KIJANA MWENYE MALENGO MAKUBWA KIUCHUMI: NIFUGE KUKU AINA GANI, MAYAI, NYAMA AU KIENYEJI? NISHAURI TAFADHALI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KIJANA MWENYE MALENGO MAKUBWA KIUCHUMI: NIFUGE KUKU AINA GANI, MAYAI, NYAMA AU KIENYEJI? NISHAURI TAFADHALI

Kijana mfugaji wa kuku

Habari mdau wa blogu hii ya jifunzeujasiriamali,

Kuanzia leo nitakuwa nikiyajibu maswali mafupi yaliyoulizwa na wasomaji wenzetu kwa siku kadhaa zilizopita na leo hii tunakwenda kujibu swali kutoka kwa Kijana mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mwenye malengo makubwa kiuchumi, na angependa kushauriwa iwapo afuge kuku wa aina gani kati ya kuku wa nyama(Broillers), kuku wa kisasa wa mayai(Layers) na kuku wa kienyeji(Indigenous chicken).

Aliuliza kama ifuatavyo;

Mimi ni kijana na nina malengo makubwa kiuchumi, nilikuwa nawazia kuanza ufugaji wa kuku ila sielewe kuku wapi nifanye, wa mayai au wa nyama, naomba ushauri wako.

Kabla sijatoa majibu yake hapo chini ni vyema ukacheki screenshots za mawasiliano yetu yalivyokuwa watsap;  
Kuku wa aina zote wawe wa kienyeji, wa kisasa wa mayai au wale broilers wa nyama, wote wana faida ukiwafuga kwa kuzingatia taratibu za kitaalamu zinazopendekezwa na wataalamu au wale walio na uzoefu wa muda mrefu katika biashara hizi za ufugaji wa kuku.

SOMA: Ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai vs kuku wa nyama ni biashara ipi inayolipa faida zaidi?

Mtu kuamua ufuge kuku wa aina gani au kundi lipi la kuku itategemea vitu(factors) mbalimbali vilivyo ndani ya mazingira yako wewe mfugaji kwa mfano,

·       Suala zima la mtaji,

·       Eneo la kufugia,

·       Nafasi na muda wako wa kuwahudumia,

·       Ujuzi uliokuwa nao nk.

Kwa mfano ikiwa mtaji uliokuwa nao ni kidogo sana siwezi kukushauri ufuge kibiashara kuku wa kisasa wa nyama(broilers)  kwakuwa hautaweza kuiona faida yake. Kuku hawa faida yake kwa kuku mmojammoja ni ndogo sana na ni mpaka pale utakapofuga idadi kubwa ya kuku ndipo utaweza kuona faida yake, pengne kuanzia hata kuku mia mbili na kuendelea..

SOMA: Kilichokuwa nyuma ya pazia ufugaji kuku wa kienyeji (Kuku wa asili) 

Watu wengi kwa mtaji kidogo wanapofuga kuku wachache wa nyama na hatimaye kubaini faida haihamasishi basi huamua kuacha na kuiona biashara ya ufugaji kuku kuwa si lolote kama walivyokuwa wakiamini mwanzoni.

Halikadhalika ikiwa kwa mfano wewe ni mwajiriwa mahali fulani ambaye ungependa kuanzisha mradi wako wa ufugaji wa kuku kwa ajili ya kukuongezea kipato cha ziada (Mfereji wa ziada wa kukutiririshia pesa) nisingekushauri ufuge kuku wa kisasa wanaohitaji uangalizi wa karibu sana, iwe ni wa mayai wa nyama au hata wale chotara kama aina ya kroiler, labda tu iwe unaye kijana/mfanyakazi unayeweza kumuachia majukumu hayo ya uangalizi wa kuku wako. 

Ni bora hata ukafuga kuku wa kienyeji kwani unaweza kuwaacha muda mrefu katika banda lao kama ni imara vya kutosha bila ya uangalizi wa karibu sana ilimradi uwe umewawekea chakula cha kutosha na maji mpaka jioni utakaporudi kutoka kazini.

 

Hivyo ushauri wangu kwako ni huu hapa;

 

Chunguza kwanza vigezo vyote nilivyokuorodheshea hapo juu na vingine utakavyoamua mwenyewe kwa kufanya upembuzi wa kila kimoja kisha ikiwezekana andaa mchanganuo rahisi wa gharama na faida ya idadi ya kuku unaotamani kufuga iwe ni kuku wa nyama, wa mayai au wa kienyeji.

Zoezi hili kwanza litakusaidia kufahamu uwezo wako na fursa ulizokuwa nazo ni zipi kabla hujaingiza vifaranga au kuku bandani. Pili litakusaidia kufahamu changamoto mbalimbali wafugaji wazokumbana nazo mara kwa mara na hivyo kujiandaa kukabiliana nazo hata kabla hazijatokea na tatu litakuwezesha kujua banda la kuku liwe na ukubwa gani, vipimo vyake, ramani na jinsi ya kulijenga.

Baada ya hapo Sasa unaweza kuamua ufuge kuku wa aina gani kulingana na mazingira yako kimtaji na katika kila hali nyingine zinazogusa eneo hili la ufugaji wa kuku kwa ujumla wake likiwemo pia suala la 

 

Asante kila la kheri!

Mwisho

…………………………………………..

Ikiwa wewe una malengo kama ya huyu kijana ya kujishughulisha na biashara hii ya ufugaji wa kuku kibiashara, utakuwa umefanya uwekezaji wa maana sana endapo utajipatia Michanganuo ya kuku niliyokwisha kuandalia tayari.

Michanganuo hii yenye kila kitu unaweza kuitumia kama kielezo kitakachokusaidia kujua na wewe uandaeje mchanganuo wako. Siyo lazima uandike kwenye karatasi, hata kitendo tu cha kuisoma michanganuo hii kitakusaidia kupanua mawazo yako kujua ufanye maamuzi yapi sahihi unapotekeleza shughuli mbalimbali kwenye biashara yako hii ya ufugaji wa kuku kisasa.

Tufike mahali tuamue kufanya vitu kitaalamu na kuachana na matamanio tu hewa ya kutajirika kupitia miradi rahisi kama hii ambayo kwa haraka haraka tunahisi ni rahisi lakini hatuna mipango wala mikakati inanayoweza kutekelezeka tukafanikiwa kupata pesa za kutosha, wengi tunaishia kufuga kuku wa kula nyama Krismasi na Iddi tu ukiuliza kwanini unaambiwa, “Kuku bwana wana changamoto

Ikiwa umeweza kuliona tangazo hili,(Kwani huwa offa zangu sitoi mara kwa mara), HONGERA!  UNA BAHATI! nipigie simu, sms au watsap kupitia namba zangu 0765553030  /  0712202244 dai ili niweze kukutumia michanganuo hiyo mitatu halafu nitakupatia na kitabu changu kikubwa cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI bure kabisa ili ukajifunze mambo mengine mengi kuhusiana na Biashara na Ujasiriamali kwa ujumla wake  mfano jinsi ya kufanya utafiti/upembuzi yakinifu wa biashara kabala hujaianza, utafutaji wa masoko kitaalamu, namna ya kusajili biashara yako Brela, Manispaa, TRA nk.

Vitu vyote vinne utalipa shilingi elfu 10 tu! Na nakutumia kwa njia ya watsap au email. Wahi tangazo likiondolewa na offa itakuwa haipo tena.

Asante sana!

Peter A. Tarimo

Business Plan Exert and small Entrepreneurs Advisor in Tanzania

0 Response to "KIJANA MWENYE MALENGO MAKUBWA KIUCHUMI: NIFUGE KUKU AINA GANI, MAYAI, NYAMA AU KIENYEJI? NISHAURI TAFADHALI"

Post a Comment