SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO(KEY TO SUCCESS) UNAIJUA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO(KEY TO SUCCESS) UNAIJUA?

Siri zako za mafanikio “keys to success” ni yale mambo ambayo unayapa kipaumbele zaidi katika biashara yako katika  kuifanya  ifanikiwe zaidi kwa mfano, biashara  ya rejareja huwa ina tabia ya kupenda kushamiri vizuri zaidi katika maeneo yenye watu wengi.

Jambo hili husababisha watu kusema kuwa siri kubwa ya mafanikio ya biashara ya rejareja ni “eneo”  eneo zuri  mfano stendi ya basi, sokoni n.k  au yaweza  kuwa  sehemu nzuri  yenye ‘parking’ ya kutosha. 

Siri  ya mafanikio inaweza pia kuwa bei nafuu, jina la biashara kwa mfano  mtu anaponunua  kitu kama Redio  au TV  huangalia  majina  makubwa mfano sonny, Hitachi nk. au simu ataangalia zile simu zenye majina mfano techno, Samsung galaxy, Nokia nk. Hivyo siri za mafanikio kwa makampuni hayo ni majina yao makubwa waliyojijengea.

Kuwa na kitu ambacho  kitakuwa ndiyo siri  yako ya mafanikio, kutakusaidia   uelekeze nguvu zako nyingi zaidi na malengo katika  jambo/kitu hicho kuhakikisha biashara yako inafanikiwa.


……………………………………………………………………..

Kwa vitabu vilivyo na course zote za biashra na ujasiriamali kwa kina tembelea  ukurasa huu, SMART BOOKS TANZANIA.

Kama hukuwa umesoma kitabu chetu cha bure, KANUNI NA SIRI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NAMAFANIKIO, Jiunge kwa kubonyeza maandishi hayo

Kwa huduma zetu nyingine fungua HUDUMA ZETU
Tupo Mbezi Kwa Msuguri stendi
0712202244  au  0765553030

Self help books Tanzania 

0 Response to "SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO(KEY TO SUCCESS) UNAIJUA?"

Post a Comment