PUUZA IMANI NA DHANA HIZI POTOFU UFANIKIWE KATIKA BIASHARA YAKO YA DUKA LA VYAKULA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PUUZA IMANI NA DHANA HIZI POTOFU UFANIKIWE KATIKA BIASHARA YAKO YA DUKA LA VYAKULA

Uchawi na chumaulete kwenye biashara
Waafrika karibu wote tuliokuwa na dini za kigeni na hata wale ambao bado wanashikilia zile imani za tangu jadi walizokuwa wakiamini mababu zetu waliotutangulia, kuna vitu ambavyo bado tunaviamini wakati mwingine bila hata kujua tunaiamini, vitu ambavyo kimsingi havina mantiki wala ukweli wowote ule.

(A). IMANI  POTOFU.
Watu wanazo  imani nyingi potofu zisizokuwa na uthibitisho juu ya biashara ya duka na biashara kwa ujumla wake. Wakati mwingine imani hizo zinaweza zikawa na athari kubwa sana kwako hasa ikiwa hautatambua ukweli wake na ukazifanya ndio zikuongoze katika suala zima la uendeshaji wa duka lako. Baadhi ya imani  hizo potofu ni kama hizi zifuatazo;

1. Kuna watu “chuma ulete” walio na uwezo wa kuiba mauzo uliyouza kwa njia za kishirikina.
Hili ni suala la kiimani zaidi na sidhani kama kuna  ukweli wowote,  Hebu jiulize swali hili jepesi “hivi  kweli kama kuna binadamu mwenye uwezo huo, ni kwa nini asiende benki kwenye mabilioni ya hela akawaibia ama kwenye maduka makubwa mjini  aje akuibie senti zako kidogo pengine zisizotosha hata kuunulia baiskeli?


Utakuta  mara nyingi hivi ni visingizio wanavyotoa watu baada ya kushindwa kuendesha maduka yao kwa ufanisi na wakati mwingine mfanyakazi/msaidizi dukani anaweza akafanya hujuma na kusingizia ni ‘chuma ulete’ wanaoiba pesa.

2. Kuwatuhumu ushirikina na kuwatilia mashaka  baadhi ya wateja bila sababu za msingi.

Utakuta  mtu na usomi wake, hata amefika chuo kikuu lakini bado hofu ya kulogwa au kuibiwa pesa kwa njia za kishirikina hazijamuisha. Wapo watu ikifika tu usiku, atakuambia vitu kibao hauzi hata ikiwa mteja unaviona live. Vitu kama chumvi, sindano, nyembe, mishumaa. Magadi, udi, na hata pini watakuambia vimeisha na kumbe vimejaa tele dukani, kisa ukiuliza wanakuambia bidhaa hizo kuna baadhi ya wateja wanaokwenda kufanyia shughuli za kishirikina au uchawi na kupungia majini.

Kikongwe, mlemavu au mgonjwa wa akili akifika dukani ni mkosi wa ajabu, utasikia, ‘oo, atakuwa chuma ulete huyo! Simuuzii’, au ‘ni ndondocha huyo katumwa aje kuchukua pesa’.

Imani hii ni kwa kila upande wapo pia wateja wenye imani za ajabu hata akikupa pesa anapotaka kununua kitu hakupi mkononi, ataiweka juu ya meza, sijui wanadanganywa na nani, bila shaka ni waganga wa jadi uchwara huko mitaani. Kwa upande wa wenye maduka wao wanaogopa sana hasa kuwapa washindani wao chenji wakihofia mauzo yao yatahamia kwao kimiujiza.


Wewe ukitaka muuza duka akupe chenji hasa nyakati za usiku, nunua hata pipi ya shilingi mia mpe elfu kumi atakurudishia elfu tisa na mia tisa lakini siyo akupe tu hivihivi.   

(B.) DHANA POTOFU.
Kama ilivyokuwa kwa imani potofu pia wenye maduka ya rejareja wengi wamezikumbatia baadhi ya dhana zisizokuwa sahihi ambazo kwa kiasi kikubwa huchangia kukwamisha mafanikio ya biashara zao. Dhana hizo ni kama hizi hapa chini;

1. Duka lina faida kidogo sana:  
Ni kweli faida katika biashara yeyote ile ya reja reja, siyo duka tu bali hata na kitu chochote kinachouzwa rejareja faida yake haiwezi kuzidi asilimia 30% ya mauzo hii ina maana kwamba bidhaa ikiuzwa shilingi 100 faida yake ni Tshs. 25 na ikizidi sana ni Tshs. 30. Kwa hiyo kusema eti biashara ya duka la rejareja haina faida au ni kidogo sana siyo sahihi kwani utapata faida katika vitu vingi na ukichanganya
pamoja huwa kubwa.

2. Duka halihitaji matangazo wala promosheni:  
Siyo kweli kabisa dhana hii kwani matangazo ni muhimu katika biashara ya aina yeyote ile, cha msingi tu ni aina gani ya matangazo na promosheni utakayoifanya.


3. Ili duka liendelee ni lazima ukae wewe, mkeo/mume au mwanao;  zaidi ya hapo watakuibia na litakufa tu.

Dhana hii ina ukweli endapo utamuajiri mtu halafu ushindwe katika suala la usimamizi hasa kwenye hesabu na vipimo kwa mfanyakazi uliyemuweka.


4. Maduka madogo hayana uwezo wa kushindana na maduka makubwa.

Huo ni uongo, duka hata liwe ni la mtaji wa shilingi laki mbili bado unao uwezo wa kushindana na duka hata la ukubwa wa ‘super market’  mbinu hapa utakayoitumia ni kutafuta upekee wa biashara yako, huduma za kipekee kwa wateja pamoja na mandhari  yakuwavutia wateja. Wateja  hawatakuwa na sababu ya kwenda katika
hiyo ‘super market’ waache duka lako dogo. Wao shida yao ni kupata huduma na siyo ukubwa wa duka.

5. Ipo siku  biashara za rejareja kwa njia ya mtandao “intanenti” zitakuja kuzipiku kabisa biashara za maduka ya rejareja ya kawaida.

Hakuna kitu kama hicho kitakachoweza kutokea, na si hapa Tanzania tu bali hata na huko intanenti yenyewe ilikoanzia, watu wamethibitika kupendelea zaidi kununua kitu wanachoweza kukiona ‘live’ na wala siyo eti kukiona  kwenye screen ya computer au simu.


Ukitaka kupata mafanikio ya uhakika katika biashara ya duka la rejareja au biashara nyingine yeyote ile, huna budi kuachana kabisa na dhana na imani hizi za karne zilizopita, hii ni karne ya sayansi na teknolojia, jiambie akilini mwako “Kama kweli imani hizi hufanya kazi jinsi wengi wanavyoamini, mbona waafrika bado tuko nyuma hivyo kimaendeleo?” Wenzetu wazungu na mataifa yaliyoendelea imani hizi si kama kwao hazipo hapana, bali baada ya maendeleo na ustaarabu kushika kasi wamezipuuzilia mbali wakafanikiwa huku sisi tukiendelea kuzikumbatia na kubakia kuwa masikini wa kutupa.


……………………………………………………………………..

Shea na mimi uzoefu wangu binafsi wa miaka 12 katika biashara ya rejareja hususani duka la mahitaji ya nyumbani kwa kusoma kitabu kifuatacho nilichotunga.


MAFANIKIO YA DUKA LA VYAKULA LA REJAREJA
Kitabu cha Duka la rejareja.

Kitabu hiki hata ikiwa unafikiri biashara ya duka ni rahisi, utakutana na mambo mengi, mengine pengine ulikuwa huyachukulii “serious” kumbe yana athari kubwa kwenye biashara yako.

Softcopy yake kwa njia ya email ni sh. Elfu 5 tu, na unaweza kutumiwa ukiwapopote pale mara tu baada ya kulipa kupitia moja kati ya namba 0712202244  au  0765553030. Unatuma pia kwa meseji anuani yako ya baruapepe-email.

HARDCOPY unaweza kupata ukifika ofisi yetu ilipo, MBEZI STENDI KWA MSUGURI, au unaweza kuagiza tukakuletea popote pale kama upo Dar es salaam, lakini unatuma nauli sh.1500/= kuonyesha kweli unahitaji kwani wapo baadhi ya watu “wanaocheat” kusema niletee kumbe hawanunui kweli.

Kama upo Mikoani, agiza mtu akuchukulie na kukutumia, au unaweza kutuma fedha pamoja na gharama za usafiri tukakutumia kwa basi linalofika ulipo.

ASANTE KWA KUSOMA
Peter A. Tarimo

Self Help Books Publishers Ltd

0 Response to "PUUZA IMANI NA DHANA HIZI POTOFU UFANIKIWE KATIKA BIASHARA YAKO YA DUKA LA VYAKULA"

Post a Comment