SIRI MADUKA YA KINA MANGI, WAPEMBA NA WAKINGA SIKU HIZI KUTOKUAJIRI MTU BAKI ZAIDI YA WAKE ZAO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SIRI MADUKA YA KINA MANGI, WAPEMBA NA WAKINGA SIKU HIZI KUTOKUAJIRI MTU BAKI ZAIDI YA WAKE ZAO

MWANAMKE AKIUZA DUKA NA MUMEWEW

Hapo zamani miaka ya nyuma kidogo jamii za Wahindi, Wachagga, Wakinga na Wapemba zilisifika sana kwenye tasnia ya biashara za maduka hususani maduka yale ya rejareja hata kukazuka majina na misemo  kama vile; dukani kwa Mangi, dukani kwa Mpemba, maduka ya wakinga kariakoo na maduka ya Wahindi au “Wadosi” katika kila mji ulioenda. 

Hata hivyo siku hizi kutokana na mwamko mkubwa wa ujasiriamali nchini dhana ya biashara hii kumilikiwa na makabila hayo machache inazidi kutoweka na kila mtu sasa kutoka makabila mengine tofautitofauti wameanza kuzichangamkia fursa za biashara hiyo maarufu nchini.

Leo tunaichunguza tabia moja ya kushangaza sana ambayo miaka mingi huko nyuma ilionekana ni tabia ya Wahindi zaidi kuliko jamii zingine, tabia ya wenye maduka ya rejareja kukaa wenyewe dukani au na wenza wao tu. Ni mwiko kumwamini mtu mwingine ashike pesa dukani kwao.

Mhindi na Mwarabu hata leo hii ukifika dukani kwake anaweza kuwa na wafanyakazi hata watano wa kuhudumia wateja lakini pale kwenye fedha(Cashier) hukaa mwenyewe habanduki na hata ikishindikana basi labda mke wake, basi. Hata mwanaye ni mara chache sana anaweza akamwamini labda tu iwe ni muda mwafaka umewadia na anamfundisha kazi kwa ajili ya mpango wa kumrithisha mali. Mhindi akitaka kwenda lunch mchana saa 7 anapiga kufuli duka na kuwaacha wahudumu wa duka nje wakilinda geti mpaka atakaporudi ndipo kazi iendelee.

Kilichonisukuma kuandika makala hii ni utafiti wangu nilioufanya kutaka kujua, je siku hizi wachagga, wakinga na wapemba huajiri kina nani kwenye maduka yao? Maana zamani hasa hasa Wachaga walipendelea sana kuajiri ndugu zao waliowatoa vijijini huko Kilimanjaro. Mtu ‘alivizia’ ule muda wa vijana kumaliza darasa la saba anakwenda kutafuta kijana na kuja kumpa kazi ya kuuza duka, kijana akikaa kwa uaminifu mwishowe anamfunguliwa na yeye duka lake ili ajiendeleze kimaisha mwenyewe kama malipo ya kufanya kazi kwake muda wote huo.

Nimegundua kwamba siku hizi watu wengi mijini na hata vijijini wameachana na kasumba hii kwa kiasi kikubwa na badala yake wanafanya kazi wenyewe ama na wenza wao tu basi, ikiwa wote hawapo basi na duka hufungwa kama wafanyavyo Wahindi.

Sababu kubwa inayofanya wenye maduka kutokuajiri watu, kwanza ni vijana wengi siku hizi kuendelea na masomo ya sekondari, watu wengi kutokuwa na uaminifu tena kwenye pesa, unamwajiri mtu leo dukani, lakini yeye anajiongeza baada ya miezi michache tu anataka amiliki lakwake, watu wengi hasa vijijini kuhofia imani potofu za kishirikina kuwa eti matajiri mijini huwachukua misukule watoto wao pindi wanapowaajiri na kupelekea vifo vya ghafla au madhara mengine mbalimbali kimwili na kiakili.

Utafiti huu mpya unasadifu kile nilichokuwa nimekiandika kwenye kitabu changu cha MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA, kwamba njia nyepesi zaidi ya usimamizi wa duka changa linaloanza ni ile ya mmiliki mwenyewe au na mwenza wake kuuza dukani basi. Uzoefu unaonyesha watu wengi waliofanikiwa kwa muda mfupi katika biashara hii ya duka la rejareja ni wale wanaouza wenyewe au na wenza wao tu.

Hii inamaanisha kwamba mtu mwingine yeyote yule anayetaka kufungua duka lakini hana muda wa kuuza mwenyewe wala mwenza wake hana muda pia, pengine wana majukumu mengine kikazi mahali, ni lazima wachague njia ya kumuajiri mfanyakazi, na kwa kuwa haiwezekani kuwapata vijana wadogowadogo kutoka kijijini hawana budi kuwaajiri watu wengine wa kawaida tu, wale hata waishio mjini hapohapo.

Kumchukua mfanyakazi wa duka kwa mtindo huo kuna changamoto moja kubwa ya mahesabu. Ni kwa namna gani utaweza kumdhibiti huyu mfanyakazi msiokuwa na uhusiano wowote ule wa damu na yeye katika jukumu lenye mtihani mkubwa namna hii la pesa?  Wahindi si wajinga na wana uzoefu wa biashara hizi kwa mamia ya miaka tokea huko kwao Uhindini, wanafahamu pesa ilivyokuwa tamu na inavyotamaniwa na kila mtu.

Kudhibiti mahesabu ya duka la rejareja kwa staili hii ya Mhindi ni nzuri na ina tija ndio maana katika kitabu niliandika kwamba huo ni mfumo unaofaa sana hasa pale mtu anapokuwa anaanza biashara ya duka bado mtaji wake ukiwa haujakua sana kiasi cha kufikiria kufungua matawi mengine. Lakini vipi kama mtu sasa umeshafikia hatua ya kujitanua unataka umiliki maduka zaidi ya moja?

Na mtu ukitaka kutajirika kwa duka moja inawezekana lakini itakuchukua muda mrefu kidogo ila ukitaka kutumia muda mfupi kutajirika huna budi kuwa na maduka zaidi ya moja. Au, ni kwa jinsi gani utajigawa ikiwa una kazi nyingine mfano ajira lakini ungetaka kuwa na duka mahali la kukuongezea kipato cha ziada? Au inakuwaje kama mmiliki wa duka bado hajaoa na angependa kumuweka msaidizi dukani?

Nimekumbuka pia Mwanafunzi mmoja hivi karibuni aliniomba ushauri afanyeje ili biashara yake ya duka la rejareja aliyoanzisha baada ya kuhitimu kidato cha nne na sasa amepata nafasi katika chuo fulani anachotarajia kujilipia ada mwenyewe kwa pesa ya hilo duka, amepanga alihamishie jirani na hicho chuo, lakini changamoto kubwa inayomkabili ni msaidizi wa kwenda kukaa pale dukani kusudi yeye awe anafika tu pale kucheki hesabu zake na kurudi chuoni. Na hata ikiwa atampata, je, ni mfumo upi rahisi wa udhibiti atakaotumia ili faida yake iendelee kuonekana laivu bila chenga na mtaji kubakia vilevile bila ya kudokolewa na msaidizi?

Majibu ya maswali yote niliyouliza katika aya mbili zilizopita yanapatikana katika ukurasa wa 99 – 101 wa KITABU CHA MAFANIKIO YA BIASHARA, DUKA LA REJAREJA toleo jipya la mwaka 2023 ambapo njia iliyokuwepo kabla ya kusimamia na kudhibiti stoku ya duka imefafanuliwa na kurahisishwa zaidi kwa mjasiriamali wa kawaida kuweza kuielewa bila ya kuhitaji msaada wowote ule. Tumeweka hatua 7 za kufuata, majedwali mtu anayoweza kubadilisha na kujaza tu namba zinazoendana na biashara yake pasipo kuanza upya moja kwa moja.

Chakufurahisha zaidi ni kwamba njia hii haihitaji mahesabu mengi na wala haijalishi ikiwa kama wewe unatumia  mifumo ya kiuhasibu ya kuweka kumbukumbu kidigitali ama daftari la kawaida la mahesabu, vyote hufanya kazi vizuri. Kifupi ni njia rahisi sana ya kudhibiti hesabu za duka la rejareja kwa wajasiriamali wa kawaida mitaani wanaoteseka na udokozi na hujuma za wasaidizi ama wafanyakazi wao.

Kitabu hiki pia kina mbinu nyingine nyingi za uanzishaji na uendeshaji wa biashara ya rejareja mwandishi alizoandika akitumia uzoefu wake binafsi kwenye biashara hii kwa takribani muda wa miaka 12, mfano ni jinsi alivyoanzisha duka la rejareja mtaa wa Msimbazi Karikoo Jijini Dar es salaam akiwa na mtaji mdogo sana, mfano huo umewekwa katika kitabu ukurasa wa 10 kwa picha za rangi tangu akianza na keki na soda mpaka anafungua duka kamili na msaidizi wa kazi ya mauzo.

Mjasiriamali anayenunua kitabu hiki pia anayo fursa ya kuwasiliana na mtunzi wa kitabu moja kwa moja kupitia namba zake, 0712202244 au 0765553030 kwa ushauri zaidi ama jambo jingine lolote lile ndani ya kitabu ama kuhusiana na biashara ya duka la rejareja, jambo ambalo anaona hajalielewa vizuri ili kupata ufafanuzi wa kutosha.

Ikiwa una duka la rejareja, biashara yeyote ile ya rejareja ama una ndoto kichwani siku moja uje ufungue biashara hii basi kitabu hiki siyo cha kukosa, ni moja kati ya asseti zako muhimu kabisa katika kufanikisha biashara itakayokutiririshia pesa mithili ya mgodi wa almasi.

Kumbuka duka la rejareja ndiyo biashara rasmi nyepesi zaidi kufungua na mtaji mdogo na imewaweka watu wengi mjini na hata vijijini kuna watu wanatajirika kwa biashara hii. Usikubali kamwe duka likufanye kuwa mtumwa wa kukaa hapo masaa yote 12, siku 7 za juma, unaweza ukaweka msaidizi ‘ukaenjoy' uhuru wako huku hesabu zako zikiwa salama pasipo kudokolewa hata senti 5

Kitabu cha biashara ya duka la rejareja 2023

UPATIKANAJI WA KITABU:

Kitabu kinapatikana kwa njia kuu 3 zifuatazo;

1. NAKALA-NGUMU (HARDCOPY)

Ukiwa Dar es salaam wasiliana na sisi kwa namba 0712202244 tutakufikishia ulipo na kulipa shilingi elfu 15 (15,000/=) nauli ni juu yetu sisi wenyewe.

Kama upo mkoa mwingine wowote ule tujulishe tutakutumia kwa njia ya basi kwa shilingi elfu 25 (25,000)

2. NAKALA-LAINI (SOFTCOPY) KWA E-MAIL

Ukiwa Popote pale duniani, lipia kitabu shilling elfu 5 (5,000/=) kupitia namba 0712202244 au 0765553030 jina, Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe watsap au sms usemao, “NATAKA KITABU CHA DUKA” kisha nitakutumia kitabu chako muda huohuo kwenye simu au kompyuta yako.

3. NAKALA-LAINI (SOFTCOPY) KUPITIA APPLICATION YA GETVALUE

Kwa kutumia simu yako ya smartphone unaweza kufuata kiungo kifuatacho ukakinunua kwenye mtandao wa GETVALUE kwa shilingi elfu 10 (10,000/=)

Fungua mtandao wa GETVALUE hapa kununua kitabu cha duka la rejareja sasa hivi.SOMA NA HIZI PIA: 


1. Jinsi ya kujua faida ya duka la rejareja kila siku jioni unapofunga hesabu zako

2. Faida Duka la mahitaji ya nyumbani: niweke akiba kiasi gani cha mapato ya siku?

3. Aina za bidhaa za duka zenye faida ndogo lakini hutoka harakaharaka

4. Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja 

5. Mtaji wa biashara ya duka la rejareja, nianze na shilingi ngapi ili nifanikiwe? 

6. Hatua sita (6) za kuanzisha biashara ya rejareja (duka) sehemu ya II

0 Response to "SIRI MADUKA YA KINA MANGI, WAPEMBA NA WAKINGA SIKU HIZI KUTOKUAJIRI MTU BAKI ZAIDI YA WAKE ZAO "

Post a Comment