NGUVU YA AJABU ALIYOTUMIA HUYU MTOTO UNAIFAHAMU? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NGUVU YA AJABU ALIYOTUMIA HUYU MTOTO UNAIFAHAMU?

Mtoto aliyefanya maajabu

Habari za muda huu mpenzi msomaji wa blogu ya jifunzeujasiriamali

Ni matumaini yangu unaendelea vizuri, leo nimekuletea somo moja kutoka kitabu cha Think and Grow Rich somo ambalo wakati mwingine tumekuwa sisi wenyewe tukilitumia kati harakati zetu za kimaisha kila siku hasa kiuchumi.

“Hapana” siyo lazima imaanishe kuwa jambo haliwezekani.”

Hivi ni ni mara ngapi umewahi kukutana na neno hili HAPANA? Basi hebu tuendelee kusoma nisijemaliza uhondo bure………!

Siku moja mchana mtu mmoja aitwaye Darby alikuwa akimsaidia mjomba wake kusaga ngano kwenye kinu cha zamani. Mjombake alikuwa na shamba kubwa ambalo ndani yake waliishi wakulima wadogowadogo waliokodisha sehemu ya shamba hilo. Taratibu mlango ulifunguliwa, na mtoto mdogo aliingia, alikuwa ni binti mdogo wa mmoja kati ya wale waliokodisha shamba,(wapangaji) aliingia ndani na kuketi karibu na mlango.

Mjomba alipotazama na kumuona yule mtoto alimpayukia kwa kelele,

“Unataka nini”

Kwa unyenyekevu yule mtoto alimjibu,

“Mama yangu anaomba umtumie senti hamsini”

“Sitamtumia” Mjomba alimjibu kwa ukali. “Sasa hivi uondoke nyumbani” “Sawa Baba” Mtoto alimjibu lakini wala hakusogea.

Mjomba aliendelea na kazi yake, huku akizama kwenye kazi kiasi kwamba hakukumbuka tena uwepo wa yule mtoto. Alipotazama na kumuona akiwa bado amesimama pale, alimpigia kelele tena,

“Nilikuambia uende nyumbani! Sasa ondoka au nitakuchapa” Yule binti alijibu “Ndiyo Baba", lakini tena hakusogea hata inchi moja. Mjomba alidondosha chini gunia la nafaka ambalo alikuwa anakaribia kulimimina kwenye kinu cha nafaka, akachukua kipande cha fimbo na kuanza kumfuata yule mtoto huku usoni akiashiria alikuwa ameghadhabishwa mno.

Darby aliyekuwa ameketi pembeni aliishiwa na pumzi, bila shaka alihisi alikuwa karibu kushuhudia mauaji ya mtoto mdogo. Alitambua mjombaake alikuwa ni mtu wa hasira kali. Mjomba alipofika pale mtoto alipokuwa amesimama, mtoto haraka alisogea mbele hatua moja, akamuangalia machoni na kupiga yowe mpaka mwisho wa sauti yake nyembamba, “NI LAZIMA MAMA YANGU APATE HIZO SENTI HAMSINI”

Mjomba alisimama akamtizama kwa dakika moja, kisha taratibu akakiweka kile kipande cha fimbo chini, akaweka mkono mifukoni akachomoa nusu dolla na kumpatia.

Mtoto alizichukua zile pesa, na taratibu akarudi kuelekea mlangoni, kamwe hakuyatoa macho yake kwa mjomba, mtu ambaye punde alikuwa amemshinda. Baada ya kuwa ameishaondoka, mjomba aliketi chini juu ya boksi na kutazama nje kupitia dirishani kwa zaidi ya dakika 10. Alikuwa akitafakari kwa heshima iliyochanganyikana na hofu juu ya pigo alilokuwa amelipata toka kwa yule mtoto mdogo.

Bwana Darby, naye pia alikuwa akiwaza. Hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia mtoto mdogo wa mpangaji  kwa makusudi akimfunza mtu mzima mwenye madaraka.

Je, yule mtoto aliwezaje kufanya vile?

Ni kitu gani kilichomfanya mjomba hasira kali zimtoke na kuwa mpole kama mwanakondoo?

Ni nguvu gani ya ajabu aliyotumia yule mtoto iliyomfanya mjomba kusalimu amri mbele ya huyu mtoto?

Maswali haya na mengine kama hayo yalimulika ndani ya akili ya Darby, lakini hakuweza kupata majibu mpaka miaka kadhaa baadaye alipokuja kusimulia hii habari.

Jibu la swali hili litapatikana kwenye kanuni 13 zilizoelezewa ndani ya kitabu cha THINK AND GROW RICH(FIKIRI & UTAJIRIKE). Jibu ni zima na lililokamilika. Lina maelezo ya kina na maelezo yanayotosheleza kumfanya mtu yeyote aelewe na kuitumia nguvu kama hiyo hiyo aliyoitumia mtoto mdogo kwa bahati tu pasipo yeye mwenyewe kufahamu kama anaitumia.

Nguvu hii isiyoweza kuzuilika mtu yeyote yule anaweza akaitumia katika kutimiza ndoto yake yeyote ile katika maisha iwe ni kupata utajiri, au hata mafanikio katika Nyanja ninginezo za kimaisha.

Kuna watu wengi wamewahi kuitumia Nguvu hii na wakafanya maajabu hapa duniani wakiwemo kina Henry Ford, Marcon, Wright Brothers , Thomas Edison na wengineo.

 

Ndugu msomaji Karibu sana kwenye group letu, tayari jana tumeanza rasmi usomaji wa kitabu cha Think & Grow Rich, kitabu chenye majibu ya mambo mengi magumu yanayotutatiza katika maisha yetu ya kila siku.

Unaweza kufuatilia kitabu cha kiingereza PDF au Audio Book ambavyo vyote tunavitoa bure kwenye group au ukaamua kufuatilia nakala ya kiswahili ambayo unaweza kuipata kwa bei ya punguzo kwenye mtandao wa GETVALUE

Kujiunga na Mastermind Group hili, lipia ada ya mwaka mzima shilingi elfu 10 tu ambapo utapata na offa ya vitu 22, Vitabu, Michanganuo na Seminars. Lipa kupitia namba 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe usemao, “NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22” namimi nitakuunganisha na kukutumia kila kitu muda huohuo.

Offa hii imeongezewa muda kutokana na maombi ya wengi wa wadau wetu mliosema muda ulikuwa hautoshi. Itaendelea kwa muda mfupi kabla haijaondolewa hivyo ni vizuri kuwahi mapema.

Ndani ya Mastermind Group la Michanganuo-online mbali na usomaji wa hiki kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE pia tunazo programu nyingine mbalimbali zinazolenga kumjengea uwezo mjasiriamali mdogo na wa kati hasa kwenye eneo la kumiliki mtaji wa uhakika kwenye biashara zake hata ikiwa hana dhamana za kutosha kukopa mahali.

 

OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO INAYOISHIA KARIBUNI NI HII HAPA CHINI;

 

                      1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

                      2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

                      3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

                      4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

                      5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

                      6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

                      7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

                      8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

                      9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

                    10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

                    11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

                    12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

                    13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

                    14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

                    15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

                    16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

                    17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

                    18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

                    19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

                    20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

                    21.    KITABU CHA SEMINA: Masomo 11 ya  michanganuo ya Biashara

 

                    22.    KITABU CHA SEMINA: Hesabu za mpango wa biashara kwa kina(Advanced Business Plan Financials)

 

0 Response to "NGUVU YA AJABU ALIYOTUMIA HUYU MTOTO UNAIFAHAMU?"

Post a Comment