JINSI YA KUJUA FAIDA YA DUKA LA REJAREJA KILA SIKU JIONI UNAPOFUNGA HESABU

Kwenye kipengele cha USHAURI, maswali na majibu leo hii tunalo swali kutoka kwa msomaji wetu mmoja kuhusiana na moja kati ya changamoto za biashara ya duka, aliyetaka kujua ikiwa kama yuko sahihi ama la katika njia anayoitumia kujua faida nayoipata kila siku katika biashara yake ya duka la rejareja, maarufu kama duka la vyakula.

SOMA: Kitabu cha Mafanikio ya biashara ya duka la rejareja Toleo jipya 2020(New Edition)

Bila ya kupoteza wakati hebu tuanze na swali lenyewe, na mimi naliweka hapo chini kama alivyouliza kupitia watsap bila ya kuongeza wala kupunguza chochote;

Habari yako ndugu Tarimo,


ni namna gani rahisi, nzuri ya kujua faida ya biashara ya duka kwa siku??


Je nipo sahihi.?

Nilipoanza kununua bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kufungua duka, niliorodhesha bidhaa zote bei ya kununulia na bei ya kuuzia, mwishoni nikapata jumla kuu na kuchukua jumla ya kuuzia nikatoa na jumla ya kununulia, hiyo tofauti niliyoipata nikaiita faida ghafi.

Sasa hiyo faida ghafi nikaga wanya na ile jumla ya kununulia  ,hapo nikapata asilimia ya ile faida ghafi kama 33%, sasa hapo nikasema asilimia 14% ni gharama za kila siku za duka na asilimia 19% ni faida baada ya matumizi (net profit)

Sasa kila siku wakat wa kufunga duka ninachukua mauzo ya siku husika ninazidisha na ile 33% hapo napata fedha kama faida ,alaf natafuta tena 14% hiyo nasema ni gharama na asilimia 19% ndio faida yangu ambayo itanisaidia kupata mlo wa familia kwa kesho yake.


Je nipo sahihi?


Swali alilouliza mdau watsap ni hili hapa

MAJIBU

Ingawa katika kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA tumeweka njia sahihi zaidi ya kujua faida unayopata katika duka larejareja kila siku lakini kwa ujumla njia yako ya kujua faida halisi ya duka unayoipata kwa siku ipo sahihi pia isipokuwa tu kuna baadhi ya sehemu ambazo ningependa kushauri ufanye marekebisho kidogo; 

Vilevile pia njia yako hii ni ya makadirio zaidi hivyo faida utakayokuwa ukikata inaweza isiwe sahihi kwa asilimia 100% ingawa itakaribiana sana au kupungua kidogo kutokana na sababu kwamba umetumia asilimia ya mauzo jambo ambalo siyo kila siku utakuwa ukiuza bidhaa zenye kiwango cha faida kinachofanana kwa asilimia 100%.

SOMA: Aina za bidhaa za duka zenye faida ndogo lakini hutoka harakaharaka

Kumbuka  kwamba unapokadiria faida ghafi ni asilimia 33% ya mauzo yote, zipo siku nyingine utauza bidhaa zenye faida ghafi kidogo zaidi na kuna siku pia utauza bidhaa nyingi zilizo na faida ghafi iliyo juu kidogo ya wastani uliokadiria wa 33%.

Hata hivyo pamoja na kasoro hiyo ndogo bado wastani huo hautapishana sana na hali halisi iwapo mtu utaamua kuitumia kwani bidhaa za duka la rejareja nyingi huwa asilimia ya faida inalingana au kukaribiana sana.


Marekebisho ninayopendekeza katika njia yako hii ni haya hapa chini japo siyo lazima:

Kwa kawaida vipengele vya Hesabu za Faida na Hasara, ukiacha MAUZO, vitu vingine vyote huwa chini yake kuanzia faida ghafi mpaka faida halisi. Kwahiyo vitu hivyo vingine mara nyingi huwa vinatafutiwa asilimia zake katika Mauzo na siyo katika bei ya kununulia  kama wewe ulivyofanya kwenye mfano wako pale juu(ingawa unaweza kutumia bei ya kununulia pia). Hivyo pale uliposema hivi;

 

 Sasa hiyo faida ghafi nikagawanya na ile jumla ya kununulia, hapo nikapata asilimia ya ile faida ghafi kama 33%

….Siwezi kusema hukuwa sahihi lakini mara nyingi zaidi huwa yanatumika mauzo kutafuta asilimia ya faida ghafi, badala yake nafikiri ungegawa faida ghafi uliyoipata kwa jumla ya bei ya kuuzia na kuzidisha mara 100, ili kupata asilimia 33% au yeyote nyingine kulingana na kiasi chako cha mauzo.

SOMA: Hatua kumi (10) za kuanzisha biashara ya rejareja - DUKA

Asilimia 14% ya gharama za kila siku ingawa hujasema umeipataje lakini bila shaka hizi ni gharama za kudumu za uendeshaji mfano kodi ya pango na pengine umeme na ushuru wa taka, ambazo hazitegemei kama umeuza au haujauza. Hapo upo sahihi ingawa “fiqure” zako zaweza kuwa tofauti ikiwa utagawa faida ghafi kwa bei ya mauzo na wala si bei ya manunuzi.

Pia hiyo asilimia 19%(Faida halisi) uliyodai ni kwa ajili ya mlo wa kila siku wa familia, mimi ningeshauri pia kwa ajili ya uendelevu wa duka lako basi usiimalizie kwenye mlo bali tenga tena hapo kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kuongezea mtaji wako wa duka, ili nalo liweze kukua vinginevyo itafika siku litazidiwa na kuzorota au hata kufa kabisa. 

SOMA: Puuza Imani na dhana hizi potofu ufanikiwe katika biashara yako ya duka la vyakula

Kwa ufafanuzi zaidi wa hesabu ya faida na hasara pamoja na kujua faida kamili ya duka kila siku jioni, soma katika kitabu changu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA kwenye sura inayohusiana na Usimamizi na Hesabu za duka la rejareja hasa kurasa za 82 – 83 pamoja na uk.  92

Jawabu nililompatia mdau wetu kupitia njia ya whatsap

Mbali na kujibu changamoto mbalimbali kubwa za biashara ya duka la rejareja na biashara nyingine zote za rejareja lakini pia kitabu hiki kina mifano ya vitabu au madaftari ya hesabu zote muhimu za biashara hii za siku na za mwezi kama vile, Mfano wa daftari la mauzo, mfano wa daftari la manunuzi ya bidhaa la kila siku, mfano wa daftari la gharama za kudumu, mfano wa daftari la wakopaji (wadaiwa), mfano wa daftari la wadai, mfano wa daftari la fedha taslimu, mfano wa daftari la mali za kudumu nk. 

SOMA: Jinsi ya kusimamia hesabu katika biashara ndogo unayomwachia mfanyakazi

Tumeangazia pia kwa kina sana changamoto sugu ya namna ya kupata mtaji wa kuanzisha duka la rejareja pamoja na mfano halisi katika picha za rangi na maandishi jinsi mwandishi wa kitabu hiki alivyoweza kuvuka kihunzi kigumu cha kupata mtaji wa biashara yake ya kwanza kabisa ya rejareja akianzia na sifuri kabisa mitaa ya msimbazi Kariakoo mpaka kumiliki duka lililotoa ajira kwa watu wengine wawili.


JINSI YA KUPATA NAKALA YA KITABU CHA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA KWA NJIA YA MTANDAO (NAKALA-TETE) ;

Lipia sh. elfu 5, (5,000/=) kwa Tigo-pesa au M-pesa na namba zetu ni, 0712202244 au 0765553030 Jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha nitakutumia kitabu kupitia WHATSAPP au EMAIL yako ndani ya dakika 3 mpaka 5 

Jalada, upande wa nyuma na mbele la kitabu cha mafanikio ya biashara ya duka la rejareja-new edition 2020

 

0 Response to "JINSI YA KUJUA FAIDA YA DUKA LA REJAREJA KILA SIKU JIONI UNAPOFUNGA HESABU"

Post a Comment