SEMINA SEHEMU YA 5: MCHANGANUO, UFUGAJI WA KUKU CHOTARA WA NYAMA KIBIASHARA – (MPANGO WA FEDHA NA VIAMBATANISHO) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA SEHEMU YA 5: MCHANGANUO, UFUGAJI WA KUKU CHOTARA WA NYAMA KIBIASHARA – (MPANGO WA FEDHA NA VIAMBATANISHO)

 

Mauzo ya nyama ya kuku chotara wa kuroiler

SEHEMU YA TANO

Mpango wa Fedha na Viambatanisho


8.0 Mpango wa Fedha

Katika Sura hii ya Fedha kunakuwa na muhtasari mdogo wa yale mambo muhimu yanayopatikana ndani ya Sura nzima kisha baada ya hapo hufuata vipengele vidogo ambavyo ni hivi;

8.1 Dhana/Makisio muhimu

8.2 Tathmini ya mauzo yakurudisha gharama (Break Even Analysis)

8.3 Makisio ya Faida na Hasara

8.4 Makisio ya Mtiririko wa Fedha Taslimu

8.5 Makisio ya Mizania ya Biashara

8.6 Sehemu muhimu za biashara

 

8.1 Dhana/Makisio muhimu

Hapa nimeorodhesha Dhana au makisio niliyotumia kukisia ripoti za mahesabu yangu, dhana hizo ni kama vile; idadi ya kuku katika mzunguko mmoja, uchakavu, bei za vyakula, bei ya kifaranga mmoja nk.

 8.2 Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama zote (Break even Analysis)

Haya ni mauzo au idadi ya bidhaa mradi utakazozalisha na kuuza katika kipindi fulani tuseme, mzunguko mmoja, mwaka au kipindi kingine chochote kile ambayo yatalingana na gharama zilizotumika. Au kwa manemo mengine unaweza ukasema; utatakiwa uuze kiasi gani kwa kipindi husika kusudi uweze kurudisha gharama zote zilizotumika katika kipindi hicho?

Ina maana kwamba ukiuza chini ya kiasi hicho unapata hasara na ukiuza juu ya kiasi hicho unapata faida.

Kwakuwa biashara hii ya CPPC uzalishaji wake unafanyika kwa mzunguko wa miezi 3, basi hatuna budi kufanya tathmini hii ya break even katika kipindi hicho cha miezi 3 badala ya kutumia kipindi cha mwezi mmoja ambacho imezoeleka zaidi kwa biashara za aina nyigine tofauti na kuku.

Katika tathmini hii huwa kuna vitu muhimu 3 ambavyo mtu unapaswa kwanza kuwa navyo kabla ya kukokotoa, navyo ni;

                         (1)     Mauzo jumla = 3,037,200/=

                         (2)     Gharama za kudumu = 55,750/=

                         (3)     Gharama zinazojirudiaa (za mauzo) = 2,223,150/=

                         (4)     Asilimia ya faida ghafi katika mauzo (Cotribution margin ratio) = 26.8%

Taarifa hizi zote 3 tunaweza tukazipata kutoka katika jedwali la faida na hasara la mzunguko mmoja wa miezi 3, tungeliweza kuzipata pia hata kama tungeliamua kutumia vipindi vya mwezi mwaka nk. Tazama jedwali hilo kwenye mchanganuo wako

Kupata Contribution margin% unaweza ukatumia kanuni ifuatayo;

CM% =Mauzo – Gharama zinazojirudia / Mauzo x 100

 = 3,037,200/ 2,223,150 x 100 = 26.8%

Na kanuni ya kukokotoa mauzo ya kurudisha gharama Break even sales nayo ni hii hapa;

B.E Sales = Gharama za kudumu / CM% = 55,750 /0.268

= 208,022

Jinsi ya Kuchora chati ya mauzo ya kurudisha gharama (Break even chart)

Ili kuchora chati hii kwanza unahitaji kuzingatia kanuni kuu ya Break even analysisi ifuatayo na ambayo ndiyo kanuni nyingine zote zinazotumika kukokotoa tathmini hii huanzia

Faida = Mauzo – Gharama zinazobadilika – Gharama za kudumu

Laini kumbuka Faida ni sifuri (0) mauzo ya kurudisha ghara yanapofikiwa, na pia Gharama zinzobadilika tunaziweka katika sehemu ya mauzo ambapo ni asilimia 73.2% x Mauzo au 0.732 ya mauzo

Kwa maana hiyo tutatengeneza jedwali la taarifa (data) za chati yetu, MAUZO VS FAIDA tukitumia kanuni hiyo huku kila penye gharama zinazobadilika tukiweka (0.732 ya Mauzo) kama ifuatavyo;

Tukianza na Mauzo =sifuri (0) faida itakuwa hivi;

Faida = 0 – 0.732(0) – 55,750 = -55,750

Kwahiyo kukiwa hamna mauzo kabisa (0) faida ni hasi -55,750 maana yake ni kuwa kuna gharama za kudumu peke yake bado hamna kazi iliyofanyika

Tukiweka mauzo yetu ni sh. 50,000/= Faida itakuwa kama ifuatavyo;

Faida = 50,000 – 0.732(50,000) – 55,750 = -42,350 Hapa tunaona bado faida ni hasi

Tukiweka mauzo = 100,000/=

Faida = 100,000 – 0.732(100,000) – 55,750 = -28,950 Hapa faida bado ni hasi lakini inazidi kuongezeka kuwa +.

Tuweke mauzo yetu ni sh. 150,000/=

Faida = 150,000 – 0.732(150,000) – 55,750 = -15,550

Tukiweka mauzo ni sh. 200,000

Faida = 200,000 – 0.732(200,000) – 55,750 = -2,150

Tuweke Mauzo ni sh. 250,000

Faida = 250,000 – 0.732(250,000) – 55,750 = 11,250 Hapa sasa unaona mauzo yakiwa sh 250,000 faida inaanza kuwa chanya na kadiri mauzo yatakavyoongezeka faida nayo itazidi kuongezeka lakini kuna mahali mauzo yatalingana na gharama ambapo faida itakuwa ni 0 na utaweza kuona kwenye jedwali letu.

Heu sasa tuweke taarifa/data zetu za kutosha kwenye jedwali hili ndipo tuchore chati yetu;

Jedwali: Mauzo vs Faida

Mauzo

Faida

0

-54,250

50,000

-42,350

100,000

-28,950

150,000

-15,550

200,000

-2,150

250,000

11,250

300,000

24,650

350,000

38,050

400,000

51,450

450,000

64,850

500,000

78,250

550,000

91,650

 

Chati: Tathmini ya Mauzo ya kurudisha gharama (Break even sales)

Kwa kutumia taarifa zetu hapo juu sasa tunaweza kuchora chati yetu kwenye Microsoft word kama ifuatavyo.

Chati ya Mauzo ya kurudisha gharama (Break even chat)


Kituo faida inapokuwa ‘0’ ukisoma kwa umakini thamani ya mauzo pale chini mstari ulipopishana utaona ni sh. 208,022 sawa na jibu tulilopata kwa kutumia kanuni ya kukokotoa Break Even sales pale juu.

8.3 Makisio ya Faida na Hasara

Miradi ya kuku hasa wa nyama ni tofauti kidogo na biashara nyingine kwenye kipindi cha makisio. Kwa kuwa kuku wa nyama huwezi kuwauza mpaka muda wa kukua ufike huwezi kukisia hesabu ya kila mwezi na badala yake utakisia hesabu ya mzunguko mzima wa kipindi chote tangu vifaranga wa siku moja mpaka unawauza, kwa kesi yetu ni miezi 3(wiki 12). Kisha hesabu za mzunguko mmoja ndiyo zinakuwa msingi wa hesabu za vipindi vingine kama mwaka mmoja na miwili.

Kumbuka taarifa zote kuanzia mauzo mpaka gharama zote tulikwisha zipata huko nyuma na hapa ni suala la kuzipachika tu kwenye jedwali letu la faida na hasara la mzunguko mmoja tukianza na Mauzo pale juu kabisa kisha tunatoa gharama zinazobadilika, tunatoa tena gharama za kudumu, toa kodi na riba na mwishoni tunapata Faida halisi.(Tazama mchanganuo wako

Makisio ya Faida na Hasara mwaka wa 1

Faida na hasara mwaka mmoja yanaundwa na makisio ya vipindi tofauti na kwa mchanganuo wetu ni vipindi 4, kwahiyo vipindi hivyo 4 tukijumlisha taarifa zake katika kila safu iliyolala ndipo tunapata taarifa za mwaka mzima kama ifuatavyo;

MAKISIO YA FAIDA NA HASARA

 

Mzunguko1

Mzunguko2

Mzunguko3

Mzunguko4

MWAKA 1

 

MAUZO

3,037,200

3,037,200

3,037,200

3,037,200

12,148,900

Gharama zinazobadilika

2,223,150

2,223150

2,223,150

2,223,150

8,892,600

Faida ghafi

814,050

814,050

814,050

814,050

3,256,200

%Faida ghafi

26.8%

26.8%

26.8%

26.8%

26.8%

 

Gharama za kudumu

 

Uchakavu wa banda

18,750

18,750

18,750

18,750

75,000

Uchakavu wa vifaa

17,000

17,000

17,000

17,000

68,000

Umeme

5,000

5,000

5,000

5,000

20,000

Matangazo na usafiri

15,000

15,000

15,000

15,000

60,000

Jumla gharama za kudumu

55,750

55,750

55,750

55,750

223,000

 

Faida kabla ya kodi na Riba

758,300

758,300

758,300

758,300

3,033,200

Kodi

0

0

0

0

0

Riba

0

0

0

0

0

Faida Halisi

758,300

758,300

758,300

758,300

3,033,200

%Faida Halisi

25%

25%

25%

25%

25%

 

Kupata jumla ya makisio ya kila mstari uliolala (rows) ambayo yatakuwa ndiyo makisio yetu ya mwaka mzima unajumlisha kila namba ya mzunguko kwa mizunguko yote 4 mfano mauzo mzunguko wa kwanza + mauzo mzunguko wa 2 nk. hadi wa nne = 12,148,900/=

Hapa sasa unakuwa tayari umekwishakamilisha makisio yako ya faida na hasara kwa mwaka wa kwanza kama uonavyo kwenye jedwali hapo chini ukisubiri kupata makisio ya miaka 2 inayofuata;

Makisio ya Faida na Hasara

 

Mw1

Mw2

Mw3

 

Sh.

Sh.

Sh.

MAUZO

12,148,800

 

 

Gharama zinazojirudia

8,892,600

 

 

Faida Ghafi

3,256,200

 

 

%Faida ghafi

26.8%

 

 

 

Gharama za kudumu za uendeshaji

 

 

 

Uchakavu wa banda

75,000

 

 

Uchakavu wa vifaa

68,000

 

 

Umeme

20,000

 

 

Matangazo/usafiri

60,000

 

 

Jumla ya Gharama za kudumu

223,000

 

 

Faida kabla ya kodi na riba

3,033,200

 

 

Riba ya mkopo.

0

 

 

Kodi ya mapato .

0

 

 

Faida halisi.

3,033,200

 

 

%Faida halisi / mauzo.

25%

 

 

 

Jinsi ya kukisia faida na hasara kwa miaka 2 inayofuata;

1. Mauzo;

Tunaanza na mauzo kwanza na kumbuka tulipokuwa tukikisia mauzo huko nyuma tulikisia kwamba mwaka wa pili mauzo yataongezeka kwa asilimia 50% na mwaka wa tatu asilimia 33.3%

Inamaana kwamba,

Mauzo ya mwaka wa pili tutakokotoa hivi;

50% x 12,148,800 + 12,148,800 = 18,223,200

 

Mauzo ya mwaka wa tatu;

33.3% x 18,223,200 + 18,223,200 = 24,297,600

2. Gharama zinazobadilika (za mauzo)

Gharama zinazobadilika tuliweka makisio ya asilimia 73.2% ya Mauzo, hivyo kwa

Mwaka wa pili tutafanya hivi;

73.2% x 18,223,200 = 13,339,384

Mwaka wa 3;

73,2% x 24,297,600 = 17,785,844

3. Gharama za kudumu

Uchakavu:

Kumbuka kwamba tulisema kila mwaka mabanda na vifaa vya chakula na maji vitaongezwa kulingana pia na ongezeko la vifaranga; hivyo mwaka wa 2 kuku 150 wataongezeka na banda pia itabidi liongezwe kwa nusu ya banda la mwaka wa kwanza ambapo gharama yake ni nusu pia ya ile ya mwaka wa kwanza

Kwahiyo tutachukua uchakavu wa mwaka wa kwanza sh. 75,000 + uchakavu wa banda lililoongezwa sh. 37,500 = 12,500 na kwa upande wa vifaa vya maji na chakula ni hivyohivyo.

Umeme na Matangazo:

Tutakisia ongezeko kidogo la shilingi elfu 10 kwenya umeme na  shilingi elfu 40 kwenye matangazo kwani inategemewa kwamba ni lazima gharama hizi zipande kidogo kulingana pia na ongezeko la shughuli za biashara, kwa hiyo ni suala tu la kutumia uzoefu wako kuamua gharama hizo kwa makisio zinaweza kuongezeka kwa kiasi gani.

Tukitoa gharama zote kutoka kwa Mauzo tunapata faida kabla ya kodi na Riba na kwa kuwa biashara yetu tumekisia hakutakuwa na kodi wala riba wakati inaanza basi faida halisi itabakia kuwa hiyohiyo sawa na faida kabla ya kodi na riba ambayo ni shilingi  4,536,316 mwaka wa pili na shilingi  6,045,756 mwaka wa tatu

Mwisho kabisa jedwali letu la Faida na hasara kwa miaka yote 3 litaonekana kama ifuatavyo;

Jeswali: Faida na Hasara miaka 3

Makisio ya Faida na Hasara

 

Mw1

Mw2

Mw3

 

Sh.

Sh.

Sh.

MAUZO

12,148,800

18,223,200

24,297,600

Gharama zinazojirudia

8,892,600

13,339,384

17,785,844

Faida Ghafi

3,256,200

4,883,816

6,511,756

%Faida ghafi

26.8%

26.8%

26.8%

 

Gharama za kudumu za uendeshaji

 

 

 

Uchakavu wa banda

75,000

112,500

150,000

Uchakavu wa vifaa

68,000

105,000

136,000

Umeme

20,000

30,000

30,000

Matangazo/usafiri

60,000

100,000

150,000

Jumla ya Gharama za kudum

223,000

347,500

466,000

Faida kabla ya kodi na riba

3,033,200

4,536,316

6,045,756

Riba ya mkopo.

0

0

0

Kodi ya mapato .

0

0

0

Faida halisi.

3,033,200

4,536,316

6,045,756

%Faida halisi / mauzo.

25%

25%

25%

 

8.4 Makisio ya Mtiririko wa Fedha taslimu

Mtiririko wa fedha taslimu tofauti na Faida na Hasara huwa unatakiwa kushughulika tu na fedha taslimu zinazoingia na kutoka kwenye biashara, kwahiyo ikiwa kuna madeni, malighafi au stoku ya bidhaa ambazo bado hazijauzwa hapa hatuwezi kuziweka vinginevyo muundo wake unafanana.

Makisio ya Mtiririko wa fedha yanaingiliana au kuhusiana na makisio ya faida na hasara na pia makisio ya mizania ya biashara, kwahiyo kuna vitu tunapokuwa tukikokotoa kwenye mtiririko wa fedha basi moja kwa moja tunakuwa tukikamilisha na baadhi ya vitu katika jedwali la mizania ya biashara. Hivyo ni lazima ripoti zote 3 zihusike

Tunaanza kwa kutumia namba zetu za jedwali la kwanza kabisa la kianzio au mizania ya biashara ya kuanzia (cheki mchanganuo wako Sura ya 2 ya maelezo ya biashara kipengele cha Kianzio, mizania ya biashara). Hapa ndipo tunapata kianzio chetu cha fedha taslimu ambacho ni sh. 2,223,150

Ili kupata makisio ya mtiririko wa fedha mwaka mzima wa 1 tutatafuta kwanza mtiririko wa fedha kwa mizunguko yote 4 ya mwaka 1 na kisha tutakuja kujumlisha safu mlalo (rows) za miezi yote 4 kupata makisio ya mwaka 1.

MAKISIO YA MTIRIRIKO WA FEDHA TASLIMU

Mzunguko1

Mzunguko2

Mzunguko3

Mzunguko4

FEDHA INGIA

TZS

TZS

TZS

TZS

Kianzio

2,223,150

 

Mauzo Taslimu

3,037,200

3,037,200

3,037,200

3,037,200

Makusanyo ya deni

0

0

0

0

Mkopo mpya

0

0

0

0

Mauzo ya rasilimali

0

0

0

0

Mtaji mpya

0

0

0

0

Jumla fedha Ingia

3,037,200

3,037,200

3,037,200

3,037,200

FEDHA TOKA

Matumizi fedha taslimu

2,520,000

2,320,000

2,220,000

2,220,000

Malipo ya bili

0

0

0

0

Malipo deni la muda mrefu

0

0

0

0

Ununuzi mali za muda mfupi

0

0

0

0

Ununuzi mali za kudumu

0

0

0

0

Utoaji gawio

0

0

0

0

Jumla ya fedha toka

2,520,000

2,320,000

2,220,000

2,220,000

Mtiririko wa fedha taslimu

517,200

717,200

817,200

817,200

SALIO LA FEDHA TASLIMU

2,740,350

3,457,550

4,274,750

5,091,950

Kuona majedwali yenye namba zilizokamilika tafadhali jipatie Semina kamili, mchanganuo wako wa kuku chotara 300 aina ya kuroiler, Kitabu pamoja na Offa ya michanganuo mingine ya aina mbalimbali.

 

FEDHA INGIA

Nitaeleza kila mstari uliolala (rows) nikianza na Fedha Ingia

1. Kianzio: Kianzio tunakipata kutoka jedwali letu la mizania ya kuanzia sh.  2,223,150

2. Mauzo taslimu: Hizi ni fedha taslimu zinazoingia kwenye biashara kupitia mauzo taslimu tu ikiwa kuna kiasi umekopesha hakihusiki hapa. Katika mzunguko wetu wa 1 na hata mizunguko mingine inayofuata tumeona kwenye jedwali la faida na hasara mauzo yetu ni fedha taslimu sh. 3,037,200 na hayabadiliki kila mzunguko, hivyo tutaweka kiasi hicho katika kila chumba cha mzunguko

3. Makusanyo ya deni

Unakisia ikiwa kama utakopesha wateja watalipa kiasi gani kila mzunguko. Lakini tumeona jedwali letu la faida na hasara hakutakuwa na mauzo ya mkopo na hivyo hakutakuwa pia na makusanyo ya madeni toka kwa wateja, hivyo nimeweka ‘0’ pale

4. Mkopo mpya:

Hakuna mkopo mpya unaotarajiwa

5. Mauzo ya rasilimali

Hakuna rasilimali zinazotarajiwa kuuzwa

6. Mtaji mpya

Hakutarajiwi mtaji mpya

 

FEDHA TOKA

Kwa upande wa fedha zinazotoka nitaanza na;

1. Matumizi ya fedha taslimu; Hapa tunatazama jedwali letu la faida na hasara ni matumizi gani yatakayohitaji kulipiwa fedha taslimu (yasiyo ya mkopo)

Kwanza kabisa kuna gharama zote zinazobadilika, zile za kudumu mfano umeme na matangazo isipokuwa uchakavu maana uchakavu hautoi fedha taslimu (cash) mfukoni, lakini pia kuna kodi na riba. Hapa inabidi tujumlishe gharama zote hizo katika kila mzunguko

Lakini kitu cha kukumbuka ni kwamba gharama zinazobadilika hutokana na malighafi ambazo nazo hununuliwa kwa fedha taslimu, kwa hiyo tunapaswa kwanza kukadiria kiasi cha malighafi zitakazokuwa zikinunuliwa kila mzunguko mmoja kwani haiwezekani ununue malighafi zinazotosheleza kiasi kamili cha gharama zinazobadilika tu; ni lazima ununue malighafi kiasi kikubwa zaidi ya gharama utakazozitumia, zikibaki unakwenda kuzitumia mzunguko unaofuata.

Jedwali la kukokotoa kiasi cha malighafi ni hili hapa chini;

 

Kukadiria Bidhaa/malighafi.

Mzung 1

Mzung 2

Mzung 3

Mzung 4

 

SH.

SH.

SH.

SH.

 

Makadirioya muda wa kukaa na bidhaa ni miezi 3

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Bidhaa za kuanzia (kutoka kipindi kilichopita)

0

276,850

353,700

330,550

 

 +Ununuzi bidhaa/malighafi.

2,500,000

2,300,000

2,200,000

2,200,000

 

-Matumizi(gharama zinazobadilika)

2,223,150

2,223,150

2,223,150

2,223,150

 

Salio la bidhaa mzunguko huu

276,850

353,700

330,550

307,400

  

1.   Penye bidhaa za kuanzia mzunguko wa 1 unatazama mizania ya kuanzia utaona hatukuwa na kitu hivyo weka 0

2.   Ununuzi wa malighafi kwa fedha taslimu mzunguko huohuo wa 1 tukadirie sasa tutanunua malighafi kiasi gani. Kwa kuwa tumesema malighafi ni lazima zizidi kidogo gharama zinazobadilika hivyo tutaweka pale kiasi kikubwa kuliko sh. 2,223,150 ambacho mimi nilikadiria sh. 2,500,000

3.   Matumizi au gharama zinazobadilika, hizi zinajulikana za mizunguko yote 4 kwamba ni sh. 2,223,150 kila mzunguko kutokana na jedwali letu la faida na hasara.

4.   Hivyo ili kupata salio la malighafi mwishoni mwa mzunguko wa 1 tunachukua

Malighafi za kuanzia jumlisha + Ununuzi wa malighafi Toa –Matumizi/ghara zinazobadilika

=0 + 2,500,000 – 2,223,150 = 276,850

Kwahiyo katika mzunguko wa 1 utaona kwamba fedha taslimu zilizotumika ni hizi za kununulia malighafi sh. 2,500,000 lakini pia kuna sh. 5,000 za umeme na sh. 15,000 za matangazo jumla zote ni, 2,500,000 + 15,000 + 5000 = 2,520,000

Katika mzunguko wa pili wa tatu na wanne napo unachukua matumizi yake ya fedha taslimu zitakazonunua malighafi kisha unajumlisha umeme na matangazo ambazo ni sh. elfu 5 na elfu 20 unapata jumla ya fedha zote zitakazotoka katika jedwali lako la mtiririko wa fedha taslimu.

Hili jedwali la kukisia Malighafi linasaidia moja kwa moja kufahamu salio la malighafi katika kila mzunguko ambacho ni kipengele kilicho kwenye jedwali la mizania ya biashara, ndio maana nikasema awali kuwa unapokuwa ukikokotoa baadhi ya vipengele kwenye jedwali la mtiririko wa fedha basi moja kwa moja unakuwa ukikamilisha na baadhi ya vipengele kwenye Mizania ya biashara.

Mistari mingine inayofuata katika Fedha toka ni,

2. Malipo ya bili:

Hapa ningejaza kama biashara ingekuwa inatazamia kulipa madeni ya wasambazaji kwa fedha taslimu lakini katika biashara hii hatutakopa malighafi mahali

3. Malipo ya deni la muda mrefu:

Hili nalo hakuna kwani biashara haijaonyesha kama itakopa fedha mahali

4. Ununuzi wa mali za muda mfupi

Pia hakuna

5. Ununuzi wa mali za kudumu

Katika mwaka mzima wa 1 hakuna mali za kudumu zitakazonunuliwa zaidi ya zile za kuanzia ila kwa miaka 2 inayofuata wa 2 na wa 3 utaona ongezeko la mabanda na vifaa ambavyo vyote ni mali za kudumu.

Mpaka hapo sasa unajumlisha na kupata jumla ya fedha zote zinazotoka.

Kisha unachukua jumla ya fedha Ingia na kutoa jumla ya fedha toka kupata Mtiririko wa fedha taslimu.

Baada ya hapo unachukua kianzio na kujumlisha mtiririko wa fedha taslimu katika kila mzunguko ili kupata salio la fedha taslimu mwishoni mwa kila mzunguko. Na hapo sasa ndio unakuwa umemaliza jedwali lako la Mtiririko wa fedha taslimu kwa mizunguko yote minne

 

Mzunguko wa fedha taslimu kwa mwaka 1

Hapa tunafanya kama kwenye lile jedwali la faida na hasara kwa kujumlisha safu zote zilizolala (rows) kupata safu iliyosimama (column) itakayowakilisha Mzunguko wa fedha taslimu kwa mwaka wa 1.

 

 

Kuona jedwali hili kamili jipatie semina na mchanganuo wako kamili. Unapata na offa ya vitu 6 (Michanganuo na Kitabu) muda huohuo bila kuchelewa

 

 

Kabla ya kwenda kutazama mwaka wa 2 na wa 3 hebu kwanza tukamilishe pia na makisio ya Mizania ya biashara kwa mizunguko 4 na mwaka wa kwanza kwani tumesema unapokamilisha mtiririko wa fedha moja kwa moja na mizania unakuwa pia umekamilisha.

8.5 Makisio ya Mizania ya Biashara

Unapokisia mizania ya biashara katika miezi au mizunguko ya mwaka wa 1 unaanza na Mizania ya mwanzo kutoka kule kwenye kianzio, unatumia pia jedwali la faida na hasara pamoja na jedwali la Mtiririko wa fedha taslimu kwa kuongeza au kupunguza katika vipengele vya jedwali hilo la mizania ya kuanzia.

Safu nilizoweka namba kwa rangi ya blue zote ni safu ambazo tayari namba zake unakuwa nazo ikiwa umeshamaliza kutengeneza ripoti za faida na hasara na mtiririko wa fedha katika mizunguko ya mwaka wa 1, kwa hiyo unazipachika tu kisha nyingine unazikokotoa 

 

MAKISIO YA MIZANIA YA BIASHARA

Kianzio

Mzung.1

Mzun.2

Mzung.3

Mzung.4

TZS

TZS

TZS

TZS

TZS

RASILIMALI

Mali za muda mfupi

Fedha taslimu

2,223,150

2,740,350

3,457,550

4,274,750

5,091,950

Wadaiwa

0

0

0

0

0

Malighafi

0

276,850

353,700

330,550

307,400

Mali nyinginezo za muda mfupi

0

0

0

0

0

Jumla mali za muda mfupi

2,223,150

3,017,200

3,811,250

4,605,300

5,399,350

Mali za kudumu

1,840,000

1,840,000

1,840,000

1,840,000

1,840,000

Uchakavu uliolimbikizwa

0

35,750

71,500

107,250

143,000

Jumla ya mali za kudumu

1,840,000

1,804,250

1,768,500

1,732,750

1,697,000

JUMLA YA RASILIMALI  ZOTE

4,063,150

4,821,450

5,579,750

6,338,050

7,096,350

MTAJI NA DENI

Wadai

0

0

0

0

0

Mkopo wa muda mfupi

0

0

0

0

0

Mkopo wa muda mrefu

0

0

0

0

0

Jumla ya Deni lote

0

0

0

0

0

Mtaji uliowekezwa

4,063,150

4,063,150

4,063,150

4,063,150

4,063,150

Faida iliyolimbikizwa

0

0

0

0

0

Faida

0

758,300

1,516,600

2,274,900

3,033,200

Jumla ya Mtaji

4,063,150

4,821,450

5,579,750

6,338,050

7,196,350

JUMLA YA MTAJI  NA DENI

4,063,150

4,821,450

5,579,750

6,338,050

7,096,350

 

 

RASILIMALI

1. Fedha Taslimu;

Katika safu hii ya mwanzo kabisa, namba zake unazitoa kwenye lile jedwali la mtiririko wa fedha taslimu kwenye salio la fedha taslimu pale chini kabisa, unakopi za mizunguko yote na kuweka hapa

2. Wadaiwa:

Katika biashara hii hatuna wadaiwa wowote

3. Malighafi:

Tunaenda moja kwa moja kwenye jedwali letu tulilokadiria malighafi tunachukua salio la malighafi katika kila mwisho wa mzunguko na kuja kupachika hapa.

4. Mali nyinginezo za muda mfupi:

Hatuna katika biashara hii

6. Mali za kudumu

Unaangalia kwenye kianzio ni shilingi ngapi kisha unaweka kiasi hicho kwenye kila mzunguko kwa mfano sisi hapa ilikuwa ni sh. 1,840,000

7. Uchakavu uliolimbikizwa

Limbikizo la Uchakavu linapunguza thamani ya mali za kudumu, uchakavu wa mzunguko huu ni limbikizo la uchakavu wa mzunguko uliopita + na wa mzunguko huu kutoka katika jedwali la faida na hasara ukianzia pale kwenye kianzio

8. Jumla ya Mali za kudumu

Hii ni baada ya kutoa uchakavu kwenye mali za kudumu katika kila mzunguko.

9. Jumla ya Rasilimali zote

Unajumlisha mali za muda mfupi na zile za kudumu

 

DENI NA MTAJI

Deni:

1. Wadaiwa

Upande wa pili tunaanza na Wadaiwa lakini biashara hii haina wadaiwa

2. Mkopo wa muda mfupi

Pia hatuna mkopo wa muda mfupi

3. Mkopo wa muda mrefu

Nao hatuna katika biashara hii

4. Jumla ya Deni

Hakuna tunaweka 0

 

Mtaji:

5. Mtaji uliowekezwa

Hapa tunaangalia kwenye kianzio na namba tunayoikuta pale mfano sisi ni, 4,063,150 inawekwa kwenye kila mzunguko

6. Faida iliyolimbikizwa

Tunaangalia kwenye kianzio na kuweka namba zake katika kila mzunguko, hii hubadilika mara moja tu kwa mwaka kwa kuongeza faida iliyopatikana kwa mwaka.

7. Faida

Hii tunaitoa moja kwa moja kutoka jedwali la faida na hasara, ni malimbikizo ya faida inayopatikana katika kila mzunguko

8. Jumla ya Mtaji:

Unajumlisha kuanzia pale namba 5 +6 +7 = jibu unapata la kila mzunguko

9. Jumla Deni na Mtaji:

Hapa unajumlisha deni na mtaji ambapo thamani yake kimahesabu ikiwa upo sahihi ni lazima ilingane na namba zilizoko kwenye Jumla ya Rasilimali zote upande ule wa kwanza kule juu ya hili jedwali.

 

Makisio ya Mizania ya biashara mwaka wa 1

Tofauti na ilivyokuwa kwenye jedwali la Faida na Haasara na lile la Fedha Taslimu, kwa upande wa hili la Mizania, namba za kukamilisha mali na madeni ya mwaka wa kwanza hatujumlishi namba za safu zilizolala kwenye mizunguko yote 4 hapana, bali tunachokifanya ni kuchukua safu nzima iliyosimama/column ya mzunguko wa mwisho(wa 4) na kuifanya ndiyo namba za mwaka wa 1

Makisio ya Mizania ya biashara Miaka 2 inayofuata

Kwenye jedwali lifuatalo vyumba nilivyoweka namba kwa rangi ya bluu maana yake tayari thamani yake inajulikana kutokana na majedwali yaliyokwishakamilika aidha lile la faida na hasara, mizania ya kuanzia au mtiririko wa fedha taslimu mwaka wa kwanza.

Rangi ya kijani ni namba zinazohitaji kukokotolewa lakini kwa kutumia kanuni iitwayo asilimia ya mauzo%.

Vyumba nilivyowekwa rangi nyekundu ni namba zinazohitaji kukokotolewa kutokana na namba zilizokwishawekwa kwenye hili jedwali.

1. Namba za mwaka wa kwanza (Safu iliyosimama) tayari tulishaipata kutokana na jedwali la mizania la mizunguko 4

2. Mtaji uliowekezwa sh. 4,063,150 tunaupata toka kwenye jedwali la mizania ya kuanzia na huwekwa katika safu nzima kwa miaka yote 3 pasipo kubadilika

3. Faida: Hizi ni faida kutoka katika kila mwaka ambazo tayari tunazipata kwenye jedwali la Faida na hasara la miaka 3.

4. Faida iliyolimbikizwa; Faida iliyolimbikizwa mwaka huu ni malimbikizo ya faida ya miaka iliyopita

5. Deni: Katika biashara hii hakuna deni lolote hivyo tunaweka 0 katika kila chumba cha deni

6. Jumla ya Mtaji na Deni: Tunajumlisha jumla ya mtaji na jumla ya deni vitu ambavyo tayari tunavyo ingawa deni ni sifuri(0).

7. Jumla ya Rasilimali zote: Kwa kuwa ipo kanuni isemayo Jumla ya rasilimali zote = Jumla ya Deni na Mtaji basi tunahamisha safu ya jumla ya Deni na Mtaji kama ilivyo mpaka kwenye safu ya Jumla ya Rasilimali zote.

8. Mali za kudumu

Zinajulikana kutokana na jedwali la Mizania ya kuanzia na hubadilika tu pale unaponunua mali nyingine au kuuza, sisi hapa mwaka wa 2 na wa 3 kuna mali za kudumu ziliongezeka yakiwemo mabanda na vifaa.

9. Uchakavu ni limbikizo la uchakavu kila mwaka ambapo mwaka wa pili unachukua uchakavu mwaka wa 1 kwenye faida na hasara unajumlisha na uchakavu mwaka wa pili kwenye faida na hasara mwaka wa pili, mwaka wa 3 ni hivyohivyo.

10. Jumla ya mali za kudumu: Unachukua mali za kudumu unatoa limbikizo la uchakavu.

11. Jumla ya mali za muda mfupi: Tunazipata kwa kuchukua jumla ya Rasilimali zote na kutoa jumla ya mali za muda mrefu vitu ambavyo tayari vipo.

12. Fedha Taslimu mwaka wa 2 na wa 3, Tutatumia kanuni ya asilimia ya mauzo% kwa kuchukua thamani ya fedha taslimu mwaka wa 1 na kugawa kwa mauzo ya mwka wa kwanza kisha uwiano tunaopata tunauzidisha mara mauzo mwaka wa pili. Na mwaka wa tatu ili kupata salio la fedha taslimu katika miaka hiyo.

13. Malighafi; Tunachukua jumla ya mali za muda mfupi na kutoa kiasi cha fedha taslimu na hapo tunakuwa tayari tumekamilisha jedwali letu la Makisio ya mizania ya biashara kwa miaka yote 3


Makisio ya mizania ya biashara

Mw1

Mw2

MW3

TZS

TZS

TZS

RASILIMALI

Mali za muda mfupi

Fedha taslimu

5,091,950

7,637,925

10,183,900

Wadaiwa

0

0

0

Malighafi

307,400

1,580,241

4,461,022

Mali nyinginezo za muda mfupi

0

0

0

Jumla mali za muda mfupi

5,399,350

9,218,166

14,644,922

Mali za kudumu

1,840,000

2,775,000

3,680,000

Uchakavu

143,000

360,500

646,500

Jumla ya mali za kudumu

1,697,000

2,414,500

3,033,500

JUMLA YA RASILIMALI  ZOTE

7,096,350

11,632,666

17,678,422

MTAJI NA DENI

Wadai

0

0

0

Mkopo wa muda mfupi

0

0

0

Mkopo wa muda mrefu

0

0

0

Jumla ya Deni lote

0

0

0

Mtaji uliowekezwa

4,063,150

4,063,150

4,063,150

Faida iliyolimbikizwa

0

3,033,200

7,569,516

Faida

3,033,200

4,536,316

6,045,756

Jumla ya Mtaji

7,096,350

11,632,666

17,678,422

JUMLA YA MTAJI  NA DENI

7,096,350

11,632,666

17,678,422

 

Mzunguko wa fedha taslimu kwa miaka 2 inayofuata

Baada ya kukamilisha majedwali ya Mizania ya biashara na Faida na Hasara miaka yote 3 sasa ni rahisi sana kukamilisha na hili la mzunguko wa fedha kwani kama nilivyotangulia kusema ripoti hizi tatu pamoja na mizania ya kuanzia zinaingiliana na kutegemeana.

Nitaanza kutaja vitu ambavyo tayari tunavyo kulingana na majedwali hayo mengine matatu na hapo chini nimevitia rangi ya bluu;

1. Mwaka wa 1 safu iliyosimama (column) tuliipata toka jedwali la mtiririko wa fedha taslimu jumla ya mizunguko ile 4

2. Kianzio tumekipata jedwali la mizania ya biashara la kianzio

3. Mauzo taslimu, haya tunayapata kutoka jedwali la faida na hasara la miaka 3

4. Ununuzi wa mali za kudumu; Kutoka jedwali la Mizania ya biashara mali za kudumu zililipiwa fedha taslimu (cash)

Kisha nitafuata vitu tutakavyokokotoa, nimeviwekea rangi ya kijani;

5. Jumla ya fedha Ingia: Tunachukua mauzo taslimu kama yalivyo kwani ndiyo pesa taslimu pekee inayoingia kwenye biashara

6. Mtiririko wa fedha taslimu: Kwa kutumia salio la fedha taslimu mwishoni na kianzio cha fedha taslimu mwanzoni ambavyo tayari vyote tunavyo tunaweza kukokotoa mtririrko wa fedha katika mwaka wa pili na watatu kama ifuatavyo;

Mwaka wa pili: Salio la fedha taslimu mwaka wa1 + Mtiririko wa fedha mwaka wa 2 = salio la fedha taslimu mwaka wa 2

=5,091,950 + y = 7,637,925

y =salio la fedha taslimu mwaka wa 1

y = 7,637,925 – 5,091,950

y = 2,545,975

Mwaka wa tatu: Salio la fedha taslimu mwaka wa 2 + Mtiririko wa fedha mwaka wa 3 = salio la fedha taslimu mwaka wa 3

Y =Mtiririko wa fedha mwaka wa 3

7,637,925 + Y = 10,183,900

Y = 2,545,975

7. Jumla ya Fedha Toka: Tutachukua Jumla ya Fedha Ingia –toa Mtiririko wa fedha kama ifuatavyo;

Mwaka wa pili:

 = 18,223,200 - 2,545,975  = 15,677,225

Mwaka wa tatu:

= 24,297,600  - 2,545,975  = 21,751,625

8. Matumizi ya fedha taslimu: Jumla ya Fedha toka – toa ununuzi wa mali za kudumu kama ifuatavyo;

Mwaka wa 2:

= 15,677,225 - 935,000 = 14,742,225

Mwaka wa 3:

= 21,751,625 - 905,000 = 20,846,625

 

Mpaka hapo tayari tumekamilisha jedwali letu la Makisio ya Mtiririko wa fedha kwa miaka yote 3 kama linavyoonekana hapo chini;

NB: Kumbuka tu kwamba, hapa maeneo mengi sijatumia kanuni maalumu bali nimekokotoa tu baadhi ya safu kulingana na uwepo tayari wa namba katika safu nyinginezo kutoka majedwali yaliyokwishakamilika huko nyuma.


Makisio ya Mtiririko wa fedha taslimu

Mw1

Mw2

MW3

FEDHA INGIA

TZS

TZS

TZS

Kianzio

2,223,150

Mauzo Taslimu

12,148,800

18,223,200

24,297,600

Makusanyo ya deni

0

Mkopo mpya

0

Mauzo ya rasilimali

0

Mtaji mpya

0

Jumla fedha Ingia

12,148,800

18,223,200

24,297,600

FEDHA TOKA

Matumizi fedha taslimu

9,280,000

14,742,225

20,846,625

Malipo ya bili

0

Malipo deni la muda mrefu

0

Ununuzi mali za muda mfupi

0

Ununuzi mali za kudumu

0

935,000

905,000

Utoaji gawio

0

Jumla ya fedha toka

9,280,000

15,677,225

21,751,625

Mtiririko wa fedha taslimu

2,868,800

2,545,975

2,545,975

SALIO LA FEDHA TASLIMU

5,091,950

7,637,925

10,183,900

 

8.6 Sehemu muhimu za biashara

Kipengele hiki kinahusu uwiano wa sehemu mbali mbali za biashara kutoka katika makisio ya ripoti zetu tatu kwa miaka 3. Hapa kunakuwa na jedwali ambalo unaweka uwiano wa zile sehemu muhimu. Kwa kawaida kuna uwiano wa aina nyingi lakini siyo lazima uweke kila mmoja hapa.

Katika jedwali kwenye huu mchanganuo tuliweka baadhi tu ya sehemu hizo. Unaweza kupata kanuni/formula za kukokotoa sehemu mbalimbali kutoka katika kitabu chako cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ukurasa ule wa 129

 

Jedwali: Sehemu muhimu za biashara

Tathmini ya Sehemu za biashara

Mw1

Mw2

MW3

Ukuaji wa mauzo

n.a.

50%

33.3%

 

 

 

 

Asilimia ya mauzo

 

 

 

Mauzo

100%

100%

100%

Faida ghafi (Gross margin)

26.8%

26.8%

26.8%

Jumla ya gharama za uendeshaji

1.84%

1.90%

1.91%

Faida halisi (Net profit margin)

25%

25%

25%

 

 

 

 

Asilimia ya Mali zote

 100%

 100%

100% 

Mauzo

171%

157%

137%

Wadaiwa

n.a.

n.a.

n.a.

Malighafi/Bidhaa

4.3%

13.5%

25%

Mali za muda mfupi

76%

79%

83%

Mali za kudumu.

24%

21%

17%

Mtaji

100%

100%

100%

 

 

 

 

Sehemu nyinginezo.

 

 

 

Uwiano sasa (current ratio)

n.a.

n.a.

n.a.

Uwiano haraka (Quick ratio)

n.a.

n.a.

n.a.

Faida/Mtaji (ROI)

43%

39%

34%

Faida/Rasilimali (ROA)

43%

39%

34%

Inventory Turnover

58

14

6

Mtaji endeshi (Net Working capital)

5,399,350/=

9,218,166/=

14,644,922/=

 

8.7 Muda wa mradi kurudisha mtaji (Pay Back Period)

Pay back period ni kukokotoa muda unaotakiwa ili kurudisha mtaji wa awali uliowekezwa kwenye biashara/mradi. Kanuni yake unachukua Mtaji uliowekezwa kisha unagawanya kwa faida (Faida inayoingia kwenye biashara kwa mwaka) ikiwa faida hiyo inalingana kila mwaka

Lakini utakuta kwa mfano biashara yetu hii faida inayoingia hutofautiana kila mwaka katika miaka 3 (Uneven profit) hivyo hatuwezi tu tukasema pay back period = Mtaji/Faida halisi.

Tutatumia jedwali lifuatalo kukokotoa pay back period yenye faida zinazopishana kila mwaka (uneven profit)

Mwaka

Faida

Faida inayolimbikizwa (cumulative profit)

0

(4,063,150)

(4,063,150)

1

3,033,200

(1,029,950)

2

4,536,316

3,506,366

3

6,045,756

9,552,122

 

Mwaka ‘0’ hakuna faida inayoingia isipokuwa kuna fedha inayowekezwa kwenye mradi sh. (4,063,150) ndio maana ikawekewa alama - hasi ikimaanisha inadaiwa haijarudi bado

Kwenye faida iliyolimbikizwa (Cumulative profit) mwaka ‘0’ pia ni deni lilelile la mtaji uliowekezwa

Mwaka wa 1 kuna faida sh. 3,033,200 inaingia, kwenye faida limbikizi kiasi hicho kitakwenda kupunguza deni la mtaji na mtaji utabaki ukidaiwa sh. (1,029,950)

Mwaka wa 2 kuna faida sh. 4,536,416 inaingia ambapo katika faida limbikizi itakwenda kufuta kabisa lile deni la mtaji sh. (1,029,950) na kuendelea kubakia limbikizo la faida chanya kiasi cha sh. 3,506,366

Sasa kanuni ya kukokotoa pay back period inasema hivi;

= Namba ya miaka yenye limbikizo la faida hasi + (Limbikizo la mwisho lenye alama hasi / Faida ya mwaka unaofuata

Namba ya miaka yenye limbikizo la faida hasi (A) = 1

Limbikizo la mwisho lenye alama hasi (B) = 1,029,950

Faida ya mwaka unaofuata (C) = 4,536,316

Pay back period

= A + B/C

= 1 +1,029,950/4,536,316

= 1 + 0.23

= miaka, 1.227

Sawa na Mwaka 1 na miezi 3

Kwa hiyo mtaji wa biashara hii au gharama zote za kuanzisha biashara zitarudi baada ya mwaka 1 na miezi 3

 

Na hapa ndiyo mwisho wa kipengele cha Mpango wa fedha, karibu kipengele kingine na cha mwisho cha Viambatanisho

 

 

9.0 Viambatanisho

Katika kipengele hiki cha Viambatanisho au vielelezo mimi nimeweka tu Majedwali ya hesabu kwa undani kila mzunguko wa wiki 12, laini kuna vitu vingi unaweza kuambatanisha ambavyo huwezi ukaviweka ndani ya mchanganuo wako

Ningeliweza pia kuweka, mikataba ya biashara CPPC iliyofanya na wadau wake mbalimbali, picha na ramani, kopi za matangazo, CV za viongozi, nyaraka za dhamana za mikopo, nyaraka za utafiti uliofanyika nk.


Msimu wa kuku blogu ya JifunzeujasiriamaliSEMINA SEHEMU YA 4                

 

 
SOMA NA HIZI HAPA;

1.   Kuku ni utajiri: angalia mchanganuo jinsi kuku wa mayai wanavyoweza kukutajirisha haraka

2.   Ufugaji bora wa kuku wa mayai: mchanganuo wa biashara, kuku 1000

3.   Soko la sungura tanzania linakua kwa kasi kuliko uzalishaji wenyewe

4.   Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako

5.   Ujenzi wa mabanda ya kuku isiwe kikwazo cha wewe kuanzisha biashara ya ufugaji wa kuku

6.   Utajuaje kama biashara yako ya ufugaji wa kuku itakupa faida?


0 Response to "SEMINA SEHEMU YA 5: MCHANGANUO, UFUGAJI WA KUKU CHOTARA WA NYAMA KIBIASHARA – (MPANGO WA FEDHA NA VIAMBATANISHO)"

Post a Comment