VITABU 3 VISIVYOCHUJA KAMWE (THREE TIMELESS CLASSIC BOOKS OF ALL TIMES) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

VITABU 3 VISIVYOCHUJA KAMWE (THREE TIMELESS CLASSIC BOOKS OF ALL TIMES)


VITATU 3 SELF HELP BOOKS TANZANIA
Duniani kuna vitu ambavyo umewahi kusikia kwamba havipitwi na muda(timeless/classic) au kwa maana nyingine ni kwamba kadiri muda unavyozidi kupita basi navyo ndio vinazidi tu kuwa bora. Nitajaribu kuvitaja baadhi ya vitu hivyo hapa chini japo najua kunaweza kuwa na vitu vingi zaidi ya hivyo.

DHAHABU:
Nikianza na madini haya adimu duniani ni kwamba inasemekana hata kabla ya kugunduliwa kwa hela yalikuwa ndiyo yanayotumika kama njia kuu ya kubadilishana vitu kutokana na dhahabu kuwa ‘timeless’. Dhahabu uitie kwenye moto mkali, uitwangetwange kwa mawe, sijui uifanyie shuruba gani ndio kwanzaa! inazidi kung’ara.

dhahabu hudumu

MVINYO (WINE)
Ukitaka kujua maajabu ya mvinyo nenda nchi kama Ufaransa, zipo chupa za mvinyo zimehifadhiwa ardhini miaka mia tatu(300) iliyopita, huwezi amini lakini bado unaambia ndio kwanza zinazidi ‘kuwiva’ na ubora wake kuongezeka mara dufu sambamba na thamani au bei yake kuongezeka pia. Si ajabu ukaambiwa chupa moja tu ya mvinyo kama huo ni shilingi za kibongo mamilioni.

MVINYO ULIODUMU MIAKA 300
Mvinyo wa miaka 300

MUZIKI MZURI:
Kuna baadhi ya nyimbo zilizowahi kuimbwa miaka mingi iliyopita lakini kila unapozisikiliza utadhania zimerekodiwa jana. Si lazima mziki ninaouona mimi ‘classic’ na mtu mwingine auone hivyohivyo lakini zipo nyimbo asilimia kubwa ya watu utasikia wakisema ni classic.  Kwa mfano Kuna vibao kama vilivyopigwa na bendi ya Less Wanyika zaidi ya miaka 30 iliyopita kama hiki cha  Ufukara siyo kilema”  hapo chini,  ukiusikiliza leo hii mashairi na hata midundo yake  utadhani ni mpya.


Vibao vya kizungu pia vipo vingi  ila hapa nitatolea mfano mmoja wa kibao cha msanii ‘Michael Learns to Rock’  kilichotoka tangu mwaka 1996, “Breaking my heart” . Ukikisikiliza hata leo bado ni kama kimetoka jana. Kuna mamia ya nyimbo zisizopitwa na wakati tukiziorodhesha hapa hapatatosha.



VITABU:
Vitabu navyo  halikadhalika vinaingia kwenye orodha, siyo kila kitabu hapana kuna baadhi yake na unapozungumzia vitabu visivyopitwa na wakati kwa kweli vipo vingi na katika tasnia mbalimbali pia. Mimi leo sitataja orodha ya vitabu hivyo kidunia, nitafanya hivyo siku nyingine ila ninachotaka kuelezea hapa tu ni juu ya vitabu 3 vya Self Help Books Tanzania. Si kama labda najifagilia au kuvutia kamba kwangu kwakuwa ni mdau wa kampuni hii hapana, bali kuelezea tu ukweli ulivyo.

KWANINI VITABU HIVI NI TIMELESS(CLASSIC)
Sababu kubwa ni kwamba, maudhui ya vitabu hivi yanahusu Biashara, Ujasiriamali na Mafanikio kwa ujumla wake vitu ambavyo pia kila siku mwanadamu amekuwa akishughulika navyo. Binadamu anapozaliwa haijalishi ni katika zama zipi lakini ni lazima atafute mafanikio katika nyanja mbalimbali hususani katika kipato kwa njia mbalimbali kubwa ikiwa ni Biashara na Ujasiriamali

Biashara & Ujasiriamali  kwa maana pana zaidi inagusa mpaka Ajira na shughuli nyingine zote zikiwamo hata zile za kujitolea kama vile kwenye Dini mbalimbali, Wachungaji, Mapadre, Mashehe, Maimamu na Watumishi wengine wa Mungu. Unapopata maarifa yaliyokuwemo katika vitabu hivi unakuwa na wewe miongoni mwa watu wasiopitwa na wakati(classic person)

Narudia tena, sina maana kuwa classic books ni hivi  “Self Help Books” tu peke yake hapana, ila nasema kwamba ni miongoni mwake, vipo vingine vingi hata hapa Tanzania ingawa unapaswa uwe makini kuchuja kipi ni kipi.



Kitu kingine ni kwamba unaweza kukuta kitabu ni classic lakini mwandishi akawa mvivu na kuweka vitu vichache huku akilenga kuja kutoa toleo la kitabu kingine aweze kupata pesa nyingi, lakini sisi Self help Books hatupo hivyo. Mpaka watu wengi wameniuliza mara nyingi Swali hili, “Kwani nyie  Self Help Books hampati  hasara kuchapisha vitabu vyenye kurasa nyingi namna hiyo?”   

Mimi huwajibu tu kwamba, waendelee kufurahia vitabu vyetu kwani dhamira yetu kubwa ni kuona wanafanikiwa kimaisha na hususani katika Nyanja za biashara na ujasiriamali.



Katika kuzidi kuvifanya vitabu hivi kuwa timeless au classic basi mwaka huu wa 2020 tumeamua kuvifanyia marekebisho makubwa vitabu vyetu vyote 3. Ingawa maudhui hayajabadilika lakini kuna baadhi ya vitu vilivyoongezwa ili kuboresha zaidi uelewa wa msomaji. Mabadiliko mengine mfano bei siyo makubwa sana na ni kwa baadhi tu ya vitabu hasa kile cha BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA ingawa pia madadiliko hayo bado hayajaanza rasmi.

Tumeboresha pia upatikanaji wa vitabu vyetu kwa kuhakikisha kwamba yeyote anayehitaji kitabu popote pale alipo tunamtumia au anapata kwa mawakala wetu Dar es salaam na mikoani.

JINSI YA KUPATA VITABU 3 VYA SELF HELP BOOKS (3 TIMELESS CLASSIC BOOKS)

1. HARDCOPY(VITABU VYA KARATASI)
Vinapatikana katika Steshenari iitwayo BRIGHT STATIONERY iliyopo Mbezi Kibanda cha mkaa. Ukifika Kibanda cha mkaa, panda bajaji au bodabona waambie wakushushe kituo cha KWA MOTA . Ni jirani na shule ya secondary ya ST. AUGUSTINO (TAGASTE)

Ukitaka uletewe kitabu/vitabu  ulipo Dar es salaam utaongeza gharama za basi sh. 2,000/=.

Mikoani tunatuma kwa njia ya mabasi na gharama za basi hutegemea aina ya basi na umbali ulipo lakini ‘maximum’ ni sh. elfu 10 mikoa mingi kwa bahasha (percel) moja ya vitabu.

2. SOFTCOPY(KWA NJIA YA MTANDAO-EMAIL)
Tunatuma kitabu/vitabu popote pale mteja anapokuwa amelipia kitabu/vitabu. Ni ndani ya dakika 5 tu na hazizidi 10 toka kutuma mpaka kupokea vitabu/kitabu

Ukitaka vitabu vingine na Michanganuo ya Biashara kutoka Self Help Books Tanzania unaweza ukatembelea DUKA LETU LA MTANDAONI LIITWALO (SMART BOOKS TANZANIA) HAPA na kuchagua ni kipi unachohitaji.



0 Response to "VITABU 3 VISIVYOCHUJA KAMWE (THREE TIMELESS CLASSIC BOOKS OF ALL TIMES)"

Post a Comment