UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI: MCHANGANUO WA BIASHARA, KUKU 1000 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI: MCHANGANUO WA BIASHARA, KUKU 1000

Ufuatao ni muhtasari wa mpango wa biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai, mchanganuo mzima wa mradi huu unapatikana katika blogu maalumu ya Darasa la michanganuo ya biashara" lililoanzishawa rasmi kwa ajili ya wale wote wenye nia ya kujua jinsi ya kuandika michanganuo kwa ufasaha. Ili kuweza kuingia katika blogu hiyo na kuwa mwanadarasa wa darasa hilo unatatakiwa kuwa na kiingilio/tiketi au ada. Tikiti hiyo ni kununua tu kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali ambacho bei yake ni shilingi elfu 10.

Ndani ya Darasa utapata fursa nyingi zikiwemo, kuuliza kitu chochote ulichoshindwa kukielewa katika kitabu cha michanganuo ya biashara na ujasiriamali, kutoa michango mbalimbali ya mawazo na hata ushauri kwa wanadarasa wengine, kushirikishana na wadau wengine katika kutafuta njia za kupata mafanikio zaidi kimaisha na kiuchumi kwa ujumla. Darasa hili ni kwa upande mwingine ni kama “MASTERMIND GROUP”, kikundi cha kupeana ushauri wa ni vipi mnaweza kusogea zaidi ya pale mlipo.

………………………………………………………...................



MCHANGANUO WA BIASHARA

MRADI WA MAYAI BORA PROJECT
(KUKU 1000)







P.0. BOX 01010
KIMARA SUKA
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Simu: 255765 553030
Email: info@mayaibora.co.tz



2/11/2016

Umeandaliwa na Barikiel Sanga
Simu: +255712 202244





MUHTASARI TENDAJI.
Waanzilishi wa mradi wa Mayai Bora Project(MBP), Bwana Barikiel Sanga na Mkewe Bibi Marieth Mdegella wana dhamira ya kuzalisha mayai bora na makubwa kwa ajili ya kuboresha afya za watu lakini wakati huohuo wakijiingizia faida itakayowasaidia katika maisha yao baada ya kustaafu utumishi wa Umma.

Malengo ya mradi huu ni kuzalisha trei zipatazo 27 kwa siku ifikapo wiki ya 18 kutoka mradi unaanza na kuendelea hadi kuku watakapofikisha wiki 90, Kutoa ajira ya kudumu kwa watu wawili, pamoja na wamiliki kujihakikishia kipato endelevu pindi watakapostaafu miaka mine kutoka sasa.

Mradi utaanza rasmi hapo Januari 2017 kwenye eneo linalomilikiwa na waanzilishi wa mradi lililopo Kimara Suka jijini Dar es salaam kandokando kabisa ya Barabara iendayo Morogoro.

Moja ya siri za mafanikio ya mradi huu itakuwa ni kuhakikisha chakula bora na cha kutosha, maji safi, vitamini, madini na chanjo kwa kuku katika muda wote mradi utakapokuwa ukiendelea. Upunguzaji gharama kwa njia za kiteknolojia kama vile, kukuza majani mabichi ya kuku(hydroponic fodders) na uthibiti wa hali ya juu kabisa wa magojwa kibaiolojia(Biosecurity measures) ni vitu pia vitakavyopewa kipaumbele cha kwanza.

Mahitaji yote ya mradi ili uweze kuanza vizuri yamekadiriwa kuwa ni shilingi za Kitanzania milioni 25, fedha hizi ndizo zitakazotumika kujenga banda, chumba cha kulala mfanyakazi, ofisi/duka la mradi pamoja na gharama nyingine zote zitakazohitajika tangu mradi unaanza siku ya 1 mpaka wiki ya 18 kuku watakapoanza kutaga mayai.



Gharama za uendeshaji mradi zinazojirudia kama vile, chakula cha kulishia kuku, maji na mishaha ya wafanyakazi peke yake ni wastani wa shilingi milioni 89 katika kipindi chote cha wiki 90(miezi 2 na nusu)

Bidhaa zitakazouzwa na kampuni ni, chakula cha kuku, mayai, kuku pindi muda wao wa kutaga utakapokuwa umefikia ukomo, mbolea na mifuko mitupu iliyokwisha chakula cha kuku.

Soko la mayai wameligawa katika makundi 2, wauzaji wa jumla wa mayai na wateja wa kawaida lakini soko watakalolipa kipaumbele zaidi ni hili la wauzaji mayai kwa jumla kutokana na ukubwa na uhakika wake. Uhitaji wa mayai Tanzania na hususani jiji la Dar bado ni mkubwa sana kama takwimu za hivi karibuni zinavyoonyesha kwamba, kwa wastani Mtanzania hula chini ya mayai 100 kwa mwaka ili-hali angepaswa ale mayai zaidi ya 250 kwa mwaka.

MBP wamezungukwa na washindani wakubwa 3 lakini siyo tishio kwake sana kwani washindani hao wote wanayalenga masoko tofauti kabisa na la kwao.

Sifa za kipekee za Mayai Bora Project ni kuzalisha mayai bora na makubwa, bei nzuri kwa wateja ukilinganisha na bei ya soko pamoja na eneo zuri linalofikika na kuonekana kwa urahisi na wateja.

Ili kuhakikisha mradi unafanikiwa watatumia mbinu mbalimbali za kimasoko zisizokuwa za gharama sana lakini zenye tija kubwa kama vile, kuweka bango, kugawa vipeperushi, mitandao ya kijamii na huduma nzuri kwa wateja ambao watatoa taarifa kwa watu wengine chini ya kaulimbiu yao, “Kuku ni Utajiri”. Vile vile watatunza taarifa muhimu za wateja wao(customer database).

Mauzo yahusianayo na kuku na mayai pekeyake yanakisiwa kufikia milioni 99 na yale yahusianayo na uuzaji wa vyakula vya kuku ni milioni 92 kwa msimu wote mmoja.

Viongozi wakuu wa mradi watakuwa ni Barikiel na mkewe Marieth ambapo watawaajiri wafanyakazi 2. Wote wawili Barikiel na mkewe wana elimu ya biashara kutoka vyuo vikuu vinavyoheshimika.

Mpaka kufikia wiki ya 90 ya mradi, faida halisi ya mradi kwa ujumla inakadiriwa itakuwa shilingi milioni 21 na faida ya mayai peke yake katika kipindi cha utagaji ni wastani wa shilingi milioni 12. Baada ya awamu hii wanatarajia kuanza tena msimu mwingine wa pili kwa idadi hiyohiyo ya kuku 1,000.


  Faida na hasara kwa ufupi ya mayai kwa wiki 72 za utagaji.
















Unaweza kuusoma mchanganuo huu wa ufugaji kuku wa mayai wote kuanzia mwazo hadi mwisho pamoja na michanganuo mingine na mawazo ya biashara zaidi ya 50 ya biashara unazoweza kuanzisha hapa Tanzania kwa kununua kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali, ambapo pia unapata fursa ya kuwa mwanachama wa kudumu wa blogu ya MICHANGANUOYA BIASHARA yenye Darasa maalumu ambamo Mipango ya biashara hufundishwa kwa kina.

Unapomaliza darasa hili hakuna tena kitu kitakachokutatiza kinachohusiana na Mpango wa Biashara na Unakuwa umepata uwezo mkubwa wa kuanzisha na kusimamia biashara yeyote ile kwa ufanisi wa hali ya juu.

Kujiunga na Shule hiyo ya Michanganuo, unatakiwa kwanza, kutuma anuani yako ya E-mail(ni lazima iwe ya GMAIL) mfano, wewe@gmail.com. Kitu cha pili muhimu, lipia kitabu cha “MICHANGANUO NA UJASIRIAMALI” chenye kurasa 410 kwa shilingi 10,000/=. 

Nami nitakutumia kitabu hicho kupitia hiyo email mara moja na Tayari sasa utakuwa umekwisha kuwa mwanachama rasmi wa darasa hili la aina yake kuwahi kuanzishwa hapa Tanzania. Hakuna gharama za ziada utajifunza kwa miezi 3-6 Ordinary Level halafu tena miezi mingine 3 Advanced Level ambapo utakuwa umewiva kwelikweli.

Ukitaka kulipia kitabu, tumia Tigo pesa au Mpesa na namba ni hizi hapa, 0712 202244   au  0765 553030 jina litatokea, Peter Augustino Tarimo.








0 Response to "UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI: MCHANGANUO WA BIASHARA, KUKU 1000"

Post a Comment