KUPATA MTAJI WA BIASHARA CHA MSINGI NI WAZO NA MUDA WAKO, PESA BAADAE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUPATA MTAJI WA BIASHARA CHA MSINGI NI WAZO NA MUDA WAKO, PESA BAADAE


Katika makala hii ya leo nitajibu swali juu ya moja kati ya changamoto inayowakumba wajasiriamali wengi hasa pale wanapotaka kuanzisha biashara zao. CHANGAMOTO YA MTAJI. Karibu usome kujua changamoto hii ni vipi tunaweza kukabiliana nayo na hatimaye kuishinda.

Karibu kila mtu utakayemgusa kuhusiana na kuanzisha biashara/ujasiriamali, kitu cha kwanza atakachokuambia ni; “Sina mtaji, mtaji nitautoa wapi, mtaji nilio nao ni kidogo mno hutoshi nk. Kwa wale waelimishaji wanaotoa elimu ya ujasiriamali kama mimi ukiwauliza ni changamoto zipi kubwa wasomaji au wasikilizaji wa semina na masomo yao wanazokutana nazo watakuambia changamoto kubwa wanayoombwa utatuzi wake ni hii ya jinsi ya kupata mtaji kwa ajili ya kuanzishia biashara.

SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara mbili ya mtaji utakaowekeza?  

Swali nitakaloenda kujibu leo, lilitoka kwa mfuatiliaji wangu mmoja kwa njia ya email, na nitalitaja jina lake moja tu, Fredi. Fredi aliniuliza kama ifuatavyo,


Nashukuru Sana Kwa mafunzo yako lakini changamoto kwetu Sisi vijana ni moja na changamoto hiyo ndio inayotufanya mawazo mengi kuozea ndani,  changamoto hiyo ni MITAJI  Vipi tutapataje MITAJI ??


MAJIBU
Ngoja nikuambie kitu kimoja Fred, Ukweli watu wengi wasioukubali ni kwamba, haiwezekani kuanzisha kitu wakati tayari unacho. Kanuni ya kimaumbile inajieleza wazi kwamba, “mtu huwa anataka kuanzisha kitu au kuwa na kitu kwa sababu kitu hicho hana” Sijui kama umenipata lakini nitafafanua zaidi usihofu.

SOMA: Biashara 5 za mtaji kidogo kuanzia elfu 2, kumi mpaka laki moja unazoweza kuanza zikakutoa.

Katika kuielezea vizuri dhana hii, nitatumia mfano au kanuni mbili maarufu (Siyo za kwangu, sijazitunga mimi) namimi nilijifunza tu mahali pengine. Kanuni hizo 2 ndiyo zinazoelezea pande zote mbili, ule wa wanaotaka kuanzisha biashara wakiwa tayari na mitaji mkononi na upande wa pili ni wa wale wanaoanzisha biashara wakiwa hawana kitu chochote kile kama mtaji isipokuwa mawazo yao pekee. Zishike vizuri kanui hizi zinaweza kukusaidia.

(1)        Kumiliki – Kufanya – Kuwa au (To have – To do – To Be)

(2)        Kuwa – Kufanya – Kumiliki au (To Be – To do - To have)
1. Maana ya kanuni ya kwanza, miliki-fanya-kuwa (have-do-be) ni kwamba, Ili uweze kuwa mtu fulani(kuwa) unahitaji kwanza uwe unamliki kitu fulani(miliki) ndipo uweze kufanya kitu fulani(kufanya) kitakachokuwezesha kuwa yule unayetaka kuwa. Kwa wale wote wanaofikiria kwamba hawawezi kuanza biashara bila kwanza kuwa na mtaji wapo kwenye kundi hili  la (have-do-be). Mtu anafikiri ili atajirike ni lazima awe na pesa kwanza ndipo afanye biashara itakayompeleka kwenye utajiri au, Ili mtu awe na mahusiano mazuri ni lazima apendwe kwanza ndipo na yeye aweze kupenda.

SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado.

Ikiwa wewe ni muumini wa kanuni hii ya kwanza ya kuwa nacho kwanza ndipo utende, haitatokea siku uje ufanikiwe kamwe, labda tu itokee umeshinda bahati na sibu jambo ambalo hutokea kwa nadra mno na kwa watu wachache. Akili ya ‘mpaka uwe nacho’ itakuzuia kabisa kuanza kitu na hata kama utalazimisha vyovyote vile bado akili hiyohiyo itakuja kukuambia tu ‘ACHA’ pale biashara kwa bahati mbaya itakapokuja kupitia  vipindi vigumu kama cha kukosa pesa(mdororo), hata ikiwa ni wa muda mfupi. Ni vigumu sana kuwa na hamasa ya kuendelea kuwekeza katika biashara yako ukiwa na mawazo ya (To have – To do – To be)

2. Kwenye kanuni ya 2, Unakuwa kwanza vile unavyotaka uwe, kabla ya mambo mengine yote(You be), kisha Unafanya(you do) na mwishoni ndio unamiliki kitu(You have). Huwa ukipanga namba mfano 3+5 jibu lake ni sawa tu na kusema 5+3 lakini kwa kanuni hizi 2 mambo ni tofauti kidogo, kumiliki – kufanya – kuwa siyo sawa na kusema, kuwa – kufanya – kumiliki. Wakati kanuni ya kwanza haileti matokeo mazuri ile ya pili ndiyo kanuni ya kimafanikio kwa wale wote wanaoanza biashara wanapaswa kuitumia.

SOMA: Kwanini vitabu na semina za elimu ya pesa na mafanikio haviwasaidii watu wngi?

Mwandishi mmoja, Stephen Covey aliwahi kusema kwamba,

“Katika maisha kila mtu huumbika mara mbili, kwanza ni katika akili yake na pili ni katika mwili wa nyama(material world)” - Stephen Covey

Tunapozungumzia (Kuwa – Kufanya – Kumiliki) tunaingia moja kwa moja kwenye mpango wa biashara. Wakati ukifanya mpango wa biashara yako unaweza kuwa huna chochote kile mfukoni lakini mpango wa biashara unakusukuma wewe kuifahamu biashara yako nje ndani kabla hata haujaianzisha. Unatengeneza Maono*Vision). Maono au vision ndio ‘To be yako/ jinsi unavyotaka uje kuwa’ miaka kadhaa ijayo. Na ndio maana katika mpango wa biashara huwa Visio na Mission tunaviweka vitu vya mwanzo mwanzo kabisa ili kutupa picha ya jinsi tunavyotaka tuje tuwe kabla hata hatujawa kiuhalisia.

SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako

Kuamua unataka kuwa nani maishani(To be) huwa haigharimu kitu chochote kile ni mawazo tu ila kinachohitajika hapo ni muda wa kufikiria pamoja na kufanya utafiti. Unawekeza muda wako katika mchakato wa kuwa yule unayetaka kuwa. Maarifa yote utakayoyapata kutokana na mchakato huo ndiyo sasa yatakayokulazimisha kufanya VITENDO, na Vitendo mwishowe ndiyo vitakavyosababisha MATOKEO umiliki kitu.

Maneno haya matatu, KUWA – KUFANYA – KUMILIKI yanaweza yakabadilisha kabisa maisha yako ikiwa utaamua kuyazingatia. Kwa mfano watu wakishafahamu kuwa wewe ni muaminifu wanaweza kukupa mali kwa malikauli tu bila ya kutoa pesa na utakapokwenda kuuza tayari unamiliki faida yake bila kuwa na mtaji wakwako mwenyewe. Hivyo Utahitaji tu muda wa kupalilia aina nyinginezo za mitaji tofauti na pesa ili kupata cha kuanzia na si lazima uwe na mtaji PESA.

SOMA: Biashara ndogondogo 7 zenye faida kubwa unazoweza kuanzisha bila mtaji kabisa.


Mtaji mwingine ni maarifa, tenga muda wako kidogo wa kupata maarifa mbalimbali mfano hata maarifa ya kuanzisha viwanda vidogovidogo kupitia Group la MICHANGANUO-ONLINE na mwisho wa siku unaanzisha kiwanda chako kidogo kwa mtaji kidogo sana au bila ya mtaji kabisa wa fedha. Usije ukakubali mawazo yako yakaozea ndani kwa ndani kisa eti ni mtaji. Kuna mitaji ya aina nyingi zaidi ya pesa unayoweza ukaitumia kuanzisha biashara yako, kinachohitajika ni ubunifu tu na muda wako, na baada ya muda pesa zitakuja zenyewe.

Sisemi kwamba mtaji wa pesa siyo muhimu hapana, pesa za kutosha ni muhimu sana hasa pale ambapo unakuwa sasa umeshatengeneza biashara endelevu inayoingiza pesa. Ijapokuwa pesa inazoingiza siyo nyingi sana lakini angalao una uhakika ni lazima kila siku au kila mwezi iingize kiasi fulani cha fedha bila kutegemea mtaji kutoka nje.

SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji wa kutosha ni wasa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini 


Sasa ikifikia hatua hii ndiyo muda muafaka wa kwenda kutafuta pesa nje kama vile kutoka mabenki na taasisi nyinginezo mbalimbali za kifedha kwani unao uhakika biashara itakuwa na uwezo wa kuzirejesha.

……………………………………………………..


TAARIFA HII NI KWA ANAYEHITAJI TU.
Taarifa au matangazo ninayoyatoa hapa chini hayahusiani na somo ulilosoma bali hii ni njia tu ya kukujulisha mambo mengine tunayotarajia kuwa nayo au tayari yapo.


1.KITABU KIPYA!
Kile kitabu nilichoahidi katika makala iliyopita kimetoka rasmi hapo jana tarehe 5 September 2019 na kinaitwa, SAIKOLOJIA NA UTAMBUZI WA HALI YA JUU KIFEDHA. Kitabu hiki bei yake ni shilingi 10,000/= na ukikinunua ndani ya wiki hii unapata na offa INAYOISHIA YA VITU14,  Semina yetu ya kiwanda cha tofali za saruji ya mwezi uliopita pamoja na kujiunga na Group la MICHANGANUO-ONLINE.

Kupata kitabu hicho na OFFA zote nilizotaja lipia sh. Elfu 10 kupitia namba, 0765553030  au 0712202244 na ujumbe wa wasap au SMS usemao, “NITUMIE KITABU CHA SAIKOLOJIA YA PESA NA OFFA INAYOISHA MUDA WAKE

2.SEMINA YA KIWANDA SEPTEMBA 15
Semina yetu ya pili kuhusu viwanda vidogo zimebakia siku 10 tokea siku ya leo. Semina itahusu, KIWANDA CHA USAGISHAJI NAFAKA na mchanganuo wake unatarajiwa kuwa na ubunifu wa kipekee hasa katika eneo la Soko. Si semina ya kukosa kabisa ikiwa wewe ni mtu mwenye maono ya kumiliki kiwanda siku moja. Kujiunga na semina hiyo lipia kama nilivyoeleza hapo juu kwenye taarifa ya Kitabu kipya.

3.MASOMO YA KILA SIKU YA FEDHA
Ndani ya group la MICHANGANUO ONLINE masomo ndiyo yanashika kasi kila siku, masomo yetu ni ya kipekee, huwezi kuyapata mahali pengine popote pale. Kujiunga lipia kama ilivyoelezwa kwenye namba 1 hapo juu.

4. KIWANDA CHANGU MWENYEWE
Niliahidi katikati ya hizi semina za kila mwezi za viwanda nitazindua kiwanda changu mwenyewe, na wewe nitakushirikisha katika uzinduzi huo. Namshukuru Mungu maandalizi yanaenda vizuri na tayari nimeshaanza kuzalisha prototype(bidhaa za mfano) Ni aina ya kiwanda kidogo lakini unaweza ukakiweka katika viwanda vya kati ikiwa mtu unazo rasilimali nyingi kidogo. Cha kuvutia zaidi kiwanda hiki umetumika ubunifu zaidi, mtaji wa pesa ni kidogo sana. Naamini nitawafundisha na wengine wengi watakaopenda kuanzisha katika maeneo yao. Habari zaidi nitaendelea kukujuza kabla ya siku ya uzinduzi wenyewe rasmi.

ASANTE KWA MUDA WAKO,

PETER A. TARIMO
WHATSAPP: 0765553030


0 Response to "KUPATA MTAJI WA BIASHARA CHA MSINGI NI WAZO NA MUDA WAKO, PESA BAADAE"

Post a Comment