WANAUME NI KUTOKA SAYARI YA MARS , WANAWAKE VENUS | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WANAUME NI KUTOKA SAYARI YA MARS , WANAWAKE VENUS


MEN ARE FROM MARS, WOMEN ARE FROM VENUS ni kitabu kinachohusu mahusiano baina ya mwanamke na mwanamume  maarufu sana na kilichowahi kuuza nakala zaidi ya milioni 50, kiliandikwa na kuchaposhwa na John Gray hapo mwaka 1992. Maudhui ya kitabu hiki ni utofauti mkubwa ulioko baina ya wanaume na wanawake kiasi kwamba tofauti hiyo inalinganishwa na viumbe hawa wawili kutokea sayari mbili tofauti yaani Mars na Venus.Mwandishi wa kitabu hiki haishii tu hapo bali anazidi kubainishakwamba, matatizo na sintofahamu nyingi  kwenye mahusiano ya mwanamke na mwanaume hutokana na wahusika kutokuzifahamu tofauti hizo zilizopo na kuzifanyia kazi ipasavyo. 


Na kunapokuwa na mikwaruzano kati ya watu wawili  mume na mke au baina ya marafiki wawili wa jinsia tofauti ujue na ufanisi katika kazi au biashara nao hupungua kwa kiasi kikubwa. Ili kuweze kuwa na maendeleo wanawake na wanaume inafaa waishi kwa masikilizano.

0 Response to "WANAUME NI KUTOKA SAYARI YA MARS , WANAWAKE VENUS"

Post a Comment