MAAJABU YA KUBADILI FIKRA ZA MAPENZI (NGONO) KUWA MAFANIKIO –SURA YA 11 (i) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAAJABU YA KUBADILI FIKRA ZA MAPENZI (NGONO) KUWA MAFANIKIO –SURA YA 11 (i)

 

Uchambuzi wa kitabu fikiri & utajirike(think & grow rich swahili

Uchambuzi Kwa kina Sura ya 11 ya kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE (THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION) – Sehemu ya i

Sura hii kwa ujumla wake inazungumzia matumizi mazuri ya mhemko wa ngono – jinsi binadamu anavyoweza kuzitumia hisia za ngono au mapenzi ya kujamiiana  ambazo ndiyo kichocheo cha akili kati ya vichocheo vingine 10 kilichokuwa na nguvu zaidi na kilicho na uwezo wa kufanya maajabu makubwa katika maisha ya binadamu kimafanikio. (kuna aina kuu nne(4) za mapenzi kwa mujibu wa kitabu hiki)

Fikra za ngono zinaweza kumjenga au kumbomoa mtu kulingana na yeye mwenyewe atakavyoamua kuzitumia.

Kwenye sura hii tutakwenda kufahamu yafuatayo;

·       Ni kwanini watu wengi mafanikio yao makubwa huja pale wanapofikisha umri kuanzia miaka 40 – 60?

·       Sababu kubwa ni kwanini kila mwanaume mwenye mafanikio makubwa au utajiri nyuma yake kuna mkono wa mwanamke?

·       Kwanini wasanii wengi na wanamichezo waliofanikiwa hujiingiza kwenye ulevi wa dawa za kulevya, pombe na bangi?

·       Kwanini wanamauzo wengi ni watu wenye  ushawishi mkubwa(kingono) kimapenzi?

·       Tofauti kubwa kati ya MAPENZI, UPENDO, NGONO, MAHABA na KUJAMIIANA

·       Kwanini wahalifu sugu wanaweza kurekebishwa kupitia ushawishi wa wapenzi wao?

·       Kwanini UPENDO ndiyo uzoefu mkubwa zaidi maishani?

·       Aina kuu 4 za Mapenzi(UPENDO) ni upi unaochoma zaidi moyoni?

·       Kwanini watu husema, “Mke anaweza kumjenga au kumbomoa mume”?

·       Chanzo kikuu cha Wanandoa kugombana.

·       Kwanini inasemekana wanaume wote wenye  mafanikio na utajiri mkubwa chanzo ni ushawishi wa wapenzi wao(wake)?

·       Kwanini Wanyama wanatuzidi binadamu kwa ustaarabu kwenye tabia za mapenzi mfano jogoo hawezi kumbaka kifaranga lakini baba mzima anaweza kumbaka hata mwanaye wa kumzaa?

Neno kubadili au kugeuza kwa lugha nyepesi ni uhamishaji wa kitu kimoja au aina ya nguvu kwenda katika kitu cha aina nyingine. Vivyo hivyo na hisia za mapenzi au ngono ndivyo zinavyoweza zikabadilishwa kutoka katika hali yake ile ya kawaida tuliyoizoea mfano hali ya kujamiiana baina ya mwanaume na mwanamke kuwa katika hisia nyingine tofauti kabisa kwa kutumia mbinu rahisi tu tutakazokwenda kujifunza katika sura yetu hii ya 11 ya kitabu maarufu cha Fikiri na Utajirike(Think & Grow Rich-swahili edition).

Mapenzi (Ngono), ijapokuwa kitabu hiki kimeelezea faida na uzuri wake kama nitakavyoorodhesha hapo chini hivi punde, lakini hisia hizi zimekuwa pia ni chanzo kikubwa cha matatizo na uchungu mwingi kwa binadamu kutokana na sababu moja tu ya sisi binadamu kutokuwa na uelewa wa kutosha au elimu sahihi kuhusiana na mhemko huu wa kipekee kabisa.

Mhemko huu umekuawa ni chanzo cha Wanafunzi wengi wa shule na vyuo kufeli mitihani yao au kukatisha masomo, chanzo cha wanaume wengi na wanawake kujiua kwa kujinyonga, chanzo cha watoto wengi wa mitaani na chanzo cha karibu kila aina ya madhila na majanga yanayozikumba ndoa na familia nyingi Duniani kama Napoleon Hill mwenyewe anavyouelezea utafiti wake wa miaka takriban 25 ndani ya sura ya 11 ya kitabu hiki cha Kanuni 13 za mafanikio kuwahi kuandikwa popote pale pengine Duniani.

Mwanzoni kabisa mwa sura yenyewe Napoleon Hill anasema kwamba, kwasababu ya ujinga juu ya mada hii, mhemko wa ngono mara nyingi huhusishwa na hali ya kimwili / kimaumbile kutokana na sababu zisizokuwa sahihi ambazo watu wengi wamekuwa wakikutana nazo wakati wa kujifunza elimu ya ngono, vitu vya kimwili vimekuwa ndiyo viunavyotawala na hii ndiyo sababu kubwa inayofanya elimu ya ngono kuwa na usirisiri fulani hivi.

Faida  kuu 3 za Mhemko wa Ngono

1.  Muendelezo wa binadamu kupitia njia ya kuzaana

2.  Kudumisha Afya

3.  Kumbadilisha mtu kutoka hali duni kabisa kwenda katika hali bora kabisa kiubunifu kupitia mageuzi (Hii ndiyo watu wengi hawaijui na ndiyo tutakayokwenda kujifunza zaidi katika Sura yetu hii ya 11

Hamu ya ngono ndiyo hamu ya binadamu iliyo na nguvu kushinda hamu nyingine zote. Watu wanaposukumwa na hamu hii hutengeneza umakini mkubwa katika kufikiri, ujasiri, utashi, msimamo na uwezo wa kiubunifu ambao hawakuwahi kuwa nao wakati mwingine.

Mguso wa kimapenzi una nguvu na msukumo kiasi kwamba watu bila kuzuiwa na chochote kile huhatarisha maisha yao na hadhi zao wakiuendekeza.

(Hii imenikumbusha stori yangu mimi mwenyewe binafsi wakati nilipokuwa nasoma sekondari katika miaka yangu ya 15 - 20 Siku nilipohatarisha maisha yangu usiku mkubwa kisa tu ikiwa ni kumuonyesha ujasiri na umwamba msichana rafiki yangu niliyekuwa nampenda. Nilikwenda kwao siku ya sikukuu, tukiwa na vijana wengine tulipiga stori huku tukinywa mbege, mpaka kila mtu anaondoka mimi niliamua niwe wa mwisho bila kujali hatari yeyote ambayo ingeliweza kwenda kunikuta usiku ule njiani tena kwa kutembea umbali mrefu kijijini, yote hii ilikuwa shauri ya hisia za mapenzi juu ya msichana yule ambapo katika hali tu ya kawaida nisingelithubutu kufanya vile)  

 

Mpenzi Msomaji wangu, tukutane tena Sehemu ya Pili ya uchambuzi wa Sura hii ya 11 ya kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE.

Asante sana!

Peter A. Tarimo.

 

Njia 2 za Kukipata Kitabu kizima cha FIKIRI & UTAJIRIKE (Think & Grow Rich-swahili

1.  Nakalatete(softcopy) kwenye Smartphone yako, Ingia kwenye mtandao huu wa GETVALUE na utaweza kukipakua ndani ya muda mfupi. 

2.  Nakala ngumu (Hardcopy), wasiliana na sisi kwa namba 0765553030 au 0712202244 tukuletee popote pale ulipo nchini.SOMA NA HIZI HAPA;

1. Think and Groe Rich kwa ufupi: Mapitio ya vitabu vya mafanikio(Books Review)

3. Downlad/ pakua hapa kitabu Fikiri Utajirike (Think and Grow Rich) kwa kiswahili, surazote 15 bure

3. Offa ya Kitabu cha Think & Grow Rich Toleo la Kiswahili 2021

0 Response to "MAAJABU YA KUBADILI FIKRA ZA MAPENZI (NGONO) KUWA MAFANIKIO –SURA YA 11 (i)"

Post a Comment