JINSI YA KUPATA MAFANIKIO MAISHANI: USIPANDE MLIMA BILA KIONGOZI

jinsi ya kupata mafanikio, usipande mlima bila kiongozi

Sina shaka unawafahamu ama umeshawahi kusikia kuhusu wale waongoza watalii wanaopanda milima mfano wa mlima Kilimanjaro, kwa kimomgo huwa wanaitwa guides. Kupanda kileleni mwa mlima kama Kilimanjaro, mlima Everest au Mlima Kenye isingelikuwa ni kazi rahisi kwa mtu ambaye hata siku moja hajawahi kufanya hivyo. Ingelimchukua muda mrefu kubahatisha huku akipotea na wakati mwingine hata kuporomokea katika mapango ya kale kitendo ambacho kingeliweza hata kuhatarisha maisha yake.

Maguide hawa au waongozaji wapanda milima, wana uzoefu wa muda mrefu na kazi hiyo, walitumia muda wao mwingi kujifunza mazingira yote ya mlimani, njia zote, vichochoro na hata kujua ni wapi palipokuwa na hatari za aina mbalimbali. Huwezi kuwadanganya kitu chochote kuhusiana na upandaji mlima. Siri ya mafanikio ya upandaji mlima hadi kufikia juu kabisa kileleni wanaijua wao.

SOMA: Siri 10 alizotumia Aliko Dangote kufika pale alipo.

Mfano huu wa wanaoongoza wapanda milima unafanya kazi karibu katika kila nyanja nyingine zote za maisha na biashara ikiwemo. Waliofanikiwa kimaisha kila sekta wanacho kitu cha kufundisha kwa wale ambao bado hawajafanikiwa kufikia levo zao. Waliofanikiwa kwenye kilimo mathalani wanajua mbinu na maarifa mengi yahusuyo kilimo na bila shaka yeyote ikiwa ndio unaanza shughuli ya kilimo huna budi kuwatafuta ili wakupe ujuzi huo. Halikadhalika na kwa waliofanikiwa kielimu, waliofanikiwa kibiashara nk.

Ni dhahiri kabisa kuwa sisi binadamu hatuna kabisa muda wa kutosha hapa Duniani kujifunza kila kitu kutokana na makosa tutakayofanya katika mchakato wa kusaka mafanikio. Wakati mwingine inabidi kutafuta njia za mkato(shortcut) na njia hiyo si nyingine bali ni  ile ya kujifunza kutoka kwa wengine ambao walishawahi kupitia hali na mazingira yanayofanana na yale unayojiandaa kukutana nayo au ambayo tayari unakutana nayo.

Hapa kuna mjadala wa wale wanaodai kuwa mtu unapaswa kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa tu na wengine hudai mtu unaweza kujifunza kutoka kwa wote, wale waliofanikiwa na hata kutoka kwa wale walioshindwa kwa mantiki  kubwa kwamba hata waliofeli nao wanacho cha kufunza kwani utajifunza kukwepa yale yaliyowafanya washindwe kufanikiwa kusudi usirudie makosa yao tena.

SOMA: Kwanini kufanikiwa kifedha si dhambi na ni kwanini kila mtu anatakiwa afanikiwe.

Makosa mengi yanaepukika kirahisi kwa kujifunza njia wengine walizotumia kuyatatua. Unapojifunza, jifunze kutoka kwa watu wenye mtazamo chanya na uzoefu ndipo utajijengea mazingira yaliyokuwa imara kabla haujaanzisha kile unachokusudia kuanzisha.

JINSI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WALIOFANIKIWA
Kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa au walio na uzoefu wa kutosha siyo jambo gunu. Dhana hii hubeba maana tofauti kulingana na mtazamo wa kila mtu. Kwa mfano wapo wanaowaita wale wanaoigwa au waaliofanikiwa kama ‘mamentor’, makocha, ‘role models’ nk. na hata unaweza usiwaite jina lolote lakini ikabakia tu kuwa wewe unafuata mfano wa mtu fulani aliyewahi kupitia njia unazotamani na wewe uzipitie kusudi uweze kutimiza ndoto yako ya maisha kutegemeana na ni kwa namna gani unavyojibu swali la mafanikio ni nini. Mafanikio pia yanaweza yakawa na maana tofauti kutegemea mtu na mtu.

Wajasiriamali waliofanikiwa kwa mfano pamoja na wasanii mashuhuri duniani ndio wanaoongoza kuwa na wafuasi wengi wanaoiga mifano yao(role models). Kufuata mfano wa mtu siyo lazima uonane naye ana kwa ana mzungumze hapana, zipo njia nyingi ikiwemo hata kusoma na kutazama taarifa zake kutoka vyombo mbalimbali vya habari na vitabu.

SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka. 

Hasahasa vitabu imekuwa ni njia nzuri sana ya watu  kuiga mifano ya watu maarufu na waliofanikiwa. Watu kama kina Bill Gates, Warren Buffet, George Weah, Ronaldo, Messi, Barack Obama, Alli Kiba, Ophra Winfrey, Wema Sepetu, Said Salim Bakhressa, Diamond, Reginald Mngi, Mohamed Dewji na wengineo wengi.Wote hawa wasingeliweza kumfikia kila mtu mmojmmoja anayehitaji kufuata mifano yao isipokuwa kwa njia ya vyombo vya habari, vitabu na magazeti.

Chagua mtu wako wa kujifunza kutoka kwake na siyo lazima awe ni mtu maarufu, kuna hata watu wanaochagua kujifunza kutoka kwa wazazi wao au ndugu zao wa karibu waliokwishapitia uzoefu fulani au mafanikio.
………………………………………………….

Ndugu msomaji wa makala hii, hata wewe na mimi pia tunavyo vitu, uzoefu au maarifa watu wengine wayoweza kuiga kutoka kwetu. Mimi binafsi kwa mfano, nina uzoefu wa miaka zaidi ya 12 katika biashara ya rejareja hususani DUKA LA REJAREJA.
Yeyote sasa anayefikiria kuanzisha au tayari anayo biashara ya DUKA au biashara yeyote ile ya rejareja, hana haja tena ya kutumia zaidi ya miaka yote hiyo 12 akijifunza ni kipi kinachofanya kazi na ni kipi kisichofanya kazi. Tayari nimeweka uzoefu wangu wote katika kitabu unachokiona hapo chini baada ya maelezo haya.

Njia ya haraka sana ninayoweza kutuma kitabu hiki kwako ni kwa kupitia email kama softcopy(PDF). Bei ni sh. Elfu 5 tu na zinatumwa kupitia namba za simu 0712202244  au  0765553030 jina Peter Augustino Tarimo

Ikiwa pia utataka kitabu cha karatasi, hardcopy unaletewa mpaka ulipo kwa sh. Elfu 12 ukiwa Dar es salaa. Mikoani agiza mtu  anayekuja dar akuchukulie.

SIMU:         0712202244
WASSAP: 0765553030

TUPO:      Mbezi kwa Msuguri karibu na stendi.0 Response to "JINSI YA KUPATA MAFANIKIO MAISHANI: USIPANDE MLIMA BILA KIONGOZI"

Post a Comment