USOMAJI WA THINK AND GROW RICH SURA YA PILI SEHEMU YA 2-3 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

USOMAJI WA THINK AND GROW RICH SURA YA PILI SEHEMU YA 2-3

SEHEMU YA 2 & 3

Habari za jioni Mwanamichanganuo-online mwenzangu,

 

Tukiwa bado tunaendelea na usomaji wa kitabu chetu cha Think & Grow Rich leo tarehe 23/6/2022 ni siku ambayo tulipaswa kusoma kurasa 6 za kitabu.

 

Kwa wale wasomaji wa nakala ya kiingereza ukurasa wa 28 hadi wa 33 na wale wa nakala ya kiswahili ukurasa wa 55 hadi wa 66

Binafsi nitashea kidogo nilivyoelewa lakini pia na wewe naomba useme chochote kile ulichojifunza katika kurasa hizi 6   

Kurasa hizi zimeendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa mtu yeyote anayetaka kufanikiwa kuwa kwanza na SHAUKU KALI ya kile anachotamani kuwa/kuwa nacho.

Akatolea mfano  wa Waotaji ndoto wa zamani (dreamers) waliohusika na uvumbuzi wa vitu muhimu kabisa  dunia inavyojivunia hivi leo kwamba haikuwa rahisi kwao kama ilivyo kwa waotaji ndoto wa leo, wengine hata walidiriki kuonekana kama vile ni wenda wazimu kwa kuwa na mawazo au fikra ngeni zisizotekelezeka mfano mvumbuzi wa redio bwana Marcon marafiki zake walimpeleka wodi ya vichaa(‘mirembe’) wakimtuhumu kuwa mawazo yake ya sauti kusafiri pasipo waya yalikuwa sawa na uchizi.

 

Ipo pia stori ya mtoto kiziwi, Blaire ambaye ni mtoto wa kumzaa wa mtunzi wa kitabu hiki mwenyewe Bwana Napoleon Hill. Hapa Napoleon anazungumzia habari inayomhusu yeye mwenyewe binafsi tofauti na stori zingine zote kwenye hiki kitabu hivyo unaweza kuona ni jinsi gani Somo la SHAUKU ya kutaka kutimiza jambo Napoleon amelifafanua kwa uzuri. Shauku yake ya kutaka mwanaye wa kumzaa asikie na kuzungumza imethibitisha kanuni hii ya SHAUKU KALI kufanya kazi pasi na shaka yeyote  ile.

Pointi muhimu tunazopata kutoka kwenye hizi kurasa 6 ni hizi hapa;

              i)      Ndoto hazizaliwi hivihivi tu kivivu pasipokuwa na malengo

             ii)     Wale wote wanaofanikiwa katika maisha, huanzia na mwanzo mbaya, na kupitia mapambano mengi yenye kuumiza moyo kabla “hawajafika”.

            iii)    Mtu hashindwi bali hushindwa tu pale atakapokubali kushindwa.

            iv)    Imani, ujasiri na uvumilivu ni hali ya akili ambayo ukiichanganya na maarifa ya kazi ya kanuni zilizoelezwa, vingine vyote utakavyohitaji vitakuja kwako utakapokuwa tayari kuvipata

             v)     Kila rafiki ambaye roho yako inamtamani mwishowe atakukumbatia.

            vi)    Akili iliyofungwa haihamasishi imani, ujasiri wala kuamini.

           vii)   Kumbuka, nguvu inayohitajika kuweka malengo makubwa maishani katika kupata mali na utajiri ni sawasawa na ile inayohitajika kuleta mateso na umasikini

          viii)  Mipaka yetu pekee ni ile tunayojiwekea ndani ya akili zetu

            ix)    Shauku ikisaidiwa na imani haijui neno liitwalo “haiwezekani”

             x)     kila mkosi huja ukiwa ndani yake umebeba mbegu ya neema inayolingana na mkosi wenyewe

            xi)    Ulemavu unaweza kubadilika  kuwa rasilimali.

 

Naomba tafadhali tuendelee kujitahidi kusoma kitabu hiki kwani kina mafunzo ambayo endapo yatafanyiwa kazi yana uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha ya mtu

Siku ya kesho tarehe 24 tutamalizia Sura hii ya pili kwa kusoma kurasa zilizobakia kuanzia ukurasa wa 34 – 39 kwa wasomaji wa nakala ya kiingereza na ukurasa wa 67 – 74

Nakala yeyote ile utakayosoma iwe ni ya kiingereza au ya Kiswahili zote maudhui yake ni yaleyale ‘mamoja’ pia hata AUDIO book kwa aliye na kifaa cha kusikilizia vizuri nayo inafaa na hurahisisha sana usomaji kwani unaweza sikiliza hata muda upo kwenye basi nk. kidownload ubadilishe kuwa mp3 kiwe katika simu au kompyuta yako.

Kwa anayehitaji nakala ya kiswahili asisahau kufuata linki hii, FIKIRI & UTAJIRIKE kisha malipo katika mtandao huo ambapo bei bado ni ya OFFA shiingi elfu 6 tu badala ya shiingi elfu 10. Kabla ya kulipia soma maelekezo jinsi ya kununua kitabu katika mtandao huo ili iwe rahisi zaidi kwako

Kwa yeyote yule anayenunua kitabu akapata changamoto tafadhali asisite kuwasiliana na mimi ili tutatue changamoto husika.


KUJIUNGA NA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE

Ikiwa unapenda kujiunga na group letu la masomo, semina na kupata OFFA ya vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara za Kitanzania zilizo na faia, lipa ada ya mwaka mzima shilingi 10,000/= kupitia namba 0712202244 au 0765553030 kisha ujumbe wa wasap au sms usemao. "NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22"

Nitakutumia kila kitu na kukuunganisha ba group muda huohuo

0 Response to "USOMAJI WA THINK AND GROW RICH SURA YA PILI SEHEMU YA 2-3"

Post a Comment