KUKU WA NYAMA BROILERS: KWANINI FAIDA NA GHARAMA ZA UFUGAJI ZINAVUNJA MOYO?

KWANINI KUKU WA NYAMA FAIDA YAKE INAVUNJA MOYO?
Kabla sijaanza mada hii ya leo ya kwanini ufugaji wa kuku wa nyama maarufu kama Broilers wana faida kidogo sana, hebu kwanza nizungumzie kwa kifupi kuhusiana na soko la mazao mbalimbali ya kilimo na mazao ya mifugo. Miongoni mwa maswali mengi ninayokutana nayo kutoka kwa wasomaji wa blogu hii ni haya hapa chini.

NITAPATA WAPI… Soko la kuku wa nyama, soko la nyanya, soko la sungura, soko la matikiti maji, soko la mahindi, soko la kuku na mayai ya kienyeji, soko la mananasi, soko la choroko, soko la kuku wa mayai, soko la pilipili hoho nk. orodha ni ndefu lakini kwa bahati mbaya sana waulizaji wengi wa maswali haya huuliza wiki chache, moja au 2 tu kabla ya mazao yao kuvunwa au kuingizwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa.


Kwa kweli utaona kwa mtindo kama huo, ni dhahiri kabisa kuwa kilimo na ufugaji ambavyo ndiyo injini ya viwanda tunavyoimba kila siku zitaendelea kuonekana ni biashara kichaa kila siku wakati shughuli za kilimo na ufugaji ni miongoni mwa biashara zenye fursa kubwa na nzuri ambazo bado kabisa hazijaguswa, fursa endelevu ya kutengeneza pesa au hata ya mtu kuweza kupata utajiri wa haraka kuliko kwenda kupoteza senti zako chache kwa kucheza kamari.

Kanuni kuu ya biashara ni hii hapa; LIJUE VIZURI SOKO LA BIDHAA/HUDUMA ZAKO KABLA HATA HAUJAANZA KUIFANYA BIASHARA ULIYOKUSUDIA KUIFAYA. Fanya kwanza utafiti(feasibility study). Kufanya utafiti wa soko la biashara yako kumeelezwa vizuri sana katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, nashauri ikiwa hujui namna ya kufanya utafiti na una wazo la kuanzisha biashara au kiwanda kidogo basi kitafute kitabu hicho bei yake ni shilingi elfu 10 tu, unapata softcopy yake utakayoisoma kama unavyosoma sasa hivi hapa.

KWANINI UFUGE KUKU WA NYAMA, NA NI KWELI HAWANA FAIDA AU WATU WANATIA CHUMVI TU KUKUKATISHA TAMAA HUKU WAO WAKITENGENEZA HELA?
Biashara ya ufugaji wa kuku wa kisasa kwa ujumla ni biashara yenye sifa zifuatazo, Ni biashara kwanza inayohitaji mtaji wa uhakika(capital intensive) hapa nitafafanua kidogo, simaanishi kila anayeanza basi anatakiwa kuwa na mtaji mkubwa sana hapana, bali namaanisha kuwa unapoianzisha basi uwe na uhakika idadi unayoanza nayo una kiasi cha mtaji unaotosha kuwahudumia mwanzo mpaka mwisho bila ubabaishaji wowote ule sijui leo umewapa pumba, kesho magimbi ya kuchemsha, keshokutwa kiporo cha ugali, hapana.  Bajeti yake ya chakula na vifaa vyote uwe nayo kabisa mkononi si ya kuungaunga.


Sifa nyingine ya biashara hii ni ‘very risky’ au kwa maneno engine ina hatari kubwa, kosa kidogo tu unaweza ukala hasara ya mwaka ukalaani kabisa ufugaji wa kuku wa kisasa. Hapa elimu na maarifa mbalimbali yanahitajika kukabiliana na hilo. Na sifa ya tatu kuku wa kisasa nikiwa na maana ya kuku wa mayai na kuku wa nyama wana faida kubwa sana, ni miongoni mwa miradi duniani inayolipa ajabu!. Mbali na sifa hizo nyingine mbili hapo juu ufugaji wa kuku wa kisasa unaweza ukakufanya kuwa milionea katika muda ambao watu wanaweza wakahisi umeshukiwa na muujiza.

KWANINI UFUGE KUKU WA NYAMA?
·       Bei ya vifaranga wa kuku wa nyama sokoni siyo kubwa sana ukilinganisha na aina nyinginezo za ufugaji wa kuku kama vile kuku wa mayai(layers) na kuku chotara.
·       Mabanda ya kuku wa nyama huchukua nafasi ndogo, kuku mpaka 10 katika square metre 1 ya mraba, hata maeneo yaliyobanana sana mijini kama dar e s salaa mtu anaweza akafuga bila wasiwasi.
·       Chakula cha kuku wa nyama ni rahisi hata mtu kutengeneza mweyewe ikiwa unajua kanuni(formula) ya uchanganyaji wa chakula cha kuku wa nyama. Isitoshe kuku wa nyama hawali chakula mifuko mingi sana kipindi chote cha ukuaji wao kutokana na kipindi hicho kuwa ni kifupi, wiki 4 mpaka 6 tu. Kwa ujumla ulishaji wa kuku wa nyama ni rahisi.
·       Biashara ya kuku wa nyama sokoni haisumbui sana ikiwa utawakuza kuku wako katika uzito unaokubalika sokoni. Hutapata washindani wengi kwani kuku ni bidhaa inayopendwa sana duniani na huliwa na kila mtu.
·       Faida na mapato ya kuku wa nyama ijapokuwa ni kidogo lakini kutokana na muda mfupi faida hiyo inayochukua mpaka kupatikana kwake bado ni biashara inayolipa na ni nzuri.

NI KWELI UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA UNAKATISHA TAMAA?
Binafsi mimi hilo nalipinga kuku wa nyama si kweli kwamba faida yake inakatisha tamaa, kwanza kitu watu wengi wasichofahamu ni kwamba katika biashara yeyote ile kuna gharama kuu za aina mbili, zile za kuanzishia biashara ambazo unanunulia vifaa na miundombinu yote kwa ujumla, halafu kuna zile gharama za uendeshaji za kila siku ambazo ndizo hubainisha faida ya mradi kila siku.


Sasa watu wengi hutegemea baada ya msimu mmoja tu wa ufugaji wa kuku wa nyama waweze kurudisha gharama zote hizi mbili jambo ambalo ni gumu na lisilowezekana, labda iwe ni katika mazingira fulani fulani tu ambayo nimeyazungumzia vyema katika moja ya mchanganuo kwenye kifurushi cha michanganuo 3 niliyoandaa spesho kwa mfugaji yeyote yule makini wa kuku wa aina zote.(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS). Kifurushi hiki nilichokizindua wiki hii kina mipango ya biashara ya kuku mitatu, kuku wa kisasa wa mayai, kuku wa kienyeji wa mayai na kuku wa kisasa wa nyama.

Umewahi kufanya biashara ya kuuza vocha zasimu za mkononi? Vipi faida yake, ndogo au kubwa? Ili upate faida nyingi unapaswa kufanya nini? Uuze kiasi kikubwa siyo. Na kuku wa kisasa ni hivyo hivyo, wanalika sana kwa hiyo isingelikuwa rahisi  faida yake iwe kubwa sana vinginevyo kila mtu angekimbilia kufuga na isingekuwa biashara tena. Katika ulimwengu wa viwanda kuna kitu wanaita, economies of scale,Wachina kwa mfano ujanja huu huutumia sana, Mchina akigundua bidhaa ina soko kubwa na la uhakika atadili nayo kwa udi na uvumba kuizalisha kwa wingi kiasi ambacho ile faida ndogondgo inayoingia hatimaye hulundikana upesi na kugeuka utajiri mkubwa.


Nimefanya makusudi kuandaa mpango wa kuku 100 wa nyama na wala siyo 500 au 1000. Katika mchanganuo huo wa kuku 100 tu unaonyesha ipo faida lakini kwa mtu anayetaka mafanikio ya usiku mmoja ni lazima atajiunga katika lile kundi la wanaobeza ufugaji wa kuku wa kisasa wa nyama akidai ni biashara kichaa isiyokuwa na faida. Ukifanikiwa kuuona jaribu kuucheki mchanganuo huo vizuri kwani umechambuliwa kwa umakini wa hali ya juu baada ya ubishani mkali na wanaopinga biashara hii.

Biashara ni mahesabu bwana asikuongopee mtu, na usipoyapiga vizuri utaishia kusema haina faida, mahesabu hapa simaanishi calculus hapana, simple maths, hesabu za kichwa ambazo hata darasa la nne anamudu kuzifanya.

Katika kifurushi hiki cha (MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) kila mchanganuo uliokuwemo ndani una upekee wake, kimezima kabisa kiu ya maswali yote yanayohusiana na biashara ya ufugaji wa kuku wa aina mbalimbali kama vile;

·       Gharama za kuanzisha miradi ya kuku
·       Faida, hasara na mapato ya ufugaji wa kuku kwa ujumla
·       Nitaanza na kuku wangapi wa mayai?
·       Nataka kufuga kuku wa kienyeji mtaji nianze na shilingi ngapi?
·       Kuku wa mayai wa kienyeji kwa mwaka hutaga mayai mangapi?
·       Kuku wa mayai na kuku wa nyama ni yupi aliye na faida zaidi.
·       Kuku wa mayai tangu kifaranga mpaka kuuzwa gharama yake ni shilingi ngapi?
·       Nikiwa na laki tatu mchanganuo wa kuku wa kienyeji upoje?
·       Gharama za ufugaji wa kuku chotara aina ya kuroila ni kiasi gani?
·       Nifuge kuku wa kienyeji au wa kisasa?


Michanganuo yote 3 ipo katika mfumo wa softcopy(PDF). PDF ya mchanganuo wa ufugaji wa kuku wa mayai, PDF ya kuku wa kienyeji na mchanganuo wa tatu ni ufugaji wa kuku wa kisasa wa nyamaPDF. Kila mchanganuo bei yake ni shilingi elfu 10 lakini kwa idadi yangu ya watu wa mwanzo nitawapa kifurushi hiki kizima kwa bei ya ofa ya shilingi elfu 10 tu. Idadi yangu ikitimia kila mchanganuo utauzwa peke yake kwa bei ya kawaida ya sh, elfu 10.

Offa nyingine kubwa nitakayotoa kwa idadi yangu maalumu ya wateja wa mwanzo watakaonunua kifurushi cha MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS ni offa ya kuunganishwa bure kwenye kundi langu la kushauriana la WHATSAPP(MASTER MIND GROUP)  ambalo kila siku tunashauriana na kujadiliana maswala mbalimbali kuhusu miradi yenye fursa kubwa, michanganuo ya biashara bunifu, na njia za kuongeza mizunguko ya fedha katika biashara zetu. 

Ndani ya group pia unapata masomo yote (complete course on business planning) kwa kiswahili rahisi, pamoja na masomo mengine ya ziada yanayotolewa kila siku usiku kupitia wasap, Vitabu mbalimbali pamoja na templates/vielezo vya mpango wa biashara unavyoweza kujaza maneno yako tu ukakamilisha kuandika mpango wa biashara yako kwa njia rahisi na ya haraka.


Kumbuka ada ya kawaida ya kujiunga na group hili bila ofa ni sh. 10,000/=. Mle utakutana na magwiji katika tasnia ya ufugaji kuku, uombe ushauri gani usishauriwe? Ma experts kama kina Frank Mapunda watakaokufundisha  ABC zote za biashara ya uuzaji na ufugaji wa kuku wa aina zote kitaalamu. Ofa hiyo nayo haitadumu muda mrefu ni ya kuwahi mapema.

.................................................................

Ukihitaji vitabu vyetu mbalimbali tembelea SMARTBOOKSTZ

SIMU:   0712202244

Wasap: 0765553030 
JINA:    Peter Augustino Tarimo


Makala hii pia ipo jamii forum

0 Response to "KUKU WA NYAMA BROILERS: KWANINI FAIDA NA GHARAMA ZA UFUGAJI ZINAVUNJA MOYO?"

Post a Comment