SEMINA SEHEMU YA 2 MCHANGANUO: UFUGAJI KUKU CHOTARA AINA YA KROILER (MUHTASARI, BIDHAA & BIASHARA) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA SEHEMU YA 2 MCHANGANUO: UFUGAJI KUKU CHOTARA AINA YA KROILER (MUHTASARI, BIDHAA & BIASHARA)

Semina kuku kuroiler siku ya 2
Katika Sehemu ya pili ya semina yetu masomo yanaanza rasmi saa 3 usiku na tumechanganua mambo matatu kama utakavyoona. Hapa katika Blogu hii ya Jifunzeujasiriamali najitahidi kuweka dondoo tu za semina na siyo semina nzima kama ilivyokuwa kwenye group maalumu. Unaweza kuona baadhi ya sentensi kuna deshi-deshi-deshi.............kuashiria kwamba kuna maelezo hayajakamilika. 

Kuna mambo mengi unaweza usiyajue ikiwa hukushiriki moja kwa moja katika hii semina, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na rejea, nikimaanisha Kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali pamoja na Mchanganuo kamili wa biashara yetu ya ufugaji wa kuku wa kuroiler kwa ajili ya nyama.

Tunaanza kwa sauti (voice note) kama uonavyo hapo chini kisha maelezo ya kawaida kwa ujumbe wa maandishi huku washiriki wenye maswali wakiruhusiwa kuuliza maswali yao muda wowote wapendao.

VOICE NOTE-1:

Baada ya kufanya utafiti wako katika mambo mbalimbali kuhusiana na biashara ya ufugaji wa kuku wa kuroiler, sasa hivi utakuwa na taarifa za kutosha kuweza kuandika mchanganuo wako bila wasiwasi.

Sehemu hii tunajifunza vipengele vitatu (3) vifuatavyo;

1.   MUHTASARI

2.   MAELEZO YA BIASHARA/KAMPUNI

3.   MAELEZO YA BIDHAA

Sehemu ya 1 kama utakumbuka nilisema huko mbele kila kipengele tutakifafanua kwa undani zaidi nikimaanisha tuta ainisha vipengele vidogovidogo vinavyounda kipengele kikubwa

1.0 MUHTASARI:

Unaweza mahali pengine ukakuta wameita Muhtasari Tendaji, majina yote mawili ni sawa tu.

Katika Muhtasari kitu cha kustaajabisha kidogo ni kwamba, ndiyo kipengele cha kwanza cha mchanganuo wa biashara lakini huwa kinaandikwa mwishoni kabisa baada ya mtu kumaliza kuandika vipengele vingine vyote na hii hutokana na sababu kwamba Muhtasari unabeba zile sehemu muhimu zote katika andiko lako zima. Unachagua zile sentensi zenye uzito katika kila kipengele.

Kwa mfano katika mchanganuo wetu huu bunifu wa biashara ya kuku wa nyama wa kroiler, kwenye muhtasari ni lazima pamoja na pointi nyinginezo tusiache kipengele kinachihusiana na ubunifu tutakaouweka katika hii biashara

Ni lazima Muhtasari wako umshawishi msomaji kwani mabosi wengine mfano kwenye mabenki na taasisi mbali mbali za fedha hawana muda wa kusoma andiko lako zima.

Kazi kubwa za Muhtasari ni zipi?  

1.   Kutoa picha kwa ufupi ya andiko lako zima kwa kuangazia maeneo yote muhimu.

2.   Kumpa msomaji wa mpango wako uelewa wa jumla wa kile unachotaka kumueleza kabla hata hajasoma andiko lenyewe zima

3.   Kumpa yule msomaji asiyekuwa na muda mwingi wa kusoma mchanganuo wako wote ufupisho utakaomsaidia kupata zile pointi muhimu. 

Urefu wa Muhtasari tendaji haupaswi................

 

2.0 MAELEZO YA BIASHARA/KAMPUNI

Maelezo kuhusu Biashara au kampuni kwa kiasi kikubwa yanahusu taarifa za ndani ya biashara zaidi kuliko kutoka nje ya biashara. Hapa chini naorodhesha vipengele vidogo nitakavyozingatia wakati nikiandika kipengele hiki kikubwa, kwa ujumla tutatoa maelezo kulingana na vipengele hivi vidogo. Siyo lazima kuandika juu ya kila kipengele kwani itategemea biashara inahitaji kitu gani, kama kitu hakina umuhimu hupaswi kukiweka 

2.1 Dhamira kuu (mission)

2.2 Vision (Maono)

2.3 Malengo (Objectives)

2.4 Siri za mafanikio 2.5 Umiliki

2.6 Jina

2.7 Usajili

2.8 Kianzio

2.9 Eneo na vifaa vilivyopo. 

Aya ya kwanza inayoanza na namba “2.0 Maelezo ya biashara/kampuni” huandiki chochote kwanza, panabaki wazi  kwani ni muhtasari mdogo wa vipengele hivyo vingine vidogo vidogo chini yake. 

Kumbuka katika kila kipengele kikubwa ni vizuri kikawa na muhtasari wake mdogo ambao baadae ndio unaokuja kuunganishwa na mihutasari kutoka vipengele vingine kuunda Muhtasa Tendaji tulioona pale juu mwanzoni  

“2.1 Dhamira kuu”

Dhamira kuu ni ile biashara unayoifanya. Kwa mfano sisi hapa kwenye mpango huu wa Kuroiler tumesema hivi;,

CPPC Dhamira yetu kuu ni ................................................”

2.2 Maono

Maono ni picha ya biashara yako unayotaka uione baada ya kipindi fulani kupita, mfano ya kwetu hapa inasema hivi;

“Ku........................................................................................”                                                                                   

2.3  Malengo

Hapa tunataja vile vitu tunavyokusudia kuvitimiza baada ya kutekeleza mpango wetu. Malengo mazuri ni lazima yawe halisi, yanayopimika, yenye kutekelezeka na yaliyokuwa na muda maalumu wa utekelezaji. Hebu tuone baadhi ya malengo ya CPPC hapa chini;

·   Kuanza na idadi ya kuku 300 chotara kwa ajili ya nyama na kisha kuja kuongeza kuku wa mayai hapo baadae mtaji ukikua

·      Kuuza ..................................................................

·      Kutoa .................................................................... 

·      Kupata ..................................................................

·       Kuhakikisha .........................................................

2.4 Umiliki wa biashara

Hapa tunataja jina la biashara yetu ambalo ni CHOTARA POULTRY PRODUCTION (CPPC), jina la mmiliki ambaye ni Amina Abdalla Katika kipengele hiki kidogo, tutataja pia aina ya umiliki wa biashara ambapo ni biashara ya mtu mmoja

2.5 Siri za mafanikio (Keys to success)

Katika siri za mafanikio tutataja vile vitu ambavyo biashara inatarajia kuvipa kipaumbele kusudi iweze kufanikiwa, vyaweza kuwa ni kitu chochote kile na hapa sisi tumevitaja vitu ifuatavyo ............................................................................... nk. unaweza kusoma vyote kweye mchanganuo wako  wa biashara ya kuku chotara wa nyama aina ya Kuroiler.

2.6 Mchango katika jamii na kwa uchumi wa Taifa

Hapa tumeelezea manufaa wanayoyapata watu mbalimbali kutokana na biashara hii mfano ajira, kilimo kutokana na mbolea itakayopatikana nk.

2.7 Eneo la Biashara

Unalitaja hapa mfano kwa upande wetu ni ................................................... taja vitu muhimu kama ukubwa ni square meter ngapi za eneo, majirani waliopakana, vitu muhimu kama shule, hospital ink vilivyo karibu na mradi vinavyoweza kuchangia ukuaji au maendeleo ya biashara yako

2.7 Kianzio

Hii ni biashara mpya na hivyo tunatakiwa kuorodhesha kwenye jedwali mahitaji yote tukianza na .......................... mfano ......................., kisha ........................................ kama ............................................................................ Namba tutakazozitumia hapa zitatokana na utafiti ule tulioufanya pale mwanzoni mfano ...............................................................

Baada ya kumaliza sasa tutarudi pale mwanzoni katika aya tuliyoiacha wazi kwenye namba “2.0 Maelezo ya Biashara.” Ilipoanzia sura yetu hii. Tutachagua katika kila kipengele kidogo tulichokwisha andika mstari mmojammoja au maneno muhimu na kuyapanga katika hii aya kutengeneza muhtasari mdogo wa kipengele au sura nzima.

Inaendelea..........................

 

3.0 MAELEZO YA BIDHAA / HUDUMA

Katika sura ama kipengele hiki cha maelezo yanayohusu bidhaa au huduma, hapa unatakiwa utoe maelezo yanayohusu kile kitu biashara yako inachouza.

Kwa biashara yetu hii ya ufugaji wa kuku aina ya Kuroiler kiubunifu bidhaa zetu kubwa ni .................................. Lakini pia unaweza kuuza hata .................................................................. 

Kama ilivyo kwa vipengele vingine vikubwa vinavyounda mpango mzima wa biashara, hiki nacho kina vipengele vyake vidogovidogo kadhaa ambavyo ndivyo huunda sura nzima au kipengele kikubwa. Vipengele hivyo vidogo ni hivi hapa chini; 

3.1 Maelezo ya bidhaa/huduma

3.2 Utofauti/upekee wa bidhaa/huduma na za washindani

3.3 Vyanzo vya malighafi/bidhaa

3.5 Teknolojia

3.6 Bidhaa / Huduma za baadae 

Kwahiyo maelezo yetu kwenye kipengele hiki yanajikita katika mada hizo ndogondogo hapo juu. Hata hivyo siyo sheria wala lazima kuweka vipengele vyote kwenye Sura yako, unaweka tu kipengele unachoona kinafaa kulingana na mazingira ya biashara yako yalivyo lakini angalao kuna vipengele kwa mfano “Maelezo yenyewe ya bidhaa/huduma" ni lazima yawepo.  

Kama tunavyoona kwenye mchanganuo wetu huu wa kuku wa Kuroiler kwa ajili ya nyama, maelezo ya bidhaa yanahusu .......................................................lakini pia, wateja na bei ya ............................................ Kwa upande wa bidhaa ya................................tumetaja wateja wake ni kina nani, kiasi cha bidhaa itakayozalishwa na bei yake

Unaweza pia badala ya kuelezea kila kipengele kidogo ukaandika maelezo mafupi tu (Muhtasari) kuhusiana na bidhaa zako kama aya mbili au tatu hivi. Lakini katika maelezo hayo hakikisha yanagusa sifa muhimu za huduma au bidhaa zako pamoja na upekee wake.


Hapa ndiyo mwisho wa sehemu ya 2 ya semina yetu , tukutane tena Sehemu ijayo

Asanteni sana kwa kusoma

Peter Tarimo

 

Ikiwa unahitaji semina hii nzima bado hujachelewa jiunge leo hii kwa kulipia kitabu na mchanganuo wako wa Kuroiler sh. elfu 10 tu kupitia namba zetu 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo kisha ujumbe watsap au sms usemao “NATAKA SEMINA YA KUROILER NA OFFA YA VITU 6”

Kisha mara moja nitakutumia Kitabu chako cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali kilichosheheni kila kitu mjasiriamali anachohitaji kufanya biashara ya kisasa lakini pia nitakutumia michanganuo mbalimbali ya Offa kama ifuatavyo;

1.   Mchanganuo wa kuku wa nyama( Tumaini Broilers)-kiingereza

2.   Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

3.   Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili

4.   Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

5.   Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

6.   Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) -kiswahili

Kila siku masaa mawili mpaka matatu kabla ya kuanza semina kwenye group maalumu huwa nawahi kwa madhumuni ya kuwafundisha kwanza wale waliochelewa kuanza, haijalishi mtu ulichelewa muda gani lakini nakunoa ili uweze kufikia viwango walivyofikia wenzako.

Staili niitumiayo ni kama ile iliyotumika na Napoleon Hill kwenye kitabu chake cha THINK & GROW RICH katika kundi lake la kushauriana(Master-Mind) na washauri wa kufikirika katika Sura ya 14 (MLANGOFAHAMU WA 6). Ukiisoma sura hii vizuri utaelewa ni nini ninachojaribu kukielezea hapa.

 


SEMINA SEHEMU YA 1                SEMINA SEHEMU YA 3





SOMA NA HIZI HAPA PIA:

1.   Gharama za ujenzi wa banda la kuku 100 chotara au kienyeji ni shilingi ngapi?

2.   Nina mtaji wa shilingi milioni moja (1000,000), naomba ushauri nitafanya biashara gani?

3.   Nguvu ya ajabu aliyotumia huyu mtoto unaifahamu?

4.   Chapati biashara ya mtaji mdogo inayohitaji ujuzi mkubwa

5.   BIashara ndogo ya mtaji wa 80,000/= niuze nini kupata faida ya haraka?

0 Response to "SEMINA SEHEMU YA 2 MCHANGANUO: UFUGAJI KUKU CHOTARA AINA YA KROILER (MUHTASARI, BIDHAA & BIASHARA)"

Post a Comment