USOMAJI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH (FIKIRI & UTAJIRIKE) KATIKA GROUP | JIFUNZE UJASIRIAMALI

USOMAJI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH (FIKIRI & UTAJIRIKE) KATIKA GROUP

Fikiri & utajirike (think & grow rich-swahili edition cover)
Habari za saa hizi msomaji wa  Jifunzeujasiriamaliblog

Juzi niliahidi tutaanza usomaji wa Kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE(THINK & GROW RICH) ndani ya Mastermind Group la Michanganuo-online na leo ndio ilikuwa siku rasmi ya kuweka ratiba na taratibu za usomaji wa kitabu hicho kilichobadilisha maisha ya watu wengi mno duniani kuliko kitabu kingine chochote kile katika tasnia hii ya fedha na mafanikio.

Si kitabu hiki tu bali ni vitabu vyote, kusoma mpaka mtu umekimaliza chote huku ukiyatia katika vitendo yale uliyojifunza kwa kweli kunahitaji kujitoa kwa hali na mali, utenge muda pamoja na kuwa na mpango mkakati uliokuwa wazi kama ambao tutakwenda kuuweka hapa leo.

Kitabu cha Think & Grow Rich nakala ya kiingereza( English version) kina kurasa zipatazo 235 wakati nakala ya kiswahili niliyotafsiri ina kurasa 420 hivyo unaweza kuona kwamba kiswahili kinahitaji maneno mengi zaidi karibu mara 2 zaidi kuelezea dhana ileile ambayo imeelezwa kwa kiingereza

Bila kupoteza muda mwingi ndugu msomaji naomba nitoe utaratibu wa namna tutakavyoendesha zoezi letu hili la usomaji wa kitabu hiki cha FIKIRI & UTAJIRIKE; ndani ya group hilo

1.  Kila siku tutasoma kurasa 6 za kitabu ikiwa ni nakala ya kiingereza, kwa watakaosoma nakala ya kiswahili watatakiwa kusoma kurasa 10 mpaka 12.

2.  Kila siku tutakuwa tukipeana mirejesho ya kile tulichojifunza pamoja na ufafanuzi wa mada ngumu kwa wale ambao watakutana na vikwazo mbalimbali ama kutokuelewa baadhi ya maneno na sexntensi

3.  Kila mwisho wa Sura pia kutakuwa na muda wa kujadili sura husika, kupeana ufafanuzi wa mada na maneno magumu kutoka kwa wadau tofautitofauti kwenye group

4.  Kitabu hiki huwezi ukakisoma mara moja tu kikakupa manufaa yanayotarajiwa, inapendekezwa kurudiwarudiwa hata zaidi ya mara 3. Hivyo na sisi tutafanya hivyo, mara ya kwanza lengo likiwa ni kuelewa mada mbalimbali na mara ya pili kufanyia kazi mambo yale tuliyojifunza

5.  Tunaanza rasmi usomaji wa kitabu hiki kurasa 13 za utangulizi leo tarehe 20/6/2022. Itachukua siku 2 kumaliza kurasa 13 ambapo kwa anayesoma nakala ya kiswahili ni kurasa 26 naye atazisoma kwa siku 2 pia yaani leo na kesho

6.  Jitahidi usome angalao kurasa 3 asubuhi unapoamka, kurasa moja mchana na kurasa mbili usiku kabla hujalala. Hata hivyo unaweza kutengeneza utaratibu wako mwenyewe ilimradi kwa siku utimize zile kurasa 6

7.  Unaposoma jitahidi uwe na notebook kwa ajili ya kurekodi baadhi ya maneno au mistari ile inayokugusa au iliyobeba ujumbe

Tumeweka katika group nakala ya kitabu kwa kiingereza pamoja na nakala ya sauti. Kwa anayehitaji nakala ya kiswahili anaweza kukipata kwa bei ya punguzo ya shilingi elfu sita tu(6,000/=) katika mtandao wa GETVALUE kupitia link ifuatayo badala ya shilingi elfu 10 ya kawaida; Fikiri & Utajirike (Think & Grow Rich-Swahili edition)

Aidha bei hii ya punguzo ya shilingi elfu 6 itadumu kwa muda mfupi sana kabla haijarudishwa ile ya kawaida ya sh. Elfu 10, hivyo wahi mapema kupakua(kudownload)  nakala yako pale ukitumia smartphone yako

0 Response to "USOMAJI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH (FIKIRI & UTAJIRIKE) KATIKA GROUP"

Post a Comment