TAFUTA PESA ILIMRADI TU HUVUNJI SHERIA KWANI HATA NYOTA ANGANI KILA MOJA HUNG’AA KWA NAFASI YAKE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TAFUTA PESA ILIMRADI TU HUVUNJI SHERIA KWANI HATA NYOTA ANGANI KILA MOJA HUNG’AA KWA NAFASI YAKE

TAFUTA PESA UHESHIMIKE, HAMNA WA KUKUZUIA KAMA ZILIVYO NYOTA HAZIZUIANI KUNGAA ANGANI

Mpendwa msomaji wangu Karibu tusome makala ya leo isemayo; 

TAFUTA PESA ILIMRADI TU HUVUNJI SHERIA ZA NCHI WALA ZA MUNGU KWANI KAMA ZILIVYO VYOTA ANGANI HUWEZI KUZUIA WALA KUZUIWA NA WATU WENGINE  KUPATA PESA. MAFANIKIO NI HAKI YA MTU YA MSINGI 

 

Hivi uliwahi kusikia pamoja na nyota angani kuwa mamilioni ipo siku hata nyota moja ilimzuia mwenzake kung’ara? Hata pamoja na kwamba Jua kuna kipindi inasemekana hupatwa na Dunia lakini hali hiyo uliwahi kusikia imedumu hata kwa siku mbili au tatu?

Sasa kwanini uanze kuhofia eti mwenzako akifanikiwa kama wewe mafanikio yako yatashuka? Au ili wewe ufanikiwe ni lazima kwanza uhakikishe mwenzako aliyefanikiwa unamshusha kwanza chini kwa kutumia mbinu zozote zile hata ikiwezekana kuutoa uhai wake?

Pamoja na kwamba waswahili husema, Tafuta pesa uheshimike na kuna mpaka nyimbo zimewahi kuimbwa redioni tafuta pesa uringe lakini haimaanishi kwamba ukishapata pesa basi wewe ndiyo ujifanye Mungu mtu hapana, pata pesa heshimika, pendwa na kila mtu, ringa lakini pia usijaribu kuzuia wengine nao kupata pesa kama wewe, wala usijaribu kuwashusha wale waliokuzidi kifedha ili wawe kama wewe.

Ukweli mchungu ni huu hapa; kitu kimoja binadau tunashindwa kufahamu ni kwamba ikiwa kila mtu duniani humu angelikukuwa na mafanikio basi dunia isingelishindwa kuhimili, wala rasilimali zilizopo zisingelimalizika kisa eti kila mmoja wetu amefanikiwa.

Lakini jambo la kustaajabisha mno ni kwamba juhudi za watu wengi iwe masikini au hata baadhi ya matajiri mara zote kwenye akili zao wamekuwa wakipoteza muda mwingi wakiwaza jinsi ya kuwashusha chini wenzao, (majirani, marafiki, ndugu na jamaa) wale waliowazidi kidogo kimafanikio ama kuwazuia walio chini yao kupanda juu. Utafutaji pesa wa jinsi hii unavunja si sheria za nchi tu bali hata na zile alizoziweka Mwenyezi Mungu katika vitabu vyake vitukufu.

Sikatai kwamba ushindani ule wenye tija haukatazwi mfano unaona mwenzako kajenga nyumba kali nzuri na wewe unajitahidi kufanya kazi kwa juhudi zote kusudi na wewe ujenge yakwako kali zaidi, laki si ule ushindani wa kuona jirani kalima mahindi yake shambani yamestawi vizuri na wewe eti unavizia na kagiza unakwenda kuyakatakata kwa upanga ili umkomoe yeye ashuke na wewe upande juu.

Ukweli ni kwamba mafanikio yako yanapaswa yapimwe na ni kwa jinsi gani umeweza kuwasaidia wenzako kwa kuwekeza kwao, na siyo tu ni mara ngapi umewapa chakula au mahitaji ya msingi. Fikiria umewahi kuwapa binadamu wenzako fursa au kuwawezesha na wao waweze kupata mafanikio kama yakwako mara ngapi na siyo wamewahi kuja kwako mara ngapi kuomba kibaba cha unga wa kupikia ugali. Ukimpa unga leo wa ugali kesho na kesho kutwa shida zake zipo palepale, je hapo umemwezesha?

Bora kipi, kuacha ‘legacy’ duniani kwa vizazi na vizazi baada ya kufa kwako mfano kina Hayati Mzee ReginaldMengi, Mwalimu Julius Nyerere, Steve Job, Mahatma Ghandi na wengineo au kuacha duniani majumba marefu, madebe ya pesa, magari ya kifahari na kila aina ya utajiri? ...................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

Mpenzi msomaji wangu somo hili lijulikanalo kama; THE SKY IS VERY WIDE, EVERY STAR CAN, ni refu na bado halijamalizika. Ili kupata somo zima lililokamilika jiunge na mimi leo tarehe 29/05/2023  usiku saa3 kwenye darasa letu maalumu la watsap

Masomo haya maalumu ya pesa yasiyopatikana mahali pengine popote pale nje na ndani ya mtandao (exclusive) hutolewa kila siku saa 3 ndani ya group la Michanganuo-online. Washiriki ni mtu yeyote mwenye kiu ya kujifunza kwa kina masomo ya fedha na Michanganuo ya biashara

Ukijifunza kuchanganua biashara nakuhakikishia umejifunza kila kitu kuhusiana na biashara kwani mpango wa biashara ni jumla ya kila kipengele kinachounda biashara nzima kuanzia Mtaji, masoko, Mauzo, hesabu zote za biashara, bidhaa/huduma, uongozi na hata changamoto na fursa ndani ya biashara husika.

Kupata nafasi ya kujifunza masomo haya kila siku unalipia ada ya mwaka mzima shilingi 10,000/= tu kupitia namba zetu; 0712202244  au  0765553030 jina Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe watsap au SMS usemao;

“NIUNGE GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA MPYA YA VITU 12”

Nitakuunganisha mara moja kwa group pamoja na kukutumia OFFA yako ya vitu 12 vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali papo hapo kama ifuatavyo;

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)


Makala hii imeandikwa na:

Peter Augustino Tarimo

Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara aina zote

(Get a comprehensive, customized Business Plan that fits your unique vision, goals and challenges)

Phone/Watsap: 0765553030 au 0712202244




Unaweza kusoma na hizi pia:

1. Kwanini kufanikiwa kifedhasi dhambi na kila mtu anastahili afanikiwe

2. Elimu ya fedha na umuhimu wake 

3. Huna mtaji wa kutosha,hukopesheki? Jaribu njia hii ya kufunga mkanda (Bootstrapping)  

4. Biashara 7 nzuri za kufanyamwaka huu, chagua moja uingize kipato cha ziada kwa urahisi

 


0 Response to "TAFUTA PESA ILIMRADI TU HUVUNJI SHERIA KWANI HATA NYOTA ANGANI KILA MOJA HUNG’AA KWA NAFASI YAKE"

Post a Comment