SIKU YA 5 TAREHE 29/12/2022 KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UPENDO CAFE HATUA KWA HATUA (MPANGO WA FEDHA) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SIKU YA 5 TAREHE 29/12/2022 KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UPENDO CAFE HATUA KWA HATUA (MPANGO WA FEDHA)

hesabu za cafe
8.0 Mpango wa Fedha

Katika mwaka wa kwanza mauzo yetu kwa mwezi yanakadiriwa kuwa shilingi milioni 8.8, katika kipindi hiki tunatarajia kuuza mchanganyiko wa vyakula ikiwemo supu, chapati, wali, ugali, chipsi nk. Kwa ujumla katika kipindi chote cha miaka 3 tunatarajia kutengeneza faida nzuri

Kama zilivyo Sura nyingine zote zilizopita hii nayo kuna muhtasari mdogo unaogusa zile sehemu muhimu za Sura yote kama unavyoona hapo juu. Lakini kabla hatujaendelea hebu kwanza tuone ni vipengele gani vidogo vinavyounda sura nzima ya fedha;  

8.1 Dhana/makisio muhimu

8.2 Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama (Break Even Analysis)

8.3 Makisio ya faida na hasara

8.4 Makisio ya mtiririko wa fedha

8.5 Makisio ya mali na madeni (mizania ya biashara)

8.6 Sehemu muhimu za biashara 

8.1 Dhana/Makisio muhimu

Kwenye makisio muhimu unaorodhesha vile vigezo (assumptions) utakazotumia katika kuamua hesabu zako ziwe vipi. Kwa mfano ukuaji wa mauzo mwaka wa pili na wa tatu upendo wametumia asilimiaa 50%, haya ni makisio (assumptions) kulingana na tafiti walizofanya.

Pia kukisia vitu kama wafanyakazi wangapi mwaka wa kwanza, kodi ya mapato na riba ya mkopo kama mpango huu ungehusisha mkopo pia vyote hivyo ni makisio muhimu ambayo yangelipaswa kuandika hapa kwa kifupi kusudi msomaji wa mpango huu atambue hesabu zimefikajefikaje hapa zilipo na wala hazikutokea tu hewani.

Upendo assumptions zao ni hizi;

·      Makisio ya mauzo kwa siku = 294,500/=

·      Wastani wa Gharama za mauzo kwa siku = 215,750/=

·      Mahitaji ya fedha za mtaji ni shilingi Milioni 3

·      Uchakavu wa vifaa kwa mwezi = 39,400/=

·      Kodi ya mauzo kwa mwaka asilimia 30%

·      Mauzo yetu yote ni kwa fedha taslimu hakuna kukopesha

·      Uchumi imara usiokuwa na misukosuko mikubwa

 

8.2 Tathmini ya Mauzo yatakayorudisha Gharama zote kwa mwezi (Break Even Analysis)

 “Break Even Analysis” ni tathmini ya kiasi cha mauzo yanayohitajika ili kurudisha gharama zote zilizotumika katika kipindi fulani, inaweza ikawa mwezi, mwaka au kipindi kingine chochote kile ila mwezi ndiyo hutumika mara nyingi zaidi. 

Namba zote zinazotumika kwenye tathmini hii zinapatikana kutoka katika jedwali la Ripoti ya Faida na Hasara, hivyo ni vizuri kuifanya tathmini hii baada ya kukamilisha jedwali hilo.  

Ili kukokotoa Mauzo hayo tutahitaji kuwa na vitu 3 muhimu vifuatavyo;

·      Wastani wa gharama za kudumu kwa mwezi

·      Asilimia ya Gharama za mauzo kwenye mauzo

·      Kanuni ya kukokotoa mauzo hayo(Break even Formula)

Katika jedwali la Faida na Hasara mwaka wa kwanza, wastani wa gharama za kudumu kwa mwezi ni zile gharama za uendeshaji kwa mwezi ambazo katika jedwali la upendo ni shilingi 914,200 baada ya kugawanya za mwaka kwa miezi 12

 

Asilimia ya Gharama za mauzo kwenye Mauzo, walichukua jumla ya gharama zinazobadilika za mauzo sh. 77,670,000 kutoka katika jedwali la makisio ya faida na hasara mwaka wa kwanza kisha wakagawa kwa Mauzo ambayo ni sh. 106,020,000/=  Hizi ukichukua za mwezi au za mwaka asilimia utapa hiyohiyo moja ambayo walipata ni asilimia 73% au 0.73

Kanuni ya kukokotoa “Break Even Sales” zipo nyingi kulingana na data/taarifa unazopewa, kwa mfano hapa tayari tuna mauzo, gharama za mauzo na gharama za kudumu; 

Kimsingi kabisa kanuni zote za kukokotoa Break even point hutokana na kanuni kuu ifuatayo;

Faida = Mauzo – Gharama za mauzo – gharama za kudumu 

 

(Nikisema Break Even sales namaanisha Mauzo ya kurudisha gharama zote zilizotumika yaani Mauzo yamelingana na gharama, hamna faida wala hasara). Hivyo;

FAIDA = 0

Kutokana na kanuni hiyo ndipo tunapata;

Break even sales = Gharama za kudumu /1-gharama za mauzo/Mauzo au


 
Break even Analysis

Na hiyo ndiyo kanuni Upendo waliyotumia kukokotoa mauzo hayo.

Ukipachika namba tulizoona pale juu jibu lake utapata = shilingi 3,385,926/=                          

 

Chati ya mauzo ya kurudisha gharama (Break even chart)

Chati ya mauzo hayo hutengenezwa kwa kutumia data za “Mauzo vs Faida” na data hizi zinapatikana kwa kutumia kanuni (formula) ile pale juu; 

Faida = Mauzo – Gharama za mauzo – gharama za kudumu

Lakini kumbuka kila thamani ya gharama za mauzo kulingana na data zao pale juu ni asilimia 73% au 0.73 ya Mauzo 

Hivyo Fomula yetu itakuwa kama ifuatavyo 

 Faida = Mauzo – 0.73Mauzo – 914,200

Baada ya hapo katika kila chumba kwenye jedwali la mauzo vs faida walitafuta thamani ya faida na kutengeneza jedwali la Mauzo vs Faida;

Chukulia  kwamba hakuna mauzo hivyo weka 0 kwenye sehemu ya mauzo na ukokotoe faida itakuwa sh. Ngapi,

Faida = 0 - 0.73(0) – 914,200 =  – 914,200

Kisha endelea kuweka namba za mauzo chukulia sasa labda umeuza milioni 5

Faida = 5,000,000 - 0.73(5,000,000) – 914,200 = 435,800

Kisha utaendelea kufanya hivyohivyo kwa milioni 10, 15 nk. Mwishoni utapata kiasi cha faida kwa kila mauzo utakayoweka halafu sasa utachora chati yako na kuangalia ni wapi faida inakuwa zero(0) na hapo ndipo mauzo ya kurudisha gharama zote yalipo. Ukicheki vizuri utaona faida ikiwa 0 mauzo ni   3,385,926/= nilipozungushia duara,  sawa na jibu la kwenye formula yetu lilivyosema.                        

Jedwali: Mauzo vs Faida

Mauzo

Faida

0

-914,200

5,000,000

435,800

10,000,000

1,785,800

15,000,000

3,135,800

20,000,000

4,485,800

25,000,000

5,335,800

30,000,000

7,185,800

35,000,000

8,535,800

40,000,000

9,885,800

 

 

 

 Chati: Mauzo ya kurudisha gharama zote(BES)

Break even analysis

 8.3 Makisio ya Faida na Hasara.

Katika ripoti hii ya faida na hasara unatumia hesabu ndogondogo ambazo zimeshajitokeza kwenye vipengele vingine vya mchanganuo huu huko nyuma. Ukichunguza mchanganuo wetu huu tangu mwanzoni mpaka sasa utagundua kuna sehemu kadhaa hesabu zimejitokeza kwa mfano kwenye

·      Sura ya ‘5.0’ kipengele kidogo cha 5.3.1 Makisio ya Mauzo na  na gharama za mauzo halafu

·      Sura ya sita Uendeshaji kipengele kidogo ch 6.4 Vifaa na Mashine (Uchakavu) na 6.5 Makisio ya mauzo kwa undani

·      Sura ya 7 Uongozi na Wafanyakazi (Mishahara)

Katika Makisio ya faida na hasara kuna vitu vikubwa 5 vifuatavyo,

1)  Mauzo

2)  Gharama za mauzo (zinazobadilika)

3)  Gharama za uendeshaji(za kudumu)

4)  Kodi

5)  Faida halisi

Kuna majedwali ya faida na hasara mawili, moja ni la miezi yote 12 na la pili ni la mwaka wa kwanza lakini unaweza ukakisia na miaka miwili inayofuata. Upendo walianza na jedwali la miezi 12 kwa kuchora safu za kusimama(columns) za miezi yote 12 pamoja na safu za kulala (rows) zenye vile vitu 5 bilivyotaja pale juu.

Walichora jedwali la Faida na hasara kwa miaka 3 kama ifuatavyo na kuweka namba za mwaka wa kwanza ambazo zote tumeshaona zimepatikana hapo juu kisha walikadiria mauzo ya mwaka wa kwanza na wa pili kwa kutumia njia ya asilimia. Ukuaji wa mauzo ni asilimia 50% hivyo walichukua 50% na kuzidisha mara mauzo ya mwaka wa kwanza halafu jibu wakajumlisha na mauzo hayo ya mwaka wa kwanza ili kupata mauzo ya mwaka wa pili.

Mauzo ya mwaka wa tatu halikadhalika walizidisha ya mwaka wa 1 kwa 50% kisha jibu wakajumlisha na mauzo hayo kupata ya mwaka wa 3

Gharama za mauzo kwa miaka ya 2 na 3 ni rahisi walichukua tu asilimia 73 ya mauzo kama ilivyo mwaka wa 1

Gharama za uendeshaji kwa mwaka wa kwanza tayari zipo kukisia za miaka ya 2 na 3 unatumia tu akili ya kuzaliwa kwa kufikiria iwapo mauzo yatakua kwa asilimia 50 vitu kama umeme na vifaa  vya usafi ni lazima vipande kidogo pengine kwa asilimia 50% nk. Msishahara itapanda kwani wafanyakazi wataongezwa, kod ya pango nayo itapanda mwala wa 3

Baada ya kumaliza walikokotoa faida halisi mwishoni kwa kila mwaka miaka yote 3


 Jedwali: Faida na hasara kwa miaka 3

 

 

Mwaka 1

Mwaka 2

Mwaka 3

 

Tsh.

Tsh.

Tsh.

Mauzo

106,020,000

159,030,000

238,545,000

Gharama za mauzo

77,670,000

116,505,000

174,757,500

Faida Ghafi

28,350,000

42,525,000

63,787,500

Faida ghafi %

27%

27%

27%

 

Gharama za uendeshaji

 

 

 

Mishahara

7,200,000

10,800,000

10,800,000

Kodi ya Pango

1,800,000

1,800,000

2,400,000

Uchakavu

470,400

470,400

470,400

Matangazo na promosheni

360,000

500,000

1,200,000

Umeme na maji

240,000

360,000

360,000

Vifaa vya usafi

360,000

720,000

1,200,000

Ushuru wa taka

60,000

60,000

60,000

Dharura

480,000

500,000

1,000,000

Jumla gharama za uendeshaji.

10,970,400

15,210,400

17,490,400

Faida kabla ya riba na kodi

17,379,600

27,314,600

46,297,100

Riba

0

0

0

Kodi ya mapato 30%

5,213,880

8,194,380

13,889,130

Faida halisi

12,165,720

19,120,220

32,407,970

Faida halisi/Mauzo%

11.5%

12%

14%

 

Baada ya hapo walianza kutengeneza jedwali la Faida na hasara kwa miezi 12 ya mwaka wa kwanza kama ifuatavyo;

Kwanza kama unakumbuka tulipokisia mauzo ya siku, mwezi na mwaka tulisema mauzo ya siku yalikuwa ni shilingi 294,500/= Hivyo katika miezi 12 mauzo hayataweza kutokana na sababu mbalimbali kama vile miezi mingine ni ya likizo watu si wengi sana mjini, kuna miezi ya mvua  nk, kwa hiyo ni lazima kila mwezi uupe mauzo yake kulingana na jinsi ulivyotafiti mauzo yako yatakuwaje.

Mfano Upendo mwezi wa kwanza kwa kuwa walikuwa wakianza walikadiria mauzo kuwa kidogo chini ya wastani ule wa tuliopata kwa siku wa sh. Milioni 8 kwa siku na kuweka milioni 6.8 Pia ukicheki miezi ya likizo kama June, Julai na Novemba mauzo yatashuka kidogo wakati miezi kama ya 4, 10 na 12 yenye pilika nyingi mauzo yapo juu

Jedwali lake lina mistari iliyosimama columns (12) na mistari iliyolala(rows) inayolingana na vitu 5 nilivyotaja pale juu,mauzo, gharama zote na mwishoni faida halisi. Kila mwezi unapewa mauzo yake na gharama kulingana na makisio ya mauzo na gharama kwa siku tulizopata wakati wa makisio ya Mauzo sura ya 5 lakini pia utazingatia vigezo vingine kama likizo, miezi ya mvua nk.

Lifuatalo ni jedwali la faida na hasara kwa la Upendo kwa miezi 12 lakini hapa tumeweka tu miezi 5 kwanza, ukitaka kuona miezi yote 12 tazama mchanganuo wa Upendo Cafe.

 

Makisio ya Faida na hasara miezi 12

Mwezi1

Mwezi 2

Mwezi 3

Month4

Mwezi 5

Tsh.

Tsh.

Tsh.

Tsh.

Tsh.

Mauzo.

6,800,000

7,500,000

8,000,000

9,200,000

9,100,000

Gharama za mauzo

4,964,000

5,475,000

5,840,000

6,716,000

6,643,000

Faida ghafi

1,836,000

2,025,000

2,160,000

2,484,000

2,457,000

Faida ghafi %.

27%

27%

27%

27%

27%

 

Gharama za uendeshaji.

Mishahara

600,000

600,000

600,000

600,000

600,000

Kodi ya pango

150,000

150,000

150,000

150,000

150,000

Uchakavu

39,200

39,200

39,200

39,200

39,200

Matangazo na promosheni

30,000

30,000

30,000

30,000

30,000

Umeme na maji

20,000

20,000

20,000

20,000

20,000

Vifaa vya usafi

30,000

30,000

30,000

30,000

30,000

Ushuru wa taka

5,000

5,000

5,000

5,000

5,000

Dharura

40,000

40,000

40,000

40,000

40,000

Jumla

914,200

914,200

914,200

914,200

914,200

Faida kabla ya riba na Kodi

921,800

1,110,800

1,245,800

1,569,800

1,542,800

Riba

0

0

0

0

0

Kodi ya mapato 30%

276,540

333,240

373,740

470,940

462,840

Faida halisi

645,260

777,560

872,060

1,098,860

1,079,960

%Faida halisi

9.5%

10%

11%

12%

12%

 

Baada ya ripoti hii ya Faida na Hasara hufuata ripoti nyingine 2 ile ya Mtiririko wa fedha taslimu, Mizania ya biashara(Rasilimali na Madeni) pamoja na Sehemu muhimu (Ratios), ni rahisi kuziandaa kwani taarifa nyingi hutokana na taarifa hii. 

.......................................................

Ili kupata Somo hili zima kwa ukamilifu wake, jiunge na Mastermind Group la MICHANGANUO-ONLINE au ujipatie kitabu kipya kiitwacho; 

SANAA & SAYANSI YA UPISHI WA CHAPATI LAINI

Ada ya group kwa mwaka ni sh. elfu 10, unapata na offa ya vitabu na Michanganuo bure.

Kujiunga lipia kwa namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe wa "NIUNGE NA MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITABU"

0 Response to "SIKU YA 5 TAREHE 29/12/2022 KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UPENDO CAFE HATUA KWA HATUA (MPANGO WA FEDHA)"

Post a Comment