kufanya mazoezi ya kupika chapati tena na tena. Siku ileile iliyofuata tukapika chapati kwa mbwe mbwe zote tukitumia utaalamu niliochukua kwa dada Mama lishe lakini chakushangaza tena matokeo hayakuwa kama nilivyotegemea. Bado chapati ziliendelea kuwa kavu na ngumu, labda uipue haijawiva sawasawa ndipo utaona ikiwa laini kidogo. Hili nalo likaendelea kutusumbua vichwa.

Ilikuja kutuchukua zaidi ya miezi 3 kupata kanuni sahihi ya kutengeneza chapati laini bila ya kubahatisha tena. Nikiamua kupika chapati najua kabisa matokeo yake yatakuwaje kulingana na hatua nitakazopitia na vipimo vya viambato mbalimbali.

Fuatana na mimi kwenye somo hili la Supu na Chapati kila siku mpaka mwisho, bado hatujafika mahali penyewe pazuri penye siri za kupika chapati laini mchambuko na supu tamu, haya bado ni maelezo tu ya awali.

Ikiwa unapenda kujifunza somo hili kikamilifu ungana na sisi kwenye Group na Channel yetu ya Telegram, MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP kwa kuchangia kiingilio cha mwaka cha shilingi 10,000/=

Kujiunga lipia kwa namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augstino Tarimo

Ukilipia mapema kabla nafasi hazijajaa unapata ZAWADI/OFFA ya kufunga mwaka ya vitabu na Michanganuo ya biashara/Business Plans, jumla vitu 22 katika mfumo wa nakalatete kwenye simu yako au kompyuta.

Baada ya kulipa sh. 10,000/= nitumie anuani yako ya E-mail na namba uliyojiunga nayo  TELEGRAMU kisha ujumbe ufuatao;

“NATAKA OFFA YA MWISHO WA MWAKA YA VITU 22”


ZAWADI HIYO YA KUFUNGIA MWAKA 2022, VITABU NA MICHANGANUO JUMLA VITU 22 NI HII IFUATAYO;

 

              1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

              2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

              3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

              4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

              5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

              6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

              7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

              8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

              9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

            10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

            11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

            12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

            13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

            14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

            15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

            16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

            17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

            18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

            19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

            20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

            21.    KITABU CHA SEMINA: Masomo 11 ya  michanganuo ya Biashara

 

            22.    Kujiunga GROUP LA WHATSAP & TELEGRAM LA MICHANGANUO-ONLINE

 

Ukishajipatia zawadi hii na pia kama ungependa kupata na kitabu cha THINK & GROW RICH nakala ya Kiswahili, na una Smartphone unaweza kujipatia kwa shilingi elfu 5 tu badala ya sh. elfu 10 bei ya kawaida. Maelezo zaidi ya namna ya kukipata tuwasiliane nikupatie. Kama hujajipatia offa hiyo hapo juu bei ya kitabu FIKIRI & UTAJIRIKE inabakia kuwa sh. Elfu 10 kama kawaida.

Offa kama hizi huwa tunazitoa mara chache sana hivyo nakuomba ikiwa upo makini na masomo ninayoyatoa basi ni fursa ya kipekee kujipatia mafunzo hayo kwa kina kwa gharama hii karibu na bure


0 Response to "UZOEFU WANGU BINAFSI KWENYE BIASHARA YA SUPU NA CHAPATI LAINI ZA KUSUKUMA"

Post a Comment