MTAJI WANGU NI MDOGO SANA LAKINI NAHITAJI KUFANYA BIASHARA NA SINA AJIRA NAOMBA USHAURI WAKO

Nina mtaji mdogo sana, nataka kufanya biashara
Kama ilivyokuwa ada sisi huwa tunapokea na kujibu kila siku maswali na changamoto fupifupi kutoka kwa wasomaji wa blog ya jifunzeujasiriamali, baadhi ya maswali huwa tunaweka majibu yake katika blogu hii na mengine tunayajibu tu kwa muulizaji basi. Leo hii ni zamu ya msomaji mmoja kutoka jijini Dar es salaa na nimeweka mawasiliano yake ya watsap namimi tangu tunasalimiana mpaka majibu kama ifuatavyo,


 MUULIZAJI SWALI: za siku ndugu, nimepata namba yako kwenye channel yako ya utubeJIFUNZEUJASIRIAMALI: Nzuri tu ndugu Karibu Sana, Mimi naitwa Peter Tarimo ni mwandishi vitabu vya ujasiriamali lakini pia blogu iitwayo jifunzeujasiriamali.co.tz

MUULIZAJI SWALI: Ninahitaji kufanya biashara, lakini mtaji wangu Ni mdogo Sana, na Sina ajira naomba ushauli wako


Nimekua nikisoma  makala mbalimbali za kutoka kwenye blog yako, vilevile kwenye utube channel yako , Sasa ninahitaji kusimama na kuanza biashara, lakini kabla cijaanza biashara nahitaji ushauri kutoka kwako Kama mjasiliamali ulienitangulia najua utakua na kitu Cha kunishauli
Asante

MAJIBU:
Ikiwa tayari una njia inayoweza kusapoti maisha yako yaani kupata mahitaji yale ya msingi ya kila siku halafu umesema kwamba una mtaji kidogo sana, hapo panaweza kuwa na njia ya wewe kuanza biashara hata kama ikiwa ni kwa ugumu(bootstrapping)

Kitu ninachokushauri ni kwamba chekecha na upate wazo la biashara ambayo unajua kabisa kwanza ina uwezekano mkubwa wa kupata wateja. 


Biashara ya kufanya ya namna hiyo mara nyingi sana ni zile biashara za bidhaa ama huduma zinazotumiwa na watu kila siku, mtu hata akinunua leo lakini kesho au keshokutwa atahitaji tena kitu hichohicho.

Wazo la biashara yenye wateja

Pia wazo la biashara hiyo hakikisha aidha unaifahamu au una uzoefu wa namna fulani nayo kusudi iwe rahisi kwako kuifanya

Wakati wa kufikiria wazo usijisumbue kabisa kuwaza kama mtaji utautoa wapi, wewe just fikiria tu uwezekano wa wewe kuifanya hiyo biashara upoje


Ukishajiridhisha kwamba wazo la biashara uliyokusudia kuifanya linatekekezeka na kuna uwezekano wa kupata wateja watakaojirudia mara kwa mara, sasa angalia ni kwa vipi au ni kwa njia gani unaweza ukaianza biashara hiyo katika hatua(level) ya chini kabisa.

Hatua ya chini kabisa namaanisha kwamba hata ikiwa kwa mfano biashara uliyowaza ni ya kumiliki kampuni ya utalii basi hatua ya chini kabisa ni kuanzisha hata blog au ukurasa wako wa facebook maalumu tu kwa ajili ya kuandika insha na dondoo zinazohusiana na maswala ya utalii, katika hiyo kurasa au website pia unaweza ukaanza  moja kwa moja kuweka matangazo ya google ya kulipia(AdSense) ili uanze kuingiza chochote mapema(pesa)


Baadae utajikuta taratibu unapata connection mbalimbali zitakazokufanya hatimaye uweze kuifikia ndoto yako ya kuwa na biashara ya utalii

Huo ni mfano tu lakini wa mtu ambaye labda ana uzoefu au mapenzi na biashara ya utalii. Zipo biashara za aina nyingi za mtaji mdogo Tanzania unazoweza kuanzisha ingawa watu wengi huwa tunazipuuzia au kuogopa watu wengine watatuonaje tutakapokuwa tukizifanya au watatucheka nk.

Biashara ya duka kwa mfano, biashara zilizosahauiika kama hii hapa na hata biashara ya kukaanga mihogo na nyinginezo nyingi nilizowahi kuandika katika blogu yangu ya jifunzeujasiriamali ni aina za biashara mtu anazoweza akaanza kwa mtaji kidogo sana huku akijiwekea mipango ya biashara kubwa zaidi. Wakati huo wa kujipanga usisahau kujifunza mambo yahusuyo ujasiriamali na biashara, unaweza kujifunza popote pale unapoona ni rahisi kwako kujifunza. Siku hizi kuna mitandao ya kijamii, vyombo mbalimbali vya habari na hata unaweza kuhudhuria semina za ujasiriamali na makongamano.


Kumbuka unaweza kuanza na biashara ndogo sana lakini lengo lako kubwa liwe ni unataka kukuza mtaji ili uje ufanye biashara kubwa zaidi hapo baadae.

Ninachokushauri ni kwamba usiogope kuanzia chini. Watu wengi uwaonao leo wana mafanikio makubwa walianzia chini sana huku wakitengeneza wateja na soko kwanza kabla ya mitaji mikubwa.

Hakuna njia ya mkato duniani ya kuanza biashara, ni lazima ukubali kuanza kidogo huku ukifikiria makubwa(Start small but think big)

Asante, naamini ushauri wangu ukichanganya na mawazo yako mwenyewe vinaweza vikakupa mwangaza walao kidogo wa kuanza biashara endelevu na mtaji mdogo uliokuwa nao.

Biashara endelevu na mtaji uliokuwa nao


……………………………………………………..


Je, una swali au changamoto yeyote ile kuhusiana na Biashara na Ujasiriamali? Tuma swali au changamoto yako fupi kupitia Whatsap: 0765553030 au e-mail: jifunzeujasirimali@gmail.com tutaijibu hapa. Hatutaji utambulisho wa mtu pasipo ridhaa yake mwenyewe. Asante

Kwa vitabu vyetu na michanganuo mbalimbali ya Biashara tembelea duka la vitabu la SMARTBOOKS TANZANIA hapa

Unaweza pia kujiunga na Group letu la Masomo ya kila siku ya fedha na Michanganuo kwa kulipa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu kwa mwaka, lipia kwa namba 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe wa “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA INAYOKARIBIA KUISHA MUDA WAKE”

Pia usisahau, kile kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA toleo la 2020 lililoboreshwa kwa kuongeza mbinu na njia za kuthibiti udokozi na usimamiaji wa mahesabu wenye tija sasa kinapatikana bonyeza Jina la kitabu hapo kukipata.

0 Response to "MTAJI WANGU NI MDOGO SANA LAKINI NAHITAJI KUFANYA BIASHARA NA SINA AJIRA NAOMBA USHAURI WAKO"

Post a Comment