UAMUZI UNAOTUMIKA KUJISHINDIA MILIKI KUBWA YA UTAJIRI WA MALI NA ROHO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UAMUZI UNAOTUMIKA KUJISHINDIA MILIKI KUBWA YA UTAJIRI WA MALI NA ROHO

THINK AND GROW RICH 8iv
Mwishowe baada ya siku kadhaa za malumbano alisimama tena na kutamka kwa sauti thabiti iliyoeleweka. “Bwana Rais tumejadili suala hili kwa siku kadhaa sasa. Ipo njia moja tu sisi kuifuata. Kwanini sasa Mheshimiwa tunachelewa zaidi? Kwanini basi tulumbane? Acha siku hii njema izae Jamhuri ya Amerika. Iache iinuke, na siyo kuteketea na kutwaa kwa nguvu, bali kuanzisha upya utawala wa amani na wa kisheria. Macho ya Ulaya yanatutazama sisi. Inataka kutoka kwetu mfano hai wa uhuru ambao unaweza kuthibitisha tofauti katika furaha kuu ya mwananchi kwa uonevu unaozidi kuongezeka.”

Kabla hoja yake mwishowe haijapigiwa kura, Lee aliitwa kurudi Virginia kutokana na sababu nzito ya kuuguliwa katika familia. Lakini kabla hajaondoka aliacha madaraka mikononi mwa rafiki yake, Thomas Jefferson ambaye aliahidi kupigana mpaka hatua zinazofaa zimechukuliwa. Muda mfupi baadae Rais wa Baraza (Hanckoc) alimchagua Jefferson kama Mwenyekiti wa Kamati ya kuandaaa tangazo la Uhuru.

Kwa udi na uvumba Kamati ililifanyia kazi andiko ambalo lingeweza kumaanisha  wakati litakapokubaliwa  na Baraza kwamba, KILA MTU ALIYESAINI, INGELIWEZA KUWA ANASAINI HATI YAKE MWENYEWE YA KIFO ikiwa makoloni yangeshindwa katika mapambano na Uingereza kitu ambacho kilikuwa dhahiri kutokea.

Andiko liliandikwa na mnamo tarehe 28 June rasimu ya awali ilisomwa mbele ya baraza. Kwa siku kadhaa ilijadiliwa, kubadilishwa na kuwa tayari. Mnamo tarehe 4 Julai 1776, Thomas Jefferson alisimama mbele ya baraza na bila ya woga akasoma uamuzi wa maana zaidi  kuwahi kuwekwa kwenye karatasi.

“Katika mwenendo wa matukio ya binadamu ni muhimu kwa watu fulani kukata utepe wa kisiasa ambao umewaunganisha pamoja na kuchukulia miongoni mwa tawala za dunia, kituo sawa na kinachojitegemea ambacho sheria za asili, na za Mungu wa asili aliwapa, heshima nzuri kwa maoni ya wanadamu huhitaji kwamba wanapaswa kutangaza sababu inayowasukuma kwenye utengano…”

Jefferson alipomaliza, mswada ulipigiwa kura, ukakubaliwa na kutiwa saini na watu 56, kila mmoja akihatarisha maisha yake juu ya uamuzi wake wa kuandika jina lake. Kwa uamuzi huo, lilizaliwa Taifa lililokusudia kumletea binadamu daima upendeleo wa kufanya maamuzi. Kwa maamuzi yanayofanywa  katika roho kama hiyo ya imani, na ni kwa maamuzi hayo tu, watu wanaweza wakatatua matatizo yao binafsi na kujishindia wenyewe milki kubwa ya utajiri wa mali na roho, hebu  tusilisahau hili!

Changanua matukio yaliyosababisha tangazo la uhuru, na ushawishike kwamba Taifa la Marekani lilizaliwa kutokana na uamuzi uliofanywa na kundi la kushauriana lililokuwa na watu 56. Zingatia vizuri ukweli kwamba ilikuwa ni uamuzi wao uliohakikisha mafanikio ya jeshi la Washington kwa sababu roho ya uamuzi ule ilikuwa ndani ya moyo wa kila mwanajeshi aliyepigana pamoja naye na kuwa kama nguvu ya kiroho isiyotambua kitu kinachoitwa kushindwa.  


Zingatia pia(kwa faida binafsi kubwa) kwamba nguvu iliyoipa Marekani Uhuru wake ni nguvu ileile ambayo ni lazima itumike na kila mtu anayejitambua. Nguvu hii imetengenezwa kwa kanuni zilizoelezwa kwenye hiki kitabu. Katika simulizi ya tangazo la Uhuru haitakuwa vigumu kugundua angalao sita ya hizi kanuni: SHAUKU, UAMUZI, IMANI, UVUMILIVU, KUSHAURIANA, na MPANGO MADHUBUTI.


 CHAGUA SURA NA SEHEMU ZOTE ZILIZOKWISHAWEKWA

0 Response to "UAMUZI UNAOTUMIKA KUJISHINDIA MILIKI KUBWA YA UTAJIRI WA MALI NA ROHO"

Post a Comment