NILIVYOJIFUNZA KUWA HOFU HAIJAWAHI KUTATUA TATIZO LA PESA KWA MTU YEYOTE YULE MAISHANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NILIVYOJIFUNZA KUWA HOFU HAIJAWAHI KUTATUA TATIZO LA PESA KWA MTU YEYOTE YULE MAISHANI

Mtu mwenye hofu na fedha

Hivi ulishawahi kuvutwa nyuma na nguvu hasi wakati ukilenga kufanikisha jambo lako fulani kubwa na muhimu maishani mfano pale ambapo watu walikuwa wamekukatia tamaa kabisa na kusema kamwe hautaweza kuyashinda magumu yaliyokuwa mbele yako, walakini kitu cha ajabu kabisa kikatokea na ukaweza kuvuka salama wasalimini kila mtu akabaki anashangaa!!! 

Je wajua ni nguvu gani hiyo iliyochangia wewe  kuvuka kizingiti hicho na ni kwa namna gani hufanya kazi? Tafadhali ungana na mimi hapa mpaka mwisho wa somo hili.

Nazungumzia uzoefu niliowahi kuupitia mwenyewe binafsi na wala siyo hadithi. Miaka kadhaa iliyopita kuna kipindi nilikabiliwa na deni lililoniumiza sana kichwa lakini mwishowe nilifanikiwa kulitatua tatizo lile kwa njia ya kustaajabisha sana kiasi kwamba mpaka leo hii sijaelewa kama ilikuwa ni muujiza, bahati au ni kitu gani.

Nilikuwa na biashara niliyokuwa nikiifanya kwenye fremu ya kukodi hapahapa jijini Dar es salaam. Muda wa kulipia upya kodi ya pango la fremu hiyo ulikuwa umewadia na mwenyenyumba hakuwa na chembe ya huruma, alikuwa anataka kodi  yake akawalipie wanawe ada ya shule.

Nilitakiwa kulipa shilingi laki tisa (900,000/=) kodi ya miezi 6. Wakati huohuo sikuwa na fedha na biashara ilikuwa imedorora kiasi ambacho sikuwa na uwezo hata wa kununua bidhaa kwa ajili ya kuuza pale dukani.

Sababu za kudorora kwa biashara hiyo zilitokana na matatizo mengine ya kifamilia yaliyokuwa yakiniandama ikiwemo ugonjwa. Tegemeo langu kubwa lilikuwa ni mkopo katika benki moja ambayo tayari nilishakuwa mteja wao kwa karibu mwaka mmoja. Nilikuwa ndiyo namalizia mkopo wa zamani niliokuwa nimekopa wa shilingi milioni moja, nikapanga safari hii kwenda kukopa shilingi milioni mbili kusudi niweze kulipa kodi ya watu laki 9 na zinazobakia milioni moja na laki moja niongeze bidhaa katika biashara yangu kama mtaji.

Mkopo wa zamani niliokuwa namalizia nilikuwa nimedhaminiwa na mtu mmoja ambaye alikuwa anamiliki kampuni moja na safari hii nilikuwa nimepanga tena kumuomba aendelee kunidhamini. Sikuwa na mashaka yeyote kuwa angeweza kunitosa kwani katika marejesho sikumsababishia usumbufu wa aina yeyote ile, nilirejesha kila mara rejesho kamili na kwa wakati.

Nilimueleza mdhamini wangu azma yangu hiyo, akanijibu hakuna shida yeyote ile, niendelee tu na process za benki siku ikifika nimjulishe tuende akanisainie kama kawaida.

Niliendelea na harakati zangu huku hali ikizidi kuwa ngumu kipesa, biashara ilikuwa imezorota kiasi kwamba wateja walikuwa wakiniuliza ni wapi nilikuwa nimepeleka mtaji. Muda huo wote ijapokuwa matatizo yalikuwa mengi lakini sikupoteza kabisa matumaini, niliamini kuwa ningetatua tatizo lile la pesa vyovyote vile hata kama benki wangeamua kunitosa. Niliifundisha akili yangu kwamba nilikuwa na uwezo wa kupata kiasi cha shilingi milioni 2 na kutatua matatizo yaliyokuwa yananikabili.

Wakati nikiwa naendelea na mchakato wa kuprocess ule mkopo, pale mtaani ulizuka uvumi mbaya kuwa, eti mimi nilikuwa  na mpango wa kuifunga ile biashara  kisha nihame mji kurudi kijijini  na mkopo niliotaka kuomba benki nilikuwa na njama za kukimbia nao kisha nimwachie yule mdhamini jumba bovu akahangaike nalo.

Mdhamini kusikia vile alianza kuingiwa na wasiwasi, nikamwona mara akija kwa yule mwenye nyumba wangu wakiteta jambo nisilolijua na kisha kuondoka zake. Baadae nilikuja kubaini kumbe vile vilikuwa ni vikao vya kunijadili mimi kwamba nataka kumuingiza mdhamini wangu choo cha kike kwa kumwachia deni la benki.

Mwenye nyumba naye kwa upande wake alianza kunionyesha wazi kuwa hakuwa ananihitaji tena pale akanipa notisi ya mwezi mmoja niwe nimemwachia chumba chake. Kule benki niliendelea na process kama kawaida, nikakamilisha makaratasi yote huku nikifocus kupata pesa ingawa nilishaanza kuingiwa na woga kiasi fulani juu ya mdhamini wangu. Hata hivyo nilijitahidi sana kupuuzia hofu ile.

Siku mbili kabla ya siku ya kwenda kusaini mikataba ya mkopo, nilimpigia simu mdhamini wangu, kwanza simu iliita weee…..bila majibu. Nikaamua kumtumia meseji baadae akanijibu kuwa hakukuwa na tatizo lolote na siku ya kusaini fomu atafika tukutane benki. Hapo tena wasiwasi ulitaka kuninyemelea lakini nikapiga moyo konde na kusema, “Nitapata milioni 2 nitatue matatizo yanayonikabili” Niliziona milioni mbili nikiwa nimezishika kwa mikono yangu akilini.

Jioni ya kuamkia siku ya kwenda kusaini nilipompigia simu mdhamini ili kumkumbusha, simu yake ilikuwa imezimwa kabisa. Bado pamoja na hayo sikuruhusu kabisa kuchanganyikiwa japo nilifahamu fika fedheha ambayo ningeweza kwenda kuipata benki baada ya kuulizwa mdhamini wako yuko wapi.

Nikajipa moyo kuwa mpaka kesho yake asubuhi kama asingepatikana kwenye simu basi ningejihimu asubuhi sana nyumbani kwake kabla hata hajakwenda ofisini japo nyumbani kwake palikuwa mbali nikajue hatma ya suala lile.

Asubuhi nilijaribu tena kumpigia simu safari hii akapokea na kunihakikishia kuwa saa nne asubuhi muda afisa wangu alioniambia tuende atakuwa amewasili benki. Niliwahi pale benki saa 2 na nusu nikakuta hata maafisa wenyewe wa benki bado hawajafika, kulikuwa na walinzi tu.

Mpaka majira ya saa tano asubuhi mdhamini wangu alikuwa hajaonyesha dalili zozote za kufika pale benki nikaamua tena kumtumia meseji, “upo wapi mkuu” akanijibu hivi, “Nimepata safari ya dharura, wewe nenda tu wakupe  mkopo halafu mimi kesho au keshokutwa nitafika hapo kusaini hizo fomu”

Badala ya kupatwa na mshituko nilishangaa ni kwa vipi benki inaweza kukupa mkopo kisha mdhamini aje siku yeyote ile anayotaka yeye kuja kukusainia makaratasi. Hata pamoja na hivyo bado akili yangu mpaka nukta ile ilikuwa timamu, ikilenga tu kupata milioni 2 siku ileile hata kama mdhamini asingetokea, sikuamini kabisa kama ningekosa ule mkopo.

Majira ya saa saba za mchana yule afisa wangu naye alianza kuingiwa na wasiwasi akaniita na kuniomba nimpe simu ili aongee na yule mdhamini moja kwa moja kujua tatizo lilikuwa wapi. Majibu ya mdhamini kwa afisa wa benki yalikuwa ni yaleyale aliyonipa mimi, “Mpe hela mimi nipo safarini nitafika kesho au keshokutwa kuja kusaini hizo fomu” akakata simu.

Hatma ya mkopo wangu sasa ilibakia mikononi mwa yule afisa na uongozi wa benki. Punde kidogo afisa aliniita chemba akaniuliza, “kwani imekuwaje tena bro?” Nikamjibu, “hata mimi nashangaa sielewi kwani tangu juzi tumekuwa tukiwasiliana na leo asubuhi kanihakikishia tutakutana hapa benki” 

Majibu yangu kwa yule afisa niliyatoa kwa ujasiri mkubwa bila kuonyesha hofu wala wasiwasi wowote ule, na hadi leo hii bado nashangaa ule ujasiri ulitoka wapi……………...........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

Ndugu msomaji wa makala hizi, makal hii isemayo; NILIVYOJIFUNZA KUWA HOFU HAIJAWAHI KUTATUA TATIZO LA PESA KWA MTU YEYOTE MAISHANI  bado haijamalizika na itaendelea leo hii tarehe 30/May 2023 saa 3 usiku ndani ya Darasa letu la kila siku la MICHANGANUO-ONINE.

Mtu yeyote yule anakaribishwa kujiunga darasa hili la watsap kwa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu mwaka mzima. Kila siku tunakuwa na somo jipya la kipekee kuhusiana na pesa au michanganuo lisilopatikana kwingine kokote.

Ukilipia tunakupatia na masomo mengine yote yaliyopita tangu darasa lianze huku ukiendelea kupokea masomo mapya kila siku. Darasa hili jipya limeanza rasmi jana tarehe 29/5/2023

Tunakupatia na offa ya vitabu na michanganuo ya biashara jumla vitu 12 free bila kulipa pesa ya ziada papo hapo ukilipia elfu 10.

Ili kulipa ada yako tumia namba; 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo kisha ujumbe usemao; “NATAKA OFFA YA VITU 12 NA KUUNGWA GROUP JIPYA LA MASOMO”

 

VITU 12 VYA OFFA NI HIVI VIFUATAVYO;

 

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABUMichanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu. – kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABUNjia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado millingkwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)

 

Karibu tukutane darasani leo usiku saa 3 tarehe 30/5/2023

 

Somo hili limeandaliwa na:

Peter Augustino Tarimo

Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara aina zote

(Get a comprehensive, customized Business Plan that fits your unique vision, goals and challenges)

Phone/Watsap: 0765553030 au 0712202244


 

SOMA NA HIZI HAPA PIA:

1. Ukisoma hapa hutokaa tena uwalaumu benki au taasisi za fedha.

2. Kutumia nyumba, kiwanja au ardhi kama rehani kupata mkopo ni sahihi? Naomba ushauri

3. Naanza utumishi Januari, nifanyeje kuwa huru kifedha au nikakope? 

4. Jinsi wanavyochukua hatari kubwa kwenye biashara wanavyofanikiwa haraka.

 

0 Response to "NILIVYOJIFUNZA KUWA HOFU HAIJAWAHI KUTATUA TATIZO LA PESA KWA MTU YEYOTE YULE MAISHANI"

Post a Comment