NINA MTAJI WA SHILINGI MILIONI MOJA (1000,000), NAOMBA USHAURI NITAFANYA BIASHARA GANI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NINA MTAJI WA SHILINGI MILIONI MOJA (1000,000), NAOMBA USHAURI NITAFANYA BIASHARA GANI?

Boashee akiuza duka la rejareja mjini

Nina mtaji wa shilingi milioni moja, mtaji wa laki moja, mtaji wa sh. laki mbili, mtaji wa elfu hamsini(50,000/=) naomba ushauri nifanye biashara gani ya kunilipa  nk. ni maswali yanayoulizwa mara nyingi sana na wajasiriamali wengi mitandaoni na hata nje ya mtandao hiyo. 

Nina mtaji wa milioni moja

Binafsi mimi kama mshauri wa wafanyabiashara wadogo na wale wa kati nimewahi kukutana na maswali yanayofanana na hili zaidi ya mara 50 wengi nikiwajibu humubumu katika blogu ya jifunzeujasiriamali lakini wengine nawajibu tu hewani kupitia sms, watsap na simu ya kawaida ya mkononi.

SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma nipeni ushauri nina wakati mgumu

Mdau aliyejitambulisha kwa jina moja la Kimaro karibuni naye aliniuliza kama ifuatavyo namimi kama kawaida yangu sipendi kuongeza wala kupunguza maneno ya waulizaji maswali, nimekuwekea hapo chini swali lake na majibu niliyomjibu kama ifuatavyo;

Swali:

Salama mkuu 

Naitwa …Kimaro

Samahani kuomba ushauri mkuu

Mimi nina mtaji wa shilingi milioni moja (1000,000), naomba unipe ushauri nitafanya biashara gani kwa mtaji huo

Majibu:

Ndugu yangu Kimario, suala la kuanzisha biashara halina tofauti kubwa na suala la mtu kujichagulia mwenza/kuoa au kuolewa. Ni suala ambalo mara nyingi halitaki mtu kutumia moja kwa moja ushauri wa mtu mwingine hata ikiwa mtu huyo wa pili ni mzazi nikimaanisha mama yako au baba yako. Sisemi ushauri wa watu wengine ni mbaya hapana, ila tumia ile falsafa maarufu ya aliyewahi kuwa Rais wa awamu ya nne Mh. JK. kumhusu mbayuyayu isemayo, Akili ya kuambiwa changanya na za kwako.

SOMA: Nataka kufungua biashara ya steshenari mtaji milioni 1.5 nifanyeje?

Hii maana yake ni kitu gani? Akili ya kuambiwa maana yake ni majibu ya utafiti utakayofanya kwenye lile jambo/biashara unayotaka kuanzisha sawa tu na mchumba unayetaka kumchumbia. Namaanisha kwamba ukitaka kuanzisha biashara yeyote ile au kuoa kuna jambo moja la msingi sana unalopaswa kulifanya kusudi uweze kufahamu biashara sahihi ya wewe kuifanya au mchumba sahihi anayeweza kuwa mke wako ni yupi.

UTAFITI AMA UPEMBUZI YAKINIFU kwa mujibu wa Kitabu changu kikubwa cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kitabu kilichokuwa na kila kitu mjasiriamali yeyote anachohitaji kufanya biashara ya kisasa, ndiyo jibu la maswali yoote niliyotangulia kuyataja pale mwanzoni ya “Nina mtaji wa shilingi milioni kadhaa nifanye biashara gani, au nina mtaji wa laki kadhaa nitafanya biashara ipi itakayonilipa vizuri.”

SOMA: Ishi kama Mbayuwayu, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Kwahiyo Mr. Kimaro majibu yangu kwa kifupi sana mimi nakushauri kama ulivyoniuliza unamaanisha sasa hivi unafanya utafiti wa wazo la biashara itakayokufaa. Sasa binafsi siwezi kukujibu kafanye biashara fulani labda genge, duka au saluni hapana, jibu la ni biashara ipi inakufaa linatakiwa litokane na mazingira yakwako wewe mwenyewe unavyoishi. Chunguza ni mahitaji gani katika jamii/eneo unaloishi watu wanataabika sana kuyapata, wazo la biashara pia linaweza likatokana na ujuzi au taaluma uliyokuwa nayo, shuleni ulikuwa unatamani sana kuja kufanya kitu gani? Je una kipaji chochote kile unachoweza ukakigeuza kuwa biashara?.

Hebu fanya ziara maeneo mbali na pale unapoishi, je hautagundua biashara ambazo hukuwa unazifahamu hapo kabla na ambazo unaweza kwenda kuzifanya katika eneo jingine?. Unaweza kubuni kitu fulani kipya kabisa kama Masudi kipanya alivyobuni gari la kutumia betri ya kuchaji kwa umeme Tanzania?

Basi ndugu yangu Kimaro(“Boashee”) hizo ni baadhi tu ya mbinu mtu unaweza kuzitumia kupata wazo la biashara ya ndoto yako  sawa sawa tu na jinsi ulivyompata mke wa ndoto yako(kama tayari umeoa lakini, kama bado subiri usiwe na papara maisha siyo rehearsal).

SOMA: Mtaji wangu ni mdogo sana lakini nahitaji kufanya biashara na sina ajira naomba ushauri wako

Mbinu zingine na vitu kibao kuhusiana na biashara na ujasiriamali kwa ujumla unaweza ukazipata kwa uzuri zaidi kwenye kitabu chetu hicho cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ambacho kukipata ni rahisi sana, kwani kwa kulipia tu shilingi elfu 10 kwa namba 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo, nakutumia nakalatete ya kitabu hicho muda huohuo kwenye simu yako ya mkononi au kompyuta iwe ile ya mezani, tablet au mpakato.


Makala hii imeandaliwa na;

Peter Tarimo

Mtaalamu wa michanganuo ya biashara na mfasiri wa kitabu cha Think & Grow Rich katika lugha adhimu ya Kiswahili.

Call/Whatsap: 0712202244 / 0765553030


 

0 Response to "NINA MTAJI WA SHILINGI MILIONI MOJA (1000,000), NAOMBA USHAURI NITAFANYA BIASHARA GANI?"

Post a Comment