FAIDA DUKA LA MAHITAJI YA NYUMBANI: NIWEKE AKIBA KIASI GANI CHA MAPATO YA SIKU? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

FAIDA DUKA LA MAHITAJI YA NYUMBANI: NIWEKE AKIBA KIASI GANI CHA MAPATO YA SIKU?

 

Duka mahesabu ni jioni
Juzi nilisema nitayajibu maswali na changamoto mbalimbali za wasomaji wa blogu hii walioniuliza hivi karibuni na huu ndio muendelezo wa majibu ya changamoto hizo. Msomaji huyu kupitia watsap aliuliza hivi, na nimeweka screenshot ya mawasiliano yangu na yeye pale chini;

(Huwa hatuutaji utambulisho halisi wa muulizaji-swali pasipo idhini yake rasmi)

 

SWALI:

Samahani Mkuu nimeaza biashara yangu ya Mtaji wa shilingi laki 4 nauza mahitaji ya nyumbani ya kawaida mfano sukari mafuta nyanya na vingine, Changamoto yake nashindwa kugawa mapato asilimia ngapi niweke kwenye Akiba na asilimia ngapi niweke kwajili ya kununulia bidhaa zilizopungua dukani kwangu, naombaaaa ushauriii mkuuu Mungu akubariki sana

 

MAJIBU:

Njema kabisa Mkuu, Karibu

 

Kiasi Cha akiba unachotakiwa kuweka kitategemea ni faida kiasi gani unachoingiza kwenye biashara yako.

Ikiwa utakuwa na uhakika ni faida kiasi fulani unachopatakila siku basi kiasi hicho cha faida ndicho unachopaswa kukigawa kwa ajili ya kuweka kama akiba na kingine kununulia bidhaa.

SOMA: Biashara ya urembo inalipa, ni ya pili kutoka haraka baada ya chakula, ni fursa kubwa 

Hata hivyo pia kwa kuwa naona mtaji ni kidogo (laki 2) kwa mujibu wa maelezo yako, sifikiri kama ni Jambo la busara kugawa faida na kuiweka akiba mapema kiasi hicho badala yake nadhani unge’focus’ zaidi katika kuongezea faida hiyo kwenye mtaji ili kuikuza zaidi biashara yako hii ya duka la mahitaji ya nyumbani.

Aidha njia ya kufahamu ni faida kiasi gani ya duka lakounayopata kwa siku au kwa mauzo unayouza ni rahisi, tumia moja kati ya njia hizo mbili hapo chini;

1.  Andika kila bidhaa inayouzika na kisha jioni wakati wa kufunga hesabu ukokotoe kila bidhaa imechangia faida kiasi gani, kisha tafuta jumla ya faida ya bidhaa zote zilizouzika kwa siku hiyo.

 

2.  Njia ya pili unaweza kukokotoa faida ya mauzo ya siku husika kwa kutumia asilimia ya mauzo. Inafahamika bidhaa nyingi za rejareja huwa na faida wastani wa asilimia 25% mpaka 30% ya mauzo, hivyo chukua mauzo yote ya siku yazidishe mara asilimia 25% au 30%  jibu ndio faida uliyopata na ndipo Sasa unaweza kuamua ugawe kiasi gani hapo kwa ajili ya akiba na siyo kuweka akiba mtaji wenyewe.

 SOMA: Mtaji wa duka la rejareja: nianze na shilingi ngapi ili nifanikiwe?

Hesabu hizi haijalishi ni duka la aina gani ilimradi ni duka au biashara ya kuuza bidhaa za rejareja. Inaweza ikawa unataka kujua faida ya duka la dawa muhimu, faida ya duka la vipodozi, faida ya duka la nguo, faida ya duka la simu za rejareja, faida kwenye biahara ya kuuza sambusa nk. ilimradi tu ni mahesabu ya duka la rejareja au biashara yeyote ile nyingine ya rejareja unapofunga mahesabu jioni kwani mahesabu ya biashara zote za rejareja mfumo wake ni uleule mmoja haubadiliki sana.

 

Asante sana!

………………………………………

Ukiwa na changamoto yeyote fupifupi kama hii unaweza kuuliza muda wowote ule na nitakujibu haraka bila malipo yeyote.

Kwa maswali mengi zaidi au majibu kwa kina zaidi unaweza kujiunga na MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE kwa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu ada ya mwaka mzima ambapo unapata na offa ya kitabu cha Michanganuo bure.

Huku unaweza kuuliza chochote bila kikomo na unapata fursa ya ‘kuaccess’ masomo zaidi ya 70 ya fedha pamoja na Michanganuo ya biashara za kipekee zinazolipa Tanzania.

 

WATSAP/CALL: 076555330 au 0712202244

Kwa vitabu zaidi na Michanganuo mbalimbali ya biashara tembelea duka la mtandaoni, SMARTBOOKSTZ

0 Response to "FAIDA DUKA LA MAHITAJI YA NYUMBANI: NIWEKE AKIBA KIASI GANI CHA MAPATO YA SIKU?"

Post a Comment