KANUNI ZA MAFANIKIO(THE SUCCESS PRINCIPLES) BY JACK CANFIELD | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KANUNI ZA MAFANIKIO(THE SUCCESS PRINCIPLES) BY JACK CANFIELD

Kanuni za mafanikio na Jack Canfield
Hakuna msomaji yeyote yule mzuri wa vitabu vya hamasa, fedha na mafanikio asiyemfahamu Jack Canfield, mwandishi na mhamasishaji mashuhuri aliyewahi kuandika kitabu kingine tena maarufu sana kijulikanacho kama “ChickenSoup for the Soul”(Supu ya kuku kwa ajili ya roho).

Katika kitabu chake hiki cha Kanuni za mafanikio(The Success Principles) Canfield anakupa kanuni 65 zitakazoyabadilisha kabisa maisha yako. Kanuni hizi zinaweza zisiwe mpya au ngeni kwako, pengine ulishawahi kuzisoma au kuzisikia mahali pengine lakini kwasababu ni vitu unavyohitaji kujikumbusha na kuvirudia mara kwa mara kusudi uweze kuyatimiza malengo yako uliyojiwekea maishani, sidhani kama zitakuchosha kuzisoma.

Kanuni hizi, Jack Canfield alijifunza wakati akiwa kwenye safari yake kuelekea kuwa mjasiriamali aliyefanikiwa, mwandishi mashuhuri wa vitabu, kocha na mzungumzaji mahiri. Sehemu 6 za kitabu hicho zitabadilisha kabisa mtazamo wako wa maisha uliokuwa nao na kuwa mtu wa kuchukua usukani wa maisha yako mwenyewe, hivyo kuweza kutoka pale ulipokuwa sasa kwenda pale unapotaka uwe.

pesa hamasa na mafanikio

Jack anakuamba hivi; “Kile watu wengine wanachofikiri kuhusiana na wewe hakikhusu kabisa

Mwisho anakupa masomo haya matatu muhimu sana;

1.  Acha kulalamika
2.  Jitengee wiki-endi moja kumalizia viporo vyako vyote vya kazi ulizokuwa hujamalizia.
3.  Unaweza kufa kwa mawazo hasi, hivyo jitahidi kufikiri chanya.

Ni kanuni rahisi na za kawaida sana lakini zenye nguvu kubwa na zinazoweza kufanya maajabu katika maisha ya mtu yeyote yule anayeamua kuzitumia.





0 Response to "KANUNI ZA MAFANIKIO(THE SUCCESS PRINCIPLES) BY JACK CANFIELD"

Post a Comment