MAELEZO KUHUSU BIASHARA/KAMPUNI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAELEZO KUHUSU BIASHARA/KAMPUNI

SOMO LA TANO SEMINA 2022
SOMO LA TANO

2.0 MAELEZO YA BIASHARA AU KAMPUNI

Utajifunza yafuatayo;-

·       Dhamira kuu

·       Maono

·       Malengo ya biashara

·       Siri za mafanikio

·       Umiliki wa biashara/ kampuni, ubia au mtu binafsi

·       Historia ya kampuni.

·       Usajili wa biashara

·       Jina na eneo biashara ilipo

Katika sehemu hii ya maelezo kuhusu biashara au kampuni kuna vitu vinne muhimu vinavyotangulia ambavyo ni; Dhamirakuu, Maono, Malengo na Siri za mafanikio. Mambo hayo manne ya msingi utakuta katika michanganuo mingine ya biashara watu wameyaweka chini ya, kwenye sehemu au kipengele kile cha kwanza cha Muhtasari na mfano mzuri unaweza ukaona katika michanganuo mingi kwenye kitabu chetu tulitumia mtindo huo.

Hata hivyo kuviweka vitu hivyo sehemu yeyote iwe ni katika sehemu hii ya maelezo ya biashara au sehemu ya chini ya muhtasari hakuwezi kuathiri chochote kile kwani sehemu zote katika mpango wa biashara hutegemeana na kuhusiana. Hapa tutaanza na vitu hivyo vinne na kisha kuendelea na maelezo mengine ya biashara/kampuni.

2.1 Dhamira kuu
Dhamira kuu ni ile biashara unayoifanya. Tuchukulie mfano
labda biashara yako ni ya mgahawa katika mji wa Iringa,
unaweza ukaiandika hivi dhamira yako kuu, “Kutoa huduma
bora ya vyakula na vinywaji kwa wakazi wa mji wa Iringa”

2.2 Maono
Wengine huamua kutokuweka maono lakini ikiwa utaamua kuyaweka basi maono ni picha ya biashara yako unayotaka uione baada ya kipindi fulani kupita tuseme labda mwaka mmoja, mitatu au kipindi chochote kile utakachoamua. Mfano unawezau kasema hivi, Maono yetu ni  “Kuja kuwa na mgahawa mkubwa zaidi mjini Iringa

2.3 Malengo.
…………………….Inaendelea kwenye group la Michanganuo-online

Semina hii iliyofanyika katika group la Michanganuo-online unaweza ukaipata muda wowote ule katika mfumo wa e-book ukiwa mwanachama wa group hilo. Unaidownload katika channel yetu ya telegram au pia tunaweza kukutumia moja kwa moja inbox katika watsap ama email yako.

Kama unahitaji kupata semina hii pamoja na masomo mengine yote yaliyowahi kufundishwa katika group letu zaidi ya masomo 70 jiunge kwa kutoa kiingilio chako sh. Elfu 10 tu na ada hii ni ya miezi 12/mwaka mzima.

Kulipia tumia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo na ujumbe watsap au sms usemao “NATAKA SEMINA KUBWA YA KUANDIKA MICHANGANUO”

  

0 Response to "MAELEZO KUHUSU BIASHARA/KAMPUNI"

Post a Comment