TULIVYOANZA USOMAJI WA KITABU THINK AND GROW RICH-SURA YA KWANZA-UTANGULIZI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TULIVYOANZA USOMAJI WA KITABU THINK AND GROW RICH-SURA YA KWANZA-UTANGULIZI

usomaji-sura ya-1 think and grow rich

Habari za jion hii Wanamichanganuo-oline wenzangu,

 

Natumaini  sote tupo poa.

 

Ni wangapi tumemaliza kusoma Utangulizi wa Fikiri & Utajirike(Think & Grow Rich?

 

Ni wangapi tumesoma nakala ya kiswahili? Nadhani wengi tutakuwa tumesoma nakala ya kiingereza kwani wengi bado hatukuwa tumejipatia nakala ya kiswahili.

 

Niwaombe pia wale walionunua nakala ya kiswahili wakapata changamoto ya kukidownload kama ndugu yangu Bernard Makachia. Hili si tatizo kubwa tutalitatua na linatokana na kutokufuata vizuri utaratibu kama ulivyoelekezwa kwenye website ya GETVALUE.

 

Kwa mfano mr. Bernard tayari kwenye system nimeona amekwishalipia kitabu lakini tatizo lipo kwenye kulog in katika app ya Getvalue au kukosea neno siri maana inatakiwa nenosiri unalojisajili nalo kwenye website liwe ndilo hilohilo utakalo login nalo katika ‘APP’ halikadhalika na email nayo ni hivyohivyo.

 

Tafadhali sana naomba tushee hapa kwenye group chochote kile kuihusu sura hii ya kwanza iwe ni ujumbe ama hata kama ni lugha imekutatiza mahali fulani unaweza kushea na wanamastermind wenzako ukapata suluhisho.

 

Baadae kidogo nitashea yakwangu lakini hebu tuendelee na mwingine yeyote mwenye mchango. Unaweza kuandika chochote ilimradi kihusiane nah ii chapter.  Kumbuka hii ni Sura ya kwanza kabisa kwa kiingereza inaitwa INTRODUCTION na kwa kiswahili nilitafsiri kama UTANGULIZI.

 

SURA YA KWANZA KWA UFUPI

Sura hii ya kwanza ni kama mwandishi alitaka msomaji kupata picha ya ujumbe wa kitabu kizima anataka kuzungumzia nini  maana amegusa dhamira kuu ya kitabu chenyewe kwamba mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa kuwa kitu halisi kinachoweza kushikika  mfano wa pesa, majumba, magari nk. kwa kutumia kanuni maalumu kama zilivyoelezwa kwenye sura 13 za kitabu hiki ukiacha sura ya kwanza, na ile ya 15.

 

Ndio maana utaona pia hata baadhi ya mada zilizozungumziwa humo na hata watu utakwenda kukutana nazo tena kwenyeSura za kitabu zinazofuata kwa undani zaidi.

 

Hivyo basi kwa kifupi kabisa mimi nimejaribu ‘kusummarize’ sura hii katika mistari michache ifuatayo;

 

v Mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa kuwa kitu halisi kinachoshikika kama vile mali au pesa kwa kutumia kanuni maalumu.

 

v Chanzo  kikubwa cha kuanguka  ni tabia ya kukata tamaa baada ya kukutana na vikwazo vya muda mfupi.

 

v Badala ya kukata tamaa unapoanguka, tumia uzoefu ulioupata kufanya vizuri zaidi.

 

v Utajiri unapoanza kukujia, huja  kwa wingi kiasi ambacho unaweza ukashangaa ni kwa nini haukuja siku zote ulizokuwa ukisubiri, na utajiri huo huanza na wazo kichwani pamoja na lengo  mahususi pasipo hata chembe ya kazi ngumu.

 

v Mafanikio humjia mtu anayewaza mafanikio, ubongo huambukizwa mawazo tunayofikiri midhili ya sumaku, na sumaku hiyo huvuta nguvu, watu na mazingira yeyote yale yanayohusiana na mafanikio.

 

v Kwa hiyo kabla hatujaanza kutengeneza utajiri ni sharti kwanza tuziambukize akili zetu hamu/shauku kubwa  ya  kutaka kutajirika baada ya hapo, kuwa na lengo na kisha kukomalia lengo hilo bila kukata tamaa mpaka pale tutakapofanikiwa. Waambukize na watu wengine uliokuwa nao karibu (washirika) ili wakusaidie kukamilisha lengo lako.

 

Natumaini kila mmoja wetu atakuwa amekamilisha kusoma sura hii ya kwanza ya kitabu cha Think & Grow Rich, INTRODUCTION/UTANGULIZI, iwe ni kwa kiingereza ama kwa Kiswahili.

 

Leo tarehe 22/06/2022 tutaanza kusoma sura ya pili, DESIRE /SHAUKU ambayo katika nakala ya kiingereza kuna kurasa 18 na ile ya Kiswahili kurasa 32

 

Ina maana kwamba itatuchukua siku 3 kumaliza sura hii, siku ya kwanza tutasoma hadi ukurasa wa 27 nakala ya kiingereza au ukurasa wa 52 kwa wanaofuatilia nakala ya kishwahili.

 

Tukutane jioni kwa ajili ya kupeana mrejesho wa hizi kurasa 6 za mwanzo za sura ya pili ya kitabu chetu pendwa SHAUKU au DESIRE.

 

Kwa anayehitaji kununua nakala ya kishwahili asiwe na wasiwasi, cha kufanya tu ni kuwa na smartphone yako, bonyeza linki hii ifuatayo kisha utaingia website ya Getvalue ukurasa wenye kitabu cha THINK & GROW RICH –SWAHILI EDITION kisha utafuata taratibu  mpaka umejisajili kwa email yako na nenosiri, halafu utalipia shilingi elfu 6 bei ya punguzo badala ya elfu 10 ya kawaida.

 

Baada ya hapo nenda play store kapakue APP ya GETVALUE, inafanana na website yake kimuonekano lakini ni vitu viwili tofauti. Ukishaipakua tumia ileile email na nenosiri ulizotumia mwanzoni kwenye website kulogin katika hiyo APP na mwishowe utaweza kusoma kitabu chako bila wasiwasi wowote.


KUJIUNGA NA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE

Ikiwa unapenda kujiunga na group letu la masomo, semina na kupata OFFA ya vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara za Kitanzania zilizo na faia, lipa ada ya mwaka mzima shilingi 10,000/= kupitia namba 0712202244 au 0765553030 kisha ujumbe wa wasap au sms usemao. "NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22"

Nitakutumia kila kitu na kukuunganisha ba group muda huohuo

0 Response to "TULIVYOANZA USOMAJI WA KITABU THINK AND GROW RICH-SURA YA KWANZA-UTANGULIZI"

Post a Comment