KWANINI WANAUME WENYE MAFANIKIO NA UTAJIRI MKUBWA CHANZO NI USHAWISHI WA WAPENZI / WAKE ZAO? (Sura ya 11 ii) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI WANAUME WENYE MAFANIKIO NA UTAJIRI MKUBWA CHANZO NI USHAWISHI WA WAPENZI / WAKE ZAO? (Sura ya 11 ii)

Wema sepetu na Diamond Platnumz

Uchambuzi Kwa kina Sura ya 11 ya kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE (THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION) – Sehemu ya ii

Mwandishi amezungumzia ngono kama kichocheo cha akili kati ya vichocheo vingine 9 vya akili ambavyo ni hivi hapa chini;

                     1.     Ngono yenyewe (shauku ya mapenzi)

                     2.     Upendo(Mapenzi)

                     3.     Shauku kali ya Umaarufu, cheo na fedha

                     4.     Muziki

                     5.     Urafiki wa jinsia moja au wa jinsia tofauti

                     6.     Ushirika wa Kushauriana(Mastermind group)

                     7.     Maumivu ya pamoja kama yale wanayopata watu walio katika mateso

                     8.     Kujishauri-binafsi

                     9.     Hofu

                   10.   Dawa za kulevya na pombe.

Vichocheo nane kati ya hivi asili yake ni chanya yaani ni vya kujenga wakati vichocheo viwili vya mwisho ni vya kubomoa au hasi. Shauku ya kujieleza kingono hukaa kileleni kabisa mwa vichocheo vingine.

Akili ya binadamu kwa kawaida huwa ina tabia ya kuitikia kwa wepesi vichocheo hivi na kufunguliwa mpaka kufikia kiasi cha juu kabisa cha mitetemo ijulikanayo kama shauku kali au Ubunifu wa kujenga / kubomoa kulingana na aina ya kichocheo inachoitikia.

Majaribio ya kisayansi juu ya historia za wanaume wenye mafanikio makubwa yamebainisha ukweli ufuatao;

·       Wanaume wenye mafanikio makubwa ni wale walio na asili ya mapenzi iliyokomaa vya kutosha au wanaume waliojifunza sanaa ya kugeuza fikra za mapenzi(ngono) kuwa katika vitu vingine vyenye faida. Hapa utaona kwamba wanaume kwa mfano mashoga au wasio na nguvu za kutosha za kiume huwa pia kufanikiwa kwao katika nyanja zingine ni vigumu. 

·       Wanaume waliopata utajiri mkubwa na umaarufu kwenye fasihi, sanaa, viwanda, uhandisi na fani nyinginezo walihamasishwa kutokana na nguvu ama ushawishi wa wapenzi wao / wake zao.

Shauku ya kujieleza kimapenzi ni ya asili na na kuzaliwa nayo, huwa haiwezi na haitakiwi kukandamizwa wala kuzuiwa bali inatakiwa kupewa njia ya kutokea kupitia aina chanya za kujieleza kimwili, kiroho na kiakili. Vinginevyo yenyewe kwa kutumia mgeuko au mabadiliko tunayoyazungumzia kwenye hii sura itatafuta njia nyingine ya kutokea kupitia njia hasi za kimwili zinazoonekana. Haina tofauti na mto wa maji, hata uujengee bwawa kubwa, utauthibiti kwa muda fulani tu lakini maji ni maji na itafika muda yatalazimisha njia ya kutokea. 

Kuthibitisha ukweli kwamba mhemko wa ngono ni nguvu isiyozuilika kwa binadamu na ni lazima mtu akitaka kuizuia lazima atumie sanaa ya kuigeuza kuwa katika nguvu nyingine chanya mwandishi anatoa mfano wa dume la ngombe au mnyama mwingine yeyote yule anapohasiwa;

Haribu matezi ya jinsia iwe ni kwa mwanaume au mnyama na utakuwa umeondoa chanzo kikubwa cha vitendo” anaendelea kusemakwamba “Ng’ombe dume hugeuka kuwa mpole kama ng’ombe jike baada ya kubadilishwa jinsia(kuhasiwa)”. Nguvu zote za kupambanandani yake huondoka. Na mabadiliko ya jinsia ya kike pia yana matokeo sawa.

Katika sura hii mwandishi ametaja mifano ya wanaume ambao mafanikio yao makubwa ya kushangaza yanahusishwa moja kwa moja na ushawishi wa wanawake ambao waliamsha vitivo jengefu vya akili zao kupitia msisimko wa hamu kubwa ya mapenzi. Mmoja wao alikuwa ni kiongozi mashuhuri sana wa kijeshi wa karne iliyopita huko Ulaya, Napoleon Bonapatre.

Bonapatre alipohamasishwa na mke wake wa kwanza Bibi Josephine alikuwa ni mtu asiyezuilika wala kushindika kwa urahisi lakini mara tu alipokuja kushawishika kumuacha akamweka pembeni  na kumchukua kimada mwingine, anguko lake lilikuwa dhahiri, akatupwa kama mfungwa kwenye Kisiwa cha St. Helen na huo ndio ukawa mwisho wake.

Hata katika vitabu vitakatifu tunasoma nguvu za ushawishi wa ajabu wa mwanamke Delila kwa Samsoni, lakini huu tunaweza tukauweka katika zile aina za ushawishi hasi.

Hata leo hii  unaweza kuona mifano ya watu wengi maarufu kama Wasanii, Wanamuziko na Wafanyabiashara wakubwa jinsi walivyoathiriwa na kuwaacha wanawake wa ujana wao, mafanikio yao yamebadilika na kushuka chini tofauti na vile walivyokuwa na ushawishi wa wapenzi wao wa mwanzo waliokuwa wakiwapenda kwa dhati.

Wengine hata ikiwa kama hawakushuka chini baada ya kuwaacha na mifano tunayo hata hapa Tanzania, lakini ukweli unabakia palepale kwamba Wanawake wao hao wa kwanza ndio waliofungua ukurasa wa mafanikio yao.

Mbali na kupata mafanikio makubwa kutokana na shauku kubwa ya mapenzi, kuna watu wengine hujishusha wenyewe kufikia hali ya wanyama wadogo kutokana na matumizi mabaya ya nguvu hii kubwa.

Sababu kubwa kwanini kila penye mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke ni kuwamba, hamu ya kujieleza kimapenzi ndiyo mhemko wenye nguvu zaidi na msukumo kuliko mihemko mingine yote ya binadamu. Na kutokana na sababu hii kubwa, hamu hii inapotumiwa na kugeuzwa katika kitendo kingine tofauti na vitendo vya kimwili inaweza ikampandisha mtu kufikia hadhi ya juu kabisa iwe ni katika mafanikio kiuchumi au hata katika uongozi.

Mwandishi anazidi kubainisha watu zaidi waliopata mafanikio makubwa baada ya ushawishi wa wanawake waliowapenda kwa kumtaja mfanyabishara mmmoja wa Kimarekani aliyekiri kwamba Katibu Muhtasi wake aliyekuwa anavutia ndiye aliyekuwa anahusika kwenye mipango yake mingi aliyokuwa anaitengeneza. Alikiri kuwa uwepo wa mrembo huyo ulimuinua hadi vileleni mwa Ubunifu Jengefu.

Anaendelea kusema kwamba mmoja wa watu waliofanikiwa zaidi Marekani anawiwa na mafanikio yake mengi kwa ushawishi wa mwanamke kijana mchangamfu sana ambaye alitumika kama chanzo chake cha ushawishi kwa zaidi ya miaka 12

 

………………………………………………

Mpenzi Msomaji wangu, tukutane Sehemu ya Tatu (iii) ya uchambuzi wa Sura hii ya 11 ya kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE.

Asante sana!

Peter A. Tarimo.

 

Njia 2 Unazoweza kukipata Kitabu kizima cha FIKIRI & UTAJIRIKE (Think & Grow Rich-swahili edition

1.  Nakalapepe(softcopy) kwenye Simujanja yako, Ingia katika mtandao huu wa GETVALUE na uweze kukipakua ndani ya muda mfupi.

2.  Kitabu cha karatasi (Hardcopy), wasiliana na sisi kwa namba 0765553030 au 0712202244 tutakuletea popote ulipo nchini Tanzania.


SOMA NA HIZI HAPA;




0 Response to "KWANINI WANAUME WENYE MAFANIKIO NA UTAJIRI MKUBWA CHANZO NI USHAWISHI WA WAPENZI / WAKE ZAO? (Sura ya 11 ii)"

Post a Comment